Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

Imam Ali (a.s)

UTHIBITISHO NA USHAHIDI

UTHIBITISHO NA USHAHIDI

UTHIBITISHO NA USHAHIDI KWAMBA IMAM ALI (A.S) NI KHALIFA WA KWANZA Ni ukweli unaoeleweka wazi duniani kote kwamba kama unataka kumshawishi mtu kuuendea ukweli wa imani yako, na ikiwa mtu mwenyewe hakubaliani na imani yako, inabidi utumie mantiki (busara) na umtolee dalili kwa kupitia vitabu vyake yeye mwenyewe anavyovikubali. Kwa mfano kama unataka kumshawishi Mkristo juu ya Utume wa Nabii Muhammad (s.a.w.w) inabidi umshawishi kwa kutumia ushahidi ulio katika kitabu chake anachokiamini : Biblia Takatifu. Halikadhalika tutatoa ushahidi kuthibitisha kuwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) alimteua Imam Ali (a.s) kwa amri ya Allah (s.w.t) kuwa wasii wake, kutoka katika Qur'an Tukufu na vitabu vya Tafsiir, vitabu vya Siirah, vitabu vya Tarikh (Historia), na vitabu vya Hadithi vilivyoandikwa na Maulamaa wa Kisunni wao wenyewe. USHAHIDI JUU YA UIMAMU WA ALI (A.S) 1- Hadithul Indhaar au Da'wat Dhul Ashirah. Katika miaka ya mwanzo ya kuutangaza Uislamu, ndipo iliposhuka aya hii: "WA ANDHIR ASHIIRATAKAL AQRABIIN" - "Na waonye jamaa zako wa karibu (As-Shu'araa 26:214), Mtume Muhammad (s.a.w.w) alimwita Imam Ali (a.s.) na akamwambia: "Ewe Ali, Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameniamrisha kuwaita jamaa (ndugu) zangu wa karibu, hivyo niitie watoto wa Abdul Muttalib na tuandalie chakula kutokana na nyama ya kondoo na maziwa".

Ufafanuzi

USHAHIDI NA UTHIBITISHO KWA KUPITIA QURAN

USHAHIDI NA UTHIBITISHO KWA KUPITIA QURAN USHAHIDI NA UTHIBITISHO KWA KUPITIA QURAN Ayatul Wilayah ni aya nyingine ya Qur'an inayothibitisha Ukhalifa wa Ali bin Abitalib (a.s), Aya hii ipo katika Suratul Maidah (5:55) ambayo inasema: "Walii wenu ni Allah, Mtume wake na waumini wanaosimamisha sala na wanaotoa zakat huku wakiwa katika hali ya rukuu". Maulamaa wote wa Tafsiir na Hadith, wa Kishia na Kisunni, wanakubali kwamba aya hii iliteremka kwa ajili ya Imam Ali bin AbiiTaalib (a.s), baadhi ya maelezo ya wasimuliaji wa hadithi wa upande wa Kisunni ni kama ifuatayo: A - Suyuti amesimulia katika tafsiir yake katika kitabu chake Tafsiir Durrul Manthur kwamba Ali bin AbiiTalib alitoa pete yake sadaka na kummpa masikini alipokuwa katika sala akirukuu; hivyo Allah akateremsha Aya hii ya Al maaida (5:55). B - Mwanazuoni wa Kisuni Tabrani katika kitabu chake "Awsat" amesimulia kuwa: "Siku moja maskini mmoja alisimama pembeni ya Ali ambaye alikuwa katika sala akirukuu (Sunnah) na akaomba chochote, hivyo Ali akampa pete yake kutoka kidole chake alipokuwa katika Rukuu. Mtume (s.a.w.w) alipokuja msikitini Imam Ali alimuarifu Mtume juu ya tukio hilo na hapo hapo ikashuka aya ya Suratul Maaida (5:55).

Ufafanuzi

VIPI QURANI NA WATU WA NYUMBA YA MTUME

VIPI QURANI NA WATU WA NYUMBA YA MTUME VIPI QURANI NA WATU WA NYUMBA YA MTUME WANALIANGALIA SUALA LA UONGOZI KWA NINI SHIA WANAAMINI KUA IMAM ALI (A.S) NI KHALIFA WA KWANZA BAADA YA MTUME? Shia Ithna Ashariya wanaamini kua Imam Ali bin Abitalib ni Khalifa na Imam wa kwanza baada ya Mtume (S.A.W.W) kwa kuzingatia sababu moja rahisi sana na iliyo wazi. Sababu hii ni kuwa; "Imam Ali bin Abii Taalib (A.S) aliteuliwa kwa amri ya Mwenyezi Mungu kua Khalifa wa kwanza wa Waislamu na Mtume mwenyewe kwa amri ya Mwenyezi Mungu (s.w. t). Hii ndio sababu na hakuna sababu nyengine. Katika Qur'an tukufu (59: 7) Mwenyezi Mungu anasema: "…….Na anachokupeni Mtume basi pokeeni na anachokukatazeni jiepusheni nacho". Qur'an (33:36): "Na haiwi kwa Muumini wa kiume wala kwa Muumini wa kike, pale Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapokata shauri, waumini hao wawe ni wenye kuyatenda mambo yao kwa rai zao au wawe chaguo katika kuyatenda yale waalioamrishwa. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hakika amepotea upotevu ulio wazi"'. Shia wanaamini kwamba maadamu Mtume (S.A.W.W) mwenyewe kwa amri ya Mwenyezi Mungu alimteua Imam Ali (a.s) kuwa Khalifa, basi Waislamu hawana hiari yoyote isipokuwa kuitii amri hii.

Ufafanuzi

USHAHIDI NA UTHIBITISHO

USHAHIDI NA UTHIBITISHO 3 USHAHIDI NA UTHIBITISHO KWA KUPITIA  HADITH AL-MANZILAH Wanazuoni wote wa Kishia na Kisunni wanakubali juu ya usahihi wa hadithi hii. Mtume Muhammad (S.A.W.W) alipokwenda katika vita vya Tabuk katika mwaka wa 9 Hijria, alimuacha Imam Ali kua Khalifa wake katika mji Madina, Tabuk (katika mpaka wa Syria) ilikuwa ni mbali sana na Mtume alipaswa kumuacha mtu madhubuti na mwenye imani kubwa ili kuulinda mji mkuu wa Dola ya Kiislamu Madina kutokana na uovu wa washirikina, na hususan wanafiki ambao walikuwa wanasubiri wapate nafasi japo ndogo ili walete mtafaruku Madina. Hivyo Mtume alimteua Imam Ali ili awe Khalifa wake katika kipindi hiki ambapo Mtume alikuwa safarini, Wanafiki walianza kumchokoza Imam Ali kuwa hakwenda Jihad ili kuokoa maisha yake na kwamba alikuwa anaogopa kifo. Imam Ali hakufurahia maneno haya, hivyo alikwenda kwa Mtume kumuomba aende naye vitani (Jihad), Mtume alijibu kwa haikuwa vizuri kwake yeye Mtume kuondoka bila kumteua Ali kama Khalifa wake, pale Madina. Kisha alisema: "AMAA TARDHAA AN TAKUUNA MINNI BI MANZILATI HAARUNA MIN MUSA, ILLAA ANNAHUU LAA NABIYYA BA'DII" - "Je hauridhiki kwamba wewe kwangu una nafasi kama ile aliyokuwa nayo Haruni kwa Musa, isipokuwa tu hakuna Mtume baada yangu?" Hadithi hii inathibitisha waziwazi kuwa nafasi ya Ali ni sawa na ile ya Haruni. Sasa tujiulize ni ipi ilikuwa nafasi ya Haruni ? Hebu tuiangalie nafasi ya Haruni katika Qur'an Tukufu. "Na nipatie Waziri kutoka katika familia yangu, Harun ndugu, na niongezee nguvu kupitia kwake na mfanye awe mshirika katika kazi yangu" (Taha 20:29-32).

Ufafanuzi

UKHALIFA

UKHALIFA UKHALIFA JAWABU KWA SHEIKH MAZRUI Baada ya kifo cha mtume Suala la Ukhalifa ni suala nyeti sana, sina budi kabla ya kumjibu Bwana Juma Mazrui niwaletee habari muhimu zilizotokea kabla ya tukio la Ukkhalifa na kama zilivyoelezwa na Hadithi sahihi na masimlizi ya Historia katika Vitabu tunavyovitegemea: Sina budi kumshukuru Bwana Juma Mazrui kwa jitihada zake za kutaka kuwaelewesha watu kuwa Seyyidna Ali hakuwa Khalifawa Kwanza wa Waisilamu, pia nawaomba wasomaji pia wawe na subira katika kusikiliza Upande wa pili wa maoni ya Waisilamu Huru usiotaka kushutumu yo yote kati ya Shia na Sunni juu ya suala hili. Kwanza kabisa, Mtume Muhammad alikufa mwaka 632 AD, alikufa kutokana na ahadi yake kufika na baada ya kupewa sumu kule Khaybar baada ya kuiteka ngome ya wayahudi wa Khaybar. Mtume Muhammad (s) baada ya ushindi wake dhidi ya Mayahudi wa Khaybar alikubaliana nao na kuwapa sharti ya kulipa jizya, walilipa nusu ya mazao wanayovuna hapo Khaybar kwa Dola ya Kiislamu ya Madina. Baada ya kufa kwa Mtume Muhammad (s) mayahudi waliobakia Khaybar waliondolewa na kufukuzwa kutoka madina na Khalifa wa pili Omar Bin al-Khattab ®. Tukirudi nyuma kwenye ushindi wa Mtume juu ya Mayahudi wa Khaybar na sababu ya kifo chake, tunasoma katika Historia kuwa, mwanamke wa kiyahudi alitayarisha chakula na kumkaribisha Mtume (s) ambaye hakujuwa kuwa ndani yake mlikuwa na sumu na akafa baada ya miaka mitatu tangu kula kwa sumu hiyo!

Ufafanuzi

UKHALIFA WA IMAMU ALI (A.S)

UKHALIFA WA IMAMU ALI (A.S) UKHALIFA WA IMAMU ALI (A.S) Tofauti kubwa iliyopo baina ya Waislamu wa Kishia na Waislamu wa Kisunni ni juu ya imani ya Ukhalifa na Uimamu baada ya kuondoka kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SA.W.W). Sisi waislamu wa Kishia tunaamini kuwa Imam Ali bin Abi Talib (a.s) ni khalifa na ni Imam wa kwanza baada ya Mtume (S.A.W.W) ambapo ndugu zetu Waislamu wa Kisunni wanaamini kwamba Seyidina Abubakar ( r.a.) alikuwa ni khalifa wa kwanza. Ingawa kuna tofauti nyingine ndogo ndogo zilizopo baina ya madhehebu makubwa ya Uislamu (Shia na Sunni) kwa mfano katika sheria (Fiqh) kama vile kukunja mikono wakati wa kusali au kuinyoosha n.k. lakini hizi ni tofauti ndogo ndogo sana ambazo zinaweza hata kupatikana ndani ya madhehebu manne ya Kisunni (Imam Shafi, Maliki, Hanafi na Hanbali ).

Ufafanuzi

IMAMU ALI (A.S) KATIKA MTAZAMO WA WASIOKUA WAISLAMU

IMAMU ALI (A.S) KATIKA MTAZAMO WA WASIOKUA WAISLAMU BSMILAHI AR-RAHMANI AR-RAHIIMI IMAMU ALI (A.S) KATIKA MTAZAMO WA WASIOKUA WAISLAMU Washington Irving (1783-1859) Aalijulikana kama "The first American man of letters": "Ali alikuwa anatokana na tawi lenye heshima kuu katika matawi ya kikureishi. Alikuwa na sifa tatu zilizokuwa zikitukuzwa sana kwa waarabu: Ujasiri, ufasaha na ukarimu. Moyo wake usio na hofu ulimpatia sifa kutoka kwa Mtume ya kuwa simba wa Mungu, mifano ya ufasaha wake imebaki katika baadhi ya semi na kuhifadhiwa miongoni mwa waarabu; na ukarimu wake ulionekana dhahiri katika kupenda kwake kugawanya na watu, kila siku ya ijumaa, kile kilichobaki katika hazina. Kuhusu utukufu wake, tumetoa mifano mara kwa mara; utukufu wake ulichukia kila kitu chenye udanganyifu na uchoyo." [Lives of the Successors of Mahomet, London, 1850, Uk. 165]" "Yeye alikuwa ni mmoja wa miongoni mwa wa mwisho na wenye thamani miongoni mwa waislamu wa kale, ambaye alikusanya nguvu ya kidini kwa ushindi akiwa na Mtume mwenyewe, na kufuata ruwaza ya mwisho kabisa ya Mtume Muhammad. Yeye ni mtu anayetajwa kwa heshima kama khalifa wa kwanza aliye kirimu na kulinda elimu. Alikuwa ndani ya mashairi yeye mwenyewe, na nyingi miongoni mwa methali na semi zake zimehifadhiwa na kufasiriwa katika lugha mbalimbali. Pete lake ulikuwa na maandishi hili: 'Ufalme ni wa Mwenyezi Mungu'. Moja katika semi zake inaonyesha jinsi alivyokuwa hathamini vivutio vinavyopita tu vya dunia, ni (kusema kwake): 'Maisha ni kivuli tu cha mawingu - ndoto ya mwenye kulala.'"

Ufafanuzi

ALI BIN ABII TAALIB (A.S)

ALI BIN ABII TAALIB (A.S) ALI BIN ABII TAALIB (A.S) IMAMU ALI KATIKA KATIKA KALAMU ZA MADHEHEBU YA AHLU SUNNA WAL-JAMAA ALI BIN ABU TALIB (RA) KHALIFA WA NNE ALIYEONGOKA Babu Yake Abdul Muttalib bin Hashim alikuwa mkuu wa kabila la Kikureshi, mbora wao na kiongozi wao wanayemtii. Sifa zake zilienea katika eneo lote la jangwa la (Bara ya) Arabuni kuanzia Kaskazini mpaka Kusini yake. Wote walikuwa wakimheshimu na wakijua kuwa yeye ndiye aliyekichimba kisima cha maji ya Zamzam kwa mikono yake. Kisima kinachoendelea kutowa maji yenye baraka mpaka wakati wetu huu. Majeshi ya Abraha Mhabeshi yalipotaka kuibomoa Al Kaaba, Abdul Muttalib alitambua kuwa hana uwezo wa kupambana nayo. Aliwataka watu wake wauhame mji na kupanda juu ya majabali. Akawakusanya kondoo zake na kuondoka nao huku akimuomba Mola wake Mtukufu ailinde nyumba Yake hiyo ya Al Kaaba. Alipoulizwa kwa nini anakimbia pamoja na wanyama wake na kuiacha Al Kaaba bila ulinzi, Abdul Muttalib alijibu: "Lilbayti rabbun yah-miyhi", maana yake; "Nyumba ina Mola wake mlezi mwenye kuilinda". Alifurahi kupita kiasi alipoletewa bishara njema ya kuzaliwa kwa mjukuu wake Muhammad bin Abdillahi bin Abdul Muttalib (SAW). Akambeba kwa mikono yake miwili na kukimbia naye mpaka ndani ya msikiti wa Al Kaaba huku akimuomba Mwenyezi Mungu na kumshukuru akisema;

Ufafanuzi

GHADIR KHUM

GHADIR KHUM GHADIR KHUM Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei alipo kutana na maelfu ya wananchi wa matabaka mbalimbali waliokwenda kuonana naye kwa mnasaba wa sikukuu ya Ghadiri Khum (siku Imam Ali bin Abi Twalib alipotawazwa rasmi na Mtume wa Mwenyezi Mungu kuwa Imam na kiongozi wa umma wa Kiislamu baadaye yake) alisema kuwa suala la Ghadir ni kigezo cha milele cha Mwenyezi Mungu kinachoainisha njia sahihi ya umma wa Kiislamu. Ayatullah Khamenei aliashiria urongo mkubwa unaoenezwa na Wazayuni na nchi za kigeni kuhusu kadhia ya nyuklia ya Iran kwa shabaha ya kupotosha fikra za walimwengu na akasema kuwa urongo huo utawafedhehesha zaidi maadui wa taifa la Iran baada ya kudhihiri ukweli wa mambo. Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amewapongeza wananchi wa Iran na Waislamu wote ulimwenguni kwa mnasaba wa sikukuu ya Ghadir. Akifafanua sababu ya sikukuu hiyo kuitwa sikukuu kubwa zaidi ya Mwenyezi Mungu (Idullahil Akbar), Ayatullah Khamenei amesema, tukio la Ghadiri Khum lilikuwa na maana kubwa zaidi kuliko idi na sikukuu nyingine za Kiislamu, kwani kwa mujibu wa vigezo vya Mwenyezi Mungu, wajibu wa Waislamu kuhusu uongozi na serikali uliainishwa katika siku hiyo.

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini