TABIA NJEMA ZA MTUME (S.A.W.W)

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

5.TABIA NJEMA ZA MTUME (S.A.W.W).

Mtume Muhammad (s.a.w.w) alikuwa na uso wenye bashasha na furaha, maneno mazuri, na moyo wenye upendo na wakati wote alionekana na tabasamu usoni mwake. Na alikuwa ni mwenye jitihada katika kuwalingania watu na kufikisha ujumbe wa Mwenyeezi Mungu. kama anavyosema Allah (s.w):-

وَإِنَّ لَكَ لاَجْراً غَيْرَ مَمْنُونٍ. وَإِنَّكَ لَعَلى خُلُقٍ عَظِيمٍ[1]

Na kwa hakika wewe una malipo yasiyo katika.

Na hakika wewe una tabia tukufu.

Vile vile alikuwa ni mnyenyekevu na Mwenye haya, kiasi ya kwamba alikuwa ni mstahamilivu alipokuwa akiona tabia mbaya za watu. Kama anavyosema Allah (s.w):-

يَا اَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لاَ تَدْخُلُوا بُيُوتَ النَّبِيِّ إِلاَّ اَن يُؤْذَنَ لَكُمْ إِلَي طَعَامٍ غَيْرَ نَاظِرِينَ إِنَاهُ وَلَكِنْ إِذَا دُعِيتُمْ فَادْخُلُوا فَإِذَا طَعِمْتُمْ فَانتَشِرُوا وَلاَ مُسْتَاْنِسِينَ لِحَدِيثٍ إِنَّ ذٰلِكُمْ كَانَ يُؤْذِى النَّبِيَّ فَيَسْتَحْيِى مِنكُمْ وَاللهُ لاَ يَسْتَحْيِى مِنَ الْحَقِّ وَإِذَا سَاَلْتُمُوهُنَّ مَتَاعاً فَاسْاَلُوهُنَّ مِن وَرَاء حِجَابٍ ذٰلِكُمْ اَطْهَرُ لِقُلُوبِكُمْ وَقُلُوبِهِنَّ وَمَا كَانَ لَكُمْ اَن تُؤْذُوا رَسُولَ اللهِ وَلاَ اَن تَنكِحُوا اَزْوَاجَهُ مِن بَعْدِهِ اَبَداً إِنَّ ذٰلِكُمْ كَانَ عِندَ اللهِ عَظِيماً[2]

Enyi mlio amini! Msiingie nyumba za Nabii ila mpewe ruhusa kwenda kula, sio kungojea kiwive. Lakini mtakapo itwa basi ingieni, na mkisha kula tawanyikeni, wala msiweke mazungumzo. Hakika hayo yanamuudhi Nabii naye anakustahini, lakini Mwenyezi Mungu hastahi kwa jambo la haki. Na mnapo wauliza wakeze haja waulizeni nyuma ya mapazia. Hivyo ndio usafi zaidi kwa nyoyo zenu na nyoyo zao. Wala haikufalieni kumuudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu, wala kuwaoa wake zake baada yake kabisa. Hakika jambo hilo ni kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu.

* Maelezo kuhusiana na aya.

Kama wakeze Mtume wangeolewa na watu wengine, isingekuwa wepesi kwa watu kwenda pata kwao habari za mambo ya dini waliyojifunza kwa Mtume.

Na wamekatazwa mwanzo wa Aya hii watu kuwa maroho – kwenda majumbani mwa watu wakati wa chakula - . Na wakikaribishwa wasiwe wepesi kula. “karibu” ni mila, “karibu” si kula. Na wakisha kula wende zao, wapate wenyewe kupumzika…

Vile vile Mtume (s.a.w.w)alipokuwa akikabiliana na marafiki au maadui zake alikuwa akizungumza nao kwa adabu na heshima, na alikuwa akiwasikiliza kwa yale waliyoyazungumza, kiasi ya kwamba Mwenyeezi Mungu alikuwa akimliwaza kutokana na maudhi au madhila aliyokuwa akifanyiwa na wanafiki, kama tunavyosoma ndani ya Qur-ani:-

وَمِنْهُمُ الَّذِينَ يُؤْذُونَ النَّبِيَّ وَيِقُولُونَ هُوَ اُذُنٌ قُلْ اُذُنُ خَيْرٍ لَّكُمْ يُؤْمِنُ بِاللهِ وَيُؤْمِنُ لِلْمُؤْمِنِينَ وَرَحْمَةٌ لِّلَّذِينَ آمَنُواْ مِنكُمْ وَالَّذِينَ يُؤْذُونَ رَسُولَ اللهِ لَهُمْ عَذَابٌ اَلِيمٌ[3]

Na miongoni mwao wapo wanao muudhi Nabii na kusema: Yeye huyu ni sikio tu. Sema: Basi ni sikio la kheri kwenu. Anamuamini Mwenyezi Mungu, na ana imani na Waumini, naye ni rehema kwa wanao amini miongoni mwenu. Na wanao muudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu watapata adhabu chungu.

* Ilivyokuwa Mtume hawadhihirishi ubaya wao – kwa ikhlaqi zake nzuri, walidhani kuwa hautambui ubaya wao.

 

[1] Surat Al_Kalam Aya ya 3 na 4.

[2] Surat Al-Ahzaab Aya ya 53

[3] Surat Tawba Aya ya 61

MWISHO