Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

WALIOWAHALIFU MITUME NO.1

0 Voti 00.0 / 5

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

WALIOWAKHALIFU MITUME NO.1

WAFUASI WAKWELI WA MITUME

* Ni alama gani zinazoonesha ukweli wa wafuasi wa Mitume?.

* Kuna athari gani katika kuwakubali na kuwafuata Mitume?.

Katika makala iliyopita tulielezea kuhusu wafuasi wa kweli wa Mitume ya Mwenyeezi Mungu (s.w) na sifa walizonazo watiifu hao. katika makala hii tutaendelea kuelezea sababu zilizowafanya baadhi ya watu kuwakhalifu Mitume ya Mwenyeezi Mungu.

* Kwa nini baadhi ya watu walisimama kidete kuwakhalifu Mitume?

* Waliowakhalifu Mitume walitumia njia gani katika kupingana na Mitume?.

DALILI ZILIZOWAFANYA WAWAKHALIFU MITUME.

Tangu hapo mwanzo, baada tu ya Mitume kupewa utume walikumbana na watu ambao waliwakhalifu kutokana na malinganio waliyokuja nayo Mitume hiyo. Kwa sababu malinganio hayo yalikuwa hayawiani na itikadi zao au manufaa yao ambayo walikuwa wakiyahitajia, hivyo watu hao walisimama kedete kuupinga ujumbe wa Mwenyeezi Mungu waliokuja nao Mitume hiyo.

Qur-ani Karym imeelezea kwa uwazi dalili zilizowafanya watu hao wawakhalifu Mitume, njia walizotumia katika kupingana nao na hatima ya watu hao, katika somo hili tutaelezea njia hizo, kwa sababu kuzifahamu njia hizo kutawapelekea wafuasi wa Mitume kuzifahamu hila za maadui wao, na kuwafanyia wepesi katika kustahamili tabu na matatizo watakayoweza kuyapata. Kama anavyosema Allah (s.w):-

وَكُـلاًّ نَّقُصُّ عَلَيْكَ مِنْ اَنبَاء الرُّسُلِ مَا نُثَبِّتُ بِهِ فُؤَادَكَ وَجَاءكَ فِى هَـذِهِ الْحَقُّ وَمَوْعِظَةٌ وَذِكْرَي لِلْمُؤْمِنِينَ[1]  

Na yote tunayo kusimulia katika khabari za Mitume ni ya kukupa nguvu moyo wako. Na katika haya imekujia haki na mawaidha na ukumbusho kwa Waumini.

Dalili na sababu zilizowafanya wawakhalifu Mitume Dalili zilizowafanya maadui kuwakhalifu Mitume kutokana na yale waliyokuja nayo ni:-

1.Kufumba macho, masikio na ulimi katika kukabiliana na haki au uhakika wa mambo.

Waliowakhalifu Mitume walijitia uziwi, ububu na upofu katika kuikubali haki, hivyo walipinga yale waliyolingania Mitume.

Qur-ani kariym inasema:-

صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لاَ يَرْجِعُونَ[2]

Viziwi, mabubu, vipofu; kwa hivyo hawatarejea.

2.Kukumbwa na mabalaa kutokana na kufuata mwenendo na sifa za shetani.

kama tunavyosoma ndani ya Qur-ani:-

تَاللهِ لَقَدْ اَرْسَلْنَا إِلَي اُمَمٍ مِّن قَبْلِكَ فَزَيَّنَ لَهُمُ الشَّيْطَانُ اَعْمَالَهُمْ فَهُوَ وَلِيُّهُمُ الْيَوْمَ وَلَهُمْ عَذَابٌ اَلِيمٌ[3]

Wallahi! Sisi tulituma Mitume kwa umati zilizo kuwa kabla yako, lakini Shetani aliwapambia vitendo vyao. Kwa hivyo leo yeye ndiye rafiki yao; nao watapata adhabu chungu.

3. Kuwa pamoja na washirikina na wenye kibri.

Mwenyeezi Mungu anasema :-

وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَي الْكِتَابَ وَقَفَّيْنَا مِن بَعْدِهِ بِالرُّسُلِ وَآتَيْنَا عِيسَي ابْنَ مَرْيَمَ الْبَيِّنَاتِ وَاَيَّدْنَاهُ بِرُوحِ الْقُدُسِ اَفَكُلَّمَا جَاءكُمْ رَسُولٌ بِمَا لاَ تَهْوَي اَنفُسُكُمُ اسْتَكْبَرْتُمْ ففَرِيقاً كَذَّبْتُمْ وَفَرِيقاً تَقْتُلُونَ[4]

Na hakika tulimpa Musa Kitabu na tukafuatisha baada yake Mitume wengine. Na tukampa Isa, mwana wa Mariamu, hoja zilizo waziwazi, na tukamtia nguvu kwa Roho Takatifu. Basi kila walipo kufikieni Mitume kwa yale ambayo hayapendwi na nafsi zenu, mlijivuna; wengine mkawakanusha, na wengine mkawauwa.

Na katika Aya nyengine anasema:-

وَمَا اَرْسَلْنَا فِى قَرْيَةٍ مِّن نَّذِيرٍ إِلاَّ قَالَ مُتْرَفُوهَا إِنَّا بِمَا اُرْسِلْتُم بِهِ كَافِرُونَ[5]

Na hatukumtuma mwonyaji yeyote kwenye mji, ila walisema walio jidekeza kwa starehe zao wa mji huo: Hakika sisi tunayakataa hayo mliyo tumwa nayo.

 

[1] Surat Hud Aya ya 120

[2] Surat Al-Baqarah Aya ya 18

[3] Surat An –Nahli Aya ya 63

[4] Surat Al-Baqarah Aya ya 87

[5] Surat Saba Aya ya 34

MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini