MAKUNDI YA WANAADAMU SIKU YA KIAMA

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
MAKUNDI YA WANAADAMU SIKU YA KIAMA

* wanaadamu watagawika makundi mangapi katika siku ya malipo na jazaa? Siku ya Kiama walimwengu watagawiwa katika makundi totfauti kwa mujibu wa itikadi na amali zao walizozifanya duniani, baadhi ya wanaadamu katika dunia walipinga malinganio ya Mitume ya Mwenyeezi Mungu, na wakaizima ile nuru ya akili na ya kifitra, basi kwa hakika watu hao wamejidhulumu wenyewe, na siku ya Kiyama watajulikanwa kwa jina la watu wa upande wa kushoto, na baadhi ya walimwengu duniani walifanya yale waliyoamrishwa na Mola wao, na wakajiepusha na yale waliyokatazwa, basi watu hao siku ya Kiyama watajulikanwa kwa jina la watu wa upande wa kulia, na baadhi ya wanaadamu walifanya amali na matendo mema, na wakavuka hatua na kufikia katika ukamilifu, basi watu hao siku ya Kiyama watakuwa karibu na Mola Mtakatifu, qur-ani kariym kuhusiana na makundi hayo matatu ya wanaadamu inasema hivi:-

ثُمَّ اَوْرَثْنَا الْكِتَابَ الَّذِينَ اصْطَفَيْنَا مِنْ عِبَادِنَا فَمِنْهُمْ ظَالِمٌ لِّنَفْسِهِ وَمِنْهُم مُّقْتَصِدٌ وَمِنْهُمْ سَابِقٌ بِالْخَيْرَاتِ بِإِذْنِ اللهِ ذٰلِكَ هُوَ الْفَضْلُ الْكَبِيرُ[1]

Kisha tumewarithisha Kitabu hao ambao tuliwateuwa miongoni mwa waja wetu. Kati yao yupo aliye jidhulumu nafsi yake, na yupo wa katikati, na yupo aliye tangulia katika mambo ya kheri, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo fadhila kuu.
Maelezo kuhusiana na Aya:
Katika Aya hii waliyoifanya kuwa ni ya 33 wamepindua muradi wa tamko la “Dhalimun Linafsihiy”, hao ni watu wabaya wanazidhulumu nafsi zao kwa kufanya mabaya, Wao wanasema hao ni watu wazuri, Saabiqun Bil Khayrat (waliotajwa hapo pia) watakuwa nani? hawaachi! Kila kundi, miongoni mwa makundi hayo matatu limearifishwa kwa mtindo wa namna tofauti, makundi hayo katika qur-ani yamearifishwa namna hii,.
- Kundi la watu madhaifu, kundi la Makhalisi, na kundi la Maurafaa. watu wa kila kundi miongoni mwa makundi hayo watanufaika na saada au watapata adhabu kulingana na mema au mabaya waliyoyatenda, ili kuelewa zaidi, tutaelezea hatima ya makundi hayo matatu siku ya Kiyama.
*Kundi la watu watakaoelekea upande wa kushoto.
Katika kamusi ya Qur-ani tukufu, neno شمال lina maana ya: upande wa kushoto, kinyume chake ni یمین .

*kundi litakaloelekea upande wa kushoto ni lile kundi la watu ambao waliishi duniani kwa matamanio ya nafsi zao, na wakapinga kutii amri za Mwenyeezi Mungu na Mitume yake, watu hao hawakuw thabiti katika kutekeleza majukumu waliyopewa na Mola wao, walifanya maovu na kumuasi Mwenyeezi Mungu, hata wakapinga kuwepo kwa siku ya Kiyama, qur-ani karym inawaarifisha watu hao kwa kusema:-

إِنَّهُمْ كَانُوا قَبْلَ ذٰلِكَ مُتْرَفِينَ . وَكَانُوا يُصِرُّونَ عَلـٰي الْحِنثِ الْعَظِيم . وَكَانُوا يَقُولُونَ اَئِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَاباً وَعِظَاماً اَئِنَّا لَمَبْعُوثُونَ[2]

Hakika hao walikuwa kabla ya haya wakiishi maisha ya anasa. Na walikuwa wakishikilia kufanya madhambi makubwa, Na walikuwa wakisema: Tutakapo kufa na tukawa udongo na mafupa, ati ndio tutafufuliwa?
Watu hao walipinga misingi ya itikadi na wakahiyari kufanya uovu na maasi, basi siku ya Kiyama watapewa daftari ya amali zao walizozitenda duniani kwa upande wa kushoto, na hiyo ni alama inayoonyesha uangamiaji na jazaa mbaya wakayopewa watu hao.

وَاَمَّا مَنْ اُوتِيَ كِتَابَهُ بِشِمَالِهِ فَيَقُولُ يَا لَيْتَنِى لَمْ اُوتَ كِتَابِيهْ[3]

Na ama atakaye pewa kitabu chake katika mkono wake wa kushoto, basi yeye atasema: Laiti nisingeli pewa kitabu changu!
Ndani ya qur-ani pia, watu hao wamearifishwa kuwa ni watu walioangamia maangamio mabaya kutokana na kuzikufuru Aya zake Allah (s.w), basi hatima ya watu hao ni adhabu kali iumizayo, adhabu ambayo wameitayarisha wenyewe kutokana na yale waliyoyatenda.

وَالَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِنَا هُمْ اَصْحَابُ الْمَشْاَمَةِ . عَلَيْهِمْ نَارٌ مُّؤْصَدَةٌ[4]

Lakini walio zikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni. Juu yao utakuwa Moto ulio fungiwa kila upande.  

 

[1] Surat Faatir Aya ya 32.

[2]SuraAl-Waqiah Aya ya 45-47.

[3] Surat Haqah Aya ya 25

[4] Suratul-Balad Aya ya 19-20