MALENGO YA WAHAKIKI WA DINI NO.1

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

MALENGO YA WAHAKIKI WA DINI NO.1

Jitihada za wahakiki zinaweza zikawa kwa ajili ya malengo na hadafu tofauti: -

-Baadhi ya wahakiki hufanya uhakiki wao kwa ajili ya kueneza na kusambaza ukoloni mambo leo, unaotoka katika mataifa makubwa wenye nia ya kutaka kuutawala ulimwengu kifikra na kiutamaduni.

-Baadhi ya wahakiki hufanya uhakiki wao kuhusiana na dini wakiwa na malengo ya kutaka kutambua ukweli na uhakika wa dini hiyo.

- Baadhi ya wahakiki huingia katika uwanja wa uhakiki wakiwa na malengo ya kuhujumu au kufosi fikra za watu na jamii kwa ujumla, wahakiki kama hao huwa na nia ya kuharibu fikra za watu na jamii kwa ujumla.

- Baadhi ya wahakika huingia katika uwanja wa tahakiki kutokana na udadisi walionao wa kutaka kutambua na kujua mambo tofauti yanayohusiana na dini au mambo mbali mbali.

-Baadhi ya wahakiki huingia katika uwanja wa uhakiki wakiwa na malengo ya kutaka kufahamu uhakika wa mambo na kujua jamii inataka mahitajio gani katika maisha yao, basi wahakiki hao hufanya jitihada zao zote ili kudhamini mahitajio yanayohitajiwa na wanaadamu.

-Baadhi ya wahakiki huingia katika uwanja wa tahakiki kwa ajili ya kuharibu na kuhujumu fikra za watu wenye dini, au walio na itikadi au imani ya dini fulani.

Hayo yalikuwa ni baadhi ya malengo tu ya wahakiki, hivyo ni wadhifa wa kila mtu mwenye fikra salama kuwa makini katika kutambua hadafu na malengo ya uhakiki wake, na wanadini wote mahasusi Waislamu inawawajibikia kukabiliana na vile vitengo vya wahakiki ambavyo malengo yao ni kuiharibu dini au kuitawala jamii.

Kwa upande mwengine Waislamu ni lazima wawe na elimu ya kutosha katika kuwapatia wahakiki majibu ya masula yao, majibu ambayo yatamtoa muhakiki katika shaka na kumridhisha kiakili na kiakida, hatimae kuelewa na kutambua haki na uhakika wa dini.

Ni wadhifa wa kila Muislamu kupokea suala, tata, au mapingaji yoyote yale yanayotolewa na wahakiki bila ya kudharau nadharia au mitazamo ya wanahakiki, kutafiti tata na masuala ambayo yanatolewa na wahakiki na kuyapatia ufumbuzi wake.

Ni wadhifa wa Waislamu kupokea tata za wahakiki kwa nia moja, na malengo mamoja ya kuzitafutia ufumbuzi wa kielimu tata hizo, na sio kuzitoa maana tata au masuala mbali mbali yanayoulizwa na wahakiki, kwa sababu kufanya hivyo hakutapelekea faida yoyote katika jamii na dini ya Kiislamu, kwani malengo makuu ya dini ya Kiislamu na Waislamu kwa ujumla ni kuitangaza dini hiyo tukufu ili kuenea katika pande zote za dunia, kwani dini hiyo ndio dini ya haki inayohitajiwa na kila mwanaadamu katika kuendeleza na kupata saada njema ya maisha yake ya duniani na Akhera.

Wahakiki wa dini katika hatua ya mwanzo ni lazima kufahamu na kutambua uhakika wa dini kupitia udhahiri wa matini za kidini, na katika hatua ya pili baada ya kufahamu kwa uzuri dhahiri ya dini basi anaweza akafanya jitihada katika kufahamu batini ya dini, lakini ni lazima azingatie kuwa analazimika kutumia dhahiri ya dini kwa ajili ya kufahamu batini ya dini, na sio kutoka nje ya dini, kwa sababu kile anachokifahamu katika undani wa dini ni ule ufahamu wa yale aliyoyakubali katika udhahiri wa dini. Kwa hiyo uhakiki wa kweli hauwezi kukubalika kwa kuhakiki katika njia za logical Politivism, kutafsiri kwa kutumia njia yaTaawiyl ( kutafsiri kwa njia ya dhahiri shahiri), au kuhakiki kwa njia ya Hermenutics. Katika paragrafu hii tutazielezea njia hizo kwa undani zaidi, kwani inawezekana baadhi ya watu wasielewe makusudio ya njia hizo ni nini.

a) Logical Politivism: Ni kitu ambacho kinaweza kufanyiwa majaribio na tajriba. Kwa maana nyengine tunaweza kusema hivi:-

Ni sentensi, mada,au tungo yoyote ile ya sheria ya kidini, jamii, serikali, ni lazima iwe na uwezo wa kuiingiza katika maabara na kutafutiwa utafiti na majaribio ambayo yataweza kuonyesha kwa kina uhakika wake, kwa mfano kama inadaiwa kuwa siku ya kiama kuna Pepo kwa watu wema, na kuna jahanamu (moto) kwa watu wabaya, basi ni lazima pafanyiwe utafiti utakaoonyesha ukweli wa Pepo na Jahanamu hiyo, na ikiwa kutokana na uhakiki au utafiti utakaofanywa hakukupatikana uhakika wala ufumbuzi wowote utakaothibitisha kuwepo kwa vitu hivyo, basi madai hayo ya kuwa kuna Pepo na moto hayatakubalika.

b)Taawili (tafsiri ya dhahiri shahiri) ni tafsiri yenye kumurika maneno kupitia darubini ya udhahiri wa mambo, na maana dhahiri za maneno zilivyo.

Taawili ni kufasiri na kutafuta maana za maneno kupitia darubini ya nguvu za kiakili zenye uwezo wa kujua maana dhahiri na kuilenga ile maana halisi iliyojificha ndani ya maneno. Kwa hiyo kwa msingi huo tunaweza kusema kuwa tafsiri ya dhahiri shahiri ni tafsiri ya wazi yenye kuonekana dhahiri shahiri bila ya mashaka yoyote.

Taawili ni tafsiri mficho ambayo maana yake ni lazima itafutwe huko mafichoni iliko, tafsiri mficho ni yenye kuyasaka na kuyatafuta maneno yaliyo mafichoni, (yaani maneno yaliyo batini, yaani maneno yaliyojificha ndani ya ibara, au sentensi). Kwa mfano:-

Mwenye kufasiri Qur-ani kwa njia ya dhahiri anatumia akili yake kwa kiwango kidogo tu, wala hatakiwi kutafakari kwa kiwango kikubwa, ama kwa yule mfasiri ambaye anaifasiri Qur-ani kwa ubatini wake, basi mfasiri huyo atakuwa anatumia akili na kiwango kikubwa cha kutafakari


MWISHO