MAYAHUDI WAZIKADHIBISHA DINI ZA ALLAH

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KAULI YA MWENYEEZI MUNGU JUU YA MAKAFIRI 2

MAKAFIRI WANAMKADHIBISHA NA KUMTUKANA MTUME (S.A.W.W)

Katika makala iliyopita kuhusiana na kauli ya Mwenyeezi Mungu juu ya makafiri tulielezea kwa muhtasari jinsi Makafiri walivyokuwa wakimkadhibisha na kumtukana Mtume muhammad (s.a.w.w.). Na vile vile hawakukiamini kitabu chake Kitukufu – Qur_ani - .

Katika makala hii basi tutaendelea kuielezea mada hiyo kwa kuzingatia Aya za Qur-ani za Mwenyeezi Mungu.

Nabii Muhammad (s.a.w.w) alikuwa na hamu kubwa kabisa ya kutaka watu wote wasilimu upesi upesi, wapewe hiyo miujiza wanayoitaka wishe udhia. Lakini Mwenyeezi Mungu alikuwa hapendi Uislamu huo, akipenda wasilimu baada ya kuyafamu vyema hayo wanayoambiwa, sio wanasilimu kwa nguvu za miujiza, kwa kuthibitisha hayo Mwenyeezi Mungu Mtukufu anasema:-

وَإِن كَانَ كَبُرَ عَلَيْكَ إِعْرَاضُهُمْ فَإِنِ اسْتَطَعْتَ اَن تَبْتَغِيَ نَفَقاً فِى الاَرْضِ اَوْ سُلَّماً فِى السَّمَاء فَتَاْتِيَهُم بِآيَةٍ وَلَوْ شَاء اللّهُ لَجَمَعَهُمْ عَلـٰي الْهُدَي فَلاَ تَكُونَنَّ مِنَ الْجَاهِلِينَ[1]

Tarjuma:

Na ikiwa ni makubwa kwako huku kukataa kwao, basi kama unaweza kutafuta njia ya chini kwa chini ya ardhi, au ngazi kwendea mbinguni ili uwaletee Ishara -- Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angependa angeli wakusanya kwenye uwongofu. Basi usiwe miongoni mwa wasio jua.

 kama alivyobainisha haya katika Aya ya 51 ya Surat Ankabuut na nyenginezo.

اَوَلَمْ يَكْفِهِمْ اَنَّا اَنزَلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ يُتْلَي عَلَيْهِمْ إِنَّ فِى ذٰلِكَ لَرَحْمَةً وَذِكْرَي لِقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ[2]

Tarjuma:

Je! Kwani hayakuwatosha ya kwamba tumekuteremshia Kitabu hiki wanacho somewa?

Hakika katika hayo zipo rehema na mawaidha kwa watu wanao amini.

Makafiri waalimwambia kama kweli yeye Mtume basi naawape hiki na hiki … na awajuulishe kabla ya kuondoka kwa safari zao za biashara kuwa, safari hii litawafika hili na watapata hivi… na wakamwambia kwa nini anakula na anaoa. Basi ndiyo akajibiwa kwa haya yaliyotajwa katika Aya hii.

قُل لاَّ اَقُولُ لَكُمْ عِندِى خَزَآئِنُ اللهِ وَلا اَعْلَمُ الْغَيْبَ وَلا اَقُولُ لَكُمْ إِنِّى مَلَكٌ إِنْ اَتَّبِعُ إِلاَّ مَا يُوحَي إِلَيَّ قُلْ هَلْ يَسْتَوِى الاَعْمَي وَالْبَصِيرُ اَفَلاَ تَتَفَكَّرُونَ[3]

Tarjuma:

Sema: Mimi sikwambiini kuwa ninazo khazina za Mwenyezi Mungu. (nikakupeni mnayoyataka), Wala (sikwambieni kuwa ) najua mambo ya siri (ya Mwenyeezi mungu nikakubainishieni yatakayokufikieni katika biashara zenu na mengineyo kama mlivyotaka nikwambieni). Wala sikwambiini kuwa mimi ni Malaika. (hata mkanambia “kwa nini unakula na kuoa”) . Mimi sifuati ila yanayo funuliwa kwangu. Sema: Je, wanakuwa sawa, kipofu na mwenye kuona. Basi hamfikiri?.Mwenyeezi Mungu anaendelea kwa kusema:-

 وَلاَ تَطْرُدِ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُم بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ مَا عَلَيْكَ مِنْ حِسَابِهِم مِّن شَيْءٍ وَمَا مِنْ حِسَابِكَ عَلَيْهِم مِّن شَيْءٍ فَتَطْرُدَهُمْ فَتَكُونَ مِنَ الظَّالِمِينَ

Wala usiwafukuze wanao mwomba Mola Mlezi wao asubuhi na jioni kwa kutaka radhi yake. Si juu yako hisabu yao hata kidogo, wala hisabu yako si juu yao hata kidogo, hata uwafukuze na uwe miongoni mwa wenye kudhulumu. [4]

Maelezo kuhusiana na Aya ya 52 ya surat al-an-aam.

Watu wakubwa wa Kikureishi katika kutafuta udhuru tu wa kutomfuata Mtume – walimwambia Mtume:-

“Sisi hatuwezi kuingia katika dini hii tukawa sawa sawa na watumwa hawa na makafiri hawa waliokufuata ukawafanya sawa sawa na bwana zao, na sawa sawa na mabwana wengine watukufu, ukitaka tukufuate wafukuze hawa wasije tena kwako, (au wawekee siku yao makhasusi (maalumu)). Hapo tutakufuata. Akaambiwa Mtume na Mwenyeezi Mungu maneno haya na akam-bainishia kuwa kila mtu ana hesabu yake – m-baya hatonufaika siku ya Kiama kwa ajili ya rafiki yake mwema aliyekuwa naye duniani, na mwema hatadhurika Kiama kwa rafiki yake m-baya aliyekuwa naye duniani maadamu alikuwa akimwasa naye hasikii.


[1] Surat ankabuut Aya ya 35

[2] Surat Ankabuut Aya ya 51

[3] Surat Al –An-aam Aya ya 50

[4] Surat Al-An-aam Aya ya 52

MWISHO