Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

MAKALA MBALIMBALI

WATU WA SABT

WATU WA SABT

WATU WA SABT Qurani Tukufu inatuambia: Sura Al-Aaraf, 7, Ayah ya 163 & 164. Na waulizeni habari za mji ambao ulikuwa kando ya bahari, (watu wa mji huo) walipokuuwa wakivunja (sheria ya) Jumamosi (ambayo waliambiwa wasifanye kazi katika sikuu hiyo, wafanye ibada tu. Na kazi yao ilikuwa uvuvi). Samaki wao walipowajia juu juu siku za Jumamosi zao; na siku isiyokuwa Jumamosi hawakuwa wakiwajia (hivyo). Basi namna hivyo tuliwatia mtihani kwa sababu ya kuasi kwao. Na (wakumbushe wakati) baadhi ya watu katika wao waliposema (kuwaonya waliovunja hishima ya Jumamosi kwa kuvua, na hali yakuwa wamekatazwa; waliposema): "Pana faida gani kuwaonya watu ambao Allah swt atawaua au atawaadhibu kwa adhabu kali ( papa hapa)?" Wakasema:"Tupate kuwa na udhuru mbele ya Mola wenu (kuwa tumewaonya lakini hatukusikilizwa) na huenda wakaogopa." Mtume Musa mwana wa Imran aliwahubiri wana wa Isra'il kuwa wawe na siku moja maalum katika juma kwa ajili ya kumwabudu Allah swt ili wao wasijishughulishe na kazi zinginezo mbali na ibada ikiwemo kuuza na kununua bidhaa za aina zote.

Ufafanuzi

TASHAHHUD

TASHAHHUD TASHAHHUD Tashahhud (Tahiyatu) : Baaa ya sijda ya pili ukae na usome: Ash- hadu al laa ilaaha illallaahu wahdahu laa shariika lah, wa ash- hadu anna Muhammadan `abduhu wa rasuluh Allaahumma swalli `alaa Muhammadin wa Aali Muhammad Nashuhudia kwa hapana Mola ila Allah, aliye wa pekee asiye na mshirika. Na nashuhudia kwamba Muhammad ni mja na mtume wake. Ewe Mola, mtakie rehma Muhammad na Aali zake. Ikiwa unaswali Swala ya Al-Fajr (Alfajiri), wacha mengine na uende kwenye maelezo ya sehemu ya Mwisho. Ikiwa unaswali Swala ya Dhuhr (Adhuhuri), ya`Asr (Alasiri), ya Maghrib (Magharibi), au ya`Isha (Usiku), endelea kwa kusimama kwa rakaa ya tatu huku ukisoma Bihawlillahi…kama ilivyoelezwa kwenye mwisho wa sehemu ya Rakaa ya kwanza. Rakaa ya tatu At-Tasbihat ul-Arba`ah (Tasbihi nne) : baada ya kuinuka na kusimama wima, hapo, aidha utasoma Surat al-Fatiha, au utasoma al-Tasbihat ul-Arba`ah mara tatu, kama ifuatavyo: Subhaanallaahi wa'l hamdu lillaahi wa laa ilaaha illallaahu wallaahu akbar Utakatifu ni wa Mwenyezi Mungu, Shukrani zote ni za Mwenyezi mungu; hapana Mola apasaye kuabudiwa ila Allah, naya ni Mkuu. Utarukuu, simama kwa muda mfupi, kisha utasujudu. Hii ni kama ilivyoelezwa katika sehemu ya maelezo ya Rakaa ya kwanza. Ikiwa unaswali Swala ya Maghrib (Magharibi), utasoma Tashahhud baadaye. Kasha wacha mengine na uende kwenye maelezo ya sehemu ya Mwisho.

Ufafanuzi

HABARI ZA WAOVU

HABARI ZA WAOVU HABARI ZA WAOVU AYA YA 34 KATIKA QUR'AN, YA SUURATUN-NAML, INASEMA: 34. (Malkia) akasema:Hakika wafalime wanapouingia mji,wanauharibu na wanawafanya watukufu wake kuwa dhalili hivyo ndivyo wanavyofanya . Iliposema:"Hakika wafalme wanapouingia mji,wanauharibu na wanawafanya watukufu wake kuwa dhalili" Tunapozungumzia juu ya Watawala,ni muhimu kutaja ijapokuwa kwa ufupi yaliyotokea huko nyuma katika miaka ya arobaini Hijria. Historia makini kabisa,inatwambia kwamba: Muawia alipoandaa kumpeleka Mughira bin Shuuba kuwa gavana wake katika mkoa wa Kuufa,mwaka wa arobaini na moja Hijria

Ufafanuzi

KUBADILISHWA KIBLA

KUBADILISHWA KIBLA KUBADILISHWA KIBLA Kubadilishwa kibla cha Waislamu kutoka Beitul Muqaddas kuelekea Makka. Katika kipindi cha miaka 13 ya kubaathiwa na Mwenyezi Mungu mjini Makka na miezi kadhaa tokea ahajiri mjini Madina, Mtume Mtukufu (saw) alikuwa akifanya ibada zake pamoja na wafuasi wake wakiwa wameelekea Beitul Muqaddas. Hili ni eneo ambalo alizaliwa Nabii Isah (as) na kituo muhimu cha Mayahudi na Wakristo. Hii ni katika hali ambayo watu wa Makka katika zama hizo waliipa Kaaba umuhimu mkubwa na kuifanya kuwa kituo cha kuabudia masanamu yao. Lakini wakati Mtume Mtukufu (saw), alipowasili mjini Madina na kuanza kutekeleza ibada zake akiwa ameelekea upande wa Beitul Muqaddas, Mayahudi waliokuwa wakiishi mjini hapo walianza kulalamika na kueneza propaganda nyingi dhidi ya Waislamu wakidai kwamba hatua yao hiyo ilikuwa ni dalili ya wazi ya kuthibitisha kwamba hawakuwa huru wala kujitawala na kwamba jambo hilo lilithibitisha kuwa Mayahudi ndio waliokuwa kwenye njia sahihi na ya haki. Jambo hilo lilichukuliwa na Mayahudi kuwa kisingizio kizuri cha kuwakejeli na kuwaudhi Waislamu wakiongozwa na Mtume Muhammad (saw).

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini