Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

utafiti mbali mbali

DUA KUMAYL

DUA KUMAYL

DUA KUMAYL Dua ni ulingano ambapo mja hudhihirisha ufukara, unyonge na udhaifu wake kwa Mola Mkwasi, Mwenye kumiliki kila kitu. Mja huinyosha mikono yake mitupu kwa unyenyekevu na unyonge, na kutaka msaada kutoka kwa Mkamilifu Muumba Mwenye uweza juu ya kila kitu, Mwingi wa huruma na ukarimu, Mwenye busara Mjuzi kwa kila jambo, Mwenye kusikia maombi ya kila anaemuomba. Dua ni lugha ya mapenzi na ni chimbuko la mahaba ya mja kwa Mola wake na ndiyo taa ya waliyokizani na ni tulizo la wanaohangaika. Twasoma katika Qur'ani tukufu:- "Asema Mola wenu: niombani nitawajibu, hakika wale wajivunao kufanya ibada yangu, bila shaka wataingia Jahannamu, wadhalilike” (Al-Mu'minuun 60).

Ufafanuzi

SALA NA ATHARI ZAKE

SALA NA ATHARI ZAKE SALA NA ATHARI ZAKE 17. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Man la Yahdhurul Faqihi, J.1, Uk. 206: “Mtu yeyote aichukuliaye sala pasi na uzito wake, basi hatokani nami. Hapana, Kwa kiapo cha Allah swt, mtu kama huyo hatafikia chemchemi ya Haudh Kawthar” 18. Amesema Al-Imam Ja’far as-Sadiq a.s., katika Bihar al-Anwaar, Juzuu 82, Ukurasa 236: “Iwapo kutakuwapo na mto unaopita nyumbani mwa mtu ambamo mtu huyo anaoga mara tano kwa siku, je kutabakiapo aina yoyote ya uchafu mwilini mwake ? Kwa hivyo sala ndivyo ilivyo mfano wa mto huo. Mtu ambaye anasali sala zake basi hujiondolea madhambi yake yote isipokuwa kutabakia madhambi yale ambayo yanamtoa katika Imani yake. 19. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., katika Bihar-ul-Anwaar, J.99, Uk. 14: “Sala iliyofaradhishwa kwa Allah swt ni sawa na kutimiza Hajj elfu moja na ‘Umrah elfu moja ambazo ni sahihi na zilizokubalika.” 20. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., katika Bihar-al-Anwaar, J.83, Uk. 14: “Kamwe musizipoteze sala zenu, kwa hakika, mtu yeyote anayezipoteza nyakati za sala zake atainuliwa pamoja na Qarun na Hamaan na itamwia haki Allah swt awatumbukize katika moto wa Jahannam pamoja na Munafiqiin (wanafiki). 21. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Bihar-ul Anwaar, Juzuu 69, Uk. 408: “Musali sala zenu kama kwamba hiyo ndiyo sala yenu ya mwisho” 22. Amesema Amir-ul-Muminiin Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. Tasnif-I-Gurar ul-Hikam, Uk.175: “Iwapo mwenye kusali angalikuwa akifahamu kiasi alichozungukwa na rehema za Allah swt, basi kamwe asingaliinua kichwa chake kutoka hali ya kusujudu” 23. Amesema Al-Imam Al-Muhammad al-Baqir a.s., katika Bihar al-Anwaar, J.7, Uk. 267: “Siku ya Qiyama, jambo la kwanza litakalo hisabiwa ni kuhusu sala; kwa hivyo, iwapo itakuwa imekubaliwa, basi matendo mengine pia yatakuwa yamekubaliwa (ama sivyo matendo yake mengine mema hayatamnusuru)”.

Ufafanuzi

HISTORIA YA UANDISHI WA HADITH KATIKA SUNNI

HISTORIA YA UANDISHI WA HADITH KATIKA SUNNI HISTORIA YA UANDISHI WA HADITH KATIKA SUNNI Kazi zote zilizopo hadi leo zinazohusu Hadith zilikuwa zimekusanywa katika kipindi cha karne 2 A.H./8 A.D. au katika karne ya 3 A.H./9 A.D. Historia inatuonyesha kuwa katika kukaribia karne ya 2 A.H. kulitokezea idadi ndogo ya Muhaddithun ambao walianza kuziandika Hadith, ingawaje hazikuwa na mpangilio. Baadaye mkusanyiko huu mdogo ulikuwa kiini cha kazi zote kubwa. Hata hivyo wingi wa Hadith zilizopo sasa kwa kukusanywa, zilienezwa kwa desturi ya kutamkwa (kusemwa), na wakati zilipokuja kuandikwa vitabuni, zilikuwa hazikuwahi kuandikwa popote kabla yake. Ucheleweshwaji katika kuandikwa kwa Hadith ni swala mojawapo muhimu katika historia ya Hadith. Umuhimu wake ni wa ukweli kwamba kucheleweshwa huu kuliathiri hasa kuhusu utunzi na idadi ya Hadith pamoja na uwepesi wao wa kuzushwa (zikaongezwa na kupunguzwa na hatimaye zikawa ni zile zilizo na uongo) na matatizo mengi mengineyo yanayohusiana. Jambo la umuhimu katika swala hili linawahusu wale ambao ndio waliokuwa wamesababisha ucheleweshwaji huo wa kuandikwa kwa Hadith. Mwelekeo wao ulikuja kama ni mfano kwa ajili ya wengine katika kutoziandika Hadith. Katika sehemu yetu hii, tutaweza kuchambua makusudio yao na athari za mwenendo wao wa aina hiyo juu ya Hadith. Kila kinachoweza kukusanywa kwa shida katika Historia ni kwamba baadhi ya Makhalifa walizuia uandikaji wa Hadith kwa sababu fulani fulani. Baada yao kikundi cha Sahaba na Tabiun waliwafuata katika swala hili. Kwa mujibu wa msemo "Watu hufuata dini ya wafalme wao," wao walijiepusha na uandikaji wa Hadith kwa kukubali na kuridhia kwa kuharamishwa hivyo.

Ufafanuzi

MASHIA NA UANDISHI WA HADITH

MASHIA NA UANDISHI WA HADITH MASHIA NA UANDISHI WA HADITH Katika sehemu hii, twategemea kuzungumzia kwa mukhtasari msimamo wa Shia kuhusu uandikaji wa Hadith kutokea mwanzoni. Itaonekana kuwa ni kinyume na msimamo wa wengine kuhusu swala hili. Msimamo wa Kishia ulisisitiza mno juu ya uandikaji wa Hadith zikisaidia uhifadhi wake wakati ambapo Maulamaa mashuhuri wa Kisunni, hata kufikia mwanzoni mwa karne ya 3A.H./9 A.D. walikuwa wakipinga uandikaji wa Hadith. Ni baada ya uandikaji wa Hadith ulipokuwa dhahiri hao wanaopinga walipoanza kwenda kinyume na Hadith walizokuwa wamezitoa wakipinga uandishi na uenezaji wake na hapo wakaanza kuziandika. Alba ibn al-Ahmad ananakili kuwa mara moja ‘Ali ibn Abi Talib a.s. wakati akitoa Hotuba juu ya mimbar, alibainisha: "Je, ni nani atakayeinunua elimu kwa Dirhamu moja?" Al-Harith ibn al-A’war alinunua karatasi yenye thamani ya Dirhamu moja na kumwijia Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. na kuandika kiasi cha kutosha cha elimu juu yake.1 Riwaya hii inatuonyesha vile Imam a.s. alivyokuwa akisisitiza juu ya uandikaji.

Ufafanuzi

MAIMAMU WA SHIA KATIKA UANDIKAJI NA UENEZAJI WA HADITH

MAIMAMU WA SHIA KATIKA UANDIKAJI NA UENEZAJI WA HADITH MAIMAMU WA SHIA KATIKA UANDIKAJI NA UENEZAJI WA HADITH Katika sehemu hii, twategemea kuzungumzia kwa mukhtasari msimamo wa Shia kuhusu uandikaji wa Hadith kutokea mwanzoni. Itaonekana kuwa ni kinyume na msimamo wa wengine kuhusu swala hili. Msimamo wa Kishia ulisisitiza mno juu ya uandikaji wa Hadith zikisaidia uhifadhi wake wakati ambapo Maulamaa mashuhuri wa Kisunni, hata kufikia mwanzoni mwa karne ya 3A.H./9 A.D. walikuwa wakipinga uandikaji wa Hadith. Ni baada ya uandikaji wa Hadith ulipokuwa dhahiri hao wanaopinga walipoanza kwenda kinyume na Hadith walizokuwa wamezitoa wakipinga uandishi na uenezaji wake na hapo wakaanza kuziandika. Alba ibn al-Ahmad ananakili kuwa mara moja ‘Ali ibn Abi Talib a.s. wakati akitoa Hotuba juu ya mimbar, alibainisha: "Je, ni nani atakayeinunua elimu kwa Dirhamu moja?" Al-Harith ibn al-A’war alinunua karatasi yenye thamani ya Dirhamu moja na kumwijia Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. na kuandika kiasi cha kutosha cha elimu juu yake.1 Riwaya hii inatuonyesha vile Imam a.s. alivyokuwa akisisitiza juu ya uandikaji.

Ufafanuzi

WATU WA 'UKHDUD' (MAHANDAKI)

WATU WA 'UKHDUD' (MAHANDAKI) WATU WA 'UKHDUD' (MAHANDAKI) Qurani Tukufu inatuambia: Sura Al-Buruj, 85, Ayah ya 4 - 9. Kuwa walioangamizwa walikuwa watu wa mahandaki. Ya Moto wenye kuni. Walipokuwa wamekaa hapo. Wakitazama yale waliyokuwa wakiwatendea waumini. Wao waliwatesa (hao) si kwa kingine ila hao walimwamini Allah, Mwenye kushinda (na) Mwenye kusifiwa. Ambaye ni Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi; na Allah ni Mwenye kuona kila kitu. Imam wa tano, Muhammad ibni-'Ali Al-Baquir a.s. anasema kuwa siku moja Imam wa kwanza, Imam 'Ali ibni Abi Talib a.s. alimtuma mtu kwenda kwa wakuu wa dini ya Wakristo wa Najran kwa kuwauliza kuhusu watu wa Mahandaki --- na baada ya kupata majibu yao, aliwatumia ujumbe kuwa: "Kile mukihadithiacho kuhusu watu hao, si hadithi ya kweli na kwa hakika hadithi ya kweli ni kama ifuatavyo." Zu Nuwas alikuwa ni mfalme wa mwisho wa kabila la Hamir mwishoni mwa karne ya sita A.D. Yeye alikuwa ni mfuasii wa dini ya Juda ( dini ya Kiyahudi) na hivyo ilikuwa ndiyo dini ya Serikali. Dini hiyo ya Juda ilikuwa imeachwa na watu baada ya kuja Mtume 'Isa a.s. Lakini Zu Nuwas aliendelea kuwaadhibu vikali mno wale wote walioifuata dini ya Mtume 'Isa a.s. na alitumia mbinu mbalimbali na hila za kuimaliza dini hiyo katika kila sehemu za ardhi. Yeye alikuwa akiwapendelea mno Mayahudi na kuwatesa vikali mno Wakristo. Yeye aliwateketeza Wakristo popote pale walipoonekana katika ufalme wake. Yeye alikuwa ameamua kuusambaza Uyahudi katika kila sehemu za dunia hii huku akizimaliza na kuzifyeka dini zingine zote. Yeye hakubakiza juhudi zake zozote katika kufikia lengo lake hilo. Yeye vile vile alikuwa akizishambulia nchi zozote zile ambazo zilikuwa zikifuata dini mbali na dini ya Juda. Na vile vile alikuwa mwepesi wa kuzishambulia sehemu zozote zile zilizokuwa zikifuata dini mbali na dini ya Juda na hatimaye kuwalazimisha kuifuata dini yake.

Ufafanuzi

SUALA LA KUPOTOSHWA QURANI

SUALA LA KUPOTOSHWA QURANI SUALA LA KUPOTOSHWA QURANI Swali: Ni vipi kuhusu zile Hadith zisemazo kwamba baadhi ya Aya si sehemu ya Qur'an? Shia hawaamini kwamba mwandishi au mpokezi ana kinga ya kutofanya makosa, na kwa hivyo hawachukulii kwamba Hadith zote ni sahihi. Kitabu pekee chenye kinga ya kutokuwa na kosa lolote ni Qur'an. Mara nyingi Hadith hizi huchukuliwa kuwa ni dhaifu au maneno uliyo teremshwa nje ya Qur'an. " Ni vizuri itajwe kwamba kuna baadhi ya Hadith kwenye Sahih al-Bukhari na Sahih Muslim zisemazo kwamba Aya nyingi za Qur'an haziko. [Al-Bukhari, Al-Sahih, Juz. 8 Uk. 208; Muslim, Al-Sahih, Juz. 3 Uk. 1317]. " Si hivyo tu, Hadith hizi za Sunni zadai kwamba Sura mbili za Qur'an hazipo, ambapo mojawapo ni kama ya Sura ya al-Bara'ah (Sura ya 9) kwa kirefu!!! [Muslim, Al-Sahih, Kitab al-Zakat, Juz. 2 Uk. 726]. " Hata kuna baadhi ya mapokezi ya Hadith ya Sunni yanayodai kuwa Sura ya al-Ahzab (33) ilikuwa ni ndefu kama ilivyo Sura ya al-Baqarah (2)!!! Ambapo hakika Sura ya al-Baqarah ndio Sura iliyo kubwa zaidi katika Qur'an. Kuna hata Hadith ndani ya Sahih al-Bukhari na Muslim ambazo zimetaja kwa urefu baadhi ya Aya ambazo hazipo. [Al-Bukhari, Al-Sahih, Juz. 8 Uk. 208].

Ufafanuzi

MAFUNZO YA QURANI

MAFUNZO YA QURANI MAFUNZO YA QURANI  Njia , haja na sababu za mabadiliko katika jamii KWA mujibu wa Qur-an zipo sababu kadhaa ambazo huchochea mabadiliko makubwa katika jamii. Miongoni mwa hizo kuu zimetajwa kuwa ni: (1). Kushitadi kwa maovu, dhulma na ukandamizaji (2) Watu wanaoamrisha mema na kukataza mabaya (3) Kutetea na kulinda maadili mema (4) Migongano na migogoro(conflicts) kati ya makundi yenye nguvu katika jamii; moja likitaka kuondoa lingine ili kuondoa au kupunguza dhulma na ukandamizaji. 1. Kushitadi kwa maovu, dhulma na ukandamizaji Kushitadi kwa maovu, ufisadi, ukandamizaji na dhulma ni sababu ya kwanza inayoweza kuchochea mabadiliko. "Hakika Firauni alitakabari katika ardhi, akawafanya watu wa huko makundi mbali mbali. Akalidhoofisha kundi moja miongoni mwao, akiwachinja watoto wao wanaume na kuwaacha hai watoto wao wanawake. Hakika yeye alikuwa miongoni mwa waharibifu(kabisa).Na tukawafanyia ihsani wale waliodhoofishwa katika ardhi hiyo na kuwafanya viongozi, na kuwafanya warithi(wa neema hizo).

Ufafanuzi

AINA ZA DHULMA NDANI YA QURANI.

AINA ZA DHULMA NDANI YA QURANI. AINA ZA DHULMA NDANI YA QURANI. Maana ya dhulma ni kuweka kitu si katika pahala pake. Na dhulma ziko aina mbalimbali. Kwa mfano Shirki yaani kumshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu na kitu kingine ni dhulma kwa sababu mambo yanayohusu Uungu yote ni haki ya Mwenyezi Mungu S.W.T. peke Yake. Atakayejaalia kitu kingine sawasawa na Mwenyezi Mungu Mtukufu atakuwa ameweka jambo si katika mahali pake. Na atakuwa amefanya mshirika katika sifa za Uungu Ambaye hashirikiyani na yeyote yule. Na kwa kuwa jambo linalohusu haki ya Mola Muumbaji wa kila kitu huwa dhulma yake ni zaidi kuliko dhulma za aina nyingine.

Ufafanuzi

KUMJUA MUNGU KUPITIA QURAN

KUMJUA MUNGU KUPITIA QURAN KUMJUA MUNGU KUPITIA QURANI Njia ya kumjua Mwenyezi Mungu katika mtazamo wa Qur'ani Mtoto mdogo anayeyashika maziwa au matiti ya mama yake kwa mikono yake, hunyonya matiti hayo kwa lengo la kupata maziwa. Bila shaka huwa anataka maziwa, na anapokichukua kitu chochte kwa mikono yake kwa lengo la kukila basi bila shaka atakielekeza katika mdomo wake. Lengo laki halisi ni kula. Iwapo atapata kuwa kitu alichokichukua hakiliki basi hukitupilia mbali. Kwa njia hiyo hiyo mwanadamu hutafuta ukweli na hakika katika kila kitendo anachokifanya. Anapopata kuwa amekosea huumia na kujuta kwa nini alijisumbua bure na kukosea katika kitendo hicho. Daima mwanadamu hujiepusha na makosa na hujaribu kuufikia ukweli na hakika, kadiri ya uwezo wake. Jambo hili linaweka wazi nukta hii kwamba, kimaumbile na kihisia mwanadamu ni mkweli. Yaani atake au asitake, daima hutafuta ukweli na kufuata haki. Mwanadamu hakufunzwa jambo hili na mtu yoyote wala kutoka sehemu yoyote ile. Iwapo mara nyingine mwanadamu hukana na kukataa haki, huwa ni kwa sababu amechanganyikiwa kutokana na makosa na kutotofautisha kati ya haki na batili na iwapo haki itambainikia, basi bila shaka hawezi kufuata batili.

Ufafanuzi

KWA NINI IMAM HUSEIN (A.S) ALISIMAMA DHIDI YA UONGZI WA YAZIDI ?

KWA NINI IMAM HUSEIN (A.S) ALISIMAMA DHIDI YA UONGZI WA YAZIDI ? Tungetaka kuchukuwa fursa hii kujaribu kutazama katika baadhi ya maswali ambayo watu wengi hujiuliza kuhusu tukio la Karbala na hususan  msimamo wa Imam Hussein(as) kuhusu hali ilivyokuwa wakati huo mpaka ikambidi achukuwe msimamo aliyouchukuwa

Ufafanuzi

UISLAMU CHANGUO LANGU (61)

UISLAMU CHANGUO LANGU (61) Hamjambo wapenzi wasomaji na karibuni kujiunga  nami katika makala hii ambayo huangazia watu ambao baada ya kufanya utafiti wa kina huamua kufuata njia iliyojaa nuru maishani, yaani Uislamu. Karibuni kujiunga nami hadi mwisho.

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini