Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

WALIOWAHALIFU MITUME NO.3

0 Voti 00.0 / 5

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

WALIOWAKHALIFU MITUME NO.3

* Kwa nini baadhi ya watu walisimama kidete kuwakhalifu Mitume?

* Waliowakhalifu Mitume walitumia njia gani katika kupingana na Mitume?.

Katika makala iliyopita tulielezea sababu zilizowafanya baadhi ya watu kuwakhalifu Mitume, katika makala hii tutaendelea kuelezea sababu na dalili nyengine.

5. WALIOWAKHALIFU MITUME.

waliowakhalifu Mitume Sio washirikina tu, bali kuna makundi na watu tofauti waliowakhalifu Mitume, miongoni mwao ni washirikina, makafiri. Maadui, n.k. na baadhi ya wakati kulitokea watu amabo kidhahiri walidai kuwa wamewaamini Mitume hiyo, lakini kwa kweli walikuwa ni wanafiki, yaani wakiwa pamoja na Mitume hudai kuwa wao wanawaamini Mitume, na wakiwa pamoja na makafiri hudai kuwa wako pamoja na makafiri, hivyo imani zao zilikuwa ni dhaifu, na walisababisha madhara zaidi katika dini ya Kiislamu kuliko hata hao makafiri, katika sehemu hii tutatoa mifano na mwenendo waliokuwa wakitumia watu kama hao:-

1. Kuwaweka watu mbali na viongozi wao wa kidini.

Uhusiano uliokuwepo baina ya watu na viongozi wao wa dini – yaani Mitume – ulisababisha kukuza imani za watu na kuiweka jamii kuwa katika amani kutokana na sehemu waliyokuwa nayo viongozi hao katika jamii, lakini wanafiki walipoona mafanikio ya Waislamu waliingiwa na kite cha roho na wasi wasi kiasi ya kwamba walifanya jitihada zao zote kuwazuilia watu na Waislamu kwa ujumla ili pasiwe na uhusiano wowote baina yao. Na iwapo palitokea hitilafu baina yao waliona bora wahukumiwe au kutaka ushauri kwa Mataghuti kuliko kuhukumiwa au kutaka ushauri kwa Mitume. Kama tunavyoona ndani ya Qur-ani:-

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْاْ إِلَي مَا اَنزَلَ اللّهُ وَإِلَي الرَّسُولِ رَاَيْتَ الْمُنَافِقِينَ يَصُدُّونَ عَنكَ صُدُودا[1]            

Na wanapo ambiwa: Njooni kwenye yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, na njooni kwa Mtume; utawaona wanaafiki wanakukwepa kwa upinzani.

2. Kuwavunjia heshima Mitume na viongozi wa kidini.

Wafuasi wa kweli na waaminifu wa Mitume siku zote walikuwa tayari kutii amri za Mola wao na Mitume yake. Na walikuwa hawafanyi jambo lolote bila ya kupata idhini kutoka kwa Mola wao au Mitume yao. Lakini kwa wale ambao walikuwa hawana itikadi na isma waliyonayo Mitume, na hawakuwa na imani kamili katika nyoyo zao, na walikuwa na ghururi na majivuno kutokana na elimu au uwezo waliokuwa nao, na waliamua mambo vile wenyewe walivyotaka, na kwa sababu hiyo basi Mwenyeezi Mungu anawatahadharisha watu hao kwa kusema:-

يَا اَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لاَ تُقَدِّمُوا بَيْنَ يَدَيِ اللهِ وَرَسُولِهِ وَاتَّقُوا اللهَ إِنَّ اللهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ[2]

Enyi mlio amini! Msitangulie mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.

* Haya ndiyo tunayoambiwa kila siku, kuwa maadamu iko kauli ya Mwenyeezi Mungu na Mtume,basi isifuatwe kauli ya mwengine.

Na vile vile kwa wale ambao wako thabiti katika imani yao, basi watu kama hao huhifadhi imani yao na kuwaheshimu viongozi wao – Mitume – na wala hawapandishi sauti zao wala kujadiliana na Mitume yao, na huzungumza kwa sauti za chini kabisa pale wanapokabiliana na Mtume wao.

یغضون أصواتهم عند رسول الله.

Na huzungumza kwa sauti ya chini wanapokabiliana na Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu.

Ama kwa wale ambao imani zao ni  dhaifu, na wametawaliwa na maradhi katika nyoyo zao, huwavunjia heshima, huleta majadiliano na kupandisha sauti zao wanapokabiliana na Mitume.  

Hivyo Mwenyeezi Mungu Mtukufu anawatahadharisha watu hao kwa kuwaambia:-

يَا اَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لاَ تَرْفَعُوا اَصْوَاتَكُمْ فَوْقَ صَوْتِ النَّبِيِّ وَلاَ تَجْهَرُوا لَهُ بِالْقَوْلِ كَجَهْرِ بَعْضِكُمْ لِبَعْضٍ اَن تَحْبَطَ اَعْمَالُكُمْ وَاَنتُمْ لاَ تَشْعُرُونَ[3]

Enyi mlio amini! Msinyanyue sauti zenu kuliko sauti ya Nabii, wala msiseme naye kwa kelele kama mnavyo semezana nyinyi kwa nyinyi, visije vitendo vyenu vikaharibika, na hali hamtambui.

*Aya hiyo inaonesha baadhi ya mambo yaliyokatazwa kufanyiwa Mitume.

 

[1] Surat Nisaa Aya ya 61

[2] Surat Al-Hujurat Aya ya 1

[3] Surat Al-Hujurat Aya ya 2

MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini