MAISHA YA MTUME LUT

MAISHA YA MTUME LUT
Mtume Lut a.s. alikuwa ni ndugu wa kijamaa wa Mtume Ibrahim a.s. yaani mtoto wa mamake mdogo na dada yake Mtume Lut a.s. aliolewa na Mtume Ibrahim a.s.
Tendo ovu kabisa lililokuwa katika ukoo wa Mtume Lut a.s. ni tendo la Ulawiti 1
TABIA MBAYA
Ulizidi ufisadi katika mji mmoja miongoni mwa miji ya zamani kiasi kwamba atakapoona mtu ufisadi unatendwa na mmoja kati yao basi hakatazwi na mtu mwingine atakapo shuhudia heri inafanywa na ndugu yake basi humkemea mpaka aache heri anayoifanya. Kila mtu katika kijiji hicho alikuwa katika upotevu na uovu na ujinga, hawasikii wala hawasikilizi ilikuwa ni mamoja kwao apatikane mtu wa kuwapa mawaidha wao au mtu wa kuwanasihi wao kulikuwa hakuna tofauti yoyote. Walikuwa ni watu waovu na wabaya zaidi na wenye tabia mbaya miongoni mwa watu, uhai wao (ulikuwa ni khiana na tabia mbaya) na wote hao wakati huo walikuwa ni wenye tabia mbaya sana na nia mbaya. Lakini unaonaje ewe msomaji je walijizuia na maovu yao haya au walizidi katika upotevu na ufijari na madhambi ?
KUENEA MAMBO YA HARAMU
Ilikuwa kama kwamba nafsi zao hazikutosheka na kule kusema uongo na kuwa na tabia mbaya na ghadr na mengineyo mengi, wakasababisha na kuleta mambo ya unyama ambayo hakutangulia kufanya yeyote kabla yao. Je ni mambo gani hayo?
Hakika waliacha mambo aliyoyahalalisha Allah swt kwao kwa wanawake na wakawa hawaoi wanawake ! Wakawaacha wake zao na kuanza maovu ya kuingiliana na wanaume wenzao. Jambo ambalo Allah swt aliliharamisha kabisa.
Na laiti wao wangesitiri haya maovu au wakajaribu kujiepusha kutoka katika maovu haya au kujiweka mbali nayo ingelikuwa afadhali lakini wao walijitumbukiza katika mambo hayo na wakawa wanayatangaza wazi wazi mpaka ukaenea ufisadi na kukaenea mambo ya haramu na zikawa tabia zao mbaya ni rahisi kiasi kwamba zikawa zimefikia daraja kubwa sana na yote hayo yalikuwa ni madhambi na ufisadi wala hawezi mtu yeyote kuyafanya wala kufikiria binaadamu au kupiga picha ya binaadamu katika akili yake.
MLINGANIO WA MTUME LUT A.S.
Na walipofikia hali yao ya ufisadi kiwango hiki ndipo Allah swt alipompa Wahyi mtu mmoja miongoni mwao jina lake Mtume Lut a.s. na kukaanza kwake yeye matangazo ya wema na heri. Allah swt alimpa Wahyi akamwamrisha kwamba afanye kazi ya kuubadilisha umma wake au kaumu yake na Mtume Lut a.s. alijibu maombi haya ya Allah swt wake na moja kwa moja akaanza kufanya kazi hii ya kuwalingania watu kwenye heri na wema na akawa anasema:
“Enyi watu wangu! Zitoharisheni nafsi zenu na acheni mambo maovu.
Enyi watu wangu! Hakika kitendo chenu hiki ni haramu na Allah swt haridhii kuwaacheni nyinyi katika hali hii bila ya kukupeni uongofu basi anayenituma mimi kwenu na mimi ni miongoni mwenu na siwezi kunyamaza juu ya jambo hili la haramu.
Enyi watu wangu! Fanyeni Tawbah ya Allah swt na mjiepushe na nia zenu kwa ajili Yake.”
KIBURI
Lakini kaumu ya Nabii Mtume Lut a.s. ambao uliwazidi wao uovu na ukawafunika wao mambo ya haramu hawakusikiliza maneno ya Mtume Lut a.s. isipokuwa walizidisha kiburi na wakapinga ‘ibada ya Allah swt na kuacha mambo haramu na wala hawakunyamaza kuyafanya maovu yao bali waliendelea kufanya kiburi na wakafanya njama kwamba wamwondoe Mtume Lut a.s. na watu walioamini maneno ya Mtume Lut a.s. katika kijiji chao kwa sababu Mtume Lut a.s. na watu walio mwamini Mtume Lut a.s. hawafanyi mambo ya uovu kama wanavyofanya wao bila wanajitoharisha. Hivyo wakamwendea Mtume Lut a.s. huku wakimwonya na wakimtaka kwamba atoke kwenye kijiji chao. Na vile vile walimwahidi kuwa atatoka tu kwani watamfanyia njama na majungu mpaka atoke kijijini humo.
MAONYO
Wakati walipoona Mtume Lut a.s. njama na kiburi kutoka kwa kaumu yake, akarudia maneno yake kwa kuwaambia wao na kuwaonya na kuwafahamisha matokeo ya njama zao watakavyo fanya na akuwaambia wao
“Enyi kaumu yangu ! Kama hamtafanya Tawbah na kuacha haya maasi basi kwa hakika Allah swt atawashushieni adhabu kutoka mbinguni. Hakika Allah swt anakuoneni nyinyi na wala hakuathirika na nyinyi na yeye hapendi ukafiri na wala ufisadi na wala hawapendi watu wanaofanya ufisadi.
Rejeeni na mfanye tawbah kwa Allah swt na acheni madhambi na mambo mauovu.
Hakika mimi naogopa adhabu ya Allah swt na mateso yake yatakayo shuka kwenu”.
Na pamoja na haya hawakusikiliza maneno yake isipokuwa walimfanyia mzaha na kumtania na wakamkemea kwamba atatoka tu pamoja na watu walio mwamiani yeye kwa sababu wao wanajitoharisha wenyewe kwa wenyewe na hawakujali wao kwamba yeye Mtume Lut a.s. ni mfanya dhambi au makosa yoyote.
KUJIBU KWA ALLAH SWT
Na hakika Allah swt hakumwacha Mtume Lut a.s. na watu walio mwamini yeye bila ya kuwanusuru na kuwapa ushindi wala hakuwaacha makafiri waliokuwa madhalimu bila ya kuwaadhibu wao.
Ni hawa makafiri ambao wamedhihirisha ufisadi na huyu Mtume Lut a.s. ambaye anawatahadharisha na kuwazuia wao bila ya kupata majibu yoyote mwisho.
Hatimaye Mtume Lut a.s. akalazimika kumwomba Allah swt awateremshie juu ya watu hawa adhabu na tutanaona kwamba madhalimu hawataweza kumtoa Mtume Lut a.s. au kuizuia au kuifukuza adhabu itakayowamiminikia juu yao.
Allah swt akajibu dua ya Mtume Lut a.s. na akaishusha !
MALAIKA WAKO KWA MTUME IBRAHIM A.S.
Allah swt amewatuma Malaika kwenda kwa watu wa mji huu wakapitia kwanza katika nyumba ya Mtume Ibrahim a.s. na Malaika hawa walikuwa katika umbile la binaadamu (Mtume Ibrahim a.s. aliwakaribisha na kuwawekea chakula ili wale, lakini wao hawakula, kwani Malaika huwa hawali chakula) Mtume Ibrahim a.s. akawaogopa wao.
Malaika wakamwambia Mtume Ibrahim a.s.
“Usiogope hakika sisi ni Malaika kutoka kwa Allah swt na tumetumwa kwa kaumu ya Mtume Lut a.s. watu waovu ili tuwaadhibu wao lakini tumepita kwako ili tukubashirie wewe kwamba utazaa mtoto.”
Mtume Ibrahim a.s. kwa kuyasikia hayo alifurahi mno yeye pamoja na mke wake (na yeye akiwa ni mwenye umri mkubwa hakuzaa mpaka hivi sasa).
Mtume Ibrahim a.s. aliwaonea huruma watu wa kaumu ya Mtume Lut a.s. na akaogopa kwamba yasije yakamfika madhara Mtume Lut a.s. kwa hiyo Malaika nao wakamjibu kwamba (hakuna hofu yoyote juu ya Mtume Lut a.s. isipokuwa mke wake alikuwa ni miongoni mwa makafiri………..!
KWENDA KWENYE KIJIJI CHA MTUME LUT A.S.
Wakamwacha Mtume Ibrahim a.s. na wakaenda zao kwa Mtume Lut a.s. wakiwa katika maumbo ya vijana wa kiume wenye sura nzuri sana wakaenda moja kwa moja mpaka kwenye kijiji cha watu wadhalimu na wakaingia katika nyumba ya Mtume Lut a.s., Mtume Lut a.s. akaogopa kwamba wasije wakamfedhehesha watu wake kwa mambo yao maovu yanayo julikana.
Mtume Lut a.s. alijaribu kuwaficha hao na habari za wageni wake bila kujua kwamba wao ni malaika lakini wale Kaumu waligundua jambo lile na wakapeana habari wao kwa wao kwamba waanze kufanya uovu wao kwa wale wageni wa Mtume Lut a.s. Basi ni nani ambaye ametangaza siri ile iliyofichwa kwamba nyumbani kwa Mtume Lut a.s. kulikuwa na wageni wazuri ?
Hakuna shaka kwamba yuko aliyejua jambo lile na akaenda kwa makafiri kuwapa habari na hakuna shaka kwamba huyu aliyeitoa habari ni kafiri kama wao na kwa sababu hii ndipo akawajulisha wao juu ya jambo hili la uovu.
