MALIPO YA KUFIKISHA UJUMBE WA ALLAH (S.W)

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

MALIPO YA KUFIKISHA UJUMBE WA ALLAH (S.W)

* Mitume ya Mwenyeezi Mungu, hawakutaka malipo yoyote kwa kuwalingania  katika njia ya Mwenyeezi Mungu .

* Ni amana gani kwa Mwenyeezi Mungu ni muhimu?.

Malipo ya kufikisha ujumbe na amana ya Mwenyeezi Mungu.

Mitume ya  Mwenyeezi Mungu,walistahamili tabu na mashaka mengi ili kuwaongoza watu katika njia iliyo sahihi. Na walifanya jitihada zao zote ili kuwaokoa watu na maisha ya kidhulma. na hawakuhitaji malipo wala ujira  kutokana na tabu ambazo walizipata.

Qur-ani takatifu kuhusiana na Nabii Nuhu (salamu juu yake). inasema hivi:-

وَيَا قَوْمِ لا اَسْاَلُكُمْ عَلَيْهِ مَالاً إِنْ اَجْرِيَ إِلاَّ عَلـٰي اللهِ وَمَا اَنَاْ بِطَارِدِ الَّذِينَ آمَنُواْ إِنَّهُم مُّلاَقُو رَبِّهِمْ وَلَـكِنِّيَ اَرَاكُمْ قَوْماً تَجْهَلُونَ[1]

"Na enyi watu wangu! Mimi sitaki ujira au mali juu ya (jambo) hili; ujira wangu ni kwa Mwenyeezi Mungu, na mimi sitawafukuza walioamini, kama mlivyotaka kwangu niwafukuze hao madhaifu, ndipo nyinyi, watukufu mukubali dini. Sitafanya hivyo); maana wao watakutana na Mola wao, (awalipe kwa mema yao na mabaya). Lakini mimi nakuoneni nyinyi ni watu mnaofanya ujinga, (mnakataa kuifuata haki  kwa sababu imefuatwa na madhaifu)!.

Mitume ya Mwenyeezi Mungu, ijapokuwa hawakutaka ujira kutoka kwa watu, lakini  wana ujira mkubwa kutoka kwa Mola wao . kama tunavyosoma kuhusiana na Nabii Muhammad (s.a.w.w).:-

وَإِنَّ لَكَ لاَجْراً غَيْرَ مَمْنُونٍ[2]

Na kwa hakika wewe una malipo yasiyo katika.

Ijapokuwa Mitume ya Mwenyeezi Mungu wana ujira mkubwa kutoka kwa Mola wao, lakini vile vile kwa sababu wamewaongoa watu. na kuwaongoza katika njia njema, njia ambayo inaweza kuwafikisha wao Peponi. Na kwa sababu hiyo, Mwenyeezi Mungu atawaongezea ujira kwa sababu wamewalingania watu na kuwaongoza katika njia njema iendayo kwa Mola mlezi. Na hayo ndio malipo bora kwa Mitume, kwa sababu kama hawakupata malipo hayo, jitihada na tabu zote zitakuwa hazina  mafanikio yoyote. Katika Qur-ani takatifu kuhusiana na Nabii Muhammad (s.a.w.w) tunasoma hivi:-

قُلْ مَا اَسْاَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ اَجْرٍ إِلاَّ مَن شَاء اَن يَتَّخِذَ إِلَي رَبِّهِ سَبِيلاً[3]

Sema: Sikukuombeni ujira juu yake; ila atakaye na ashike njia iendayo kwa Mola wake Mlezi.

Baada ya kuamini Mwenyeezi Mungu na Mtume wake, njia bora inayoweza kumuokoa Mwanaadamu na kumuongoza katika uongofu ni kunufaika na elimu ya Maimamu, na kuukubali Uwalii wao, kama tunavyosoma ndani ya qur-ani:-

ذٰلِكَ الَّذِى يُبَشِّرُ اللهُ عِبَادَهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ قُل لاَّ اَسْاَلُكُمْ عَلَيْهِ اَجْراً إِلاَّ الْمَوَدَّةَ فِى الْقُرْبَي وَمَن يَقْتَرِفْ حَسَنَةً نَّزِدْ لَهُ فِيهَا حُسْناً إِنَّ اللهَ غَفُورٌ شَكُورٌ[4]

Hayo ndiyo aliyo wabashiria Mwenyezi Mungu waja wake walio amini na wakatenda mema. Sema: Sikuombeni malipo yoyote kwenu ila mapenzi katika kujikurubisha. Na anaye fanya wema tutamzidishia wema. Hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu Mwenye shukrani.

katika maelezo ya hapo juu tulielezea kuwa uongofu wa wanaadamu utathibitika pindi wakiamini Mwenyeezi Mungu, Mitume yake, na  Ahlulbayt, ni lazima tuzingatie kuwa madhumuni ya Ahlulbayt, ni wale watu walio karibu na Mtume (s.a.w.w), watu ambao huwaongoza wanaadamu ili kufikia katika saada ya dunia na akhera. kwa kutiiwa watu hao , madhumuni ya Nabii Muhammad yanaweza kuthibitika katika jamii. kama tunavyosoma ndani ya Qur-ani:-

قُلْ مَا سَاَلْتُكُم مِّنْ اَجْرٍ فَهُوَ لَكُمْ إِنْ اَجْرِيَ إِلاَّ عَلـٰي اللهِ وَهُوَ عَلـٰي كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ[5]

Sema: Ujira nilio kuombeni ni wenu nyinyi. Sina ujira ila kwa Mwenyezi Mungu. Na Yeye ni Shahidi juu ya kila kitu.

* Tukizingatia kwa makini, Aya zilizobainishwa hapo juu, tutafahamu kuwa ili tuwe miongoni mwa waliofuata njia ya Mwenyeezi Mungu , kwanza ni lazima tuwaamini Maimamu, na kuna uwiano baina ya vitu hivyo viwili, kwa hiyo yule anayeamini Maimamu atakuwa ni miongoni mwa waongofu na atakuwa yuko katika njia ya Mwenyeezi Mungu. Na kwa yule asiyewaamini Maimamu  atakuwa miongoni mwa waliopotea.

[1] Surat Hud Aya ya 29

[2] Surat qalam Aya ya 3

[3] Surat Alfurqaan Aya ya 57

[4] Surat Shuura Aya ya 23

[5] Surat Saba Aya ya 47

MWISHO