FUNGAMANO LA MALI NA WATOTO

 BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
FUNGAMANO LA MALI NA WATOTO
1. FUNGAMANO AMBALO LINATOKANA NA MALI NA WATOTO
Kwa wale watu ambao katika dunia ili kuonyesha nguvu na uwezo wao hutegemea mali na watoto wao kwa ajili ya kuondoa athari mbaya na nuhusi katika maisha yao, basi ni lazima waelewe kuwa siku ya Kiama sio mali wala sio watoto wao havitawaletea faida yoyote siku ya Kiama, kama tunavyosoma ndani ya Qur-ani takatifu:-

يَوْمَ لاَ يَنفَعُ مَالٌ وَلاَ بَنُونَ[1]

Siku ambayo kwamba mali hayato faa kitu wala wana.
Ikiwa rasilimali ya watu waovu ni ile milki yao wanayoimiliki katika ardhi hii, wakataka kuitoa rasilimali hiyo au mara mbili zaidi ya kile wanachokimiliki ili wapate kuokoka na kuepukana na adhabu za siku ya Kiama hapana shaka hawatakubaliwa kwayo, kama anavyosema Allah (s.w):

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُواْ لَوْ اَنَّ لَهُم مَّا فِى الاَرْضِ جَمِيعاً وَمِثْلَهُ مَعَهُ لِيَفْتَدُواْ بِهِ مِنْ عَذَابِ يَوْمِ الْقِيَامَةِ مَا تُقُبِّلَ مِنْهُمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ اَلِيمٌ[2]

Hakika walio kufuru lau wange kuwa na yote yaliyomo duniani, na mengine kama hayo, ili watoe fidia ya kuepukana na adhabu ya Siku ya Kiyama, yasingeli pokelewa kwao; na watapata adhabu chungu.

Kwa hiyo siku ya Kiama kila mtu atakuwa na amali zake na akida zake tu na sio kitu chengine, kama anavyosema Allah (s.w):

كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ رَهِينَةٌ[3]

Kila nafsi imo rahanini kwa mabaya iliyo yachuma. (Kila nafsi itafungika motoni kwa amali mbovu ilizozichuma).

Ama kwa wale watu wema ambao walikuwa ni watumwa wa Mwenyeezi Mungu, na wakazikinga na kuzitakasa nafsi zao na maovu, na wakajiepusha na kufanya amali na matendo mabaya, na hawakutegemea mali wala watoto wao, bali waliishi kwa kufuata maamrisho ya Mola wao, basi siku ya Kiama pia hawatakuwa na mahitajio yoyote watakayoyahitaji kutoka kwa mali zao au watoto wao, na wataingia Peponi bila ya vikwazo vyovyote, kama anavyosema Allah (s.w):

إِلاَّ اَصْحَابَ الْيَمِينِ . فِى جَنَّاتٍ يَتَسَاءلُونَ[4]

Isipo kuwa watu wa kuliani. (watu wa kheri).

Hao watakuwa katika Mabustani, wawe wanaulizana.

[1] Surat Shuaraa Aya ya 88

[2] Suratul-Maidah Aya ya 36.

[3] Surat-Al-Muddaththir Aya ya 38.

[4] Surat Muddathir Aya ya 39-40

MWISHO