Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

MAKALA MBALIMBALI

RAMADHANI NA UTULIVU WA MOYO

RAMADHANI NA UTULIVU WA MOYO

RAMADHANI NA UTULIVU WA MOYO Wataalamu wa masuala ya nafsi au wanasaikolojia wanasema: "Sisi wanaadamu katika uwepo wetu,  tuna uwezo mkubwa wa kupokea mapenzi na mahaba na iwapo moja ya hilo litatoweka, tutahisi tumekosa kitu na hivyo kuingiwa na wasiwasi. Nukta muhimu zaidi ya uwezo huu wa mahaba ni mapenzi kwa Mwenyezi Mungu ambayo hutupatia hisia chanya na utulivu. Kwa hakika utulivu ni nukta muhimu sana katika maisha ya mwanadamu kwa kadiri kwamba tunaweza kusema kuwa, sababu kuu ya jitihada za mwanadamu ni kufikia utulivu. Wengi hutafuta mali na utajiri ili wapate utulivu. Kwa mfano kununua nyumba au ardhi hufanyika kwa ajili ya kufikia utulivu. Wengi hutafuta maisha ya kifahari ili wapate utulivu na pia kuna wengi ambao humuabudu Mwenyezi Mungu ili waweze kupata utulivu. Lakini kati ya yote hayo tuliyoyataja ni lipi lenye kumletea mwanadamu utulivu wa kudumu?" Erich Seligmann Fromm, mwanasaikolojia wa Ujeurmani anaandika hivi : "Tujaalie kuwa, maisha ya kimaada na kuishi maisha bora ni mambo ambayo huandamana na furaha na utulivu.  Uzalisahji usio na mipaka , uhuru usio na mipaka na ustawi wa kustaajibisha ni mambo yanayoweza kuifanya dunia iwe ni pepo na kuifanya ichukue sehemu ya pepo iliyoahidiwa. Lakini ukweli ni kuwa, katika zama zetu hizi za kiviwanda, mwanadamu amegonga mwamba katika kufikia malengo yake makubwa, Mwanadamu ametambua kuwa, kupata anasa kupita kiasi hakuwezi kumdhaminia utulivu na furaha." Naye Albert Schweitze, tabibu Mjerumani ambaye mwaka 1952 alipata Tuzo ya Amani ya Nobel wakati alipokuwa akipokea zawadi hiyo aliwahutubu walimwengu kwa kusema: "Mwanadamu amekuwa mtu mwenye uwezo wa kupita kiasi. Lakini mtu huyu mwenye uwezo wa kupita kiasi hajaweza kufikia hekima na fikra ya juu. Kadiri ambavyo uwezo wa mwanadamu unavyozidi kuongozeka, anazidi kudhoofika na kudhoofika zaidi na hili ni jambo linalopaswa kututikisa nafsi zetu."

Ufafanuzi

MWALIKO WA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI

MWALIKO WA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI MWALIKO WA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI Tuko katika siku tukufu za ibada ya funga ya mwezi wa Ramadhani na sote tumealikwa kuwa wageni wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Mtu anapoalikwa kwenye karamu au shughuli yoyote ya ugeni, hali hiyo humsisimua na kumfanya awe ni mwenye furaha wakati wote hadi wakati wa kushiriki karamu au ugeni huo. Sote tunajua ya kwamba jambo linalomfanya mwalikwa kuwa na furaha hiyo ni ile hamu ya kutaka kukutana na mwenyeji wake pamoja na wageni wengine walioalikwa kwenye karamu hiyo ambapo mazingira mapya ya kuonana na kujuliana hali wageni hujitokeza, mapenzi na upendo kudhihirishwa na wakati mwingine zawadi kutolewa na mwenyeji wao. Kabla ya kushiriki kwenye mwaliko, jambo la kwanza ambalo mwalikwa hukabiliana nalo ni jinsi atakavyovalia vizuri, kutembea vizuri na kuzungumza vizuri. Tunapofahamu kuwa mwenyeji wetu atakuwa anatusubiri mlangoni kwa ajili ya kutulaki, hapo kasi ya hatua hatua zetu kumuelekea huongezeka. Mwanzo wa kila mwaliko huwa ni kuzingatia na kufungamana kimawazo na mwenyeji, ambapo kila mara mfungamano huo unapokuwa ni wa kirafiki zaidi, ugeni nao hunoga na kuvutia zaidi. Hivi sasa na kwa mara nyingine tumealikwa na mwenyeji ambaye ni rafiki mwema wa kuvutia, mwenye huruma na anayesamehe zaidi kati ya wenyeji wengine wote tunaowajua sisi wanadamu. Mwenyezi Mungu ni Muumba wa pekee na Mwenye Hekima ambaye jina lake hutuliza nyoyo zinazosononeka na kutaabika.

