YALIYO MUHIMU NDANI YA DINI

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
YALIYO MUHIMU NDANI YA DINI

Msingi wa kuyapa mgongo mambo asili na yaliyo muhimu ndani ya dini.
Misingi asili ya dini iliyosukumwa nyuma.

Ijapokuwa katika uwanja wa dini kuna baadhi ya vitengo vya uhakiki wa dini vinavyopingana na nadharia mpya zinazotolewa kuhusiana na dini, na vitengo hivyo vina wasiwasi wa kupotea misingi asili ya dini, misingi ambayo inawezekana ikawa ndio kiungo cha dini, kwa upande mwengine, katika uwanja huo huo wa dini kuna madai yanayodaiwa na baadhi ya watu ya kuwepo kwa uhakika wa dini tofauti, (yaani baadhi ya watu wana itikadi ya kuwa dini zote zinabainisha mambo ya uhakika), madai hayo yamejitokeza kwa sababu baadhi ya wahakiki huchukua mambo ya dini na kuyahalili kwa mtazamo wao binafsi, na kuyapeleka au kuyabainisha mambo hayo katika elimu tofauti, kwa mfano muhakiki anaweza kuchukua misingi fulani ya dini, na kwa sababu ni mwenye kupenda taaluma fulani ya elimu, basi huihalili misingi hiyo katika elimu ile ile aliyo na mapenzi nayo, kwa mfano, elimu ya kalamu (akida), au elimu ya falsafa, muhakiki huyo huchukua mambo yote ya dini akayafanyia tahalili katika elimu ya akida, au elimu ya falsafa tu, hali ya kwamba kufanya hivyo kunaweza kupelekea kupotea au kupotosha baadhi ya mambo msingi ya dini yaliyo na uhakika, kwa hiyo kwa uhalili wa muhakiki kama huyo anaweza kupata natija ya kuwa kila kitu ni kufuru tu, hali ya kwamba kila kinachobainishwa ndani ya dini takatifu katika dini takatifu.

Msingi wa kutoishambulia misingi ya dini.
Miongoni mwa misingi mengine ya uhakiki wa dini ni kutambua kuwa uongozi na usimamizi wa dini hauhitaji kuendeshwa kimagubegube, bali unahitaji kuendeshwa kielimu na kitaaluma kwa mujibu wa dalili za kimantiki na zinazokubalika kiakili, kwa hiyo, Waislamu, wahakiki na vitengo vya uhakiki vinapaswa kuelewa kuwa dini haithibitishwi kwa mashambulizi wala kwa matusi, baadhi ya wahakiki wa dini wanadhani kuwa umahiri na ujuzi wa uhakiki wa dini hupatikana katika tarjuma za vitabu au katika udhahiri wa makamusi tu, hali ya kwamba uhakiki kama huo kwa wahakiki ni sumu inayoihilikisha jamii na wale wahakiki walioingia katika uwanja huo kwa matarajio ya kuitambua dini hiyo, kwa hiyo, kwa yule muhakiki aliye na malengo ya kutambua haki na uhakika halisi wa dini, mbali ya kutalii vitabu vya kidini, vile vile ni lazima aitambue dini kupitia wanazuoni na mafaqihi walio wajuzi wanaoitambua dini kwa udhati wake,muhakiki anaweza kuitambua thamani ya dini kupitia Maulamaa na Mawalii wake (Mitume na Ahlulbayt (a.s)) Mwenyeezi Mungu bila ya kuwa mbali na Wahyi aliouteremsha Yeye Mola Mtakatifu (s.w).

 

MWISHO