MKE WA MTUME LUT A.S.
Hakika mke wa Mtume Lut a.s. ndiye aliyetoa habari kuwapa wale watu na kuwafahamisha jambo la wageni na kwamba yeye huyo mwanamke alikuwa kafiri na alitangaza ukafiri na akaitoa nje siri na haraka wakaja makafiri katika nyuma ya Mtume Lut a.s. wakawa wanamtaka Mtume Lut a.s. awakabidhi wao wageni wake ili wawafanyie mabaya.
Akaogopa Mtume Lut a.s. na akawaomba wao wajitenge na kujiepusha kabisa na jambo hilo lakini wao walikuwa ni makafiri na watu waovu kabisa ambao wamefikia daraja kwamba hawasikii nasaha ya mtu yeyote na wala hawawezi kujiepusha na maovu.
Mtume Lut a.s. alifunga milango mbele yao na aliwaghadhabikia sana na katika dakika chache tu wao kwa ujeuri wakaingia kwenye nyumba na wakataka kufanya ulawiti juu ya wageni wa Mtume Lut a.s.
UKWELI
Alikaa Mtume Lut a.s. akiwa mwenye kuhuzunika kwa kuingia waovu ndani ya nyumba yake lakini wale wageni ambao walikuwa mle ndani walicheka tu kwa kuingia watu hawa ndani ya nyumba ya Mtume Lut a.s. na waligeuza nyuso zao kumwelekea Mtume Lut a.s.na wakamtuliza yeye kwa kumwambia kuwa wao ni Malaika kutoka kwa Allah swt na wakamwambia Mtume Lut a.s. :
“Hakika sisi tumekuja kukuokoa wewe pamoja na waliokuamini wewe. Usituogopa na tunakuomba uiache nyumba yako wakati wa mwisho wa usiku.
Wewe pamoja na wafuasi wako mutajitenga mbali na kutoka katika kijiji hiki ambacho kitashushiwa adhabu kutoka kwa Allah swt.
Na tunakuomba umwache mkeo kwani yeye ni Kafiri aliye pamoja na watakao adhibiwa naye ni mfano wao anafanya na kuwapa msaada watu waovu.”
Na baada ya hapo alifurahi mjumbe wa Allah swt na ikamwondokea hofu moyoni mwake.
MWISHO WA WOGA
Akatoka Mtume Lut a.s. na watu wake (isipokuwa mkewe) Mtume Lut a.s. akakiacha kile kijiji bila ya kukisikitikia mpaka akawa mbali kabisa na kile kijiji na ikaja amri kutoka kwa Allah swt ya kushushiwa adhabu. Yakashuka mawe na ikatikisika ardhi na yakapinduliwa majumba na kubomoka na zikaanguka sakafuni na ikawa ardhi yao juu chini na chini juu.
Je nini kimepita ? Hiyo ni adhabu ya Allah swt na hayo ndiyo mateso hakika wamekuwa makafiri chini ya kupondwa pondwa na kuharibiwa majumba yao na kubomolewa na mizoga yao kutawanyika yote haya ndio malipo ya kazi yao mbaya ya ukafiri na ubishi wao kwani wao walifanya kiburi na wakapinga uongofu.
MWISHO WA HAKI
Na baada ya kufa makafiri je kwa maoni yako nani alibakia ? Ni nani alipata ushindi na akaishi ?
Jibu ni kwamba wale walioamini ( Mtume Lut a.s. na watu wake ambao walimwamini yeye) ama mke wake ambaye alishiriki na makafiri na hivyo alikufa pamoja na makafiri na hivyo ndivyo ilivyo uongofu siku zote huwa juu na uovu hurudi chini na hali hii ni ya kudumu.
Enyi ndugu zangu kwa hivyo tutakapopigana Jihadi, tukasubiri na kuvumilia magumu, hakika ushindi utakuja kuwa pamoja nasi mwisho wake na Allah swt atawagharikisha wale wenye kiburi. Hakika Allah swt yu pamoja na wacha Mungu ambao wao ndio wenye kufanya wema.
Na ninataka kukuulizeni enyi vijana mashujaa kabla sijawaageni mwisho wa kisa hiki :
Je mnajua kwa nini tunasoma visa hivi?
Kwa hakika sisi tunasoma visa hivi ili tufahamu haki kutokana na visa hivi na hakika ya sisi tutazichukua nafsi zetu moja kwa moja kufuata haki hii na tutafuata maneno yaliyo mazuri na maana iliyo nzuri na sisi tuko pamoja na Allah swt na wanao mcha Allah swt na waumini na tunamshukuru Allah swt kwa kutoa neema ya imani ya ucha Mungu.
•    1. Mimi nimekitarjumu kitabu kimoja katika kiswahili juu ya Maudhui haya Katika Islam Uharamisho wa ulawiti. Hivyo unaweza kusoma ukapata kujua ni kwa nini Uislamu umeharamisha ulawiti.

MWISHO