Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

Waliotajwa ndani ya tarehe

KUZALIWA KWA NABII MUSA NA NABII HARUUN.

KUZALIWA KWA NABII MUSA NA NABII HARUUN.

KUZALIWA KWA NABII MUSA NA NABII HARUUN. Siku moja Firauni aliota usingizini mwake ndoto ya moto umetoka Baitul Muqaddas ukielekea Misri kisha ukaunguza nyumba zote wanazoishi ndani yake Wamisri isipokuwa nyumba za Ma-Bani Israil. Mara tu alipoamka aliwaita haraka wachawi wake na wapiga ramli ili wamfasirie ndoto yake. Wakamfasiria wakamwambia, "Atatokea kijana miongoni mwa Ma-Bani Israil ambaye ndiye atakuwa sababu ya kuangamiza utawala wako na kubadili dini yako ewe mfalme!" Mmoja wao akamshauri Firauni ya kwamba, kila mtoto atakayezaliwa wa kiume wa Kibani-Israil auwawe. Firauni lilimpendeza sana shauri hili. Ndio maana tokeya hapo Firauni aliwatuma askari zake wamchinje kila mtoto mchanga wa kiume wa Ki-Bani Israil. Lakini wakubwa wanaosimamia kazi za ujenzi wa majumba ya Firauni wakashtaki kwa Firauni wakamwambia wakasema: "Ukiwa mtindo huu wa kuwauwa watoto wakiume utaendelea baadaye watapungua wafanya kazi wanaume wa Ki-Bani Israil wanaotengeneza matofali ya kuchomwa." Firauni alifikiri kisha alilikubali ombi lao akatoa shauri zuri la kuwaridhisha wajengaji akasema Firauni: "Mwaka mmoja nitasimamisha wasichinjwe watoto wakiume na mwaka mwingine wachinjwe ili wasizidi idadi yao. Na pia wakati ule ule watakuwa wanao wafanyakazi wa kutosha." Kwa bahati nzuri mke wa Imraan akamzaa Nabii Haruun A.S. katika mwaka ule ambao wasiochinjwa watoto wa kiume wa Ki-Bani Israil. Hivyo hakufanywa kitu chochote kile. Lakini kwa bahati mbaya Nabii Musa A.S. alizaliwa katika ule mwaka ambao wanachinjwa watoto wa kiume. Hivyo mama yake Musa hakujua jinsi ya kufanya ili kusudi amuokoe mwanawe. Lakini kwa kuwa Mwenyezi Mungu S.W.T. ni Mjuzi wa mambo yote yanayotokea mbinguni na ardhini, hivyo alimfundisha kwa ilhamu njia ya kumuokoa Nabii Musa, akamfunulia kwamba ikiwa atakhofia kumweka nyumbani kwake, basi amtiye mwanae kwenye kisanduku na kisha akitie katika mto wa Nile na Mwenyezi Mungu Mtukufu atapitisha jambo la kumuokoa. Akafanya hivyo kama alivyoamrishwa na Mola wake, kisha akakitia kisanduku kile mtoni kikawa kinachukuliwa na maji. Lakini hata hivyo wasiwasi ulimwingia moyoni mwake kumfikiria mwanae, kwa hali hiyo akamtuma dada yake Nabii Musa akifuatie kile kisanduku mpaka mahali kitakapofikia. Akaondoka kukifuata akawa akimwangalia kwa mbali na huku akijihadhari asitambulikane na Firauni na watu wake kama ni dada ya Nabii Musa.

Ufafanuzi

NABII NUUH A.S.

