MADHARA YA DUNIANI NA AKHERA

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

MADHARA YA DUNIANI NA AKHERA.

4. Madhara ya duniani na Akhera.

Watu ambao hawako thabiti katika njia iliyonyooka, wanapopata matatizo madogo tu maishani mwao hujizuilia na kukiuka hukumu za Mwenyeezi Mungu, au huenda katika vikundi vya  watu waovu, watu kama hao hukutwa na madhara Duniani na Akhera. Kama anavyosema Allah (s.w) kuhusiana na watu hao:-

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَعْبُدُ اللهَ عَلـٰي حَرْفٍ فَإِنْ اَصَابَهُ خَيْرٌ اطْمَاَنَّ بِهِ وَإِنْ اَصَابَتْهُ فِتْنَةٌ انقَلَبَ عَلـٰي وَجْهِهِ خَسِرَ الدُّنْيَا وَالآخِرَةَ ذٰلِكَ هُوَ الْخُسْرَانُ الْمُبِينُ[1]

Na katika watu wapo wanao muabudu Mwenyezi Mungu kwa ukingoni. Ikimfikia kheri hutulia kwayo, na ukimfikia msukosuko hugeuza uso wake. Amekhasiri dunia na Akhera; hiyo ndiyo khasara iliyo wazi.

* Maelezo kuhusiana na Aya.

Tumeletwa ulimwenguni tufanyiwe mitihani ili tusafike barabara kabla ya kwenda Akhera; kama inavyosafishwa dhahabu na kutiwa motoni. Basi natuvumilie na tushike hayo tuliyoambiwa na Mwenyeezi Mungu na Mtume wake. Na kila namna: Baada ya dhiki ni faraji tu. Tusikate tama lakini tupanie barabara katika kujitenga na hizo balaa  zisitufikilie, na zikitufikia tustahamili, na huku tunajitatua nazo kwa mwisho wa uweza wetu, na kumuomba Mwenyeezi Mungu, siyo kuomba mizimu na mapepo, kama tulivyobainishiwa katika Aya ya 12 kuwa hawawezi kunufaisha wala kuondosha madhara. Mambo yote ni ya Mungu: Atakalo ndilo huwa. Ndiye Pweke Mwenye Quwa:Mwenye amri na shani.

5. Fungamano la laana katika Dunia na Akhera.

Kuna fungamano miongoni mwa laana  na kuwa mbali na rehema za Mwenyeezi Mungu duniani na Akhera. Kiasi ya kwamba kwa wale wanaofanya matendo maovu hawatapata mafanikio yoyote duniani na siku ya Kiama wataadhibiwa kwa adhabu kali iumizayo. Kama anavyosema Mwenyeezi Mungu (s.w) kuhusiana na wale wanaowasingizia waumini maovu:-

إِنَّ الَّذِينَ يَرْمُونَ الْمُحْصَنَاتِ الْغَافِلاَتِ الْمُؤْمِنَاتِ لُعِنُوا فِى الدُّنْيَا وَالآخِرَةِ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ[2]

Hakika wanao wasingizia wanawake, wanao jihishimu, walio ghafilika, Waumini, wamelaaniwa duniani na Akhera, nao watapata adhabu kubwa. Na vile vile katika Aya nyengine, kuhusiana na wale ambao kwa mazungumzo na matendo yao wanamuudhi Mtume Muhammad (s.a.w.w). kama tunavyosoma ndani ya Qur_ani:-

إِنَّ الَّذِينَ يُؤْذُونَ اللهَ وَرَسُولَهُ لَعَنَهُمُ اللهُ فِى الدُّنْيَا وَالآخِرَةِ وَاَعَدَّ لَهُمْ عَذَاباً مُّهِيناً[3]

Hakika wanao muudhi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Mwenyezi Mungu amewalaani duniani na Akhera, na amewaandalia adhabu ya kufedhehi. Na vile vile kuhusiana na kuzama firauna na wafuasi wake duniani, na kwenda motoni watu hao siku ya Kiama tunasoma hivi:-

وَاُتْبِعُواْ فِى هَـذِهِ لَعْنَةً وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ بِئْسَ الرِّفْدُ الْمَرْفُودُ[4]

Nao wamefuatishiwa laana hapa duniani na Siku ya Kiyama. Ni mabaya yalioje watakayo pewa!

 

[1] Surat Hajj Aya ya 11

[2] Surat An-Nur Aya ya 23.

[3] Surat Ahzaab Aya ya 57

[4] Surat Hud Aya ya 99.

 

MWISHO