MSINGI YAKINI KATIKA UHAKIKI WA DINI

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
MSINGI YAKINI KATIKA UHAKIKI WA DINI

Msingi muhimu wa kupatikana yakini katika uhakiki wa dini.

Baadhi ya wahakiki wa dini, badala ya kupata ya kupata natija ya uhakika na iliyo yakini kutokana na kile walichokifanyia uhakiki kuhusiana na dini, muhakiki huyo hubakiwa na dhana tu akilini mwake bila ya kufikia au kuona natija yoyote, hii inaweza ikawa ni kwa sababu ya kuwa malengo ya muhakiki huyo hayakuendana sambamba na uhakiki wake, inawezekana muhakiki huo katika uhakiki wake alikuwa na uadui fulani kuhusiana na dini, basi muhakiki kama huyo atakuwa kaufanya uadui wake huo kuwa ni malengo ya kuharibu taratibu za uhakiki, na sio kupata malengo ambayo ndiyo hadafu asili ya uhakiki wake, basi muhakiki wa kweli, aliyeingia katika uwanja wa uhakiki kwa nia ya kutambua hali halisi ya uhakika wa dini hiyo anayoifanyia uhakiki, (ikiwa dini iliyokusudiwa hapa ni dini ya haki, ambayo ni dini ya Kiislamu) basi ni lazima afikie katika natija inayokubalika kiakili na kimantiki, natija ambayo itaonekana kwa uwazi ndani ya kile alichokifanyia uhakiki, na sio kupinga uhakika na haki ya dini hiyo takatifu bila kutoa dalili zozote zinazokubalika kiakili na kimantiki.

Msingi wa kutoifanya dini au uhakiki wa dini kama ni chombo cha habari.

Wahakiki wa dini inawapasa kufanya uhakiki wao kwa malengo yanayokubalika na kila akili salama, hivyo wahakiki wa dini haiwapasi kuifanya dini kama ni chombo cha habari chenye kuweka bomba zake katika siasa mbovu, baadhi ya wahakiki wa dini wameifanya dini kama ni nyenzo ya kufikia katika malengo yao, malengo hayo yanaweza yakawa ni kuitangaza siasa mbovu isiyoendana sambamba na misingi ya dini, au malengo hayo yanaweza yakawa ni kuharibu siasa za watu wengine, nap engine inawezekana siasa hizo zikawa zinaendana sambamba na misingi ya dini, wahakiki kama hao badala ya kuifanya dini kuwa ndio malengo yao, huitumia dini kama ni nyenzo ya kufikia katika malengo yao, kwa malengo kama hayo basi hakuwezi kupatikana natija yoyote isipokuwa kuikimbia na kuiwacha dini, hali ya kwamba hadafu, malengo, na hatima ya uhakiki wa dini ni kupatikana ufumbuzi wa mambo mbali mbali na kupata muelekeo mzuri kuhusiana na dini, muelekeo ambao utamfanya muhakiki awe na mapenzi na kuyapokea kwa moyo mkunjufu yale aliyoyafanyia uhakiki, na sio kuwawekea wanaadamu vikwazo na kuwaweka mbali na dini.

Msingi wa kuweka uadilifu:

Kuweka uadilifu katika mitazamo ya uhakiki wa dini ndani ya uwanja wa dini.

Msingi mwengine wa uhakiki wa dini, ni kuwepo uadilifu baina ya uhakiki wa dini, na yale yanayofanyiwa uhakiki katika uwanja wa dini, ni jambo lisilokubalika kiakili wala kimantiki kuifunga dini katika mitazamo yote, mitazamo ambayo haiyendani sambamba na mitazamo ya dini hiyo inayofanyiwa uhakiki, baadhi ya wahakiki huutawanya na kuusambaza uwanja wa dini kiasi ya kwamba kila jambo hulipa uhusiano na dini, hali ya kwamba pengine jambo hilo halina uhusiano wowote na dini au linapingana na misingi ya dini, hivyo muhakiki ni lazima afanye uhakiki wake kwa insafu na uadilifu, siyo azidishe mambo na kuyahusisha na misingi ya dini, na sio apunguze mambo na kuyahusisha na misingi ya dini, ikiwa muhakiki atafanya uhakiki wake kwa mtindo kama huo, basi atakuwa ameitoa dini katika uwanja wake wa asili, na ikiwa hadafu na malengo ya muhakiki sio kuitoa dini katika uwanja wake, basi katika uhakiki wa dini ni lazima kuzingatiwe mitizamo ya pande zote mbili, hapo panaweza kupatikana natija ya kiadilifu, na kwa mujibu wa natija hiyo basi, muhakiki ataitambua njia iliyo sahihi na ile isiyo sahihi.


MWISHO