NABII NUUH A.S. NABII NUUH A.S. Hapo zamani palikuwapo na watu watano walioishi katika nchi ya baina ya mito miwili nayo hivi sasa inaitwa nchi ya Iraq. Hawa watu walikuwa wema wakimuabudu Mwenyezi Mungu mmoja na wakiisimamia mipaka Yake kwa watu; na wakiwafanyia watu wema na ihsani. Ukaendelea vizuri mwendo wao na kujulikana sifa zao nzuri. Watu wakawapenda sana; na ikafika ajali yao wakafa wote. Watu wakawahuzunikia sana baadaye wakaanza kufikiri jinsi ya kuwakumbuka daima, mmoja wao akasema wachoreni ili tupate kuwakumbuka na tukumbuke ile ibada yao ya Mwenyezi Mungu S.W.T. na tutabakia katika hali hiyo. Kisha wakawachora vikapita vizazi wakasahau sababu ya kuwachora wakakumbuka tu ibada na kuzitukuza hizo picha. Wakachonga masanamu akaja adui Shetani akawafundisha jinsi ya kuyatukuza na kuyaabudu masanamu hayo yaliyotengenezwa kwa mikono yao. Wakapotezwa na Shetani na kuwakhadaa kwamba ati wale watu waliopita kabla yao walikuwa wakiyatumia hayo masanamu kwa kuombea mvua, kheri na wakiyaabudu. Pole pole ikaanza kuingia ile ibada katika nyoyo zao mpaka ikawaingia barabara na wakabadili kutoka katika ibada ya Mwenyezi Mungu Mtukufu mpaka ibada ya kuyaabudu masanamu. Ambayo yaliitwa kwa yale majina ya watu watano waliokufa: Waddi, Suwaa, Yaghutha, Ya`uqa na Nasra. Wakaendelea hivyo vizazi na vizazi katika ujinga na kufuru na upotofu. Lakini Mola wa walimwengu wote hawaachi watu wakapotea bila kuwaongoza. Kwa hivyo akawatumia Nabii Nuuh A.S. bin Laamik ambaye aliyezaliwa baada ya kufa Nabii Adam kwa miaka 10,000. Alikuwa Mtume wa kwanza kutumwa ulimwenguni ili awatoe watu wake katika upotofu na awaonye adhabu ya Mola Mtukufu ikiwa watamkanusha.

Ufafanuzi

KUANGAMIZWA KWA WATU WA NABII LUUT

KUANGAMIZWA KWA WATU WA NABII LUUT KUANGAMIZWA KWA WATU WA NABII LUUT. Nabii Ibrahim alipojua makusudio ya Malaika waliokuja kumbashiria kwa kuzaa mtoto atakayeitwa Is-haaq ya kutaka kuwaangamiza watu wa Nabii Luut alianza kujadiliana nao, kwamba kuna idadi ya Waislamu katika kaumu Luut; lakini Malaika walipochungua walikuta ni nyumba moja tu ya Waislamu nayo ni nyumba ya Nabii Luut peke yake. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu S.W.T. katika Surat Dh-dhariyaat aya ya 36, " Maana yake, "Lakini hatukupata humo (katika kaumu ya Nabii Luut) ila nyumba moja tu (ya Nabii Luut) yenye Waislamu. Ssuddiyy kasema: "Malaika hao walipotoka kwa Nabii Ibrahim waliendelea na safari yao moja kwa moja mpaka karibu na kijiji cha kaumu ya Nabii Luut, wakaufikia nusu ya mchana, walipofika katika mto wa Sodom wakamkuta mtoto wa kike wa Luut anateka maji kwa ajili ya ahli yake. Na Nabii Luut alikuwa na watoto wawili wa kike, Wakamuuliza "Ewe msichana! Jee, una nyumba?" Akawajibu: "Msiuingie mji huu mpaka kwanza nikuijieni." Kwani aliwakhofia kaumu yake wasije wakawachukua kisha wakawafanyia mambo machafu, kwa sababu kaumu Luut walikuwa ni watu ambao wakiwaingilia wanaume wenzao. Msichana akamjia baba yake akamwambia: "Ewe baba yangu! Wanakutaka vijana kwenye mlango wa mji; sijaona watu wenye sura nzuri kabisa kama wao, nami nakhofia wasije wakachukuliwa na watu wako kisha wakawafedhehesha.

Ufafanuzi

KUANGAMIZWA KWA KAUMU YA NABII SHU`AIB A.S

KUANGAMIZWA KWA KAUMU YA NABII SHU`AIB A.S KUANGAMIZWA KWA KAUMU YA NABII SHU`AIB A.S Watu wa kaumu ya Shu`aib wakamsingizia kuwa ati Mtume wao karogwa. Na wakamwambia: "Ungelikuwa kweli ni Mtume basi ungetuijia kwa umbo la Kimalaika au mwenye sifa tofauti na mwanadamu. Kwa hiyo tunakudhania wewe ni muongo." Kama alivyosema Mwenyezi Mungu S.W.T. katika Surat Sh-shua`raa aya ya 185 na ya 186, Maana yake, "Wakasema: "Hakika wewe ni miongoni mwa waliorogwa. Na wewe si chochote ila ni mtu tu kama sisi, na kwa yakini tunakuona wewe ni katika waongo." Wakazidi kumwambia: "Ikiwa wewe ni Mtume wa kweli basi tuangushie vipande vya mbingu." Kama alivyosema Mwenyezi Mungu S.W.T. katika Surat Sh-shua`raa aya ya 187, " Maana yake, "Hebu tuangushie vipande vya mbingu ikiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli." Nabii Shu`aib akawajibu majibu ya mtu muumini mkweli wa imani kama ilivyokuja katika Surat Sh-shua`raa aya ya 188, " Maana yake, "…Mola wangu anajua zaidi mnayoyatenda." Wakaja wakubwa waliotakabari wa kaumu yake kwa Mtume Shu`aib wakimtishia na kumwahidi kwamba watamtoa katika mji wao yeye pamoja na wale waliomwamini.

Ufafanuzi

Nabii Issa (A.S) katika Quran.

Nabii Issa (A.S) katika Quran. NABII ISSA (A.S) KATIKA QUR"ANI Na hakika tulimpa Musa Kitabu na tukafuatisha baada yake Mitume wengine. Na tukampa Isa (Yesu), mwana wa Mariamu, hoja zilizo waziwazi, na tukamtia nguvu kwa Roho Takatifu. Basi kila walipo kufikieni Mitume kwa yale ambayo hayapendwi na nafsi zenu, mlijivuna; wengine mkawakanusha, na wengine mkawauwa. Semeni nyinyi: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyo teremshiwa sisi, na yaliyo teremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu zake, na waliyo pewa Musa na Isa (Yesu), na pia waliyo pewa Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi; hatutafautishi baina ya yeyote katika hao, na sisi tumesilimu kwake. MITUME hao tumewatukuza baadhi yao juu ya wengineo. Katika wao wapo ambao Mwenyezi Mungu alisema nao, na wengine akawapandisha vyeo. Na tukampa Isa (Yesu) mwana wa Mariyam hoja zilizo wazi, na tukamtia nguvu kwa Roho Takatifu. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu alipenda wasingeli pigana walio kuwa baada yao baada ya kuwajia hoja zilizo wazi. Lakini walikhitalifiana. Basi wapo kati yao walio amini, na wengine kati yao walio kufuru. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu alipenda wasingeli pigana. Lakini Mwenyezi Mungu hutenda atakavyo. Na pale Malaika walipo sema: Ewe Maryamu! Hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria (mwana) kwa neno litokalo kwake. Jina lake ni Masihi Isa (Yesu) mwana wa Maryamu, mwenye hishima katika dunia na Akhera, na miongoni mwa walio karibishwa (kwa Mwenyezi Mungu). Isa (Yesu) alipo hisi kuwa kati yao pana ukafiri alisema: Nani wasaidizi wangu kwa Mwenyezi Mungu? Wanafunzi wake wakasema: Sisi ni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu. Tumemuamini Mwenyezi Mungu, na shuhudia kwamba sisi hakika ni Waislamu. 3:52 Hakika mfano wa Isa (Yesu) kwa Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam; alimuumba kwa udongo kisha akamwambia: Kuwa! Basi akawa. Sema: Tumemuamini Mwenyezi Mungu, na tuliyo teremshiwa sisi, na aliyo teremshiwa Ibrahim, na Ismail, na Is-haak na Yaakub na wajukuu zao, na aliyo pewa Musa na Isa (Yesu) na Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi. Hatubagui baina yao hata mmoja, na sisi ni wenye kusilimu kwake. Na kwa kusema kwao: Sisi tumemuuwa Masihi Isa (Yesu), mwana wa Maryamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu - nao hawakumuuwa wala hawakumsalibu, bali walifananishiwa tu. Na hakika walio khitalifiana katika haya wamo katika shaka nayo. Wao hawana ujuzi nayo wowote, ila ni kufuata dhana tu. Wala hawakumuuwa kwa yakini.

Ufafanuzi

NABII SALEH A.S

NABII SALEH A.S NABII SALEH A.S Thamuud ni kabila mashuhuri la Kiarabu lililokuwa likiishi Hajjar, na Hajjar ipo kati ya Hijaaz na Tabuuk. Na Mtume wetu S.A.W alipita katika magofu yaliyobakia ya mji wa Thamuud wakati ule walipokuwa wakienda kwenye vita vya mwisho vya Tabuuk. Akawaomba Waislamu wasiuingie mji huo ila iwe kwao ni ibra (fundisho) yaliyowafika kina Thamuud; na bora wauepuke. Hivyo Waislamu wakauepuka kuuingia mji huo. Na kabila la Thamuud lilikuwepo zamani baada ya kabila la Adi ambao wametajwa sana katika Qur-aani Tukufu. Na zile khabari za kina Adi na Thamuud zilikuwa maarufu hapo zamani. Mwenyezi Mungu S.W.T. alimtuma kwa kabila la Thamuud ndugu yao Saleh bin `Abiyd awalinganie ili wamwamini Mungu mmoja; lakini haukuwazidishia wito wake ila kuasi na upotofu juu ya upotofu. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu S.W.T. katika Suratil A`araaf aya ya 73, " Maana yake, "Na kwa Thamud tulimpeleka ndugu yao, Saleh. Akasema: "Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye.." Siku moja walipokuwa wamekusanyika katika mikutano yao akawaijia Nabii Saleh akirudishia kuwaambiya wito wake.

Ufafanuzi

KUANGAMIZWA KWA WATU WA NABII SALEH A.S

KUANGAMIZWA KWA WATU WA NABII SALEH A.S KUANGAMIZWA KWA WATU WA NABII SALEH A.S Kaumu ya Nabii Saleh A.S. iliangamizwa kwa sababu ya kumuuwa ngamia wa Mwenyezi Mungu na ilhali kabla ya hapo Mtume wao aliwaonya kwa onyo kali la kushukiwa na adhabu ya haraka kabisa ikiwa watamuuwa yule ngamia jike. Ingawa walionywa kwa hilo onyo kali lakini hata hivyo watu wabaya hawakumsikia wala kumjali Mtume wao. Siku ya Jumatano wakamfukuza yule ngamia wa Mwenyezi Mungu na alipopita karibu ya Masda`a akamrushia mshale, na alipofika karibu na kijana aliyeitwa Qaddaar bin Saalif akamuuwa ngamia kwa upanga kwa amri ya wenzake. Kisha wakamchinja wakagawana nyama yake wakaila. Lakini mtoto wa ngamia aliwahi kukimbilia jabalini, na inasemekana aliingia jabalini akapotea humo. Kama ilivyobainika katika Suratil Qamar aya ya 29, " Maana yake, "Basi wakamwita rafiki yao (Qaddaar naye kashika upanga) akamchinja (yule ngamia wa Mwenyezi Mungu wakamla)." Na pia Mwenyezi Mungu S.W.T. kasema katika Surat Sh-shams aya ya 14, Maana yake, "Lakini walimkadhibisha (Mtume wao) na wakamchinja ngamia (wa Mwenyezi Mungu), kwa hivyo Mola wao aliwaangamiza kwa sababu ya dhambi zao na akawafuta kabisa (duniani)."

Ufafanuzi

KISA CHA MAYAHUDI WALIOVUNJA SABATO

KISA CHA MAYAHUDI WALIOVUNJA SABATO KISA CHA MAYAHUDI WALIOVUNJA SABATO Kisa hiki kimetajwa ndani ya Qurani tukufu. Na watu hawa walikuwa ni Mayahudi ambao walivunja taadhima ya siku hiyo ya Jumamosi. Nao walikuwa wakaazi wa mji ulioitwa Ayla, mji huo ulioko kati ya Madyan na Tuwr ambao uko kando ya bahari. Hawa Mayahudi walikuwa ni wavuvi wa samaki. Ibn Abbaas R.A.A. kasema: "Walikuwa wameshika dini ya Taurati iliyoharamisha kufanya kazi siku hiyo ya Jumamosi katika zama zao. Na sheria iliyokuwamo ndani ya Taurati iliwaharamishia kuvua samaki siku hiyo ya Jumamosi. Licha ya kuharamishwa kuvua samaki bali ilikuwa hata haramu kufanya kazi yoyote ile ya kujipatia fedha, kwani haikuwa ni siku ya kufanya kazi bali Mola Mtukufu aliifanya iwe ni siku ya ibada yao tu ya kumtukuza Mwenyezi Mungu. Mola alijalia siku hiyo ya mapumziko wawe samaki wengi sana juu ya bahari, na uwingi wao ulikuwa kuliko siku yoyote ile nyingine. Na hayo hayakutokea isipokuwa ulikuwa ni mtihani na majaribio makubwa uliotoka kwa Mola wao wa kutii na kuasi, na hii haikuwa ila baada ya kuzidi zile kufuru zao walizokuwa wakizifanya. Kwa hali hiyo baadhi yao wakavutika kuwaona samaki wengi wakiogelea juu ya bahari siku hiyo ya Jumamosi ambayo walikatazwa kuvua samaki, hivyo wakafanya ujanja wa kuweka nyavu zao za kutegea samaki siku ya Ijumaa pamoja na kuchimba mifereji ya maji kutoka baharini mpaka kwenye mitego ya samaki waliyounda wao wenyewe. Na kila samaki aliyeingia humo mferejini alishindwa kutoka. Nao wakawa wakienda kuwachukuwa samaki hao siku ya Jumapili. Ikawa siku ya Jumamosi haikupita bure bila kazi. Vitendo vyao hivi vilimghadhibisha sana Mola Mtukufu kisha akawalani kwa kule kwenda kinyume na kuvunja amri Yake kwa kufanya hila ambazo zilikuwa wazi kabisa kwa mtu yeyote yule mwenye kuona. Na walipokwenda kinyume na ile amri ya Mola Mtukufu, baadhi yao ambao hawakuvunja sheria ya Jumamosi waligawanyika makundi mawili. Kundi moja liliwalaumu na kuwakataza wale watu wakosefu waliokwenda kinyume na sheria hiyo ya kuvua samaki. Na kundi la pili hawakufanya hivyo wala hawakukataza bali waliwalaumu wale watu waliokataza kufanya kile kitendo cha uovu cha kuvua smaki wakasema: "Faida gani ya kuwakataza watu ambao tanguwapo Mwenyezi Mungu atawateketeza au atawaadhibu adhabu kali?"

Ufafanuzi

NABII YAHYA A.S

NABII YAHYA A.S

Ufafanuzi

KISA CHA MFALME TAALUWT

   	  KISA CHA MFALME TAALUWT KISA CHA MFALME TAALUWT Kisa cha mfalme Taawlut kimetolewa ndani ya Qurani Tukufu. Kisa hiki kilitokea baada ya kifo cha Nabii Musa A.S., wakubwa wa Ki-Bani Israil waliomba waletewe mfalme, hivyo kwa rehma za Mwenyezi Mungu S.W.T. alimletea wahyi Mtume Wake wa zama zile aliyeitwa Shamuweli A.S. kwamba awaambie watu wake kuwa Mola wao amewachagulia Taaluwt awe ndiye mfalme wao. Na huyu Taaluwt alikuwa ni mmoja katika askari wao na hakutokana na ukoo wa kifalme. Lakini hata hivyo Mabani Israil hawakuridhika na shauri hilo lililotoka kwa Mola wao bali walimlalamikia Mtume wao wakasema: "Vipi atatutawala na hali yeye hakutokana na sisi, na sisi tuna haki zaidi yake, na juu ya hivyo yeye ni mtu fakiri?" Lakini Mtume wao aliwajibu akasema: "Mwenyezi Mungu S.W.T. Ndiye Aliyemchagua Taaluwt si mimi na akamzidishia elimu na nguvu." Na kufafanua zaidi yaani mfalme huhitajia kuwa na elimu ya kivita na nguvu ya kimwili ili kupambana na maadui, na kuwa na ustahamilivu wa hali ya juu. Mtume wao akaendelea kuwajibu: "Mwenyezi Mungu humpa ufalme yule mtu amtakae na anayemuona anafaa si hovyo tu." Na Mtume wao akawaambia kwamba: "Alama ya kumjua Taaluwt amechaguliwa kuwa mfalme wenu ni Mwenyezi Mungu kukurejesheeni sanduku ambalo lilichukuliwa zamani kutoka kwenu, na ndani yake mna kitulizo cha nyoyo."

Ufafanuzi

LIKO WAPI KABURI LA YESU

LIKO WAPI KABURI LA YESU LIKO WAPI KABURI LA YESU Bismillah Al-Rahman Al-Rahiim Wapendwa Wasomaji wa Qadiani/Ahmadiya Amani iwe juu ya wale wanaofuata uwongofu Mirza Ghulam Ahmad Qadiani, Mwasisi wa Jumuiya ya Ahmadiyah, alidai hivi: Mungu kanifunulia katika ufunuo maalum kuwa Masihi Ibn Maryam amekufa." (Tauzeeh-e-Maram, Roohani Khazain juz. 3 uk. 402). "Nimefahamishwa kaburi la Issa (nchini Kashmir). Na nimefahamishwa na Qur'an Tukufu pamoja na ufunuo wa Mungu kwangu kuhusu kifo cha Yesu." (Roohani Khazain juz 18 uk.358,361) Je hili ndilo kaburi la Yesu? "Kaburi la Kristo" (7/24) Katika kitovu cha Ukristo, fumbo la muda mrefu kama ilivyo imani ya Ukristo, sasa liko jirani kufumbuliwa. Timu ya wataalamu wa mabaki ya kale kutoka Chuo Kikuu cha Oxford imekuwa katika pilikapilika kubwa za kujaribu kuthibitisha kuwa lile Kanisa la kaburi la Jerusalem ndipo mahali penyewe alipozikwa Yesu. Baada ya muongo mmoja, Martin Biddle na mkewe, Birthe Kj?lbye-Biddle, wame*****ua mabaki ya vitu vya kale katika eneo hilo pamoja na kaburi lenyewe la jabali la kuchongwa lililofichikana ndani ya kuta za kibanda au "kijumba" kilichokuwepo hadi karne ya 19. Kikiaminika kuwa ni alama ya kaburi la Kristo, kibanda hicho, mpaka sasa, bado hakijafanyiwa aina yoyote ya utafiti wa mabaki ya kale au uchunguzi wa kisayansi.

Ufafanuzi

MTOTO WA NABII NUUH (KAN`AAN).

MTOTO WA NABII NUUH (KAN`AAN). MTOTO WA NABII NUUH (KAN`AAN).      Mwenyezi Mungu S.W.T. alimtuma Nabii Nuuh A.S. kuwaonya watu wake kabla ya kujiwa na adhabu iumizayo. Akawalingania kwa muda wa miaka 950 katika ibada ya Mwenyezi Mungu mmoja na kuacha ibada yao ya upotofu ya kuabudu masanamu. Alitumia kila njia ili watu wake wafuate dini ya haki, lakini wapi! Walijivuna na wakaendelea katika upotofu na ukafiri wao bila ya kujali adhabu itakayowapata watu wasiomtii Mola Mtukufu. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu S.W.T. kwa kauli ya Nabii Nuuh katika Surat Nuuh tangu aya ya 5 mpaka 7, " Maana yake, "…Ewe Mola wangu! Kwa hakika nimewalingania, (nimewaita) watu wangu usiku na mchana. Lakini wito wangu haukuwazidishia ila kukimbia. Na kila mara nilipowaita uwasamehe, waliziba masikio yao kwa vidole vyao, na walijifunika nguo zao (gubigubi), na walizidi kuendelea (na kufuru) na wakafanya kiburi kingi." Nabii Nuuh A.S. alipokata tamaa kwamba watu wake hawatamwamini, hivyo Mwenyezi Mungu S.W.T. akamwamrisha Nabii Nuuh A.S. atengeneze jahazi mbele ya nyumba yake ili kusudi limbebe yeye pamoja na watu waliomwamini tu na ili makafiri wagharikike majini. Mke wa Nabii Nuuh na mwanae aliyeitwa Kan`aan walikuwa miongoni mwa watu makafiri. Na jahazi lilipokuwa tayari limekamilika na hakuna tena tamaa ya watu wake kuamini; Nabii Nuuh alimuomba Mola wake amuokoe na awaangamize makafiri.

Ufafanuzi

NABII ISA (A.S)

NABII ISA (A.S) NABII ISA (A.S) Tarehe 25 Disemba inasadifiana na siku ya kuzaliwa Nabii Issa Masiih amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake. Kuzaliwa kwa mtukufu huyu kulihuisha moyo wa udugu, imani, upendo na mahaba kati ya wanadamu. Issa Masiih (as) alizaliwa katika kizazi kilichokuwa mashuhuri kwa usafi na utukufu. Alitumwa kuondoa ujinga na dhulma na kueneza nuru ya imani, maarifa na upendo baina ya Banii Israel. Bibi Maryam mtakasifu, mama yake Nabii Issa (as) alipopata habari kuwa ni mja mzito, alishikwa na mshangao mkubwa na huzuni na baadaye kidogo akajiwa na bishara njema kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Malaika wa wahyi na ufunuo alimwendea na kumwambia: Ewe Maryam! Mola wako amesema kazi hii ni nyepesi mno kwangu, ili tumfanye muujiza kwa watu na rehema kutoka kwatu na jambo hilo limekwishahukumiwa". (Maryam-21) Nabii Issa ambaye alizaliwa kwa muujiza wa Mola Muumba alitumwa akiwa na ujumbe wa nuru na mwangaza kutoka kwa Mola wake. Mwenyezi Mungu alizungumza na Mtume wake mteule Issa akisema Ewe Issa! Mimi ni Mola wako Mlezi. Mungu Mmoja niliyeumba kila kitu. Nitaje na kunikumbuka na unipende mimi rohoni mwako. Ewe Issa! Wewe ndiye Masiih kwa amri yangu mimi. Utaumba vitu kutokana na udongo kwa ruhusa yangu na kuhuisha wafu kwa idhini yangu. Ewe Issa! Umebarikiwa utotoni na ukubwani na utakuwa na baraka popote utakapokuwa. Nitegemee mimi ili nikutosheleze." Katika aya zake nyingi Qur'ani tukufu inazungumzia na kutoa picha ya maisha ya Mitume na Manabii wa Mwenyezi Mungu. Kwa mujibu wa kitabu hicho kitukufu, Mitume wote walitumwa kuja kuwaongoza wanadamu kwenye tauhidi na imani ya Mungu Mmoja, kusimamisha uadilifu na kupambana na dhulma.

Ufafanuzi

NABII YUUNUS A.S

NABII YUUNUS A.S NABII YUUNUS A.S Mwenyezi Mungu S.W.T. alimtuma Nabii Yuunus A.S. kwa watu wa mji wa Ninawah ulioko nchi ya Iraq, kwani watu hawa walikuwa wakiabudu masanamu. Nabii Yuunus A.S. alikuwa na sauti nzuri sana hata inasemekana wakati alipokuwa akisoma wanyama wa porini walikuwa wakimsikilza sauti yake, kama alivyokuwa akifanya Nabii Daud A.S. katika zama zake. Alipowaijia watu wake aliwakataza ukafiri na akawalingania katika ibada ya Mungu mmoja. Lakini watu wake walimkadhibisha, na wakakataa wito wake na jambo hili liliendelea kwa muda mrefu. Nabii Yuunus A.S. alipokata tamaa alitoka nje ya mji kwa kukhofia adhabu na huku ameghadhibika akiwaahidi watu wake kushukiwa na adhabu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Alipowaacha watu wake, nyuma yake Mwenyezi Mungu S.W.T. akatia toba na imani katika nyoyo zao kisha wakajuta ubaya waliomfanyia Mtume wao. Na haijatokea mji wa watu wake kamili uliomuamini Mtume wake ila mji wa Nabii Yuunus. Kwani wote walipomuamini Mwenyezi Mungu S.W.T. aliwasamehe na akawaondolea adhabu ambayo ingeliwapata duniani kwa ile kufuru yao kama ilivyowapata kina Adi na Thamuwd na walio mfano na wao.

Ufafanuzi

NABII MUSA (A.S) NA SIASA YA KUWAKABILI WATAWALA

NABII MUSA (A.S) NA SIASA YA KUWAKABILI WATAWALA PUNDE tu Nabii Mussa alipoteuliwa kuwa Mtume,  hakuanza kwa kufanya yale mambo ambayo sisi hivi leo huyaona kuwa ndio dini yaani kama vile kuswali, kufunga, kutoa zaka na kadhalika. Bali jukumu la awali alilopewa ni lile la kwenda Ikulu kumkabili Firauni aliyekuwa akitawala kidhalimu. "...Wakumbushe watu Mola wako alipomwita Musa, akamwambia nenda kwa wale watu madhalimu. (26:10) Na kwa yakini tulimtuma Musa kwa Firauni na Hamana na Karuni (40:24) Nenda kwa Firauni. Bila shaka yeye amepindukia mipaka (20:24) Nendeni kwa Firauni kwa hakika amepindukia mipaka (20:43) Kwa mujibu wa aya zote hizo, ni sahihi kusema kuwa Nabii Musa alianza kazi ya Utume kisiasa, kwa sababu hicho alichokifanya ndicho kinachofanywa na wanasiasa wa upinzani hivi leo, tofauti tu ni kwamba yeye alifanya hivyo kwa muongozo wa Mwenyezi Mungu. Kwa maana hiyo basi, wanadini ambao ndio warithi wa Mitume ndio wanaopaswa kubeba jukumu alilobeba Musa. Kwa mantiki hiyo, wao ndio hasa wanaotakiwa kuwa mstari wa mbele katika harakati za kuondoa serikali za kidhalimu kwa misingi ya kisiasa. Lakini jambo la kustaajabisha kuwa baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakiunga mkono madai ni kuwa dini isichanganywe na siasa! Matokeo yake wakandamizaji wanathubutu hata kusema maneno ya uongo dhidi ya Mitume. Mathalan yule aliyedai kuwa Mtume Muhammad (s.a.w.) hakufundisha siasa Misikitini!

Ufafanuzi

Mtazamo wa Imam Hussein na Nabii Issa (a.s)

Mtazamo wa Imam Hussein na Nabii Issa (a.s) MTAZAMO WA IMAM HUSSEINI NA NABII ISSA (A.S) Haki na Uadilifu katika Mtazamo wa Imam Hussein na Nabii Issa Masiih (as) Tarehe 25 Disemba inasadifiana na siku ya kuzaliwa Nabii Issa Masiih amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake. Kuzaliwa kwa mtukufu huyu kulihuisha moyo wa udugu, imani, upendo na mahaba kati ya wanadamu. Issa Masiih (as) alizaliwa katika kizazi kilichokuwa mashuhuri kwa usafi na utukufu. Alitumwa kuondoa ujinga na dhulma na kueneza nuru ya imani, maarifa na upendo baina ya Banii Israel. Bibi Maryam mtakasifu, mama yake Nabii Issa (as) alipopata habari kuwa ni mja mzito, alishikwa na mshangao mkubwa na huzuni na baadaye kidogo akajiwa na bishara njema kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Malaika wa wahyi na ufunuo alimwendea na kumwambia: Ewe Maryam! Mola wako amesema kazi hii ni nyepesi mno kwangu, ili tumfanye muujiza kwa watu na rehema kutoka kwatu na jambo hilo limekwishahukumiwa". (Maryam-21)

