AINA TOFAUTI ZA AMANA

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

AINA TOFAUTI ZA AMANA

KUTOA AMANA.

kutoa amana ni:-

Mwanaadamu kuipeleka haki ambayo  aliweka ahadi ya kuitoa amana hiyo, na kinyume chake ni khiyana.

Kuna aina tofauti za amana, miongoni mwa hizo ni:-

1. Baadhi ya amana ni haki za Mwenyeezi Mungu kwa wanaadamu, kwa mfano:- Hukumu za kisheria na ibada.

2. Na baadhi ya amana ni haki za Mitume ya Mwenyeezi Mungu kwa wanaadamu. kwa mfano:- Hukumu za Serikali, na sunna za Mitume.

3. Baadhi ya amana, ni haki za watu miongoni mwa watu wengine, kwa mfano:-

mali, na vyenginevyo.

4. baadhi ya amana, ni haki ya Mwenyeezi Mungu na Mtume wake, na amana za aina hiyo, zinaweza zikawa na faida au madhara kwa wanaadamu, kwa mfano:-

kufichua siri za nidhamu za kiislamu, na kufanya khiyana ya aina hiyo , ni kumfanyia khiyana Mwenyeezi Mungu , Mtume wake, na Waumini. Na Mwenyeezi Mungu katika Qur-ani ametukataza tusifanye khiyana hizo. Pale aliposema:-

يَا اَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ لاَ تَخُونُواْ اللّهَ وَالرَّسُولَ وَتَخُونُواْ اَمَانَاتِكُمْ وَاَنتُمْ تَعْلَمُونَ[1]

Enyi mlio amini! Msimfanyie khiana Mwenyezi Mungu na Mtume, wala msikhini amana zenu, nanyi mnajua.

Amana kubwa ya Mwenyeezi Mungu, ambayo ni haki ya Mtume (s.a.w.w) na wanaadamu wanashirikiana katika haki hiyo ni:-

Ni haki ya kuiongoza Serikali ya Kiislamu, haki ambayo ni lazima wapewe watu wanaostahiki kuiongoza Serikali ya Kiislamu, na hakuna mtu yoyote mwenye haki ya kuichukua haki hiyo isipokuwa kwa idhini ya Mwenyeezi Mungu na Mitume yake.

Kwa hiyo, kama tunavyoelewa kuwa wanaadamu ni lazima wawe wakweli baina yao, na wajikinge na kufanyiana khiyana kwa amana walizonazo baina yao, na kwa wale wenye elimu wakiwemo Mayahudi - Ahlulkitaab - wanatakiwa kuihifadhi amana ya Mwenyeezi Mungu pale wanapowaita watu kwa kuwapa taaluma ya dini. Na wala hawatakiwi kuwaficha wafuasi wao kuhusu alama za Mtume Muhammad (s.a.w.w) na kuwepo kwake Mtume huyo Mtukufu. Na wacha Mungu ni lazima watimize ahadi zao, na wasifanye khiyana kuhusiana na hukumu za Mwenyeezi Mungu na sunna za Mitume. Na kwa upande mwengine,  Waislamu ni lazima wafanye jitihada za kuidumisha jamii ya Kiislamu ili mategemeo makubwa ya Mwenyeezi Mungu na Mtume wake yatimie,mategemeo hayo ni kuwapa watu wanaostahiki cheo cha Uwalii. Kwa sababu Maimamu wote waliihifadhi amana hiyo, na kila mmoja alimkabidhi amana hiyo Imamu aliyefuata, na baada ya Kutoweka Maimamu amana hiyo ni lazima wapewe Mafaqihi wanaostahiki kupewa amana hiyo. Na watu wote ni lazima wafanye jitihada ili amana hiyo wapewe watu ambao wana sifa zinazolingana na sifa za Mitume na Maimamu, watu ambao wanaweza kutimiza wajibu wao na kuhifadhi amana hiyo. kama anavyosema Allah (s.w):-

إِنَّ اللّهَ يَاْمُرُكُمْ اَن تُؤدُّواْ الاَمَانَاتِ إِلَي اَهْلِهَا وَإِذَا حَكَمْتُم بَيْنَ النَّاسِ اَن تَحْكُمُواْ بِالْعَدْلِ إِنَّ اللّهَ نِعِمَّا يَعِظُكُم بِهِ إِنَّ اللّهَ كَانَ سَمِيعاً بَصِيراً[2]

Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni mzirudishe amana kwa wenyewe. Na mnapo hukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu. Hakika haya anayo kuwaidhini Mwenyezi Mungu ni mazuri sana. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kuona.

* Kuna baadhi ya watu wanapoachiwa amana na mtu, akaja akafa wala hakuweka mashahidi - au shahada ile haina nguvu - basi hujirusha mbali. Isiwe hivyo, Sio Uislamu huo. Mwislamu sharti awe muaminifu, hata juu ya wasiokuwa Waislamu.

[1] Surat Anfaal Aya ya 27.

[2] Surat Nisaa Aya ya 58

MWISHO