Ufafanuzi

FALSAFA NA HEKIMA YA FUNGA

FALSAFA NA HEKIMA YA FUNGA  MAMBO YA KUJICHUNGA KATIKA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI FALSAFA NA HEKIMA YA FUNGA Kuhusu falsafa na hekima ya funga au saumu, yamezungumzwa mengi ndani ya Qur’ani tukufu, Hadithi pamoja na kauli za maulamaa wa dini. Katika kubainisha hukumu ya kufaradhishwa na kuwajibishwa kufunga, Qur’ani tukufu imeitaja taqwa na uchaMungu kuwa moja ya hekima za kufaradhishwa amali hiyo tukufu. Aya ya 183 ya Suratul Baqarah inasema: Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama walivyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamungu. Funga ni moja ya amali bora kabisa za kumwezesha muumini kudhibiti ghariza za kihayawani na kuhuisha moyo wa uchaji Mungu ndani ya nafsi yake. Kama ilivyoelezwa katika Hadithi ni kwamba: “Funga ni ngao (ya Moto wa Jahannamu)”. Yaani mtu atanusurika na kuokoka na Moto wa Jahannamu kutokana na kufunga. Na sababu ni kuwa, kutokana na t’aa, ibada anazofanya mtu na kuzidhibiti na kuzidhoofisha hawaa na matamanio ya nafsi hatimaye huweza kumdhibiti na kumshinda shetani wa ndani na nje ya nafsi yake. Na ni kutokana na hayo ndipo Bwana Mtume Muhammad SAW akasema: “Ndani ya mwezi huu mashetani hufungwa pingu na minyororo, basi mwombeni Mwenyezi Mungu asiwasalitishe juu yenu”.

Ufafanuzi

FUNGA YA RAMADHAN, HUKUMU, FADHILA, ADABU ZAKE

FUNGA YA RAMADHAN, HUKUMU, FADHILA, ADABU ZAKE FUNGA YA RAMADHAN, HUKUMU, FADHILA, ADABU ZAKE UTANGULIZI Sifa zote njema zinamstahikia Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) na sala na salamu zimfikie Mtume wake (Swalla Allahu alayhi Wasallam) pamoja na ndugu na maswahaba zake. Baada ya kumshukuru  Allah (Subhaanahu Wata’ala)  na kumtakia rehma na amani Mtume Muhammad (Swalla Allahu alayhi Wasallam) pamoja na ndugu zake na maswahaba zake wote, basi kwa hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu (Subhaanahu Wata’ala)  amejaalia kwa waja wake  miongo [misimu] ya kuzidisha ndani yake matendo mema  na Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala)  huzidisha pia malipo ya matendo hayo kwa waja wake, na miongoni mwa miongo hiyo ni huu  mwezi mtukufu wa Ramadhani. Basi katika makala haya nitaelezea kwa ufupi juu ya funga na yale yanayoambatana nayo ikiwa ni pamoja na  hukumu, fadhila na adabu zake. Ninamwomba Allah (Subhaanahu wa Ta’ala)  awanufaishe Waislamu kwa yale nitakayoyaelezea, na aturuzuku ikh-laswi [kutaka radhi zake pekee] katika matendo yetu yote,  amiiin. Kwake pekee ndiyo kwenye mafanikio ya dunia na akhera.

Ufafanuzi

FUNGA YA RAMADHAN, HUKUMU, FADHILA, ADABU ZAKE

FUNGA YA RAMADHAN, HUKUMU, FADHILA, ADABU ZAKE FUNGA YA RAMADHAN, HUKUMU, FADHILA, ADABU ZAKE UTANGULIZI Sifa zote njema zinamstahikia Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) na sala na salamu zimfikie Mtume wake (Swalla Allahu alayhi Wasallam) pamoja na ndugu na maswahaba zake. Baada ya kumshukuru  Allah (Subhaanahu Wata’ala)  na kumtakia rehma na amani Mtume Muhammad (Swalla Allahu alayhi Wasallam) pamoja na ndugu zake na maswahaba zake wote, basi kwa hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu (Subhaanahu Wata’ala)  amejaalia kwa waja wake  miongo [misimu] ya kuzidisha ndani yake matendo mema  na Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala)  huzidisha pia malipo ya matendo hayo kwa waja wake, na miongoni mwa miongo hiyo ni huu  mwezi mtukufu wa Ramadhani. Basi katika makala haya nitaelezea kwa ufupi juu ya funga na yale yanayoambatana nayo ikiwa ni pamoja na  hukumu, fadhila na adabu zake. Ninamwomba Allah (Subhaanahu wa Ta’ala)  awanufaishe Waislamu kwa yale nitakayoyaelezea, na aturuzuku ikh-laswi [kutaka radhi zake pekee] katika matendo yetu yote,  amiiin. Kwake pekee ndiyo kwenye mafanikio ya dunia na akhera.

Ufafanuzi

HOTUBA YA MTUME KUHUSU MWEZI WA RAMADHANI

HOTUBA YA MTUME  KUHUSU MWEZI WA RAMADHANI HOTUBA YA MTUME  KUHUSU MWEZI WA RAMADHANI wasomi wa Hadithi wamenakiliwa kutoka kwa Mtukufu Mtume Muhammadi (s.aw.w) kuwa: ilipokaribia Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Mtukufu Mtume aliwahutubia Maswaha wake kuhusu Mwezi huo, na akawazungumzi na kuwafafanulia mambo mbali mbali kuhusiana na mwezi huu mtukufu. kuanzia fadhila zake, na ni mambo gani wanapaswa kuzingatia ndani ya mwezi huu mtukufu. miongoni mwa mambo muhimu aliyazungumzia mtukufu huyo juu ya mwezi huu wa ramadhani, ilikuwa ni kuwafuturisha watu hata kwa kuwapa maji au tende moja, lakini pia kuwatanabahisha kuwa: muovo ni ambae atakakosa kughufuriwa madhambi yake katika mwezi huu, na kwamba wanapaswa kujua kuwa: huu ni mwezi ambao watu wamealikwa katika dhifa ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, hivyo hatupaswi kuip[oteza fursa hii, kwani kwa mwaka hutufikia mara moja tu. mtkufu msomaji ili kuipata hotuba kamili ya mtukufu Mtume (s.a.w.w) aliitoa kuhusu mwezi Mtukufu wa Radhani, nakuomba ungana nami katika makala hii maalumu juu ya hotuba hiyo mpaka tamati.  

Ufafanuzi

YESU (A.S)

YESU (A.S) YESU (A.S) YESU - NABII ALIYETOKA NAZARETI MTUMISHI WA MUNGU Masih hataona uvunjifu kuwa mtumwa wa Mwenyezi Mungu.(Qur'ani) An Nisaa 4.172 Biblia inahakikisha ukweli huu wa Qur'ani. Mara nyingi tunaona Yesu anatafakhari kujitangaza kuwa yeye ametumwa na Mungu, na mara nyingi anaitwa "mtumishi wa Mungu". Katika Injili ya Yohana mathalan tunasoma: Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye. Yohana 17.3-4 Kwa unyenyekevu wa safi ya niya Yesu anamkhatibu Mola wake, "Mungu wa pekee wa kweli", siye mungu wa uwongo miongoni wa miungu ya uwongo uwongo iliyokuwa ikiabudiwa na makafiri. Ajuulikane Mwenyezi Mungu na kadhaalika ajuulikane yeye Yesu Kristo, Mtume na mtumishi wa Mwenyezi Mungu. Katika kitabu cha Matendo ya Mitume kiliomo katika Agano Jipya la Biblia tunasoma: Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili kuwabarikia kwa kumwepusha kila mmoja wenu na maovu yake. Matendo 3.26

Ufafanuzi

KIFO MSALABANI

KIFO MSALABANI KIFO MSALABANI Mtume Muhammad ndiye aliyekuja kumtukuza Yesu. Aliyapinga madai ya Mayahudi kumshutumu Maryam na kumshutumu Yesu, na akauhakikisha ulimwengu kuwa Yesu ni mwana wa halali, ni Nabii mtukufu aliyetumwa kwa Wana wa Israili, wala si maluuni kama walivyodai Mayahudi, na wala si mungu wa bandia wa kishirikina, kama walivyomfanya Wakristo bila ya wenyewe kutambua nini walitendalo. Kwa watu wanaoamini kuwa Adam alikuwa hana baba wala mama kwa nini ikawa ni vigumu kuamini kuwa Yesu alikuwa hana baba? Yohana Mbatizaji anasema: Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimu watoto. Mathayo 3.9 Je, Mungu awezaye kuinua watoto katika mawe, kama alivyomuumba Adam kutokana na udongo, atashindwa kumzalisha mwanamke bila ya mume? Mtume Muhammad aliwahakikishia maadui wa Kiyahudi kuwa Yesu ndiye Kristo, ndiye Masihi ambaye amebashiriwa katika maandiko yao wenyewe. Aliwakanya Mayahudi walipodai kuwa Yesu amelaanika kwa sababu wao waliweza kumuua kwa kumbandika msalabani. Qur'ani imesema: Hali hawakumuua wala hawakumsalibu, bali walifananishiwa. Na kwa hakika wale waliokhitilafiana katika haya wamo katika shaka nayo. Wao hawana yakini juu yake, isipokuwa wanafuata dhana tu. Na hawakumuua kwa yakini.

Ufafanuzi

Majibu kwa bwana Juma Mazrui

Majibu kwa bwana Juma Mazrui MAJIBU KWA BWANA JUMA MAZRUI Allah amesema: "Ewe Mtume, fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako; na kama hutafanya, basi hujafikisha ujumbe wake, na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu". (Qur'an: 5, 67) Shia wanaamini kwamba agizo lililotajwa na Aya hiyo ya Qur'an lilitekelezwa na Mtume (s.a.w.w.) alipomteua Imam 'Ali bin Abi Talib (a.s.) kuwa wasii wake kwenye siku ya Ghadir Khumm. Aliposikia majibu haya, yule mtu aligeuka na kumuelekea ngamia wake huku akisema: "Ee Mwenyezi Mungu! Ikiwa haya ayasemayo Muhammad ni sahihi, basi tuteremshie jiwe kutoka mbinguni na utuadhibu vikali." Basi mtu huyo kabla hajamfikia ngamia wake, Mwenyezi Mungu alimteremshia jiwe lililomwingia mwilini mwake kupitia kichwani kwake na kumwacha akiwa amekufa. Ilikuwa katika tukio hili ndipo Mwenyezi Mungu Mtukufu alipoteremsha Aya ifuatayo: Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayotokea. Juu ya Makafiri - ambayo hapana awezaye kuzuia. Kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye utukufu mkubwa. (Qur'an 70:1-3) Je Wanavyuoni wa Sunni hulichukulia tukio hili kuwa ni la kweli? Idadi kubwa ya Wanavyuoni wa Sunni waliosimulia tukio hili, kwa urefu na kwa muhtasari, ni ya kushangaza! Tukio hili la kihistoria limesimuliwa na Maswahaba wa Mtume 110, pia Tabiina (waliokuwako baada ya Maswahaba) wapatao 84, na Wanavyuoni wengi wa ulimwengu wa Kiislamu, kutoka karne ya 1 AH hadi karne ya 14 AH (Karne ya saba hadi ya ishirini CE). Takwimu hizi ni zile tu za wapokezi waliotajwa katika Hadith zilizopokewa na Wanavyuoni wa Sunni!

Ufafanuzi

DINI YA AHMADIA

DINI YA AHMADIA DINI YA AHMADIA Mapenzi juu ya Mohammad (SAW) ni mali adhimu ya kila muislamu yeyote. Ambaye hana chembe ya mapenzi katika moyo wake imani yake sio kamili. Muumini wa kweli ni yule ambaye humtambua Mtukufu Mtume Mohammad (SAW) kuwa ni bora kuliko maisha yake, watoto wake, wazazi wake na hata mali yake yote iliyopo duniani. Ni kwa kuwa na mapenzi makubwa kwa Mtume (SAW) ambayo hata mja asiyemcha Mungu hatavumilia shutuma yeyote kwa Mtume (SAW). Hali hiyo imefikia kwamba kila wakati Rajpal anaposema maneno mabaya dhidi ya mtume basi Ghazi Alan hufa shahiid kwa ajili ya Mtume wake. Makafiri daima wamekuwa wakiwalinda wahuni wamtukanao mtume. Salman Rushdi na mwanamama Tasleema Nasrin ni mfano wa waandishi waliolindwa na makafiri baada ya kudhihirisha chuki zao kwa Mtume (SAW). Mirza Ghulam Ahmad Qadiani Mwanzilishi wa jumuia ya Ahmadiyya ni mtu mmoja aliyeshamiri chini ya usimamizi na huruma ya Raj wa kiingereza huko India. Maisha yake yote yalitumika katika kuendeleza maslahi ya mabwana zake hali ya kufanya kufuru dhidi ya Mtume Mtukufu (SAW) na Ahlibait na maswahaba wake na mitume wote wengine. Maandishi yake yanatoa ushahidi ulio wazi ya kufuru yake hiyo.

Ufafanuzi

SHIA ISMAILIYYAH

SHIA ISMAILIYYAH SHIA ISMAILIYYAH ONGEZA MAARIFA YAKO!!! JE, UNAFAHAMU MADHEHEBU YA SHIA ISMAILIYA? Nalo ni kundi la Kiislamu ambalo linaamini Uimamu wa Maimamu sita (6) watoharifu (a.s) (yaani kuanzia Imam Ali (a.s) hadi Imam Jaafar Swadiq (a.s), kisha wanaacha Uimamu na Imam Musa Al-Kadhim (a.s) na badala yake wanaamini Uimamu wa ndugu yake (Al-Kadhim) aitwaye Ismail bin Jaafar Al-Swadiq (a.s). ISMAIL: Na wameitwa "Maismailiyyah" kwa kujinasibisha na "Ismail" Bin Jaafar As-Swadiq (a.s), naye alikuwa ni mtoto wa kwanza wa Imam Jaafar, Imam alikuwa akimpenda sana, mpaka watu wakadhani kuwa yeye ndiye atakuwa Imam baada ya baba yake, lakini alikufa na kuzikwa Baqii, Madinah. Na baba yake ( yaani Imam Jaafar (a.s) alimuhuzunikia sana na akalitangulia jeneza lake, akiwa miguu peku na bila kuvaa joho, na akawa akiamrisha walitue jeneza lake chini kabla ya kumzika, na alikuwa akifunua uso wake na kumuangalia, ili kuwasisitizia watu kufa kwake, ili isije dhaniwa kuwa huyu ndiye Khalifa. Lakini pamoja na mambo yote hayo, bado Maismailiyyah waliendelea kuamini kuwa yeye ndiye Imam. Nao wametofautiana kuhusu kifo cha Ismail. Katika uhai wa baba yake; basi wakawa katika makundi tofauti yafuatayo: (A) Kundi linalosema kuwa Ismail hakufa, bali baba yake alidhihirisha kwamba amekufa kwa kuogopa na kujiepusha na wale watawala waovu; na wakadai kwamba hatokufa mpaka aitawale dunia na kuijaza uadilifu, kwa sababu yeye ndiye Al-Qaim (Al-Mahdi). (B) Na kundi lingine lililokiri kufa kwa Ismail kabla ya baba yake, lakini linasema kuwa Ismaili ndiye ambaye aliyeelezea kuhusu Uimamu wa mwanae" MUHAMMAD." (C) Na kundi la tatu limekubali pia kuwa alikufa kabla ya baba yake, na wakadai kuwa Imam Jaafar Swadiq alikuwa amekwisha elezea Uimamu wake (Ismail), hapo ikimaanisha kwamba Uimamu utahamia kwa kizazi chake (Ismaili hata kama yeye mwenye hatotawala kama Imam).

Ufafanuzi

GHADIR KHUM

GHADIR KHUM GHADIR KHUM Kumetokea nini katika siku ya Ghadir Khum? Ghadir Khum ni sehemu iliyoko maili kadhaa kutoka Makka katika njia inayoelekea Madina. Wakati Mtume (s.a.w) alipopita sehemu hiyo tarehe 18 Dhul'Hijja (10 March 632) wakati anarudi kutoka Hijja yake ya mwago, aya, "Ewe Mtume fikisha uliyoteremshiwa…." Iliteremshwa, kwa hiyo alisimama ili kutangaza kwa mahujaji ambao alifuatana nao kutoka Makka na ambao walikuwa watawanyike njia panda hapo kila mtu kuelekea sehemu yake. Kwa amri ya Mtume (s.a.w) mimbari maalum ilitengenezwa kwa kutumia matandiko ya ngamia kwa ajili yake. Baada ya Salat ya mchana Mtume .(s.a.w) alipanda mimbari na akatoa Khutuba yake ya mwisho mbele ya mkusanyiko mkubwa kabla ya kifo chake miezi mitatu baadae. Sehemu ya kuvutia ya Khutuba yake, ni pake alipomchukuwa 'Ali (a.s) kwa mkono wake, Mtume s.a.w. aliwauliza wafuasi wake iwapo yeye ana mamlaka zaidi (awla) kwa waumini kuliko wao wenyewe. Kundi kubwa lile la watu likaitikia kwa sauti kubwa "Hivyo ndivyo ilivyo , Ewe Mtume wa Allah". Kisha akatangaza: "Yule ambaye kwamba mimi ni (mawla) mwenye kumtawalia mambo yake, huyu Ali vile vile ni (mawla) mwenye mkumtawalia mambo yake. Ewe Allah, kuwa rafiki kwa yule ambaye ni rafiki, na uwe adui kwa yule ambaye ni adui kwake." Mara tu baada ya Mtume (s.a.w) kumaliza khutuba yake, aya ifuatayo iliteremshwa: "………. Leo nimekukamilishieni dini yenu, na kuwakamilishieni yangu kwenu, na nimewaridhieni kwamba Uislamu ndiyo dini yenu." (Q:5:3) Baada ya Khutuba yake Mtume (s.a.w) alimtaka kila mtu kula kiapo cha utii kwa 'Ali (a.s) na kumpongeza. Miongoni mwa waliofanya hivyo ni Umar bin al-Khattab, ambaye alisema: "Hongera Ali Ibn Abi Talib! Leo umekuwa bwana wa waumini wote wanaume na wanawake."

Ufafanuzi

NENO SHIA

NENO SHIA NENO SHIA Lakini vipi Mtume (s.a.w.w.) atumie neno la kuleta mgawanyiko? Je Nabii Ibrahim alikuwa ni wa ki-madhehebu? Vipi kuhusu Nabii Nuh na Nabii Musa? Ikiwa neno Shi'ah ni la kuleta mgawanyiko au la ki-madhehebu, basi Mwenyezi Mungu asingelilitumia kwa Mitume wake wenye daraja ya juu, na wala Mtume Muhammad (s.a.w.w.) asingeliwatukuza. Ni lazima isisitizwe kwamba Mtume Muhammad (s.a.w.w.) hakutaka kuwagawaya Waislamu kwa makundi. Bali aliwaamuru watu wote wamfuate Imam Ali (a.s.) akiwa ni mwakilishi wake wakati alipokuwa hai, na akiwa ni mrithi na khalifa wake baada yake. Lakini kwa bahati mbaya waliokubali kufuata matakwa yake walikuwa ni wachache, na walijulikana kama "Shi'ah wa Ali". Walipatwa na kila aina ya ubaguzi na mateso, na waliteseka kuanzia ile siku aliyofariki rehma ya umma, Mtume Muhammad (s.a.w.w.). Lau Waislamu wote wangelitii na kufuata vile Mtume (s.a.w.w.) alivyotaka, kusingelikuwa na makundi au madhehebu ndani ya Uislamu.

Ufafanuzi

SHIA NA SWAHABA

SHIA NA SWAHABA MTIZAMO WASHIA KWA MASWAHABA Wasomi wa Sunni wanautumia mfano huu hasa wa swahaba fasiki (fasiq) Walid kuruhusu kuswalishwa na mtenda dhambi wa dhahiri!! " 'Ali al-Qari al-Harawi al-Hanafi, Sharh Fiqh al-Akbar, chini ya Sura 'Inaruhusiwa kswalishwa na mtu mwema au muovu', Uk. 90 " Ibn Taymiyyah, Majmu' Fatawa, (Riyadh, 1381), Juz. 3, Uk. 281 Lakini kwa nini 'tusisahau yaliyopita?' Wakati tunapoyataja makosa ya maswahaba kama huyu Walid, si kwa sababu ya nia mbaya ya kutaka kusengenya tu, bali ni kwa sababu Waislamu wanahitajika wawe waangalifu sana juu ya wapi wanapopata habari zao kuhusiana na mafunzo ya kiislamu na sunnah za Mtume (s.a.w.w.). Na hii itaweza kupatikana tu kwa kuyaangalia kwa makini sana maisha ya maswahaba wote wa Mtume (s.a.w.w.), na kuziacha tabia zao zenyewe ziseme juu ya maadili na uaminifu wao. Isitoshe, Mtume (s.a.w.w.) tayari ameshatuonya kwamba: " "Nitafika kwenye hodhi (birika) kabla yenu, na atakayepita kwangu atakunywa hapo, na atakayekunywa katika hilo hatahisi kiu. Na watakuja kwangu watu niwajuao na wanijuao, lakini nitatengwa nao, kisha nitasema, 'maswahaba wangu'. Na hapo jibu litakuja, 'Wewe hujui hao walifanya nini baada yako.' Kisha nitasema, 'Basi niwe mbali nao hao waliobadilika baada yangu.'" [Sahih al-Bukhari (Tafsiri ya kiingereza), Juz 8, Kitabu 76, Namba 585]

Ufafanuzi

UISLAMU KATIKA NDIMI ZA WAMAGHARIBI

UISLAMU KATIKA NDIMI ZA WAMAGHARIBI UISLAMU KATIKA NDIMI ZA WAMAGHARIBI Sarojini Naidu (1879-1949) Mwanamke huyu ni Mwandishi, Mshairi, ambaye pia alikuwa ni mmoja mwa viongozi mashuhuri India kabla ya uhuru. Rais wa chama cha Indian National Congress na ni Gavana wa kwanza mwanamke baada ya India kupata uhuru. Amesema: " "Uadilifu ni moja kati ya maadili mazuri zaidi ya Uislamu, kwa kuwa nisomapo Qur'an nakuta kwamba misingi hii maisha, si nadharia tu bali ni maadili hasa ya kivitendo katika maisha ya kila siku yanayofaa kwa ulimwengu mzima." " "Ilikuwa ni dini ya kwanza iliyohubiri na kutekeleza kwa vitendo demokrasia, kwani kunapoadhiniwa na waaabuduo wanapokusanyika, ndipo demokrasia ya kiislamu inapodhihirika mara tano kwa siku, pale mfalme na mkulima wanapoinama bega kwa bega na kusema: "Mwenyezi Mungu pekee ndiye Mkuu." Nimekuwa nikiathiriwa mara kwa mara na umoja huu wa kiislamu usiogawanyika unaomfanya mtu moja kwa moja kumpenda mwingine na kumfanya kuwa nduguye."

Ufafanuzi

DALILI YA UIMAM.

DALILI YA UIMAM. DALILI YA UIMAM. Bila shaka Mwanadamu ni moja wapo ya viumbe vya Mwenyeezi Mungu (s.w),ikiwa hili litakuwa wazi kwa kila mtu kwamba mwanadamu naye ni kiumbe wa Mwenyeezi Mungu (s.w), basi hakutakuwa na ubishi juu ya kauli hii kwamba:(Naye analazimika kufuata nji hiyo hiyo ya kuongozwa ili kulifikia lengo maalum la kuumbwa kwake ambalo ni: Ukamilifu na saada.) Kwa kuwa Mwenyeezi Ndiye mwenye kumuongoza mwanadamu ili kuufikia ukamilifu huo na saada,ukamilifu huo mwanadamu ataweza kuufikia kupitia njia aliyoiweka Mwenyeezi Mungu (s.w) kuelekea ukamilifu wa mwanadamu na Saada hiyo.Hivyo yeye ndiye atakayechagua kiongozi wa kuwaongoza wanadamu,hakuna mtu atakuwa na jukumu hili la kumchagua kiongozi ili kuwaongoza wanadamu kwani njia ya kuufikia ukamilifu na saada haijui ispokuwa yule aliyemuumba mwanadamu na anayemjua mwanadamu kwa maana nzima ya kumjua. Mfano Mwenyeezi Mungu (s.w) ndiye anayemchagua Nabii ili kuwaongoza wanadamu,hivyo hakuna mtu yeyote mwenye uwezo au mwenye jukumu la kumchagua Nabii ili awe kiongozi kwa wanadamu,bali jukumu hilo ni la yule aliyemuumba mwanadamu ambaye ndiye anayejua njia bora ambayo kwayo mwanadamu anaweza kuufikia ukamilifu na saada. Kwa mantiki hiyo,uongozi wa Mwenyeezi Mungu (s.w) kwa mwanadamu hasa,unapaswa kufikiwa kupitia mwito,ulinganiaji na mawasiliano ya dini na sheria zake kupitia Manabii ili mwanadamu asije kuwa na hoja yoyote dhidi ya mfumo huu wa Mwenyeezi Mungu (s.w), au kwa ibara nyingine:Ili mwanadamu asijekuwa na hoja mbele ya Mola wake na kusema:{Mimi nilitaka kuufikia ukamilifu na saada lakini sikupata wa kuniongoza kuelekea ukamilifu huo hivyo sikujua ni pitie njia ipi}.

Ufafanuzi

JE YAHOVA NA ALLAH NI MIUNGU TOFAUTI

JE YAHOVA NA ALLAH NI MIUNGU TOFAUTI JE YAHOVA NA ALLAH NI MIUNGU TOFAUTI " Biblia yatofautisha dini ya Yehova na dini ya mungu-mtu " Ibada za kipagani ni chukizo na najisi kwa Yehova Na Muhibu Said KATIKA toleo lililopita tuliona jinsi Biblia tukufu inavyozipambanua dini za Yehova na dini ya Kikristo mungu-mtu ya kwa kudhihirisha uhusiano wa ibada za Kikristo na ibada za dini ya kipagani, ambazo tuliona jinsi Yehova anavyowataka wanadamu wajiepushe nazo mbali kabisa. Baadhi ya ibada hizo za kipagani zilizomo leo katika Ukristo, tuliona kuwa ni pamoja na kuua wana kama kafara ya dhambi, kujishughulisha na pepo na kuwaomba wafu. Tukaona kwamba Wakristo kuzitenda ibada hizo ni uthibitisho wa wazi kuwa hawamwabudu Yehova, Mungu wa Nabii Ibrahim, Ismaili, Isaka, Yakobo, Musa, Yesu, Muhammad na Mitume na Manabii wengine wote aliowatuma duniani. Kwa kuwa (ibada hizo) hazitokani na yeye (Yehova). Endelea. Kuabudu Sanamu Hii pia ni ibada ya msingi katika dini ya Kikristo ambapo sala za waumini wake (Wakristo) huwa hazitimii bila ya kuomba na kuabudu sanamu. Masanamu yanayohusishwa zaidi katika ibada hizo ni pamoja na sanamu la mungu-mtu Yesu wa Kikristo akiwa amebebwa na mama yake na kwenye sanamu lingine akiwa amekufa msalabani, sanamu la "Bikira Maria", sanamu la malaika na masanamu mengine mengi ya watakatifu wa Kikristo waliokufa! Kama maandiko ya Biblia tukufu yafundishavyo, ibada hii (ya sanamu) ifanywayo na Wakristo, kiasili imetokana na watu wa mataifa (wapagani). Uthibitisho wa hilo tunaupata katika maandiko yafuatayo: "Bali walijichanganya na mataifa, wakajifunza matendo yao. Wakazitumikia sanamu zao, Nazo zikawa mtego kwao". (Zaburi 106:35-36).

Ufafanuzi

ATHARI YA KUJIULIZA

ATHARI YA KUJIULIZA ATHARI YA KUJIULIZA KATIKA MAISHA YA MWANADAMU. Assalaam Alaikum Warahmatullah Wabarakatuh. Iwapo mwanadamu atayajibu vizuri maswali yanayohusiana na Muumba wa Ulimwengu na Mwanzilishi wa mfumo wake, maswali yanayomjia kutokana na maumbile yake ya kutaka kujua uhakika wa vitu,basi bila shaka atathibitisha Muumba wa Ulimwengu huu na Mfumo wake wa ajabu asiyekuwa na mwanzo wala mwisho.Jambo hili pia litamfanya akiunganishe kila kitu na azma yake thabiti inayotegemea uwezo na elimu yake isiyokuwa na mwisho. Hatimaye mwanadamu atajipata kuwa na joto la kadiri na matumaini.Hukabiliana inavyopaswa na matatizo yanayomkumba maishani mwake na kamwe hakati tamaa kuhusiana na yale matatizo asitoweza kuyatatua.Hii ni kwasabu hutambua kuwa kila kitu humu duniani kiwe na uwezo mkubwa kitakavyokuwa nao,kiko chini ya uwezo na uthibiti wa Mwenyeezi Mungu (s.w). Mtu kama huyo huwa si rahisi kwake kusalimu amri kirahisi mbele ya mambo mbali mbali yanayomkumba maishani mwake.Hata akiona kuwa kila kitu kiko katika manufaa na faida yake huwa hajivuni wala kuwa na wivu ili asije akasahau nafasi yake na ile ya Ulimwengu.Hii ni kwa sababu hutambua kila chanzo na sababu iliyomo humu duniani haifanyi kazi wala kusababisha kutokea kwa jambo jingine yenyewe bali husababisha kutokea kwa jambo hilo kwa mujibu wa utaratibu aliouweka mwenyeezi mungu (s.w).Mwisho mtu kama huyo huamua kuwa hakuna mtu apaswaye kutiiwa ispokuwa Mwenyeezi Mungu (s.w) na kuwa hapaswi kutii moja kwa moja amri za mtu yeyote yule ispokuwa amri za Mwenyeezi Mungu (s.w) Muumbwa wa kila kitu.

Ufafanuzi

KUZURU MAKABURI

KUZURU MAKABURI KUZURU MAKABURI Katika mambo yasiyo na shaka ndani yake ni kuwa, kuzuru makaburi huwa kuna jumuisha kupatikana athari muhimu za tabia njema na mafunzo mengine mema. Tunaonyesha kwa ufupi kama ifuatavyo: Kushuhudia uwanja uliotulizana kimya, ambao chini yake kuna idadi kubwa ya watu waliopata kuishi katika dunia hii kisha wakafariki, wakiwemo masikini na matajiri, wanyonge na wenye nguvu, kipindi hicho wakiwa hawana wanachokimiliki isipokuwa sanda, hali hii huutingisha moyo na roho ya mtu na kumpunguzia furaha na tamaa ya dunia na starehe zake. Lau mtu atauangalia uwanja huu wa makaburi kwa jicho Ia mazingatio, hakika atabadili mwenendo wake katika hii dunia na kuweka mazingatio yake akhera, na atakuwa akijiwaidhi mwenyewe kwa kusema: "Hakika maisha ya dunia ni ya muda na yatatoweka tu, na kwamba kipindi cha maisha ninayoishi kina mwisho na matokeo yake nitazikwa kaburini na kukandamizwa na rundo la udongo, na huko akhera kuna malipo ima mema au mabaya. Kwa hiyo ataona kuwa maisha haya ya dunia haifai kwa mtu kusumbuka kutafuta mali na heshima na cheo kwa kumdhulumu huyu au yule, kitu ambacho kitamfanya achume dhambi na mambo maovu. Mtazamo wa makini kwenye uwanja hun uliotulia kimya, hulainisha moyo hata kama ulikuwa mgumu, na humfanya mtu asikie hata kama alikuwa kiziwi, na kuyafungua macho hata kama yalikuwa hayaoni, na zaidi ya hapo humfanya mtu asahihishe tabia yake na maisha yake na ajihisi kuwa analo jukumu kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu Mutukufu na watu.

Ufafanuzi

SHAHIDI MUTAHHARI NA SIFA ZA DINI

SHAHIDI MUTAHHARI NA SIFA ZA DINI SHAHIDI MUTAHHARI NA SIFA ZA DINI Kwa mnasaba wa kuwadia siku ya kuuawa shahidi Murtadha Mutahhari, msomi na mwanafalsafa mashuhuri wa Kiislamu nchini Iran, tumeona ni bora tuzungumzie, angalau kwa ufupi, nafasi ya msomi huyo maarufu wa Kiislamu katika kueneza Uislamu. Kila mwaka Shahid Murtadha Mutahhari, hukumbukwa, kuenziwa na kutukuzwa nchini Iran kupitia makumbusho ambayo hufanyika kote nchini kwa ajili ya kukumbuka nafasi yake ya kielimu na mchango mkubwa alioutoa kwa ajili ya mfumo wa Kiislamu wa Iran kabla na muda mfupi baada ya ushindi wa mapinduzi ya Kiislamu nchini. Makumbusho hayo hutukumbusha kwamba ulimwengu wa Kiislamu unahitajia wasomi na wanafikra wakubwa kama Shahid Mutahhari kwa ajili ya kuwaongoza Waislamu katika njia ya kufikia malengo yao matukufu. Shahid Murtadha Mutahhari anaweza kuchukuliwa kuwa nembo na mfano muhimu wa kuigwa na wanafikra pamoja na wasomi wengine wa Kiislamu katika kuungoza umma wa Kiislamu kwenye njia panda iliyojaa matatizo na njama za maadui wa Uislamu.

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini