HATUA NA MALENGO YA PLURALISM No.2

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
HATUA NA MALENGO YA PLURALISM NO.2
Hatua ya tatu:

Katika hatua hiyo ya tatu, ili kuvunja imani madhubuti walizokuwa nazo watu wenye dini, Liberalism waliitumia siasa kama ni njia ya kufikia katika dini, na wakanufaika na dini kutokana na malengo yao ya kisiasa, (yaani waliitumia dini kama ni nyenzo ya kuwafikisha katika malengo na mafanikio yao), wakiwa na matumaini pengine kwa kufanya hivyo wanaweza kuondoa ile thamani ya dini, wakawatawala watu kifikra kwa kuwaambia kuwa ni lazima wastahamiliane na kuvumiliana, huku wakitia fikra zao zisizo za kidini na zinazopingana na dini, hatimae baadhi ya watu walirtadi na kupingana na yale yaliyomo katika dini, basi waliendelea na propaganda zao hizo, hatimae badala ya kunufaika na dini na Wahyi wake Allah (s.w) waliiweka mbali na kuiondoa dini hiyo, ni dini yake Mola, baadae wakaweka yao yale yaliyowatawala katika fikra zao.

Hivyo wananchi wetu wa Irani, mnapaswa kutambua kuwa; mbali ya njia hizo walizotumia mabepari hao, vile vile kumepangwa mipango na njia nyengine zinazotekelezwa na watu wa nchi za kimagharibi, kwa madai ya kusahihisha na kuleta suluhu, watu hao wamepanga program hatari ili kuwapotosha watu kwa ajili ya kufikia malengo yao, malengo asili yanaweza kuwa ni kuutawala ulimwengu kibepari, kwa hiyo inawapasa wananchi wa Irani kuwa na mzingatio ya kutosha ili wasije wakaingia katika mtego wa watu hao.

Mipango ya watu hao hadi sasa iko njiani kutekelezwa, kwa manufaa na mafanikio yao, miongoni mwa manufaa hayo, ni haya yafuatayo:-

1. Mipango ya kueneza na kusambaza sheria na kanuni zao potofu, kwa ajili ya kuwaweka watu katika shaka na wasiwasi juu ya itikadi na imani walizonazo juu ya dini.

2. Mipango ya kupinga kuwepo kwa Mwanafaqihi wa kidini, kutokana na dalili ya kuwepo nadharia na mitazamo tofauti ya wanafaqihi juu ya dini, ambapo natija ya hayo sio kitu chengine isipokuwa ni kufuta na kutokomeza itikadi ya wana dini juu ya kuwakalidi viongozi na wanazuoni wao wa kifiqhi.

3. Programu na mipango inayotumiwa na Pluralism katika kueneza tafakuri zao, mipango ambayo haikuashiriwa natija au athari zozote nzuri zinazoweza kupatikana kwa kufuata fikra hizo, inaweza ikaleta natija hatari na athari zilizo mbaya kifikra katika jamii, na hata vyombo vya habari.

4. Masisitizo ya Pluralism katika kuwabainishia watu mitazamo ya fikra zao hayawezi kuwaletea watu faida wala hayaendani sambamba na natija zinazohitajiwa na watu kwa ajili ya kuwafikisha katika ukamilifu na kuwaletea maendeleo. Fikra za Pluralism za kidini ni kuwa;

Kutokuwepo na ghasia au vurugu zozote katika dini, kuwepo uvumilivu na ustahamilivu katika dini, kupewa uhuru wale wanaopinga dini, walio na shaka au wasi wasi kuhusiana na uhakika wa dini, n.k.

Mabainisho ya nadharia hizo hayawezi kukubalika bila ya kuashiriwa natija au athari nzuri zinazoweza kupatikana kwa kuzikubali nadharia hizo za kidini za pluralism, kwa hakika nadharia hizo hazileti maslahi yoyote katika jamii, na hazileti manufaa yoyote yatakayoweza kuwafikisha wanaadamu katika saada njema ya duniani na Akhera, basi la msingi linalopaswa kutambuliwa ni kuwa Pluralism wana malengo yao wanayotaka kuyafikia kutokana na fikra hizo, na ili kuyafikia malengo hayo wanawatumia na kuwatawala watu kifikra ili kukubaliana nao katika fikra hizo, kwani hawawezi kufikia katika malengo yao bila ya watu kukubaliana na nadharia au fikra hizo na kukubali mfumo wa kidini wa pluralism.


MWISHO