IMAMU ALI (A.S) ANAPASWA KUTIIWA

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

IMAMU ALI (A.S) NDIYE KHALIFA ANAYEPASWA KUTIIWA

Imamu Ali (salamu ziwe juu yake) tangu utotoni mwake alikuwa ni mfuasi wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), na katika kipindi chote cha uhai wake hakumlaumu Mtume, au kwenda kinyume na Amri zake (s.a.w.w).

Imamu Ali (a.s) anasema:-

ولقد کنت أتبعه اتباع الفصیل اثر امه[1]

Mimi nilikuwa namtafuta Mtume (s.a.w.w), na nilikuwa pamoja naye kila anapokwenda, mfano wa mtoto wa ngamia anayemtafuta mama yake.

Na vile vile Imamu Ali (a.s) ni mtu wa mwanzo aliyesilimu baada ya Mtume (s.a.w.w). kama tunavyoona ndani ya Nahjulbalagha:-

و لم یجمع بیت واحدیومئذ فی الاسلام غیر رسول الله صلی الله علیه واله وخدیجة وأناثالثهما[2]

Katika zama hizo, kulikuwa hakuna nyumba hata moja iliyokuwa na Muislamu, isipokuwa nyumba ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.) na mkewe Khadija, na mimi (Ali) ni  watatu wao.

Natija tunayoipata kutokana na maelezo hayo ni:-

Watu walio karibu na Mtume, ni wale ambao wanafuata mwenendo wa Mtume . kama tunavyosoma kuhusiana na Nabii Ibrahimu (salamu juu yake).

إِنَّ اَوْلَي النَّاسِ بِإِبْرَاهِيمَ لَلَّذِينَ اتَّبَعُوهُ وَهَـذَا النَّبِيُّ وَالَّذِينَ آمَنُواْ وَاللّهُ وَلِيُّ الْمُؤْمِنِينَ[3]

Watu wanao mkaribia zaidi Ibrahim ni wale walio mfuata yeye na Nabii huyu na walio amini. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wa Waumini.

* Kwani dini aliyokuja nayo Nabii Ibrahimu inawafikiana kabisa na aliyokuja nayo Nabii Muhammad, na hiyo ya Nabii Mussa na ya Nabii Issa ilikuwa hivi hivi, kabla ya kuharibiwa na Mayahudi na Manasara.

* Mitume yote ya Mwenyeezi Mungu imekuja kuwalingania watu dini moja, lakini Mayahudi na Manasara wameziharibu dini zao.

Kwa hiyo watu bora wanaostahiki kuiongoza jamii ya Kiislamu, ni wale ambao wanaweza kuwa na sifa hizo za Mtume, na Maimamu ndio watu wa mwanzo walio bora wenye sifa kama hizo,wakifuatiwa na Maulamaa,mashujaa na waadilifu, kwa hiyo kuwatii watu hao ni jambo la lazima, na kila Muislamu ana wadhifa wa kufanya jitihada zake zote ili kuwasaidia watu kama hao katika kuiimarisha dini ya Kiislamu.

Kama anavyosema Mwenyeezi Mungu Mtukufu:-

يَا اَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اَطِيعُواْ اللّهَ وَاَطِيعُواْ الرَّسُولَ وَاُوْلِى الاَمْرِ مِنكُمْ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِى شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَي اللهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللهِ وَالْيَوْمِ الآخِرِ ذٰلِكَ خَيْرٌ وَاَحْسَنُ تَاْوِيلاً[4]

Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema.

* Waislamu inawapasa kuwatii viongozi wa Kiislamu wanaoamrisha mambo mema, kwa sababu kama hapatakuwa na kiongozi katika jamii, ni rahisi kutokea fujo.  Na dini ya Kiislamu haipendi fujo, dhulma wala jeuri, kwa sababu hiyo  tumeambiwa tuwaheshimu viongozi wetu pindi wakituamrisha kufanya mambo mema, na ikiwa wataamrisha mabaya hakuna ulazima wa kuwatii.

* Na pindi inapotokea mizozano, - viongozi wanaona kuwa kufanya jambo fulani ni bora, na wananchi wakaona kuwa kufanya jambo hilo sio sahihi - ili kuondoa mizozano hiyo, wanatakiwa kutizama katika sheria za Mwenyeezi Mungu na Mtume wake wameamrishwa nini? ikiwa Mwenyeezi Mungu na Mtume wake wameamrisha kufanya jambo hilo ni lazima lifanywe. ijapokuwa kiongozi wao amesema lisifanywe, na vile vile wananchi hawatakiwi kufanya jambo wasilolijua sheria yake. kwa hiyo, viongozi na wananchi wanatakiwa wategemee sheria za Mwenyeezi Mungu na Mtume wake.

* Neno (Uwlil-amr) katika Aya iliyopita lina maana ya Maimamu, au kama tukitizama maana ya jumla inakusudiwa viongozi wengine wa Kiislamu, na tunathibitisha hayo kwa sababu, aya nyengine zinakataza kuwatii madhalimu na mafasiki.

Maelezo kwa ufupi kuhusiana na makala zilizopita.

* Mitume ya Mwenyeezi Mungu inafanya jitihada ili kuijenga jamii katika maadili ya kiislamu, kwa hiyo sio jambo linalokubalika kiakili kuacha jitihada zao zote hizo kupotea bila ya kuwa na mafanikio yoyote.

* Mitume ya Mwenyeezi Mungu, siku zote walikuwa wakimchagua mtu na kumpa wadhifa wa kuiongoza jamii ya kiislamu wakati wanapoondoka kwenda sehemu nyengine, au hata baada ya kufariki kwao.

*Kuna watu wabaya wa aina tofauti ambo hawapaswi kutiiwa. miongoni mwao ni:-

Watu wenye kufanya israfu, wenye kufanya ufisadi katika jamii, wenye kufanya maasi, madhalimu na watu waongo.

* Watu wanaostahiki kuchaguliwa kuwa viongozi baada ya kuondoka Mitume ya Mwenyeezi Mungu, wanatakiwa kuwa na sifa hizi zifuatazo:-

Wenye elimu, uadilifu, ushujaa, waweze kutambua hila za maadui wao, na wawe ni wenye kushikamana na dini.

Maswali

1. Mitume ya Mwenyeezi Mungu ilikuwa na mategemeo gani?.

2. Qur-ani takatifu, katika kuchagua viongozi wanaokuja baada ya Mitume ya Mwenyeezi Mungu, imeelezea nini?  3.Qur-ani Kariym, inakataza watu kuwafuata watu wa aina gani?.

4. Elezea kwa ufupi sifa za Mitume ya Mwenyeezi Mungu .

[1] Nahjulbalagha Feydh, خ 234. Nahjulbalagha subhiy. 192.

[2] Nahjulbalagha Feydh, خ 234. Nahjulbalagha subhiy. 192.

[3] Surat Al-Imrani Aya ya 68

[4] Suratun Nisaa Aya ya 59

MWISHO