Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

ATHARI YA DINI TAKATIFU

0 Voti 00.0 / 5

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI                                                                                                                                KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

ATHARI YA TAWHIYD KATIKA KUKAMILIKA MWANAADAMU KIELIMU

Itikadi ya kuamini Mola mmoja ni alama inayoonesha ukamilifu wa mwanaadamu kielimu, na ubora wa mwanaadamu kuliko malaika.

Mwenyeezi Mungu Mtukufu anasema:-

شَهِدَ اللّهُ اَنَّهُ لاَ إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ وَالْمَلاَئِكَةُ وَاُوْلُواْ الْعِلْمِ قَآئِمَاً بِالْقِسْطِ لاَ إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ[1]

Mwenyezi Mungu, na Malaika, na wenye ilimu, wameshuhudia kuwa hakika hapana mungu ila Yeye, ndiye Mwenye kusimamisha uadilifu; hapana mungu ila Yeye Mwenye nguvu na Mwenye hikima.

Basi iwapo mtu atauona utukufu wa Mwenyeenzi Mungu na uumbaji wa ulimwengu, na akazishuhudia aya za Mwenyeezi Mungu, lakini asiamini Mola mmoja huyo, basi mtu huyo atakuwa ni miongoni mwa majahili, na ni alama moja wapo inayoonesha ujahili wa mtu huyo.Kama vile Qur-ani inavyosema:-

اَمَّن جَعَلَ الاَرْضَ قَرَاراً وَجَعَلَ خِلاَلَهَا اَنْهَاراً وَجَعَلَ لَهَا رَوَاسِيَ وَجَعَلَ بَيْنَ الْبَحْرَيْنِ حَاجِزاً اَإِلَهٌ مَّعَ اللهِ بَلْ اَكْثَرُهُمْ لاَ يَعْلَمُونَ[2]

Au nani yule aliye ifanya ardhi mahali pa kutua, na akajaalia ndani yake mito, na akaweka milima? Na akaweka baina ya bahari mbili kiziwizi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Bali wengi wao hawajui.

Na kwa wale ambao hawaamini ya kuwa Mola ni mmoja tu ijapokuwa ni wenye kutoa nadhari katika elimu mbali mbali mfano elimu ya tajruba, au wakawa wana cheo katika jamii, lakini kwa upande wa elimu ya Qur-ani na tamaduni ya kiislamu wakawa ni majahili, basi Mwenyeenzi Mungu anawaambia watu hao kwa kusema:-

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ آمِنُواْ كَمَا آمَنَ النَّاسُ قَالُواْ اَنُؤْمِنُ كَمَا آمَنَ السُّفَهَاء اَلا إِنَّهُمْ هُمُ السُّفَهَاء وَلَـكِن لاَّ يَعْلَمُونَ[3]

Na wanapo ambiwa: Aminini kama walivyo amini watu. Husema: Tuamini kama walivyo amini wapumbavu? Hakika wao ndio wapumbavu, lakini hawajui tu.

Maelezo kuhusiana na aya

Mayahudi walikuwa wakiwafanya wale Waislamu waliotoka Makka wakatupa watu wao na mali zao, wakahamia Madina kumfuata Mtume na kuhifadhi dini yao. Na wale Waislamu wa Madina ambao waliwapokea waislamu wa Makka na kuwagawia mali yao, wakiwafanya wote ni wapumbavu.

Hakika Tawhiyd (kuamini Mola mmoja bila ya kumshirikisha na mwengine), ni jambo la uhakika na lisilo na pingamizi yoyote, na hakuna mtu yoyote anayeweza kulipinga jambo hilo,basi yule mtu ambaye hana akida hiyo, na wala haamini ya kuwa Mola mmoja tu ndiye anayestahiki kuabudiwa, basi mtu huyo atakuwa amefanya madhambi makubwa yasiyosameheka, kama vile Allah (s.w) anavyosema:-

إِنَّ اللّهَ لاَ يَغْفِرُ اَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ وَمَن يُشْرِكْ بِاللهِ فَقَدِ افْتَرَي إِثْماً عَظِيماً[4]

Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye. Na anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu basi hakika amezua dhambi kubwa.

3- ATHARI YA TAWHIYD KATIKA MATENDO YA MWANAADAMU

Wanaadamu wengi kutokana na kutojua wanatafuta nini na wanategemea kufanya nini katika maisha yao ya kila siku, huwa hawako katika utulivu, na wala hawana raha ya maisha, yote hayo yanasababishwa na kutokuamini Mola mmoja, na hufanya mambo yao kwa kumshirikisha Mwenyeenzi mungu na mwengine, katika hali ya kwamba pindi mwanaadamu anapomkumbuka Mola wake kila wakati, na akaamini kuwa Mola wake tu ndiye anayestahiki kuabudiwa na kuombwa, na akamtegemea Mwenyeenzi Mungu kwa kila hali, hapana shaka mtu huyo atakuwa katika utulivu, na kuishi duniani bila na kukumbwana mabalaa yasiyoweza kustahamilika.

Mwenyeezi Mungu katika kitabu chake kitukufu kuhusiana na watu ambao hawamuamini Mola wao bali humshirikisha, na shirki husababisha misuko suko na mabalaa katika maisha ya mwanaadamu anasema:-

ضَرَبَ اللهُ مَثَلاً رَّجُلاً فِيهِ شُرَكَاء مُتَشَاكِسُونَ وَرَجُلاً سَلَماً لِّرَجُلٍ هَلْ يَسْتَوِيَانِ مَثَلاً الْحَمْدُ للهِ بَلْ اَكْثَرُهُمْ لاَ يَعْلَمُونَ[5]

 Mwenyeezi Mungu anakupigieni mfano wa mtu mwenye mabwana washirika wanaogombana, na wa mtu (mwengine aliyehusika na bwana mmoja tu. Je! Wako sawa katika hali zao? Alhamdulilahi, lakini wengi wao hawajui. (Basi shughulika na bwana wako mmoja tu Mwenyeenzi Mungu).

Na kutoka katika kauli ya hadharati yussuf (a.s) anaelezea kwa kusema:-

يَا صَاحِبَيِ السِّجْنِ اَاَرْبَابٌ مُّتَفَرِّقُونَ خَيْرٌ اَمِ اللّهُ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ[6]

Enyi wafungwa wenzangu wawili! Je, mabwana wengi wanao farikiana wao kwa wao ni bora au Mwenyezi Mungu Mmoja Mwenye nguvu? Maelezo kuhusiana na aya Anawabainishia baadhi ya Tawhidi ya Mwenyeenzi Mungu. Mtu huchukua fursa ya kufundisha popote pale anapopata wasaa, usiitupe fursa ukiipata, usije ukajuta.

Na Mwenyeezi Mungu anaelezea kundi ambalo linamkumbuka na kumuamini Mwenyeezi Mungu, na kwa sababu ya kumkumbuka Mwenyeenzi Mungu basi hutua nyoyo zao.

الَّذِينَ آمَنُواْ وَتَطْمَئِنُّ قُلُوبُهُم بِذِكْرِ اللهِ اَلاَ بِذِكْرِ اللهِ تَطْمَئِنُّ الْقُلُوبُ[7]

Wale walio amini na zikatua nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Hakika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu ndio nyoyo hutua!

Na mwisho (natija) ya watu ambao kwa sababu ya kumkumbuka Mwenyeezi Mungu hutua nyoyo zao, na hawashughulishwi na matamanio yoyote ya dunia. Mwenyeenzi Mungu kuhusiana na watu hao anasema:-

رِجَالٌ لاَّ تُلْهِيهِمْ تِجَارَةٌ وَلاَ بَيْعٌ عَن ذِكْرِ اللهِ وَإِقَامِ الصَّلاَةِ وَإِيتَاء الزَّكَاةِ يَخَافُونَ يَوْماً تَتَقَلَّبُ فِيهِ الْقُلُوبُ وَالاَبْصَارُ[8]

Watu ambao biashara wala kuuza hakuwashughulishi na kumdhukuru Mwenyezi Mungu, na kushika Sala, na kutoa Zaka. Wanaikhofu Siku ambayo nyoyo na macho yatageuka.

Mwenyeenzi Mungu anasema:-

مَّا جَعَلَ اللهُ لِرَجُلٍ مِّن قَلْبَيْنِ فِى جَوْفِهِ وَمَا جَعَلَ اَزْوَاجَكُمُ اللاَّئِى تُظَاهِرُونَ مِنْهُنَّ اُمَّهَاتِكُمْ وَمَا جَعَلَ اَدْعِيَاءكُمْ اَبْنَاءكُمْ ذٰلِكُمْ قَوْلُكُم بِاَفْوَاهِكُمْ وَاللهُ يَقُولُ الْحَقَّ وَهُوَ يَهْدِى السَّبِيلَ[9]

Mwenyezi Mungu hakumwekea mtu yeyote kuwa ana nyoyo mbili ndani ya mwili wake. Wala hakuwafanya wake zenu - ambao mnawalinganisha migongo yao na migongo ya mama zenu - kuwa ni mama zenu. Wala hakuwafanya watoto wenu wa kupanga kuwa ni wana wenu khasa. Hayo ni maneno ya vinywa vyenu tu. Na Mwenyezi Mungu ndiye anaye sema kweli, naye ndiye anaye ongoa Njia.

Maelezo kuhusiana na aya Katika zama za jahiliya mtu akitaka kumuadhibu mkewe alikuwa akimwambia,:

“ Wewe kwangu ni kama mgongo wa mama yangu.” Hivi ni kumwambia,

“ Wewe ni haramu juu yangu”. Akisha kusema hivi, mwanamke yule huwa ni haramu juu yake maisha, wala hawezi kuolewa na mume mwengine Na talaka hii wakiita “Dhihaar”. Hapa wanakatazwa ada hii mbaya. Na katika surat Almujadilah aya ya 2-4 imetajwa hukumu yake na kafara yake

الَّذِينَ يُظَاهِرُونَ مِنكُم مِّن نِّسَائِهِم مَّا هُنَّ اُمَّهَاتِهِمْ إِنْ اُمَّهَاتُهُمْ إِلاَّ اللاَّئِى وَلَدْنَهُمْ وَإِنَّهُمْ لَيَقُولُونَ مُنكَراً مِّنَ الْقَوْلِ وَزُوراً وَإِنَّ اللهَ لَعَفُوٌّ غَفُور وَالَّذِينَ يُظَاهِرُونَ مِن نِّسَائِهِمْ ثُمَّ يَعُودُونَ لِمَا قَالُوا فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مِّن قَبْلِ اَن يَتَمَاسَّا ذٰلِكُمْ تُوعَظُونَ بِهِ وَاللهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ شَهْرَيْنِ مُتَتَابِعَيْنِ مِن قَبْلِ اَن يَتَمَاسَّا فَمَن لَّمْ يَسْتَطِعْ فَإِطْعَامُ سِتِّينَ مِسْكِيناً ذٰلِكَ لِتُؤْمِنُوا بِاللهِ وَرَسُولِهِ وَتِلْكَ حُدُودُ اللهِ وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ اَلِيمٌ[10]

- Wale miongoni mwenu wanao watenga wake zao, hao si mama zao. Hawakuwa mama zao ila wale walio wazaa. Na hakika hao wanasema neno linalo chusha, na la uwongo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kughufiria, Mwenye kusamehe.- Na wale wanao jitenga na wake zao, kisha wakarudia katika yale waliyo yasema, basi wamkomboe mtumwa kabla hawajagusana. Mnapewa maonyo kwa hayo. Na Mwenyezi Mungu anayajua yote mnayo yatenda.- Na asiye pata mtumwa kumkomboa, basi na afunge miezi miwili mfululizo kabla hawajagusana. Na asiye weza hayo basi awalishe masikini sitini. Hayo ni hivyo ili mumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na kwa makafiri iko adhabu chungu.

Vile vile katika aya hii na ya pili yake inakatazwa kumfanya mtoto wa kupanga kama uliyemzaa.

Tukizingatia natija inayopatikana katika aya hiyo tutaelewa kuwa itikadi ya kuamini Mola mmoja inawiana na nidhamu ya uumbaji, na shirki inahitilafiana na uumbaji, kwa sababu kama kungelikuwa na nafsi mbili tofauti ingeliwezekana kuwa na itikadi mbili tofauti (yaani itikadi ya kuamini Mola mmoja, na itikadi ya kumshirikisha Mwenyeenzi Mungu), lakini nafsi moja haiwezi ikakubali akida mbili tofauti.

Maelezo kwa ufupi kuhusiana na somo lilopita.

Kuamini Mola mmoja na kuwa na itikadi ya kuwa Yeye hana mshirika inatutanabahisha sisi wanaadamu kuwa makini katika nidhamu ya uumbaji wa vitu vyote duniani, vitabu vyote vya Mwenyeenzi Mungu vimekuja kutufunza sheria moja nayo ni kuamini Mola mmoja, na hii inawapelekea wanaadamu wote kuwa kitu kimoja, na kuwasaidia kuishi kwa utulivu katika amali na matendo.

Masuala.

1- Kwa nini kuamini Mola mmoja ni nguzo muhimu iliyolinganiwa na Mitume yote ya Mwenyeenzi Mungu kuwaongoza wanaadamu katika njia iliyonyooka?.

2- Qur-ani kariym kwa kuzingatia nidhamu ya vitu vyote duniani vipi imethibitisha na kutoa dalili ya kuamini Mola mmoja?.

3- Kwa kuzingatia kauli ya Imamu Aliy (a.s) vipi unaweza ukathibitisha kuamini Mola mmoja?

4- elezea kwa ufupi faida za kuamini Mola mmoja.

 

[1] Surat-Al-imrani aya ya 18

[2] Surat Namli aya ya 61

[3] Suratul-Baqara aya ya 13

[4] Surat nisaa aya ya 48

[5] Surat Zumar aya ya 29

[6] Surat Yussuf aya ya 39

[7] Surat raad aya ya 28

[8] Surat nur aya ya 37

[9] Surat Ahzaab aya ya 4

[10] Suratul-Almujadilah aya ya 2-4

MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini