MITAZAMO KUHUSIANA NA DINI

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

MITAZAMO KUHUSIANA NA DINI

Katika makala zilizopita tulielezea kuhusu hali halisi ya dini, katika makala hii natutupilie macho ule mtazamo wa wale  wanaodai kuwa:-

“Nidhamu ya mfumo wa serikali ndio inayoweza kuisaidia dini ili kupata uhakika wake kamili na kuipa sura kamili ya dini, na mafunzo ya dini huja yakakumbana na uhakika wa mambo ulivyo, mafunzo ya dini ni fikra na mtazamo maalumu ambao unapokuja katika ulimwengu wa matendo zinakumbana na uhakika wa mambo yalivyo”. Kauli hiyo sio sahihi na wala haikubaliki kwa sababu:-

*Picha kamili ya dini na mfumo wa siasa ya dini ni kitu kimoja, na sio mfumo wa siasa ya dini ndio unaotoa sura kamili ya dini, mfumo wa siasa ya dini ni sehemu tu ya sura ya dini (yaani ni kiungo cha dini) .

Moja: Kwa mujibu wa nadharia za watu hao, inathibitika kuwa watu hao wamebagua baina ya Serikali ya dini na uhakika wa elimu na mafunzo ya dini, hali ya kwamba Serikali ya dini sio kitu chengine isipokuwa ni huo huo uhakika wa dini na ni hayo hayo mafunzo na elimu ya dini, (yaani Serikali ya dini dini inatokana na elimu ya dini), mtu hawezi kuitambua serikali ya dini kama hakuwa na elimu ya dini. Kwa hiyo fikra hizo sio kitu chengine isipokuwa ni hila na udanganyifu wa watu hao wa kutaka kuipotoa na kuivuruga dini takatifu.

Mbili: Mitihani na majaribio hufanyika wakati inapotambuliwa au kushakiwa kuwa panaweza kutokea makosa fulani, hali ya kwamba katika dini hakuna shaka kama hiyo kiasi ya kwamba pafanyike majaribio na mitihani.

Tatu: Katika hali kama hiyo mwenye kufanya majaribio au mitihani hiyo litakuwa ni kundi ambalo kigezo chake au fikra na mtizamo wake sio wa kidini, na ikiwa ni mtu ndiye anayefanya majaribio hayo, basi atakuwa ni mtu asiye na itikadi wala imani yoyote kuhusuiana na dini. Hali ya kwamba kwa mtazamo wa dini, na kwa mtazamo wa wenye dini ikiwa patafanywa utafiti basi utafiti huo hufanyika kwa kufuata maamrisho ya dini na katika njia za dini, kwa hiyo utafiti wa dini haufanyiki katika njia zisizokuwa za dini au kufanywa na watu wasio na dini, kwani fikra hizo hazikubaliki kiakili wala kimantiki.

Vile vile ni lazima tuzingatie kuwa, Maulamaa wa kidini ni wenye kubainisha taaluma na mafunzo ya elimu ya dini, na sio kubainisha mambo ambayo hayana budi kubainishwa (yaani kutumia njia zozote zile ijapokuwa sio njia zilizoamrishwa na kukubalika katika elimu ya dini), kwa sababu maamuzi yasiyo budi kuchukuliwa hufanyika pale ambapo panashakiwa kuwa pana upungufu, hali ya kwamba katika dini hakuna shaka wala upungufu wowote utakaoweza kuwasababishia wana dini kutafuta njia zisizobudi kuchukuliwa kwa ajili ya kupata utafiti au ufumbuzi wa mambo fulani, kwa hiyo dini ambayo wanadini au wafuasi wake huyatafutia mambo ufumbuzi bila ya kuzingatia maamrisho ya dini hiyo kwa hakika hiyo sio dini, na watu kama hao hawawezi kuitwa wana dini. Baadhi ya watu wamedai kuwa:-

Serikali ya dini siku zote inaitumia dini kama ni silaha ya vita na mapambano kwa madai ya kutetea haki, na mafunzo ya dini yanatumika kama ni maabara ya kufanyia majaribio na mitihani kwa ajili ya kukabiliana na uhakika[1]

Kauli hiyo si sahihi na madai hayo hayana uhakika wowote na hayakubaliki kutokana na dalili hizi za Qur-ani;

*Dalili za Qur-ani:-

 Ikiwa serikali ya dini itapigana vita ni kwa ajili ya kutetea haki ya dini hiyo na wafuasi wake, na ikiwa viongozi wa Serikali hiyo wamepigana vita basi ni kwa idhini yake Allah (s.w) kutokana na dhulma walizofanyiwa wafuasi wa serikali hiyo ya kidini, kwa mfano kama pale Allah alipowaruhusu Waislamu kupigana vita kutokana na dhulma walizokuwa wakifanyiwa. Allah (s.w) anasema:-

اُذِنَ لِلَّذِينَ يُقَاتَلُونَ بِاَنَّهُمْ ظُلِمُوا وَإِنَّ اللهَ عَلـٰي نَصْرِهِمْ لَقَدِيرٌ . الَّذِينَ اُخْرِجُوا مِن دِيَارِهِمْ بِغَيْرِ حَقٍّ إِلاَّ اَن يَقُولُوا رَبُّنَا اللهُ وَلَوْلاَ دَفْعُ اللهِ النَّاسَ بَعْضَهُم بِبَعْضٍ لَّهُدِّمَتْ صَوَامِعُ وَبِيَعٌ وَصَلَوَاتٌ وَمَسَاجِدُ يُذْكَرُ فِيهَا اسْمُ اللهِ كَثِيراً وَلَيَنصُرَنَّ اللهُ مَن يَنصُرُهُ إِنَّ اللهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌ[2]

-Wameruhusiwa kupigana wale wanao pigwa vita kwa sababu wamedhulumiwa - na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwasaidia .

-Wale ambao wametolewa majumbani mwao pasipo haki, ila kwa kuwa wanasema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu! Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawakingi watu kwa watu, basi hapana shaka zingeli vunjwa nymba za wat'awa, na makanisa, na masinagogi, na misikiti, ambamo ndani yake jina la Mwenyezi Mungu linatajwa kwa wingi. Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu.

Maelezo kuhusiana na Aya:

Waislamu waliishi Makka muda wa miaka kumi na tatu, wakiadhibiwa kwa adhabu zisizostahamilika, na juu ya hayo hawakupewa ruhusa ya kujetetea. Na mwisho wakapewa ruhusa ya kutupa watani wao, mali yao na watu wao, wahamie Madina. Huko ndiko ilikoshuka Aya hii kuwapa ruhusa ya kujitetea.

Katika Aya nyengine Allah (s.w) anasema:-

وَقَاتِلُواْ فِى سَبِيلِ اللهِ الَّذِينَ يُقَاتِلُونَكُمْ وَلاَ تَعْتَدُواْ إِنَّ اللّهَ لاَ يُحِبِّ الْمُعْتَدِينَ[3]

Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanao kupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui.

Maelezo kuhusiana na Aya:-

Hii ni moja katika Aya zinazofedhehi uwongo wa wanaosema kuwa Uislamu umesimama kwa upanga, kwa kuwapiga watu bure ili waingie katika dini ya Kiislamu, huo ni uwongo, inaonekana hapa kuwa wanapewa ruhusa wapigane na wale wanaowapiga.

Na katika surat Mumtahinah anasema hivi:-

لاَ يَنْهَاكُمُ اللهُ عَنِ الَّذِينَ لَمْ يُقَاتِلُوكُمْ فِى الدِّينِ وَلَمْ يُخْرِجُوكُم مِّن دِيَارِكُمْ اَن تَبَرُّوهُمْ وَتُقْسِطُوا إِلَيْهِمْ إِنَّ اللهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ . إِنَّمَا يَنْهَاكُمُ اللهُ عَنِ الَّذِينَ قَاتَلُوكُمْ فِى الدِّينِ وَاَخْرَجُوكُم مِّن دِيَارِكُمْ وَظَاهَرُوا عَلـٰي إِخْرَاجِكُمْ اَن تَوَلَّوْهُمْ وَمَن يَتَوَلَّهُمْ فَاُوْلَئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ[4]

Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu.

Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale walio kupigeni vita, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanao wafanya hao marafiki basi hao ndio madhaalimu.

5.Elimu ya dini, na uhakika wa dini ni kitu kimoja, na hakuna tofauti yoyote baina ya vitu viwili hivyo, kwa sababu malengo ya vitu viwili hivyo ni mamoja. Na mafunzo ya dini yanaonyesha uhakika wa taaluma zote za dini katika Nyanja na mambo mbali mbali yanayohusiana na wanaadamu, au hata yanayohusiana na viumbe wengine (wanyama, miti, mimea, n.k.), Kwa hiyo utawala wa serikali ya siasa ya dini sio kitu chengine isipokuwa ni jitihada za wanadini kwa ajili ya kuwathibitishia walimwengu hali halisi ya uhakika wa dini,
 

Ikiwa dini ya haki ni moja tu, basi haiwezekani kuwepo dini tofauti na zote zikawa ni za haki, ikiwa kuwepo mitazamo na mifumo tofauti ndani ya dini moja, mifumo ambayo haioani na elimu au mafunzo ya dini

hiyo inamaanisha kuwa dini hiyo si ya haki, basi itawezekana vipi dini moja kuwa na mitizamo na fikra mbali mbali ambazo haziendani sambamba na malengo ya serikali ya dini?

 

 

[1] Mustafa Malikiyan, Joygoh Navondishiy Diyniy, (nafasi ya akili ndani ya dini),jarida la habari za elimu ya dini, mwaka wa kwanza, nambari moja.

 

[2]   Surat Hajj Aya ya 39-40

 

[3] Surat Albaqarah aya ya 190.

 

[4] Surat Mumtahinah aya ya 8-9


 

MWISHO