MUISLAMU WA MWANZO

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

1. MUISLAMU WA MWANZO.

Katika kamusi ya Qur-ani Majiyd (Muslim) ni mtu ambaye amesalimu katika kutii amri za Mola wake, kama alivyosema Mfalme (Malkia)Sabaa:-

قِيلَ لَهَا ادْخُلِى الصَّرْحَ فَلَمَّا رَاَتْهُ حَسِبَتْهُ لُجَّةً وَكَشَفَتْ عَن سَاقَيْهَا قَالَ إِنَّهُ صَرْحٌ مُّمَرَّدٌ مِّن قَوَارِيرَ قَالَتْ رَبِّ إِنِّى ظَلَمْتُ نَفْسِى وَاَسْلَمْتُ مَعَ سُلَيْمَانَ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ[1]

Akaambiwa: Liingie behewa la hili jumba. Alipo liona alidhani ni maji, na akapandisha nguo mpaka kwenye miundi yake. (Sulaiman) akasema:Hakika hilo ni behewa lilio sakafiwa kwa viyoo! Akasema (Malkia): Mola wangu Mlezi! Mimi nimejidhulumu nafsi yangu, na sasa nanyenyekea pamoja na Sulaiman kwa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote. Kwa maana hiyo basi, Mitume na wajumbe wote wa Mwenyeezi Mungu walikuwa ni Waislamu, yaani hawakuwa washirikina wala walikuwa hawafuati dini zilizoharifiwa, kama tunavyosoma kuhusiana na Nabii Ibrahimu (a.s):-

مَا كَانَ إِبْرَاهِيمُ يَهُودِيّاً وَلاَ نَصْرَانِيّاً وَلَكِن كَانَ حَنِيفاً مُّسْلِماً وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ[2]

Ibrahim hakuwa Yahudi wala Mkristo, lakini alikuwa mwongofu Muislamu, wala hakuwa katika washirikina.

Vile vile Mitume iliwaelezea kwa uwazi kabisa watu kutokana na kuwa wao ni waislamu, kama tunavyosoma kuhusiana na nabii Nuhu (a.s):-

فَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَمَا سَاَلْتُكُم مِّنْ اَجْرٍ إِنْ اَجْرِيَ إِلاَّ عَلـٰي اللهِ وَاُمِرْتُ اَنْ اَكُونَ مِنَ الْمُسْلِمِينَ[3]

Lakini mkigeuka, basi mimi sikukuombeni ujira. Ujira wangu hauko ila kwa Mwenyezi Mungu. Na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Waislamu.

Vile vile siku zote Mitume ilikuwa ikiomba kwa Mwenyeezi Mungu wabakie kuwa Waislamu, na waage dunia hali ya kuwa wao ni waislamu,kama tunavyosoma kuhusiana na Nabii Yussuf (a.s):-

رَبِّ قَدْ آتَيْتَنِى مِنَ الْمُلْكِ وَعَلَّمْتَنِى مِن تَاْوِيلِ الاَحَادِيثِ فَاطِرَ السَّمَاوَاتِ وَالاَرْضِ اَنتَ وَلِيِّى فِى الدُّنُيَا وَالآخِرَةِ تَوَفَّنِى مُسْلِماً وَاَلْحِقْنِى بِالصَّالِحِينَ[4]

Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika umenipa utawala, na umenifunza tafsiri ya mambo. Ewe Muumba wa mbingu na ardhi! Wewe ndiye Mlinzi wangu katika dunia na Akhera. Nifishe hali ya kuwa ni Muislamu na nichanganyishe na watendao mema.

Lakini ni lazima tuelewe kwamba miongoni mwa Mitume yote hiyo, ni Mtume Muhammad (s..a.w.w) tu ndiye aliyepewa ruhusa ya kujiarifisha mwenyewe kuwa Yeye ni “وَاَنَاْ اَوَّلُ الْمُسْلِمِينَ”- yaani, na mimi ni wa kwanza wa Waislamu. - kama anavyosema Allah (s.w):-

لاَ شَرِيكَ لَهُ وَبِذٰلِكَ اُمِرْتُ وَاَنَاْ اَوَّلُ الْمُسْلِمِينَ[5]

Hana mshirika wake. Na hayo ndiyo niliyo amrishwa, na mimi ni wa kwanza wa Waislamu.

Na hii ni kwa sababu yeye ni mwenye na daraja kwanza kiimani na katika kusalimu na kutii amri za Mola wake, na ni Mtume wa mwisho miongoni mwa Mitume yote ya Mwenyeezi Mungu. katika Qur-ani tunasoma:-

قُلْ إِنِّى اُمِرْتُ اَنْ اَعْبُدَ اللهَ مُخْلِصاً لَّهُ الدِّينَ . وَاُمِرْتُ لِاَنْ اَكُونَ اَوَّلَ الْمُسْلِمِينَ[6]

Sema: “Hakika nimeamrishwa nimuabudu Mwenyeezi Mungu kwa kumuitakidi kuwa Mola ni Yeye tu”.

“Na pia nimeamrishwa niwe wa kwanza wa (viumbe) wanaojisalimisha kwa (Mwenyeezi Mungu).”

[1] Suratun Naml Aya ya 44

[2] Surat Al-Imrani Aya ya 67

[3] Surat Yunus Aya ya 72

[4] Surat Yussuf Aya ya 101

[5] Surat Al-An-aam Aya ya 163

[6] Surat Azumar Aya ya11-12.

MWISHO