UPORWAJI NA WAPORAJI WA FADAK 1

UPORWAJI NA WAPORAJI WA FADAK

MASHI'AH WATATAFUTA FIDIA YA HALI YA MAMBO SIKU YA HUKUMU

Sulayman:

Sasa mnaweza mkaona wenyewe kwamba tukieleza ukweli huu, ambao umeandikwa na maulamaa wenu Ahlisuna wakubwa kama Abi l Hadid na wengine, mara moja tunalengwa kushambuliwa eti kwa sababu tumemtukana Khalifa, lakini hakuna kikwazo kwa Abi l Hadid na maulamaa wengine ambao wameandika habari hizi. Kwa kweli hatuna nia ya kumtukana mtu yeyote. Sisi tunasimulia mambo ya kihistoria tu, na mnatuangalia kwa macho ya dharau. Mnayapuuza mambo hayo.

Mashi'ah watakuwa na malalamiko mengi siku ya Hukumu dhidi ya Ulamaa wenu, Ulimwengu utatoweka lakini lazima msimame mbele ya Mahakama Adilifu ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kujibu uonevu wenu.

Malik :

Tafadhali niambie ni kwa uonevu upi ambao mtatafuta haki siku ya hukumu?

Sulayman:

Kuna mifano ambayo naweza Kuionyesha. Wakati siku ya hukumu Tukufu itakapowadia, kwa hakika tutaitafuta haki.

Malik:

Nakuomba usichochee mihemuko ya watu wengine. Tuambie ni uonevu gani uliowapata.

Sulayman:

Uonevu wa dhulma sio jambo geni leo kwetu sisi. Lakini msingi wake ulijengwa mara tu baada ya kufariki Mtukufu Mtume saww. Haki ya bibi yetu mdhulumiwa, Fatimah Zahraa ambayo aliachiwa na baba yake, Mtukufu Mtume saww, kwa ajili ya kuwalea watoto wake, iliporwa. Hakuna kujali kokote kulikofanywa kwa ajili ya malalamiko na upingaji wake wa dhati. Hatimaye alifariki katika ujana wake akiwa amevunjika moyo.

Malik:

Tafadhali, unawachochea watu bila sababu yoyote. Tuambie ni haki gani ya Fatimah iliyoporwa? Tafadhali kumbuka kwamba kama utashindwa kuthibitisha dai lako, kwa kiasi fulani utashindwa katika Mahakama Tukufu ya haki. Jione uko katika Mahakama ya Mwenyezi Mungu ya Uadilifu na utetee kesi yako.

Sulayman:

Siku moja tutakuwa mbele ya Mahakama Tukufu. Tunategemea tutapata haki. Kama wewe pia unayo hisia ya Uadilifu, yakupasa kama Hakim muadilifu kusikiliza hoja yangu bila chuki. Naamini utakubali uhalali wa dai letu.

Malik:

Naapa kwamba sina chuki wala ukaidi. Hakika Umeona katika mijadala hii kwamba sihoji kipumbavu. Wakati niliposikia hoja zenye mantiki nilizikubali. Kunyamaza kwangu kwenyewe kulikuwa kunaonyesha kwamba nimekubaliana na mwenendo huu wa haki. Kwa asili mimi si mtu wa kupenda mizozo. Nakiri kwamba kabla sijakutana na wewe hapa, nilitaka nikushinde.

Lakini nimevutiwa mno na usafi wako, upole wako, tabia nzuri, wepesi wa hisia ya kweli kiasi kwamba nimeweka nadhiri mbele ya Mwenyezi Mungu kwamba nasalimu amri kukubali ukweli wote wenye mantiki ingawa msimamo huu utavunja mioyo juu ya matarajio ya wengine. Niamini mimi, siyo mtu yule wa siku ya kwanza. Nakueleza kwa ukweli na uwazi kabisa kwamba hoja zako zimeacha athari ya ndani mno katika moyo wangu. Kwa dhati kabisa natumaini kwamba nitaweza kufa pamoja na mapenzi na upendo kwa Mtukufu Mtume saww na kizazi chake, ili kwamba niweze kusimama kwa furaha na kuridhia mbele ya Mtukufu Mtume saww.

FADAK NA UPORWAJI WAKE

Sulayman:

 Wakati ngome imara ya Khaibarah iliposhindwa na kutekwa, malodi, makabaila na watu mashuhuri wa Fadak walikuja kwa Mtukufu Mtume saww. Fadaki ilikuwa ni eneo katika bonde la milima ya Madina. Lilikuwa na vijiji saba ambavyo vimeenea mpaka kwenye mwambao wa bahari. Vingi vilikuwa na rutuba sana na kulikuwepo na chemchem nyingi zenye miti (Oasis). Walifanya mkataba wa amani na watu hao, mkataba unaosema kwamba nusu yote ya Fadak Itakuwa chini ya miliki yao na nusu nyingine Itakuwa mali ya Mtukufu Mtume saww.

Ukweli huu imesimuliwa na Yaqut Hamawi, mwandishi wa "Majimuul Buldan", katika kitabu chake" "Futuhul Buldan, Jz 6 UK 343; Ahmad bin Yahya Baladhuri Baghdadi aliyefariki mwaka 279 hijiria, katika kitabu chake Tarikh; Ibn Abi Hadid Muutazili katika Sherehe Nahjul Balagha iliyochapishwa Misri, Jz 4 UK 79, akinukuu kutoka kwa Abu Bakr Ahmad bin Abdu l Aziz Jauhari; Muhammad bin Jariri Tabar katika kitabu chake Ta'rekh Kabiir na wengine katika Muhadithina na wanahistoria wenu Ahlisuna.