Ufafanuzi

DA'AWA KWA WATU WA THAMUUD

DA'AWA KWA WATU WA THAMUUD DA'AWA KWA WATU WA THAMUUD Nabii Swaalih  alikuwa ni Mtume katika kabila maarufu ambalo jina lake linatokana na jina la Babu yao Thamuud ambaye ni katika ukoo wa Nabii Nuuh Kwa hivyo jina lake ni Swaalih ibn 'Ubayd ibn Maasih ibn 'Ubayd ibn Haajir ibn Thamuud, ibn 'Aabir ibn Iram, ibn Saam, ibn Nuuh. Naye Swaalih na watu wake wa Thamuud ni waarabu waliokuwa wakiishi Hijr ambayo iko baina ya Hijaaz na Tabuuk (Kaskazini magharibi ya Madiynah) ambako siku moja Mtume alipita wakati wanaelekea kwenda kwenya vita vya Tabuuk kama tutakavyoelezea mwisho wa kisa hiki. Hiki ndio kisa chake Nabii Swaalih  na watu wake kama tulivyoelezewa katika aya mbali mbali za Qur'aan Watu wa Thamuud walikuwa ni watu baada ya Nabii Huud ambao walikuwa wakiabudu masanamu na baada ya kuletewa Nabii Huud na kumkanusha Allaah Aliwaangamiza. Na baada ya miaka, watu wa Thamuud wakaibuka na kuwa na nguvu na ufahari. Nao pia waliabudu masanamu, kwa hivyo Allaah Akawatumia mjumbe miongoni mwao naye ni Nabii Swaalih ambaye naye kama kawaida ya Mitume alikuja na wito uleule wa kuwaita watu katika Tawhiiyd ya Allaah yaani kumuabudu Yeye pekee bila ya kumshirikisha na kitu, na kuwanasihi waache ibada ya masanamu na pia kuwataka watubu kwa Mola wao kwa kufuru wanayoifanya.

Ufafanuzi

KUZALIWA KWA NABII YAHYA (A.S)

KUZALIWA KWA NABII YAHYA (A.S) KUZALIWA KWA NABII YAHYA (A.S) Kuzaliwa kwa Nabii Yahya ni kutokana na dua ya Baba yake Nabii Zakaria wakati alipomuona Sayyida Mariam akiruzukiwa na Mola wake vyakula na matunda wakati ambao ilikuwa si musimu wake. Nabii Zakaria akapata matumaini makubwa ya kumuomba Mola wake ili naye amruzuku mtoto ambaye atashika mahali pake baada ya kifo chake. Baada ya Nabii Zakaria kumuomba Mola wake kwa siri, Mwenyezi Mungu S.W.T. alimuahidi kwamba atazaa mtoto atakayemwita Yahya. Mwenyezi Mungu S.W.T. amemsifu sana Mtume Wake Yahya ndani ya Qur-ani Tukufu kwamba alikuwa Nabii mchaMungu sana na hata inasemekana siku moja watoto wenzake walimwendea wakamwambiya: “Ewe Yahya! Twende tukacheze.” Akawajibu: “Mimi sikuumbwa kucheza.” Kwa ile khofu aliyokuwa nayo Yahya A.S., Nabii Zakaria alikuwa akitaka kuwatolea mawaidha Ma-Bani Israil, basi kwanza hugeuka kushoto na kulia kumwangalia Yahya, ikiwa yupo nao, basi alikuwa hazungumzii kuhusu “Moto na Pepo.” Kwani siku moja Nabii Zakaria alizungumzia kuhusu “Moto na Pepo” na Yahya A.S. alikuwa nao lakini kajificha mahali, mara tu aliposikia kuhusu khabari za Moto na adhabu zake Yahya A.S. alikimbia mbio kisha wakaanza kumtafuta mpaka wakampata. Yahya A.S. alimuomba mama yake amshonee nguo za sufi ili naye akashiriki katika ibada katika Msikiti wa Baitil Muqaddas, lakini mama yake alimwambia kwamba mpaka akubali baba yake, Nabii Zakaria alipoelezewa akamjibu Yahya A.S.

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini