FAIDA ZA KUIKUMBUKA SIKU YA KIAMA NO.2

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

FAIDA ZA KUIKUMBUKA SIKU YA KIAMA NO. 2.

Kauli muhimu za Mitume ya Mwenyeezi Mungu ni kuwalingania watu kuamini Mola mmoja na kuwakumbusha maisha baada ya mauti. Jitihada kubwa walizozifanya Mitume baada ya kuwalingania watu kuabudu Mola mmoja ni kuihuisha Siku ya Kiama katika nyoyo za watu. katika makala iliyopita tulielezea baadhi ya faida za kuikumbuka siku ya Kiama katika makala hii tutaendelea kuelezea faida nyengine.

3. Kuhifadhi uhuru.

Kuwa na upeo wa hali ya juu, na kuwa huru katika matendo na tabia kunakuja baada ya kuamini Mwenyeezi Mungu na siku ya Kiama. Waumini  wanaamini kuwa maisha ya dunia ni yenye kupita, na wala hawakubali kuwa na kibri kwa sababu ya maisha mafupi ya dunia, na hawako tayari kunufaika  na mali au vyeo vilivyopo katika mikononi mwa watu madhalimu wenye kibri, kama walivyosema wachawi katika zama za Firauna kuwa; Kwa hakika tutaishi maisha ya kidhalili kwa kuamini Mwenyeezi Mungu na kuikumbuka siku ya Kiama. Watu hao  walitangaza uhuru wao kwa kusema:-

قَالُوا لَن نُّؤْثِرَكَ عَلـٰي مَا جَاءنَا مِنَ الْبَيِّنَاتِ وَالَّذِى فَطَرَنَا فَاقْضِ مَا اَنتَ قَاضٍ إِنَّمَا تَقْضِى هَذِهِ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا[1]

Wakasema: Hatutokukhiari wewe kuliko ishara waziwazi zilizo tujia, na kuliko yule aliye tuumba. Basi hukumu utavyo hukumu; kwani wewe unahukumu haya ya maisha ya duniani tu.

Watu hao waliweza kukabiliana na madhila waliyokuwa wakifanyiwa na Firauna na walisema:-

قَالُوا لاَ ضَيْرَ إِنَّا إِلَي رَبِّنَا مُنقَلِبُونَ[2]

Wakasema: Haidhuru, kwani sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi.

3. Kuwa thabiti na kukabiliana na Mataluti.

Kuwa na itikadi ya siku ya Kiama sio tu inamuweka mwanaadamu kuwa tayari katika kuhifadhi uhuru wake, na kutenda yale aliyoamrishwa na Mola wake, bali pindi anapopatwa na matatizo huingiwa na moyo wa ustahamilivu wa tabu na mashaka. Na wala hawi na shaka kwa imani na itikadi yake, kama alipokuwa thabiti mke wa Firauna na akakabiliana na taghoot, akasema:-

وَضَرَبَ اللهُ مَثَلاً لِّلَّذِينَ آمَنُوا اِمْرَاَةَ فِرْعَوْنَ إِذْ قَالَتْ رَبِّ ابْنِ لِى عِندَكَ بَيْتاً فِى الْجَنَّةِ وَنَجِّنِى مِن فِرْعَوْنَ وَعَمَلِهِ وَنَجِّنِى مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ[3]

Na Mwenyezi Mungu amewapigia mfano walio amini - mkewe Firauni, alipo sema: Mola wangu Mlezi! Nijengee kwako nyumba Peponi, na uniokoe na Firauni na vitendo vyake, na uniokoe na watu madhaalimu.

*Na hapa inabainishwa kuwa watu wema hawatawafikwa na balaa inayoweza kuwafikia watu walio wabaya, kila mtu atalipwa kwa amali zake. Wanacholipwa watu wema na wabaya ni amali si ujamaa.

Mke wa Firauna alistahamili mashaka na madhila yote aliyokuwa akifanyiwa na Firauna, na wala hakuritadi akida yake na hakuwa miongoni mwa Makafiri.

5.Jihadi na Ushahidi.

Miongoni mwa dalili muhimu zinazoweza kumfanyia mwanaadamu wepesi, aweze kustahamili mashaka ya vita, au aweze kukabiliana na makundi ya maadui  bila ya hofu yoyote, hata kukubali mauti na kufa Shahidi, na kurejea kwa Mola wake kwa shauku na furaha ni kuwa na imani ya kuwepo siku ya Qiyamah.

Kama tunavyosoma kuhusiana na wafuasi wa Taaghuut:

فَلَمَّا فَصَلَ طَالُوتُ بِالْجُنُودِ قَالَ إِنَّ اللّهَ مُبْتَلِيكُم بِنَهَرٍ فَمَن شَرِبَ مِنْهُ فَلَيْسَ مِنِّى وَمَن لَّمْ يَطْعَمْهُ فَإِنَّهُ مِنِّى إِلاَّ مَنِ اغْتَرَفَ غُرْفَةً بِيَدِهِ فَشَرِبُواْ مِنْهُ إِلاَّ قَلِيلاً مِّنْهُمْ فَلَمَّا جَاوَزَهُ هُوَ وَالَّذِينَ آمَنُواْ مَعَهُ قَالُواْ لاَ طَاقَةَ لَنَا الْيَوْمَ بِجَالُوتَ وَجُنودِهِ قَالَ الَّذِينَ يَظُنُّونَ اَنَّهُم مُّلاَقُو اللهِ كَم مِّن فِئَةٍ قَلِيلَةٍ غَلَبَتْ فِئَةً كَثِيرَةً بِإِذْنِ اللهِ وَاللّهُ مَعَ الصَّابِرِينَ[4]

Basi Taluti alipo ondoka na majeshi alisema: Mwenyezi Mungu atakujaribuni kwa mto. Atakaye kunywa humo si pamoja nami, na asiye kunywa atakuwa pamoja nami: ila atakaye teka kiasi ya kitanga cha mkono wake. Lakini walikunywa humo isipo kuwa wachache tu miongoni mwao. Alipo vuka mto yeye na wale walio amini pamoja naye, walisema: Leo hatumwezi Jaluti (Goliati) na majeshi yake. Wakasema wale wenye yakini ya kukutana na Mwenyezi Mungu: Makundi mangapi madogo yameshinda makundi makubwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kusubiri.

Kutii ni kitu kikubwa kabisa katika kutengenea mambo ya watu. Watu wasiokuwa na taa ya kutii mamb yao huharibikiwa tu. Na hapa anatoka Mfalme huyu. Taluti na jeshi kubwa , wala halijui utiifu wake, basi Mwenyeezi Mungu ndio akamwambia awafanyie mtihani huu wa kutokunywa mpaka kukata kiu. Na wale wasiotii asiwachukue kwenda huko kwenye  midani ya vita wasije wakakhalifu wanayoambiwa.

Ni jambo lililo wazi kabisa kuwa, kukumbuka neema za Peponi kunawafanya wenye kupigana jihadi kuwa na shauku na hamasa ya kwenda kwenye midani ya vita. Na kukumbuka mashaka ya siku ya Qiyamah kunawapa tahadhari watu wasikimbie vita.

Kama tunavyosoma katika Qur-ani:-

فَرِحَ الْمُخَلَّفُونَ بِمَقْعَدِهِمْ خِلاَفَ رَسُولِ اللهِ وَكَرِهُواْ اَن يُجَاهِدُواْ بِاَمْوَالِهِمْ وَاَنفُسِهِمْ فِى سَبِيلِ اللهِ وَقَالُواْ لاَ

تَنفِرُواْ فِى الْحَرِّ قُلْ نَارُ جَهَنَّمَ اَشَدُّ حَرّاً لَّوْ كَانُوايَفْقَهُونَ[5]

Walifurahi walio achwa nyuma kwa kule kubakia kwao nyuma na kumuacha Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walichukia kupigana Jihadi kwa mali zao na nafsi zao, na wakasema: Msitoke nje katika joto! Sema: Moto wa Jahannamu una joto zaidi, laiti wangeli fahamu!.

Maimamu vile vile waliwataka watu wenye kupigana jihadi wawe thabiti na kupata mafanikio kwa kuamini siku ya Qiyamah.

Kama anavyosema Imam Sajaad katika dua yake:-

واجعل الجنة نصب أعینهم....حتی لا یهم أحد منهم باالادبارولا یحدث نفسه عن قرنه بفرار[6]

 Ewe Mola wangu tuwekee Pepo yako mbele ya macho yetu, ili asitokee mtu hata mmoja atakayeweza kubadilisha uamuzi wake na kuwafuata maadui , na wala usiwape fikra zinazoweza

kuwafanya wao kuwakimbia maadui zao.

[1] Surat Taha Aya ya 72

[2] Surat Shuaraa Aya ya 50

[3] Surat tahriym Aya ya 11

[4] Surat-Albaqarah Aya ya 249.

[5] Surat –Tawba Aya ya 81

[6] Sahifa Sajjadiyah, dua ya 27

 

MWISHO