Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

WALIOWAHALIFU MITUME NO.4

0 Voti 00.0 / 5

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

WALIOWAKHALIFU MITUME NO.4

* Kwa nini baadhi ya watu walisimama kidete kuwakhalifu Mitume?

* Waliowakhalifu Mitume walitumia njia gani katika kupingana na Mitume?.

Katika makala iliyopita tulielezea sababu zilizowafanya baadhi ya watu kuwakhalifu Mitume, katika makala hii tutaendelea kuelezea sababu na dalili nyengine.

5. WALIOWAKHALIFU MITUME.

waliowakhalifu Mitume Sio washirikina tu, bali kuna makundi na watu tofauti waliowakhalifu Mitume, miongoni mwao ni washirikina, makafiri. Maadui, n.k. na baadhi ya wakati kulitokea watu amabo kidhahiri walidai kuwa wamewaamini Mitume hiyo, lakini kwa kweli walikuwa ni wanafiki, yaani wakiwa pamoja na Mitume hudai kuwa wao wanawaamini Mitume, na wakiwa pamoja na makafiri hudai kuwa wako pamoja na makafiri, hivyo imani zao zilikuwa ni dhaifu, na walisababisha madhara zaidi katika dini ya Kiislamu kuliko hata hao makafiri, katika sehemu hii tutaendelea kutoa mifano na mienendo waliokuwa wakitumia watu kama hao:-

3. Kutoshiriki katika vita na kutofanya kazi za kheri katika jamii.

Baadhi ya watu kutokana na imani dhaifu walizokuwa nazo, hawakuwa tayari kushiriki katika vita wala kufanya kazi ambazo zinaweza kuleta manufaa katika jamii, na waliishi maisha ya kifahari yaliyowaletea manufaa yao binafsi, watu kama hao basi wamejiharamishia Pepo wao wenyewe kwa kughilibiwa na anasa za dunia, na matendo yao mabaya waliyoyafanya. Mwenyeezi Mungu anasema:-

يَا اَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ انفِرُواْ فِى سَبِيلِ اللهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَي الاَرْضِ اَرَضِيتُم بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِى الآخِرَةِ إِلاَّ قَلِيلٌ[1]

Enyi mlio amini! Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache.

Hatima ya waliowakhalifu Mitume.

Waliowakhalifu Mitume na waliopanga njama za kuwauwa Mitume hawakupata faida yoyote isipokuwa kujidhulumu nafsi zao wao wenyewe binafsi, kwa sababu hawakuweza kuutumia umri wao kwa kuwaletea faida na mafanikio katika maisha yao, bali walijiletea madhara na kupotoka katika njia ya Mwenyeezi Mungu, kama tunavyosoma ndani ya Qur-ani:-

وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلاَ مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَي اللهُ وَرَسُولُهُ اَمْراً اَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ اَمْرِهِمْ وَمَن يَعْصِ اللهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلاَلاً مُّبِيناً[2]

Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapo kata shauri katika jambo lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi hakika amepotea upotofu ulio wazi.

Katika sehemu hii tutaashiria baadhi ya athari zilizowapata wale waliowakhalifu Mitume.

1. Kudhalilika.

Katika kipindi chote cha Tarekhe imethibitika kuwa mwenye kutaka haki ndiye anayepata mafanikio na ushindi, na maadui wa Kiislamu pia hawakuweza kupata yale waliyoyataka, hawakupata ushindi wala mafanikio yoyote katika maisha yao. Natija ya uadui wao basi haikuwa kitu chengine isipokuwa kudhalilika na kujidhalilisha wao wenyewe. Kama anavyosema Allah (s.w):-

إِنَّ الَّذِينَ يُحَادُّونَ اللهَ وَرَسُولَهُ كُبِتُوا كَمَا كُبِتَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَقَدْ اَنزَلْنَا آيَاتٍ بَيِّنَاتٍ وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ مُّهِينٌ[3]

Hakika wanao pinzana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, watadhalilishwa kama walivyo dhalilishwa wale walio kuwa kabla yao. Na tulikwisha teremsha Ishara zilizo wazi. Na makafiri watapata adhabu ya kufedhehesha.

2. Kuharibika kwa matendo na amali zao walizozitenda.

Inaeleweka kuwa, matendo mema huondoa athari za matendo maovu, basi na matendo maovu yaliyofanywa na wale waliowakhalifu Mitume, na wakawavunjia heshima zao, huondoa athari ya matendo mema, kama anavyosema Allah (s.w) kuwaambia wale waliowauwa Mitume na viongozi wa kidini:-

اُولَـئِكَ الَّذِينَ حَبِطَتْ اَعْمَالُهُمْ فِى الدُّنْيَا وَالآخِرَةِ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ[4]

Hao ndio ambao vitendo vyao vimeharibika duniani na Akhera. Nao hawatapata wa kuwanusuru.

Na Mwenyeezi Mungu anawatanabahisha watu hao waliowavunjia heshima Mitume yao, na wakanyanyua sauti zao kujibizana na Mitume hiyo kwa kuwaambia:-

يَا اَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لاَ تَرْفَعُوا اَصْوَاتَكُمْ فَوْقَ صَوْتِ النَّبِيِّ وَلاَ تَجْهَرُوا لَهُ بِالْقَوْلِ كَجَهْرِ بَعْضِكُمْ لِبَعْضٍ اَن تَحْبَطَ اَعْمَالُكُمْ وَاَنتُمْ لاَ تَشْعُرُونَ[5]

Enyi mlio amini! Msinyanyue sauti zenu kuliko sauti ya Nabii, wala msiseme naye kwa kelele kama mnavyo semezana nyinyi kwa nyinyi, visije vitendo vyenu vikaharibika, na hali hamtambui.

 

[1] Surat Tawba Aya ya 38

[2] Surat Al-Ahzaab Aya ya 36

[3] Surat Mujadilah Aya ya 5

[4] Surat Al-Imrani Aya ya 22

[5] Surat Hujurat Aya ya 2

MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini