UTAFITI KUHUSIANA NA DINI

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
UTAFITI KUHUSIANA NA DINI
Msingi wa kutegemea nyenzo ya Wahyi katika uhakiki wa dini.

Tahakiki nyingi zinazofanywa kwa jina la uhakiki wa dini ziko nje ya ukweli wa hali halisi ya uhakika wa dini na taaluma ya dini, au tahakiki hizo zimeichukulia dini kama ni uhakika usio thabiti unaoweza kutolewa nadharia na watu binafsi na sio kuthibitishwa uhakika huo kutokana na ukweli na haki inayoshuhudiwa katika dini hiyo takatifu. Baadhi ya wahakiki wa dini hupotea katika uhakiki wao kwa kutoweza kuhalili yale mambo ambayo yanahusiana na uhakika huo wa dini, kwa hiyo wahakiki wote ni lazima wazingatie pindi wanapofanya uhakiki wao, ijapokuwa muhakiki ndiye anayehalili kile alichokifanyia tahakiki, lakini katika hatua ya mwanzo kitengo cha uhakiki ndicho kinachoweza kumbainishia muhakiki huyo yale yanayohitajiwa kufanyiwa tahalili, kwa sababu kitengo hicho kimewekwa kwa ajili ya kuwapa huduma na kuwasaidia wahakiki na kuwaongoza katika njia sahihi, kitengo hicho kina elimu na taaluma za kutosha kuhusiana na mambo tofauti yanayohusiana na dini, kwa upande mwengine inawezekana muhakiki akawa hana taaluma au elimu yoyote ile kuhusiana na dini, hivyo ni lazima kuwepo njia ambayo itamuongoza muhakiki huyo katika njia iliyo sahihi. Mbali ya hayo kile kilichofanyiwa tahakiki na muhakiki hakitokuwa na thamani yoyote ile na atabakiwa na shaka au dhana akilini mwake ya kuwa kile alichokifanyia tahakiki na akakifanyia tahalili amepata natija iliyo sahihi au la.

Kwa hiyo ili kuondoa shaka au dhana hiyo ni vyema akapata muongozo kutoka katika kitengo cha uhakiki.

Msingi wa kutumia dalili katika uhakiki wa dini.

Ni sahihi kuwa; kufahamu mambo mengi yanayohusiana na hali halisi ya uhakika wa dini, katika hatua ya mwanzo kunahitaji dalili za kimantiki, lakini kila itikadi iliyomo katika dhati ya binaadamu ni lazima ithibitishwe kutokana na dalili za kiakili, ili yaweze kutambulika yale yanayokubalika na yasiyokubalika kiakili. Basini lazima mambo hayp yatafakariwe kwa ajili ya kufahamiwa uhakika wake na kutafutiwa ufumbuzi. Wahakiki wengi hujitosheleza na mabainisho yaliyo dhahiri ya matini tu, hali ya kwamba kufanya tahakiki ndani ya dini, na kufanya uhakiki wa dini kunakubalika ikiwa patatumiwa dalili zitakazokubalika kimaandiko na kiakili, ili kuepukana na kupata natija zitakazotokana na elimu iliyomo katika nafsi zetu, katika uhakiki wa dini ni lazima kuthibitisha mambo kutokana na dalili za kiakili na kimantiki, hivyo ni jambo lisilokubalika mtu kuwa na imani na elimu iliyo katika nafsi yake tu, kuitumia elimu hiyo na kuibainisha kwa watu bila ya dalili yoyote. Kwa mfano:- Ikiwa wahyi umeteremshwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni lazima uthibitishwe kimantiki ili watu waweze kukubali, mbali ya hayo mtu hawezi kuinakili dini kama kisa cha paukwa pakawa, bali katika kubainisha mabainisho ya dini kunatakiwa kutolewa ufafanuzi na kufasiri ibara za dini kwa njia ambayo ni rahisi watu kufahamu, na zitolewe dalili ambazo zitasimama juu ya mstari wa dalili za kimantiki na ziendazo sambamba na akili ya mwanaadamu, vile vile ni lazima tuzingatie kuwa dalili hizo hazitakiwi kulaa juu ya dhana zilizoegemea kwenye mawazo ghafi.


MWISHO