Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

MAKALA MBALIMBALI

KISA CHA KUIJENGA L-KA`ABA

KISA CHA KUIJENGA L-KA`ABA

KISA CHA KUIJENGA L-KA`ABA Mtume S.A.W. alikuwa na umri wa miaka 35 wakati Ma-Quraishi walipokutana pamoja kuijenga L-Ka`aba. Waliijenga kwa sababu mafuriko ya maji yalibomoa kuta za L-Ka`aba. Kabila zote za Ki-Quraishi zilikusanya mawe ya kujengea. Kila kabila ilijenga sehemu yake maalum bila kuingilia sehemu ya kabila nyingine. Mpaka ujenzi ulipofikia kwenye jiwe jeusi hapo ulitokea mzozano mkubwa, kwani kila kabila ilitaka iwe yenye kuliweka lile jiwe jeusi. Wakabaki hivi hivi kwa siku wametofautiana mpaka ilitaka kutokea fitina (ugomvi) mkubwa baina yao. Lakini Mwenyezi Mungu S.W.T. akajaalia mmoja wao mwenye akili aliyeitwa Abu Umayya bin Mughiyra L-Makhzuumy kutoa shauri la kuumaliza ugomvi huo; wakakubaliana wote, na shauri lile lilikuwa kama ifuatavyo: Yeyote yule atakaeingia mwanzo kwenye mlango wa L-Ka`aba (ambao hivi sasa unaitwa Baabu Ssalaami) ndiye atakayekuwa Hakimu wa kuwahukumu baina yao.

Ufafanuzi

MAZINGATIO

MAZINGATIO MAZINGATIO Maafa mengi yamezidi siku hizi duniani na baada ya kutokea maafa ya mitetemeko ya ardhi baharini inayoitwa Tsunami, ambayo ni makubwa mno kuwahi kutokea, inatupasa tuelewe kuwa kuna mazingatio makubwa ndani yake. Mengi tumesikia, na kuona kwa kila aina ya rangi katika televisheni na radio na kusikitika sana kuona maafa yaliyowapata wenzetu. Lakini tujiulize maswali yafuatayo: Je, nini sababu ya kutokea maafa hayo? Au mazingatio gani yanatupasa tuyatie akilini mwetu? Au mafundisho gani tumepata kwa matukio hayo? Na baada ya kujuwa yote hayo je, inatupasa tufanye nini? Sababu kubwa ni kuwa watu wamezidi kufanya maasi na ufisadi duniani. Na katika maafa haya kuna waliokuwa hawamjui kabisa Mola wao, na kuna waliokuwa wanamjua lakini hawafuati amri Zake na makatazo kwa hiyo Allaah  سبحانه وتعالى huwateremshia ghadhabu Yake ili watanabahi wajirekebishe na warudi Kwake.

Ufafanuzi

WAISLAMU UMAGHARIBINI

WAISLAMU UMAGHARIBINI WAISLAMU UMAGHARIBINI Baraza la Mahusiano ya Waislamu la Amerika limeripoti kuwa mwaka 2002, kulikuwa na malalamiko 602 ya ubaguzi dhidi ya jamii ya Waislamu. Hili lilikuwa ni ongezeko la asilimia 15 kulinganisha na mwaka wa nyuma yake.  Mikasa ya ubaguzi ilitokea mashuleni, makazini, kwenye maeneo ya kijamii, kwenye viwanja vya ndege na kwingineko. Mikasa hiyo ilijumuisha ubaguzi katika ajira, bugudha ya maneno, kunyimwa fursa za kidini na kadhalika.  Matendo haya ya ubaguzi yalihusiana moja kwa moja na rangi au dini ya mtu hasahasa kwa watu ambao utambulisho wa dini yao unabainika kwa vazi la Hijab au shungi. Je Waislamu wayajibu vipi matukio ya namna hiyo?  Wanawake wa Kiislamu ndio wahanga wakubwa wa aina mbalimbali za unyanyasaji na ubaguzi kutokana na ishara za mavazi yao ya Kiislamu.

Ufafanuzi

MATATIZO YA BIBLIA

MATATIZO YA BIBLIA MATATIZO YA BIBLIA Tatizo la Kutafsiri Wataliano wana usemo usemao "Wafasiri ni waongo". Msemo huu una ukweli ndani yake na umetokana na uchunguzi makini. Kuchukua kitu fulani kilichoandikwa katika lugha fulani na kujaribu kukiingiza katika lugha nyingine huwa inaleta matatizo kwa sababu mara nyingi wafasiri hupambana na maneno katika lugha moja ambayo hayamo katika lugha nyingine. Neno jingine badala yake lazima litumike na matokeo yake ni kubadilika kwa maana. Agano la kale mwanzo kabisa liliandikwa kwa Kiebrania, lakini lilitafsiriwa katika karne ya tatu kwenda katika lugha ya Kigiriki kwa ajili ya Wayahudi waliokuwa wanaishi nje ya Palestina (ambao walikuwa wanaongea Kigiriki - badala ya Kiebrania). Tafsiri hii iliitwa "septuagint" na ilitumika sana hata na wakristo wa mwanzo. Agano Jipya liliandikwa katika lugha ya Kigiriki lakini maadam Yesu mwenyewe alitumia lugha ya kiaramaiki, hii ina maana kwamba maneno yake yalilazimika kutafsiriwa na hivyo kusababisha uwezekano wa makosa.

Ufafanuzi

ANGALIA UTAFAKARI

ANGALIA UTAFAKARI ANGALIA UTAFAKARI KUYAANGALIA MAMBO KWA MUSTAKBALI WAKE Utambuzi wa mu’min kuwa yumo kwenye mtihani humuongoza azingatie mambo yake kwa sura ya kuyaangalia mbeleni. Lakini “kuyaangalia mambo mbeleni” kunamaanisha nini hasa? Ijapo taabu na shida humkumba binadamu, hali hio hakika si ya kudumu milele bali ni ya muda wa kupita tu. Mtu, kwa mfano, anaweza kutuhumiwa kiuwongo kuwa amefanya hatia fulani na kudhulumiwa. Bila shaka utakuja wakati ukweli wa mambo utadhihirika. Hata kama taabu inayompata mtu huyo haitakwisha hapa duniani, kwa ajili ya dhuluma hiyo, wale waliosababisha hiyo dhuluma watapata jazaa yao kamili siku ya Kiyama. Na vilevile, yule aliyedhulumiwa anatarajia kupokea zawadi nzuri sana kwa subira yake katika siku hiyo. Wakati unakwenda haraka sana, na kama mambo mengine yale, hali hii itawadia mwishowe kama vile kasi ya mwendo wa kufumba na kufumbua jicho. Pia Qur’ani inadhihirisha kuwa dhiki hufuatiwa  na faraja kwa Mwislamu: Basi kwa hakika baada ya dhiki faraja. Hakika baada ya dhiki faraja. (Surat Al-Inshirah, 5-6)

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini