SIFA WANAZOTAKIWA MAKHALIFA KUWA NAZO NO.3

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

SIFA WANAZOTAKIWA MAKHALIFA KUWA NAZO NO.3

Katika makala zilizopita tulielezea kuhusiana na sifa wanazotakiwa makhalifa kuwa nazo. katika makala hii tutaendelea na mada yetu inayohusiana na maudhui hayo hayo.

5. ushujaa.

Kiongozi wa kiislamu ni lazima awe na uhakika katika kuhukumu hukumu za kiislam, na baada ya kuelewa hila za maadui wake, ni lazima akabiliane na maadui hao bila kuogopa au kuwa na hofu ya kitu chochote. na vile vile anatakiwa kuwafahamu  watu wanafiki waliomo ndani na nje ya nchi.  kwa kufanya hivyo atakuwa ametimiza wadhifa aliopewa na Mola wake. kama anavyosema Mwenyeezi Mungu Mtukufu:-

فَبِمَا رَحْمَةٍ مِّنَ اللهِ لِنتَ لَهُمْ وَلَوْ كُنتَ فَظّاً غَلِيظَ الْقَلْبِ لاَنفَضُّواْ مِنْ حَوْلِكَ فَاعْفُ عَنْهُمْ وَاسْتَغْفِرْ لَهُمْ وَشَاوِرْهُمْ فِى الاَمْرِ فَإِذَا عَزَمْتَ فَتَوَكَّلْ عَلـٰي اللهِ إِنَّ اللّهَ يُحِبُّ الْمُتَوَكِّلِينَ[1]

Basi ni kwa sababu ya rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu ndio umekuwa laini kwao. Na lau ungeli kuwa mkali, mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangeli kukimbia. Basi wasamehe, na

waombee maghfira, na shauriana nao katika mambo. Na ukisha kata shauri basi mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao mtegemea.

* Hapa Mwenyeezi Mungu anamtia nguvu Mtume, kuendelea na sifa yake ya upole na ustahamilivu juu ya yote yale anayofanyiwa na watu. Na anamuonyesha kuwa kupewa upole huo ni rehema

kubwa inayotoka kwa Mwenyeezi Mungu.

Na anahimizwa Mtume anapotaka kufanya jambo ashauriane na watu wake, asikate mwenyewe tu peke yake. Kwani kutakana ushauri kuna nafuu kubwa, na anawakataza wasiwe vigeu geu –

wakisha kushauriana wakaona wafanye kitu fulani , basi nawamtegemee Mwenyeezi Mungu wakifanye tu kitu hicho. Wasitie tena hili wala hili.

hapana shaka kuwa baada ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), Imam Ali (salamu juu yake) ndiye aliyekuwa shujaa bora katika jamii ya Kiislamu, na hayo yamethibitishwa katika elimu ya historia.

tunasoma katika Nahjulbalagha :-

والله لو تظاهرت العرب علی قتالی لما ولیت عنها[2]

Naapa kwa jina la Mola wangu, Ikiwa watu wote wa jamii ya Kiarabu watakusanyika pamoja ili kupigana nami, basi sitawaogopa wala kuwakimbia.

6. kushikamana kimatendo na kiamali na hukumu za kiislamu.

Watu ambao wanastahiki kuwa viongozi ndani ya jamii ya kiislamu, ni lazima kushikamana na hukumu za Kiislamu, kulinganisha na watu wengine. kama tunavyosoma ndani ya qur-ani:-

إِنَّمَا وَلِيُّكُمُ اللّهُ وَرَسُولُهُ وَالَّذِينَ آمَنُواْ الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلاَةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُمْ رَاكِعُونَ[3]
Rafiki yenu khasa (ambaye mnatakiwa kuwa pamoja naye), ni Mwenyeezi Mungu na Mtume wake, na walioamini, ambao husimamisha sala na hutoa zaka, na hali ya kuwa wananyenyekea.

[1] Surat Al-Imrani Aya ya 159

[2] Nahjulbalagha, barua ya 45

[3] Suratu-Al-maidah Aya ya 55

MWISHO