NJIA ZA MAADUI KUPINGANA NA MITUME

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

NJIA ZA MAADUI KATIKA KUPINGANA NA MITUME NO.1

Katika makala zilizopita tulielezea dalili zilizowafanya maadui wa Kiislamu kupingana na Mitume ya Mwenyeezi Mungu, katika makala hii tutaelezea njia walizotumia maadui hao katika kukabiliana na Mitume hiyo Mitukufu.

Tangu hapo mwanzo, baada tu ya Mitume kupewa utume walikumbana na watu ambao waliwakhalifu kutokana na malinganio waliyokuja nayo Mitume hiyo. Kwa sababu malinganio hayo yalikuwa hayawiani na itikadi zao au manufaa yao ambayo walikuwa wakiyahitajia, hivyo watu hao walisimama kedete kuupinga ujumbe wa Mwenyeezi Mungu waliokuja nao Mitume hiyo.

Qur-ani Karym imeelezea kwa uwazi dalili zilizowafanya watu hao wawakhalifu Mitume, njia walizotumia katika kupingana nao na hatima ya watu hao, katika somo hili tutaelezea njia hizo, kwa sababu kuzifahamu njia hizo kutawapelekea wafuasi wa Mitume kuzifahamu hila za maadui wao, na kuwafanyia wepesi katika kustahamili tabu na matatizo watakayoweza kuyapata.

Mitume siku zote walikuwa wakisumbuliwa na kuudhiwa na maadui wa kiislamu, wenye kibri, wenye mali, majahili, n.k. kila mmoja kati yao walikuwa wakiwapa mateso wafuasi wa Mitume kwa upande wake, na walikuwa wakiweka vikwazo na vizuizi ili harakati za Kiislamu zisiendelee, miongoni mwa njia walizotumia maadui hao wa Kiislamu ni:-

3.KUWAPA TABU NA MATESO.

Mitume na wafuasi wao siku zote walikuwa wakifanyiwa mateso na maadui wa Kiislamu, kama inavyosema qur-ani:-

وهمت کل امة برسلهم لیأخذوه[1]

Kila umati ulikuwa ukitafuta mbinu za kuwapa mateso Mitume.

Na walifanya jitihada za kuwahamisha na kuwatoa katika miji na ardhi zao ili kuuzuia ujumbe wa Mwenyeezi Mungu waliokuja nao Mitume usisambazike duniani:-

وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُواْ لِرُسُلِهِمْ لَنُخْرِجَنَّـكُم مِّنْ اَرْضِنَا اَوْ لَتَعُودُنَّ فِى مِلَّتِنَا فَاَوْحَي إِلَيْهِمْ رَبُّهُمْ لَنُهْلِكَنَّ الظَّالِمِينَ[2]

Na walio kufuru wakawaambia Mitume wao: Tutakutoeni katika nchi yetu, au mrudi katika mila yetu. Basi Mola wao Mlezi aliwaletea wahyi: Hakika tutawaangamiza walio dhulumu!

Vile vile waliweka vikwazo vya kiuchumi ili kuwaparaganya wafuasi wa Mitume, kama wanavyosema wanafiki:-

هُمُ الَّذِينَ يَقُولُونَ لاَ تُنفِقُوا عَلـٰي مَنْ عِندَ رَسُولِ اللهِ حَتَّي يَنفَضُّوا وَلِلَّهِ خَزَائِنُ السَّمَاوَاتِ وَالاَرْضِ وَلَكِنَّ الْمُنَافِقِينَ لاَ يَفْقَهُونَ[3]

Hao ndio wanao sema: Msitoe mali kwa ajili ya walioko kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, ili waondokelee mbali! Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye khazina za mbingu na ardhi, lakini wanaafiki hawafahamu.

4.KUWAFUNGA GEREZANI NA KUWAUWA.

Maadui wa kikafiri mbali ya kufanya mbinu za kuwafunga jela Mitume, vile vile walifanya mbinu za kuwauwa, kama anavyosema Allah (s.w):-

وَإِذْ يَمْكُرُ بِكَ الَّذِينَ كَفَرُواْ لِيُثْبِتُوكَ اَوْ يَقْتُلُوكَ اَوْ يُخْرِجُوكَ وَيَمْكُرُونَ وَيَمْكُرُ اللّهُ وَاللّهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ

Na walipo kupangia mpango walio kufuru wakufunge, au wakuuwe, au wakutoe. Wakapanga mipango yao, na Mwenyezi Mungu akapanga yake. Na Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa mipango.

*Hapa inatajwa ile ile mitingi yao Maqureishi waliyoifanya Makka kabla Mtume hajaondoka, walikutanika katika jumba lao la mitingi wakatoa shauri kutafuta lipi la kumfanyia Nabii Muhammad(s.a.w.w) limuangamize. Wengine walisema afungwe huko Makka bila ya kupewa chakula – au kwa kupewa chakula kidogo kabisa – mpaka afe, wengine wakasema azibwe macho, azibwe mdomo, atiwe pingu za mikono na miguu, apandishwe juu ya ngamia, aliyetiwa vitunga vya macho, akatupwe majangwani huko, ahangaike mpaka afe kwa kiu na njaa na jua.

Wengine wakasema wachaguliwe vijana watukufu wamshambulie mara moja wote na kumuuwa, na hii sehemu ya mwisho ndiyo iliyokubaliwa.lakini usiku ule Mtume alihama kwenda Madina,wasiwahi lolote.


[1] Ghaar Aya ya 5

[2] Surat Ibrahim Aya ya 13

[3] Surat Munafiquuna Aya ya 7
MWISHO