Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

Imam Mahdi (A.S)

IMAM MAHDI NDANI YA RIWAYA ZA KISUNNI 1

IMAM MAHDI NDANI YA RIWAYA ZA KISUNNI 1

IMAM MAHDI NDANI YA RIWAYA ZA KISUNNI 1 WANAVYUONI WA MADHEHEBU YA SUNNI WAMEKIRI KUWA IMAM MAHDI (A.S.) AMESHAZALIWA Kuna matamko mengi ya kukiri kuwa Imam Mahdi (a.s.) ameshazaliwa ambayo Sunni wameyasajili kwa kalamu zao. Na baadhi wamefanya kazi ya kuchunguza kukiri huku katika uchambuzi hasa unaojitegemea, hivyo uchunguzi huu ulikuwa unafuatana zama kwa zama kiasi kwamba haishindikani mwenye kukiri sasa kuhusu kuzaliwa kwa Mahdi kukutana na aliyekiri zama zilizotangulia, na hilo ni kuanzia zama za ghaibu fupi ya Imam Mahdi (a.s.) (260 – 329 A.H.) Na mpaka zama zetu hizi. Sisi tutafupisha kwa kuwataja baadhi yao, ama atakayetaka kwa urefu na upana ni juu yake kurejea uchunguzi uliotangulia kuhusu kukiri huko,1 na hao baadhi ni: 1. Ibnul-Athir Al-Jazariy Izud-Din aliyefariki mwaka 360 A.H. Amesema ndani ya kitabu chake Al-Kamil fit-Tarikh kwenye mlango wa matukio ya mwaka 260 A.H. kuwa: “Ndani ya mwaka huo alifariki Abu Muhammad Al-Alawi Al-Askari, naye ni mmoja wa Maimamu kumi na wawili wa madhahebu ya Imamiyya, na yeye ndiye mzazi wa Muhammad ambaye wanamwamini kuwa ndiye anayengojewa.”2 2. Ibnu Khallakan aliyefariki mwaka 681 A.H. Amesema ndani ya kitabu Wafayatul-Aayan: “Abu Qasim Muhammad bin Hasan Al-Askari bin Ali Al-Hadiy bin Muhammad Al-Jawwad aliyetajwa kabla ni Imam wa kumi na mbili kwa mujibu wa imani ya Shia Imamiyya maarufu kwa sifa ya Hujah….mazazi yake yalikuwa siku ya Ijumaa nusu ya Shabani mwaka mia mbili hamsini na tano.” Kisha akanukuu kutoka kwa mwanahistoria Ar-Rahalah Ibnul-Azraqu Al-Fariqiy aliyefariki mwaka 577 A.H. kuwa amesema ndani ya kitabu Tarikh Mayyafariqina kuwa: “Hakika Hujjah aliyetajwa amezaliwa Mfunguo sita mwaka mia mbili hamsini na nane, na imesemekana kuwa ni mwezi nane Shabani mwaka hamsini na sita, na ndio kauli sahihi mno.”3 Nasema: Kauli sahihi kuhusu siku ya kuzaliwa kwake (a.s.) ni ile aliyoise- ma mwanzo Ibnu Khallakan, nayo ni siku ya ijumaa nusu ya mwezi wa Shaban mwaka mia mbili hamsini na tano, kauli hiyo wameafikiana Shia wote. Wametoa riwaya nyingi sahihi kuhusu hilo huku wanavyuoni wao waliotangulia wakithibitisha hilo, hakika Sheikh Al-Kulayni aliyeishi zama za ghaibu ndogo ameitoa tarehe hii kwa ukamilifu, kutoa kulikosal- imika na akaitanguliza kabla ya riwaya zinazoikhalifu tarehe hiyo. Amesema kwenye mlango unaohusu kuzaliwa kwake (a.s.): “Amezaliwa (a.s.) nusu ya Shaban mwaka mia mbili hamsini na tano.”4

Ufafanuzi

IMAM MAHDI NDANI YA RIWAYA ZA KISUNNI (UTANGULIZI)

IMAM MAHDI NDANI YA RIWAYA ZA KISUNNI (UTANGULIZI) IMAM MAHDI NDANI YA RIWAYA ZA KISUNNI UTANGULIZI Imani ya ulazima wa kudhihiri suluhisho la ulimwengu huu na kusimamisha dola yake ni imani isiyohusu watu wa dini tu, bali inayajumuisha hata makundi ya kitheolojia na kifilosofia yasiyokuwa ya kidini. Kwa mfano kundi la wapagani wajulikanao kwa jina la Al-Jadliyyah ambalo limefasiri historia kwa kigezo cha kutokuwepo uwiano kinaamini kuwa ipo siku iliyoahidiwa mpishano huo utatoweka na nafasi yake kuchukuliwa na uwiano na amani.1 Kama pia tunavyowakuta baadhi ya wanafikra wasiokuwa wanadini waki- amini ulazima huu, kwa mfano mwanafikra mashuhuri wa kiingereza Bertrand Russell anasema: “Hakika ulimwengu unalingojea suluhisho litakaloukusanya chini ya bendera moja na tamko moja.”2 Na kauli yenye maana hii hii ameisema mfizikia maarufu Albert Einstein kwa kusema: “Hakika haiko mbali siku ambayo ulimwengu wote utatawaliwa na amani na usafi na watu kuwa katika hali ya kupendana na undugu.”3 Ama mwanafikra wa kiayalandi Bernard Shaw yeye katamka wazi mno na kwa undani kuliko uwazi na undani wa hawa wiwili, katika kutoa wasifu wa suluhisho na kuelezea ulazima wa umri wake kuwa mrefu kabla ya kudhihiri kwake amesema: “Hakika yeye ni mwanadamu hai mwenye mwili wenye afya bora na nguvu ya kiakili isiyokuwa ya kawaida. Ni mwanadamu wa hali ya juu kiasi kwamba mwanadamu huyu wa chini anamfikia baada ya juhudi za muda mrefu. Na hakika umri wake utarefu- ka mpaka avuke miaka mia tatu, na anaweza kunufaika na yale aliyoyaku- sanya ndani ya muda wote wa uhai wake mrefu.”4 Ama upande wa dini za kimungu zenyewe zimeashiria ulazima wa kudhi- hiri suluhisho la ulimwengu, na atakayefuatilia utabiri wa kimungu ndani ya vitabu vya biblia atavikuta vinaelekeza kwa huyu Mahdi ambaye ndiye anaaminiwa na madhehebu ya Ahlul-Bayt (a.s.), kama ulivyothibitisha hilo uchambuzi mbalimbali unaohusu maelezo ya nukuu hizo za utabiri.5 Al-Qadhi As-Sabatwiy amezungumzia moja ya utabiri unaopatikana ndani ya kitabu cha Yoshua kutoka ndani ya Agano la kale ndani ya biblia unaoli- husu suluhisho la ulimwengu, akasema: “Maelezo haya yanamzungumzia Mahdi (a.s.).” Akaendelea mpaka akasema: “Shia Imamiyya wamesema: Yeye ndiye Muhammad bin Hasan Al-Askari ambaye alizaliwa mwaka mia mbili na hamsini na tano na mjakazi wa Hasani Al-Askari aitwaye Nargis huko Samrau zama za mtawala Al-Muutamid, kisha akaenda ghaibu muda wa mwaka mmoja6, kisha akadhihiri na kisha akaenda tena ghaibu na hiyo ndio ghaibu kubwa, na baada ya hapo harejei ila pindi Mwenyezi Mungu atakapotaka.

Ufafanuzi

KUTABIRIWA KWAKE NA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W)

KUTABIRIWA KWAKE NA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W) KUTABIRIWA KWAKE NA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W) Karibu katika vitabu vyote mashuhuri vya Hadithi za Mtukufu Mtume (s.a.w.) mna bishara zimhusuzo Imamu Mahdi na waandishi kadhaa; walikusanya hadithi zenye bishara hizo. Bwana Hafidh Muhammad-bin-Yusuf Shaffi katika kitabu chake kiitwacho "Al-Bayan-fi-Akhbar-i-Sahibiz-zaman". Bwana Hafidh Abu Na'im Isfahani amezikusanya hadithi hizi katika kitabu chake kiitwacho "dhikr Ni't Al-Mahdi", Bwana Abu Dawud Sajistani katika kitabu chake kiitwacho "Sunan" chini ya kichwa cha habari maalum cha "Al-Mahdi", Bwana Tirmidh katika kitabu chake kiitwacho "Sahih Tirmidhiy", Bwana Ibn Majah katika kitabu chake kiitwacho "Sunan Ibnu Maaja" na Bwana Hakim katika kitabu chake kiitwacho "Mustadrak" wameziandika hadithi kadha wa kadha kuhusu jambo hili, mojawapo ikiwa imesimuliwa na Bwana Ibn-i-Abbas, inasema kwamba, Mtukufu Mtume (s.a.w) alisema, "Mimi ni kiongozi wa Mitume na Ali ni kiongozi wa Mawalii. Wa kwanza katika Mawalii wangu kumi na mbili atakuwa Ali na wa mwisho ni Al-Mahdi (a.s.)". (2) Kutabiriwa kwake na Bibi Fatimah (a.s.) bint wa Mtukufu Mtume (s.a.w.): Kufuatana na hadithi katika kitabu kiitwacho "Usulil Kafi" cha Bwana Kulaini kimenukuu kua Jabir-bin-Abdullah Ansar alisema kwamba, Bibi Fatimah (a.s.) alikuwa na ubao ulioandikwa majina yote ya Mawalii na Maimamu na aliwataja Maimamu wote kumi na wawili kwa majina yao, watatu walikuwa wanaitwa Muhammad na wanne wanaitwa Ali na wa mwisho atakuwa wa kudumu.

Ufafanuzi

JE UNAMTAMBUA IMAMU MAHDI (A.S)

JE UNAMTAMBUA IMAMU MAHDI (A.S) JE UNAMTAMBUA IMAMU MAHDI (A.S) JINA NA UKOO WA IMAMU MAHDI (A.S) Alikuwa ni mwana wa Imamu Hasan Askari,ambaye ni Imamu wa kumi na moja miongoni mwa maimamu wanaotokana na ukoo wa Mtume (s.a.w.) naye ametokana na kizazi cha Husain (a.s.), aliyekuwa mwana wa Fatima (a.s.) binti wa Mtume (s.a.w.) na Bwana Ali (a.s.) binamu wa Fatima (a.s) (Imani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yao wote). Na Imamu Mahdi (a.s) mepewa jina Ia Mtukufu Mtume (s.a.w.) na ana umbo lifananalo na umbile la Mtume (s.a.w.w). Mama yake ni Bibi Nargis (Narcissus), mjukuu (atokanaye na binti) wa Mfalme wa Urumi na naye anatokana na kizazi cha Simon, mwanafunzi wa Nabii Issa (a.s.).

Ufafanuzi

UGHAIBU (KUTOWEKA) KWA IMAMU (A.S)

UGHAIBU (KUTOWEKA) KWA IMAMU (A.S) UGHAIBU (KUTOWEKA) KWA IMAMU (A.S) Muda wa kazi yake ya Uimamu umegawanyika katika sehemu mbili za Ughaibu. Moja inaitwa "Ghaibat-Sughra" (Ughaibu mfupi) na nyengine inaitwa "Ghaibati-i-Kubra" (Ughaibu mrefu). Yote hayo yamebashiriwa na dhuria wa Mtume (s.a.w.), kwa mfano: (i) Mtume (s.a.w.) amesema, "Yeye ataendelea katika ughaibu mrefu wakati watu wengi wataingia katika kiza". (ii) "Katika muda wa ughaibu wake, wale watakuobakia katika kuamini watakuwa wachache kama kibiriti". (iii) Ali (a.s.) alisema, "Wa mwisho wetu sisi atakuwa ghaibu kwa muda mrefu. Ninaona jinsi wakati ule marafiki zetu watakavyohangaika kama ng'ombe wafanyavyo wanapotafuta chakula. (iv) Mahala pengine Imamu Ali (a.s.) anasema, "Atadhihirika baada ya muda mrefu sana usiotambulika, wakati ambapo wenye imani ya kweli ndio watakaoweza kubakia na imani. UGHAIBU (KUTOWEKA) KWA IMAMU (A.S) Muda wa kazi yake ya Uimamu umegawanyika katika sehemu mbili za Ughaibu. Moja inaitwa "Ghaibat-Sughra" (Ughaibu mfupi) na nyengine inaitwa "Ghaibati-i-Kubra" (Ughaibu mrefu). Yote hayo yamebashiriwa na dhuria wa Mtume (s.a.w.), kwa mfano: (i) Mtume (s.a.w.) amesema, "Yeye ataendelea katika ughaibu mrefu wakati watu wengi wataingia katika kiza".

Ufafanuzi

KUZALIWA KWA IMAM MAHDI (A.S)

KUZALIWA KWA IMAM MAHDI (A.S) KUZALIWA KWAKE Wakati ukawadia na mnamo tarehe 15 Shaaban mwaka 255 Hijiriya katika Mji wa Samarraa (nchini Iraq) alizaliwa mtoto Mtukufu wakati wa usiku. Imamu Hasan Askari (a.s.) alitoa sadaka ya mikate mingi na nyama nyingi na akachinja mbuzi kadhaa wakati wa sherehe ya "Aqiqah” (kunyolewa kwa nywele za kichwa alizozaliwa nazo). KUKUA NA MALEZI Haikuwa kitu kipya kwa ukoo wa Mtume (s.a.w.) kwa watoto wao kutopata elimu ya nje. Ipo mifano mingine kabla ya 'Anayengojewa'. Kwa mfano, babu yake, Imamu Ali Naqi (a.s.) alikuwa na umri wa miaka sita na miezi michache tu alipofariki baba yake Imamu Muhammad Taqi (a.s.) ambaye yeye mwenyewe pia alikuwa na umri wa miaka minane tu alipofariki baba yake Imamu Ali Ridha (a.s.). Ni dhahiri kwamba, muda huo mfupi ukilinganishwa na desturi ya ukuaji wa watoto wa kawaida hautoshi kwa elimu ya nje. Lakini tunapokubali kwamba wamebarikiwa kwa baraka za Mwenyezi Mungu, basi swala la umri halitazingatiwa hata kidogo.

Ufafanuzi

UPELELEZI WA WATAWALA WA ZA ZAMA ZILE

UPELELEZI WA WATAWALA WA ZA ZAMA ZILE UPELELEZI WA WATAWALA ZA ZAMA ZILE Kama vile ambavyo Firauni aliposikia kwamba mtoto atazaliwa katika Mayahudi, atakayeangamiza utawala wake, hakuacha hata njia moja ya kujaribia kuzuia kuzaliwa kwa yule mtoto, na hata ikiwa mtoto huyo keshazaliwa, kujaribu kumwua, vile vile mtawala wa ukoo wa Bani Abbas alijua kwa njia ya hadithi za mara kwa mara zisimuliwazo kuwa atazaliwa mwana wa Imamu Hasan Askari (a.s.) atakayekuwa mwangamizaji wa serikali yake hiyo ovu. Hivyo, alijaribu kuzuia kuzaliwa kwa mtoto huyo na akamweka Imamu Hasan Askari (a.s.) katika kifungo cha maisha. Lakini, kama vile Nabii Musa (a.s.) alivyozaliwa Iicha ya juhudi zote za Firauni, vivyo hivyo, Imamu “anayengojewa” alikuja duniani. Na kuzaliwa kwake, kufuatana na Maamrisho ya Mwenyezi Mungu na Rehma Yake, kulikuwa siri.

