UJUMBE WA SIKU YA ASHURA

UJUMBE WA SIKU YA ASHURA

Katika Mji mtakatifu wa Qum, Irani; Ayatullah Al-Mirza Jawwad At -Tabrezi ameelezea rambirambi zake za dhati kwa wafuasi wa Aal-e-Muhammad (a.s.) kwa tukio hili linalowagusa la masaibu ya Karbala.

Katika ujumbe wake kwenye tukio la siku ya Ashura, mtukufu Ayatullah At-Tabrezi alisema kifo cha Bwana wa Mashahidi Hazrat Aba Abdillah Al-Hussain (a.s.) ni njia inayong’ara na itoayo mwanga kwa Waumini, wapigania Uhuru, wanaonyanyaswa na kwa kila tabaka la jamii na pia kwa Dini na Imani zote.

Ayatullah alisema kuwa fundisho linalopatikana katika tukio hili la huzuni ni kuwa ushindi kati ya Haki na Batili wakati wote upo pamoja na Haki (ukweli).

UJUMBE WA SIKU YA ASHURA

Siku ya Ashura hutonesha majeraha yetu, na hupelekea macho yetu kububujikwa na machozi kutokana na vipenzi vyetu kuuliwa mashahidi katika ardhi ya Karbala, na kutuweka katika usumbufu na majuto hadi siku ya Hisabu (Kiyama). Hivyo, huyu ni Husain (a.s.) ambaye watu wapaswa kumlilia (na kuomboleza) kwa kuuliwa shahidi.(Imam Ali Raza (a.s.)).

Sisi na ndugu zetu wote tunakumbuka (mahali hapa) katika siku hizi maalumu za matukio ya Imam Husain (a.s.), pia Mapinduzi ya Kiislamu katika nyanja zote yakiongozwa na Imam Husain (a.s.), Ahlul Bayt wake, Mashaba, Wanamume, Wanawake, Wazee, Vijana na Watoto kwa upande mmoja na matendo ya kikatili yaliyotendwa na Madhalimu wa mauaji haya kwa upande mwingine.

Tunapenda kuziangalia baadhi ya nukta ili tupate mafunzo kutoka kwenye ujumbe wa Imam Husain (a.s.), uliotikisa utawala wa Madhalimu katika kila zama na kuuhuisha Uislamu kwa faida ya kizazi kijacho.

Ili kupata mafanikio katika wakati huu mambo yafuatayo yapaswa kufuatwa: -

* Kuonyesha majuto na huzuni kufuatana na mwenendo wa Ahlul Bayt (a.s.). Katika Hadithi yake Imam Raza (a.s.) anasema “Mwanzoni mwa mwezi wa Muharram, baba yangu alikuwa hacheki na alionekana amejawa na huzuni mwezi mzima na ilipowadia siku ya kumi ya Mwezi wa Muharram, siku ya usumbufu, matatizo na maombolezo alisema “ Hii ni siku ambayo Imam Husain (a.s.) aliuliwa (kikatili)”.

* Kujiandaa na kushiriki katika Aza (maombolezo) ya Imamu Husain (a.s.) katika Misikiti, Husainia, n.k. kwa kuwa matendo haya ni utukufu wa alama za Allah (s.w.t.) kama Qur’ani inavyosema: “Namna hivi, anayeziheshimu alama za (dini ya) Mwenyezi Mungu, basi hilo ni jambo la Utawala (ucha Mungu) wa nyoyo” (Hajj:32).

MWISHO