Ufafanuzi

KUMUELEWA NA KUMTAMBUA IMAM

KUMUELEWA NA KUMTAMBUA IMAM MLANGO WA PILI KUMUELEWA NA KUMTAMBUA IMAM SEHEMU YA KWANZA. MTIZAMO KUHUSU IMAM MAHDI (A.S). Imam Mahdiy ni Imamu wa kumi na mbili na ni Imamu wa mwisho katika madhehebu ya mashia, Imam Mahdiy amezaliwa siku ya Ijumaa mwezi wa shabani katika mwaka 255 hijria Qamaria, (868 miyladiy) katika mmoja wa mitaa ya nchi ya Irak unaojulikana kwa jina la Samarraa. baba yake Imam Mahdiy anaitwa Imam Hassan Askariy, na yeye ni Imam wa kumi na Moja katika madhehebu ya mashia, mama yake Imam Mahdiy ambae ni mwanamke mtukufu katika historia ya kiislamu anaitwa bibi Nargis, ama kuhusu historia ya mwanamke huyo kuna hadithi mbali mbali zilizonakiliwa kuhusu mama huyo, kuna hadithi isemayo kwamba bibi Nargis ni mtoto wa (Yushuw), Yushuw ni mtoto wa mtawala wa Roma (yaani ni mtoto wa Mtawala wa nchi ya Urumi). Ama kuhusu mama yake inasemekana kwamba mama yake ni kutoka katika ukoo wa (Sham-uun) Sham-uun ni mrithi wa Nabii Issa (a.s) Kutokana na hadithi zilizonakiliwa imethibitishwa kwamba mama Nar-gis aliingia katika dini ya kiislamu, na Imam Askari (a.s) alimuongoa mwanamke huyo katika watekwa ambao walitekwa na Waislamu katika vita vilivyotokea baina ya jeshi la Roma na Waislamu, Imam Askari (a.s) alimtuma mtu ili kumnunua mwanamke huyo na baadae mtu huyo akampeleka bibi Nar-gis katika mtaa wa Samarraa. (rejea kitabu Kamalud Din juzuu ya 2, mlango wa 41, ukurasa wa 132). Na hadithi hiyo pia imenukuliwa katika kitabu cha (Biharul-an-war, juzuu ya 5. ukurasa wa 11 hadi ukurasa wa 22). Jambo lililo muhimu na linalofaa kuzingatiwa ni kwamba bibi Nar-gis amelelewa katika nyumba ya bibi (Hakima Khatun) bibi Khatuwn ni dada wa Imam Haadi(a.s) na mama huyo ni mwenye kuheshimiwa sana na Imam Haadi (a.s).

Ufafanuzi

SUALI KUHUSU MAHDI (A.S)

SUALI KUHUSU  MAHDI (A.S) SUALI KUHUSU  MAHDI (A.S) Hivi karibuni nilisoma kitabu kimoja kinachosema kuwa Imam Hassan Askari (AS) alibaidishwa na Mutawakil al-Abbasi na kupelekwa katika mji wa Samarra. Hatimaye alifungwa katika mojawapo ya jela za mji huo na kufia humohumo. Mwandishi wa kitabu hicho alisema, baada ya kufariki dunia Imam Hassan Askari, mwanawe aliyekuwa na umri wa miaka mitano ndiye aliyechukua nafasi ya uongozi wa umma wa Kiislamu. Baada ya kupewa jukumu hilo alienda katika mojawapo ya mapango ya karibu na kwamba hakuonekana tena baada ya hapo. Kitabu hicho kinasema kwamba, jambo hilo lilipelekea kutokea imani hii miongoni mwa Washia kwamba, mtoto huyo wa Imam Hassan Askari (AS), ndiye Imam Mahdi muahidiwa ambaye atadhihiri tena kwa lengo la kuleta uadilifu na usawa duniani baada ya kujaa dhulma na uonevu. Kitabu hicho kinasema kuwa, suala hilo ni bida'a katika Uslamu, kuendelea kudai kwamba suala hilo pia limeashiriwa katika dini za Kizartoshti na Kikristo, na kwamba, ni aina moja ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu katika dini tukufu ya Kiislamu. Kwa hivyo, nielezeni ukweli wa jambo hili.- Abdulrahiim Musa Dungu wa Mtwara Tanzania.

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini