Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

Elimu ya fiq-hi

RUHUSA YA KUWALILIA WAFU

RUHUSA YA KUWALILIA WAFU

RUHUSA YA KUWALILIA WAFU Hapana shaka kwamba kuwalilia wafu Waumini ni jambo linalofaa katika Uislamu kutokana na dalili ya kitendo cha Mtume (s.a.w.w) kuhusu jambo hilo. Mtume kulitenda tendo hili kumekaririka mara nyingi na pahala pengi kama ifuatavyo: Mara ya kwanza ni siku alipofariki ami yake na mlezi wake Bwana Abu Talib. Ya pili ni siku alipouawa kishahidi ami yake Mtume Bwana Hamza katika vita vya Uhud. Ya tatu siku alipopata Shahada (kuuawa) Bwana Jaafar Bin Abi Talib na Bwana Zaid Bin Harith na Bwana Abdallah Bin Ruwah, wote hawa waliuawa katika vita ya Muuta. Ya nnei, ni siku alipofariki Bwana Ibrahim ambaye ni mtoto wake mwenyewe Mtume (s.a.w.w). Mtume (s.a.w.w) alimlilia mwanawe huyu kiasi ambacho kilimfanya Bwana Abdurahman bin Auf amwambie Mtume (s.a.w.w): "Na wewe unalia Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu"? Bwana Mtume (s.a.w.w) akasema: "Ewe mwana wa Auf hiyo ni alama ya Huruma".

Ufafanuzi

KUUNGANISHA SALA MBILI

KUUNGANISHA SALA MBILI KWA NINI MASHIA HUSALI KWA KUUNGANISHA SALA KWA PAMOJA DHOHR – ASR NA MAGHRIB – ISHA Baadhi ya watu huuliza ni kwa nini Mashia’ husali kwa kuunganisha pamoja sala ya Adhuhuri – Alasiri na Maghrib – ‘Isha wakati ambapo wengi wa Waislamu husali kwa kutenganisha sala hizo ? Kwa kulijibu swali hili sisi tutawaleteeni kwa mapana maamrisho yote tunayoyafuata yanatokana na kumfuata Mtume Muhammad s.a.w.w. Ama kuhusu sala, namna ya kusali, nyakati zake na namna ya kufanya wudhu na shariah zote zimetokana na Qur’n, Mtume Muhammad s.a.w.w.na Ahlul Bayt a.s. Ingawaje Madhehbu mengine yanadai kuwa wanafuata Quran na Sunnah, lakini madai yao matupu bila ya uthibitisho, haiwezi kuthibitisha ukweli wowote. Kwa hakika sisi tunavyofuata kwa vithibitisho na Sunnah, ni kwa hakika kweli na hakiki kwa kutokana na shakhsiyyah wenyewe i.e. Ahul-Bayt a.s. ambao ni wananyumba ya Mtume Muhammad s.a.w.w. na ambao walikuwa wakiishi nae na walijua kila kitu kuhusu misemo na matendo yake yote. Bila shaka hakuna wa kukana ukweli na uhakika huu ! Kutafsiri na kuielewa Quran Tukufu inategemea sana Ahadith. Na hapa ni lazima kabisa kutegemea Ahadith zile zilizo sahihi na kweli (zisiwe zimebuniwa ). Hakuna shaka kuwa sisi Mashia’ tunafuata Sunnah sahihi na kweli kabisa ambayo tumeipokea kutoka kwa Ahlul Bayt a.s. ya Mtume Muhammad s.a.w.w. na ndiyo mwongozo wetu sahihi wa kuifuata Qur'an Tukufu na Mtume Muhammad s.a.w.w. .

Ufafanuzi

KWANI NI LAZIMA KUSUJUDU JUU YA UDONGO WA KARBALA?

KWANI NI LAZIMA KUSUJUDU JUU YA UDONGO WA KARBALA? KWANI NI LAZIMA KUSUJUDU JUU YA UDONGO WA KARBALA? Hapana si lazima! Bali Mashia wanapendelea kusujudu juu ya mchanga uliotoka mji wa Karbala kwa sababu ya umuhimu wake uliopewa na Mtume (s.a.w.w.) na Maimam kutoka kwenye kizazi chake (Ahl al-Bayt). Na baada ya kuuwawa shahid kwa Imam Husein (a.s.), mwanawe Imam Zayn al-'Abidin (a.s.) aliuteka mchanga wa hapo kidogo na akautangaza kwamba huo ni mchanga mtukufu na akauhifadhi kwenye mkoba. Na Maimam (a.s.) walikuwa waki sujudu juu ya udongo huo wa Karbala na wakiutengenezea tasbih, kwa kumtakasa Mwenyezi Mungu kwayo. [Ibn Shahrashub, al-Manaqib, Juz. 2, Uk. 251] Vilevile waliwahimiza Mashia kusujudu juu ya udongo huo, kwa kuelewa kwamba si wajib, bali kwa mtazamo wa kupata thawabu zaidi. Maimam (a.s.) wamesisitiza kwamba kumsujudia Mwenyezi Mungu ni lazima kufanywe juu ya ardhi tohara tu, na hivyo wakapendelea kufanywe juu ya udongo wa Karbala. [al-Tusi, Misbah al-Mutahajjad, Uk. 511] [al-Saduq, Man la yahduruhu'l faqih, Juz. 1, Uk. 174] Mashia, kwa muda mrefu wameuhifadhi udongo huu. Na kwa kuchelea usije ukavunjiwa heshima, ndipo wakautengeneza vipande vidogo vidogo vinavyoitwa Muhr au Turbah. Wakati wa Swala, tunasujudu juu ya udongo huo, lakini si kwa kuwa ni wajib, bali ni kwa mtazamo wa kuwa huo ni umbile maalum. Vinginevyo, tunapokuwa hatuna udongo tohara, tunasujudu kwenye ardhi liyo tohara, au juu ya kitu kinachotokana nayo.

Ufafanuzi

KUCHANGANYA SWALA

KUCHANGANYA SWALA KUCHANGANYA SWALA Hata kama imeruhusiwa, kwa nini kufanya hivyo? Hakuna anayesema kuwa kuna ubaya kuziswali Swala bila ya kuzikusanya. Swala za Dhuhr na `Asr, pia Maghrib na 'Isha' zinaweza kuswaliwa, aidha, kwa kukusanywa au kwa kutenganishwa. Hata hivyo, kukusanya Swala mbili kulikofanywa na Mtume (s.a.w.w.) kunaonyesha huruma ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ya kuwarahisishia ummah, na ziko sababu kwa nini imekuwa ni ada miongoni mwa Mashia, nazo ni: " Watu mara nyingi wana shughuli na majukumu yao mengi, hususan katika nchi ambazo utaratibu wa nchi hizo wa kielimu na kikazi haukidhi mahitaji ya Waislamu ya kuweza kuswali Swala zao tano za kila siku. Baadhi ya kazi hufanywa kwa masaa mengi mfululizo, bila ya kuingiliwa. Kwa hivyo, ni vizuri, na ili kujiepusha na kukosa Swala ya pili, Shia huziswali mbili katika kipindi kimoja, iwe ni mapema au baadaye katika wakati wanaouchagua. " Ni pale watu wanapokutana kutoka mbali ili kuswali mojawapo ya Swala hizo mbili; na kwa kuwa imeruhusiwa kukusanya zote mbili, wao huziswali zote mbili kwa jamaa, moja baada ya nyingine. Kwa njia hii wanakuwa wametekeleza yote, wajib na kuswali kwa jamaa (jama'ah) na hivyo kupata thawabu zaidi. Hebu mathalan angalia mfano wa Swala ya Ijumaa. Tumeona kwamba maelfu ya ndugu zetu wa kisunni huswali Swala za Ijumaa kwa wakati wake kabisa, lakini wengi wao hawapati kuswali Swala ya `Asr, wacha kuswali kwa jamaa. Kwa upande mwingine Mwislamu Mshia anayeswali Swala ya Ijumaa, ataweza kuiswali Swala ya `Asr kwa jama'ah.

Ufafanuzi

SWALA KWA MUJIBU WA QUR-ANI NA SUNNAH

SWALA KWA MUJIBU WA QUR-ANI NA SUNNAH A: SWALA KWA MUJIBU WA QUR-ANI NA SUNNAH Ewe ndugu yangu mpenzi; hebu kwa msaada wa Mwenyezi Mungu Mtukufu tuzianze nasaha zetu kwa kumuomba Mola wetu Mtukufu atuwafikshe na kutuongoza katika kuijua haki, kuikubali na ksha kuifuata-Aamiyn Baada ya dua hiyo, hebu sasa tutazame kwa pamoja natujiulize nini hukumu ya ibada ya swala ndipo tutafahamu ni ipi nafasi na hukumu ya mtu asiye swali . Ndugu yangu mpenzi, elewa na ufahamu kwamba swali katika sheria ni FARDH yaani WAJIBU. ishara na dalili bayana kwamba swala ndio kielelezo kikubwa cha Imani ya mja. Kwa maneno mengine tunaweza kusema kuwa hana Imani, mtu asiyeswali. Ikiwa mtu hana Imani , vipi unamtazamia kuwa na dini? Hii ndio maana Bwana Mtume -Rehema na Amani zimshukie akasema: Mkimuona mtu aizoya Msikiti basi mshudieni kuwa yuna Imani kauli hii ya Bwana Mtume inazidi kutuonyesha ukweli usio pingika kwamba swala ndio nembo na kielelezo kikubwa cha Imani ya mja. Tukilizingatia neno la mwanzo lilotumika katika aya (HIFADHINI) tukaliweka katika sarufi ya kiarabu (Arabic Grammar), tutaambiwa na watu wa fani ya lugha kuwa neno hili ni tendo la amri. Kwa hivyo basi neno hili (HIFADHINI) linamaanisha kuwa suala la kuhifadhi swala ni amri itokayo kwa Mwenyezi Mungu kuja kwa waja wake na wala sio ombi. Sasa kama tunakubaliana na ukweli huu ulio dhahiri kuwa swala ni amri ya Mola amuamrisha mja wake, je! Huoni kwamba kuacha swala ni kupinga na kuivunja amri ya Muumba wako? Avunjaye na kupinga amri ya Bwana wake hufanywaje na Bwana wake, hasa ukizingatia kwamba siku zote amri hutoka kwa Mkubwa aliye kuja juu kwa mdogo aliye chini kama ambavyo ombi hutoka kwa aliye chini kuja kwa aliye juu. Hebu jaribu kuwa mkweli, mwanao au mkeo akivunja amri yako, unakuwaje na unchukua hatua gani? Ukiukir ukweli huu ndipo utaiona nafasi yako mbele ya Mola wako wewe usiyetaka kumsujudia Mola wako.

Ufafanuzi

SWALA ZA WAJIBU

SWALA ZA WAJIBU SWALA ZA WAJIBU ASSALAAM ALAIKUM Katika sehemu iliyopita kwa ufupi tumezungumzia umuhimu wa Swala, tukasema kwamba mtu mwenye kuswali ni lazima ajue anapokuwa anaswali anazungumza na nani?,kitendo cha kutambua anazungumza na nani kitamfanya kuzingatia swala hiyo anayoiswali au anayotaka kuiswali,ama yule anayeswali pasina kuzingatia swala yake ni kama mtu asiye swali kabisa bali anakuwa miongoni mwa wale ambao Allah (s.w) kawazungumzia katika Qur'an Tukufu akisema: "Basi ole wao wanao swali, ambao wanapuuza (maamrisho ya) Swala zao." Ama somo letu la leo tutazungumzia kuhusu swala za wajibu. Swala za wajibu ni sita. 1-Swala tano za kila siku 2-Swala ya Ayaat 3-Swala Maiti 4-Swala ya Twawafu (ya wajibu) 5-Swala ya Qadhaa ya baba na mama. Ikiwa baba au mama amekufa na alikuwa na swala ambayo ilikuwa wajibu kwake aiswali na hakuiswali kwa sababu kadhaa wa kadhaa,basi itabidi amhusie mtoto wake wa kwanza wa kiume alipe swala hiyo au swala hizo,na ikiwa hakuacha usia,ikiwa motto atajua kuwa baba au mama alikuwa na swala kadhaa hakuziswali na niza wajibu,basi itatakiwa ni wajibu kwake kuswali swala hizo.Hivyo swala hii/hizi huitwa swala ya/za Qadha ya/za baba au mama {yaani swala ya/za kulipa zile swala ambazo zilikuwa katika dhimma ya baba au mama au zilikuwa ni wajibu kwa baba au mama kuziswali}.Swala hii ya Qadha ni wajibu kwa motto wa kwanza wa kiume kuziswali.

Ufafanuzi

MAFUZO YA KIISLAAM SEHEMU YA PILI

MAFUZO YA KIISLAAM SEHEMU YA PILI SWALA ZA WAJIBU ASSALAAM ALAIKUM Katika sehemu iliyopita kwa ufupi tumezungumzia umuhimu wa Swala, tukasema kwamba mtu mwenye kuswali ni lazima ajue anapokuwa anaswali anazungumza na nani?,kitendo cha kutambua anazungumza na nani kitamfanya kuzingatia swala hiyo anayoiswali au anayotaka kuiswali,ama yule anayeswali pasina kuzingatia swala yake ni kama mtu asiye swali kabisa bali anakuwa miongoni mwa wale ambao Allah (s.w) kawazungumzia katika Qur'an Tukufu akisema: "Basi ole wao wanao swali, ambao wanapuuza (maamrisho ya) Swala zao." Ama somo letu la leo tutazungumzia kuhusu swala za wajibu. Swala za wajibu ni sita. 1-Swala tano za kila siku 2-Swala ya Ayaat 3-Swala Maiti 4-Swala ya Twawafu (ya wajibu) 5-Swala ya Qadhaa ya baba na mama. Ikiwa baba au mama amekufa na alikuwa na swala ambayo ilikuwa wajibu kwake aiswali na hakuiswali kwa sababu kadhaa wa kadhaa,basi itabidi amhusie mtoto wake wa kwanza wa kiume alipe swala hiyo au swala hizo,na ikiwa hakuacha usia,ikiwa motto atajua kuwa baba au mama alikuwa na swala kadhaa hakuziswali na niza wajibu,basi itatakiwa ni wajibu kwake kuswali swala hizo.Hivyo swala hii/hizi huitwa swala ya/za Qadha ya/za baba au mama {yaani swala ya/za kulipa zile swala ambazo zilikuwa katika dhimma ya baba au mama au zilikuwa ni wajibu kwa baba au mama kuziswali}.Swala hii ya Qadha ni wajibu kwa motto wa kwanza wa kiume kuziswali.

Ufafanuzi

HOTUBA YA IJUMAA

HOTUBA YA IJUMAA VITENDO VYA MWENYEZI MUNGU Lazima iwepo sababu juu ya kila kitu kilichoumbwa na Mwenyezi Mungu. Lakini si lazima tuifahamu kila sababu. Tunasema kwamba kila kazi ya Mwenyezi Mungu ni ya ajabu na ikiwa jambo barabara kutendwa. Mara nyingi tunasumbuka kutokana na baadhi ya matukio au baadhi ya matatizo kwa sababu hatujui ni nini hasa sababu zilizo nyuma yake. Mfano unaweza kuonekana katika Qurani, ambapo kukutana kwa Nabii Musa (a.s.) na mtu mwingine mwenye elimu zaidi kuliko Nabii Musa (a.s.) unaelezwa. Mtaalamu alimruhusu Musa kufuatana naye kwa sharti kwamba "Usiniulize kuhusu jambo lolote mpaka mimi mwenyewe nikuelezee." Hii ni hadithi nzima:- "Akasema (yule mtaalamu): Hakika wewe huwezi kuvumilia kuwa pamoja nami. Na unawezaje kuvumilia juu ya lile usilolijua? Akasema (Musa): Kwa yakini Akipenda Mwenyezi Mungu utanikuta mvumilivu wala sitaasi amri yako (18:67 69) Nabii Musa (a.s.) na mtalaamu walipanda jahazini. Na walipokuwa jahazini, mtaalamu akalitoboa. Musa akapinga, na wakaelekea mjini, huko mtaalamu alimkuta kijana mmoja, akamkamata na kumchinja. Kwa jambo hilo, Musa hakuweza kujizuia, akamlaumu kwa maneno makali. Akakumbushwa tena ile ahadi yake ya kutouliza maswali.

Ufafanuzi

IBADA YA HIJA

IBADA YA HIJA IBADA YA HIJA Hija ni ibada kubwa inayokusanya ibada kadhaa. Umuhimu wa ibada ya hija umo katika ahadi iliyowekwa baina ya mja na Mola wake Muumba. Imepokelewa katika hadithi zinazotaja utukufu wa ibada ya hija kwamba "Mtu anayefariki dunia hutamani kwamba laiti angetoa dunia na yaliyomo kwa ajili ya kufanya hija walau mara moja katika maisha yake. Imam Ja'far Sadiq (as) ambaye ni miongoni mwa Watu wa Nyumba tukufu ya Mtume wetu Muhammad (saw) amesema: "Watu wanaofanya hija au umra ni wageni wa Mwenyezi Mungu. Kama watakuwa na haja basi atawakidhia, na kama watamuomba, atajibu maombi yao, na iwapo watanyamaza kimya na wasimuombe chochote, basi Yeye Mwenyezi Mungu atawapa bila ya wao kumuomba." Hija ni ibada inayokusanya mambo mengi yanayomkurubisha mja kwa Mola wake Karima. Ni shule ya kutoa malezi na maarifa kwa waja kwa msingi wa tauhidi na kumpwekesha Mwenyezi Mungu. Safari hiyo ya hija huanza kwa kuwekwa nia safi na ikhlasi na kukamilika kwa ibada na amali makhsusi. Mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu huanza ibada hiyo kwa kufanya ihram katika maeneo maalumu yanayojulikana kwa jina la Miqaat na hapo huvaa vazi la ihram.

Ufafanuzi

HIJA NA UMUHIMU WAKE

HIJA NA UMUHIMU WAKE HIJA NA UMUHIMU WAKE Msimu wa Hija ni machipuo ya umaanawi na kung'ara kwa tauhidi katika upeo wa dunia; na ibada ya Hija, ni chemchemi safi inayoweza kuwatakasa mahujaji na uchafu wa madhambi na mghafala, na kurejesha ndani ya nyoyo na nafsi zao atia ya Mwenyezi Mungu ya nuru ya fitra na maumbile. Kulivua vazi la majivuno na la kujipambanua na wengine katika makutano ya Hija, na kuvaa vazi la pamoja na la rangi moja la Ihramu, ni alama na nembo ya kuwa na hali moja umma wa Kiislamu, na ni hukumu ya dhihirisho la umoja na kuwa kitu kimoja Waislamu wa sehemu zote duniani. Msimu wa Hija ni machipuo ya umaanawi na kung'ara kwa tauhidi katika upeo wa dunia; na ibada ya Hija, ni chemchemi safi inayoweza kuwatakasa mahujaji na uchafu wa madhambi na mghafala, na kurejesha ndani ya nyoyo na nafsi zao atia ya Mwenyezi Mungu ya nuru ya fitra na maumbile. Kulivua vazi la majivuno na la kujipambanua na wengine katika makutano ya Hija, na kuvaa vazi la pamoja na la rangi moja la Ihramu, ni alama na nembo ya kuwa na hali moja umma wa Kiislamu, na ni hukumu ya dhihirisho la umoja na kuwa kitu kimoja Waislamu wa sehemu zote duniani.

Ufafanuzi

NYAMA YA NGURUWE

NYAMA YA NGURUWE KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU NYAMA YA NGURUWE BAYANA YA KISAYANSI Mwenyezi Mungu Amesema : " Sema; " Sioni katika yale niliyofunuliwa mimi kitu kilichoharamishwa kwa mlaji kukila isipokuwa kiwe ni mzoga au damu inayomwagika au nyama ya nguruwe, kwani hiyo ni uchafu; au kile ambacho kwa kuhalifiwa amri ya Mwenyezi Mungu kimechinjwa kwa jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Lakini aliyelazimika kula pasipo kupenda wala kuchupa mipaka, basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe na Mwingi wa kurehemu." Aya ya 145, Suratul An-aam. UHAKIKA WA KISAYANSI Imekuja elimu kudiriki baadhi ya mambo yaliyokatazwa na sheria ya Kiislamu iliyohifadhiwa na wafuasi wake karne kwa karne kabla ya kugunduliwa kwa darubini na kwa mpangilio huo huo : Mzoga ambao bakteria hukua ndani yake, damu ambayo bakteria hukua ndani yake kwa kasi kubwa zaidi, hasa ikiwa ni nyingi, na mwisho nguruwe ambapo katika mwili wake hukusanyika jumla ya vijiumbe maradhi visivyoondoka kwa kuoshwa. Mdomo ni maficho ya vijidudu, bakteria na virusi vinavyokwenda kwa binadamu na wanyama. Baadhi yake vinamhusu nguruwe, mfano wa kidudu kiitwacho Trchinella, nywelenywele ziitwazo Balantidium Dysentery, wadudu wa tumbo (Taenia Solium) na mchango wa nguruwe (Spiralis). Baadhi yake huingizwa kwenye maradhi mengi ya pamoja baina ya binadamu ( Cysticercosis & Influenza) na wanyama. Minyoo (Ascaris na Fasciolopsis Buski) hupatikana kwa wingi nchini China. Maradhi ya Balantidiasis hupatikana kwa wachunga nguruwe na wenye kuchanganyika nao, na yanaweza kuenea kwa sura ya mlipuko kama ilivyotokea katika moja ya visiwa vya bahari ya Pacific baada ya kimbunga.

Ufafanuzi

IBADA ZA VITENDO

IBADA ZA VITENDO IBADA ZA VITENDO 1) Kusimamisha Sala MwenyeziMungu anasema: "Wala hawakuamrishwa ila kumwabudu MwenyeziMungu kwa kumtakasia dini, wawache dini za upotofu (upotevu) na wasimamishe Sala na kutoa Zaka, hiyo ndio dini iliyo sawa . (Suratul - Bayyinah - 5) Na anasema katika kuelezea wasfu wa walioamini: "Watu ambao biashara wala kuuza hakuwashughulishi (hakuwasahaulishi) kumkumbuka MwenyeziMungu na kusimamisha Sala na kutoa Zaka, wanaiogopa siku ambayo nyoyo zitadahadari na macho pia", (An - Nur -37). Na anasema: "Wale ambao tukiwamakinisha (tukiwaweka uzuri) katika ardhi, husimamisha Sala na wakatoa Zaka na Wakaamrisha yalio mema na Wakakataza yalio mabaya. Na marejeo ya mambo ni kwa MwenyeziMungu". (Al - Hajj - 41). Na anasema:- "Na waamrishe watu wako kusali na uendelee mwenyewe kwa hayo. Hatukuombi riziki bali Sisi ndio tunaokuruzuku na mwisho mwema utawathubutukia wamchao Mungu." (Taha - 132)

Ufafanuzi

IBADA ZA MATAMSHI

IBADA ZA MATAMSHI IBADA ZA MATAMSHI 1- Kuzitamka Shahada Mbili Hauwi sahihi Uislamu wa mtu iwapo hajazitamka shahada mbili, isipokuwa bubu ambaye vinatosheleza vitendo vyake vitakavyoonyesha dalili ya imani yake. Mtume (SAW)amesema: Nimeamrishwa nipigane vita mpaka watu washuhudie kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa isipokuwa Allah na kwamba Muhammad ni Mtume wa MwenyeziMungu na wasimamishe Sala na Watoe Zaka. Watakapotimiza hayo watakuwa wamezuilika kwangu damu zao na mali zao ila kwa haki ya Uislamu [6]na hesabu yao itakuwa kwa MwenyeziMungu>>. (Bukhari na Muslim). 2- Kumtaja na kumtukuza Mungu Kumdhukuru(kumtaja) MwenyeziMungu, Kumsabihi(kumtukuza) na Kumwomba Maghufira MwenyeziMungu anasema: "Enyi mlioamini! Mkumbukeni MwenyeziMungu kwa wingi na mtukuzeni asubuhi na jioni".

Ufafanuzi

VUNJA JUNGU NI MAASI

VUNJA JUNGU NI MAASI VUNJA JUNGU NI MAASI Assalaamu Alaykum Warahmatullah! Ni baada ya siku chache tu kwa msaada wake Allah Karim utakuwa unapumua na kuishi ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani. Mwezi ambao huwapa waislamu fursa ya kuitekeleza mojawapo ya nguzo tano za Uislamu, swaumu ya Ramadhani. Katika kuuheshimu, kuutukuza na kuuenzi mwezi huu mtukufu. Naam, Ramadhani hiyo mlangoni mwako inabisha hodi. Wewe kama muislamu umejiandaje kuupokea mwezi wako huu mtukufu? Je, wewe ni mmoja wa wale wanaoupokea mwezi wa Ramadhani kwa kile kinachojulikana kama VUNJA JUNGU? Hebu na tujiulize kwa pamoja, tulivunjao hilo jungu mwaka hata mwaka na wale tusiolivunja, vunja jungu ni nini khasa? Bila ya shaka mtakubaliana nasi kwamba vunja jungu kama litafsirikanavyo kutokana na matendo yatendwayo na wavunja jungu katika kulivunja kwao hilo jungu. Ni mkono wa kwaheri unaopungwa kwa maasi mbalimbali kwa ajili ya kuingia kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Wavunja jungu huitumia fursa ya zile siku mbili tatu kabla ya kuandama kwa mwezi mwandamo unaoashiria kuanza kwa funga tukufu ya Ramadhani.

Ufafanuzi

SHAABANI

SHAABANI MWEZI SHAABANI FADHILA ZA MWEZI WASHAABAN Kuna habari zilizo pokelewa kutoka kwa Mtume mkarimu (s.a.w.w) na pia kutoka kwa maimamu waongofu (a.s) zijulishazo kuwa ubora wa mwezi huu mtukufu na mkubwa ni nyingi  sana na malipo ndani ya mwezi huu ni mara dufu, kwa hakika imekuja na kupolekewa habari kutoka kwa ibnu Abbas ya kuwa amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) wakati maswahaba wake walipo kuwa wakizungumzia fadhila za mwezi wa Shaaban mbele yake: Ni mwezi mtukufu, nao ni mwezi wangu, na wabebaji wa Arshi ya Mwenyezi Mungu wanautukuza na wanafahamu haki ya mwezi huu, nao ni mwezi ambao huzidishwa ndani yake riziki za waumini kama ulivyo mwezi wa Ramadhan, na pepo hupambwa ndani ya mwezi huu, …nao ni mwezi ambao kufanya  matendo ndani yake hulipwa mara dufu, jema moja hulipwa kwa wema sabini, na kosa huanguka na kusamehewa, na madhambi hughufiriwa, na mema hukubaliwa, na Mwenye nguvu mwenyezi Mungu alie takasika Huwaelewa ndani ya mwezi huu waja wake, na huwaangali wafungaji  wa mwezi huu na wasimamji kwa ajili ya ibada, na kujifakharisha nao kwa wabebaji wa Arshi).

Ufafanuzi

NURU YA RAMADHANI

NURU YA RAMADHANI NURU YA RAMADHANI Ule mwezi mtukufu wa Ramadhani umetufikia tena Waislam kote ulimwenguni ni kipindi chetu cha kuzidisha Ibada kwani saumu ni tendo la Ucha mungu. Kula na kunywa kuanzia kurubio la kutoka usiku mkubwa kuingia alfajiri hadi kuchwa kwa jua yaani Magharibi. Mbali ya kuzuiliwa huko na kiamsha tumbo na kupooza koo, lakini pia yapo mambo kadhaa ni halali nayo kwa kuadhimisha na kuitikia wito na amri ya Mola nayo yamekatazwa kwa nyakati za mchana na kuidhinishwa yaendelee nyakati za usiku kwa waliostahiki ikiwemo taratibu za wana ndoa . Yale yote yaliyokuwa haramu khasa , nayo uharamu wake unabaki vilevile na kuyatenda katika mwezi huu mtukufu ni dhambi za hali ya juu zaidi na ni jeuri kwa Muumba. Mwezi huu una siri nyingi kwa wafungao, ikiwemo utengenezaji wa afya zao, maadili yao ya kuishi na utafutaji wao wa ridhiki. Miji na nyumba huwa baridi, magomvi hupungua huruma huzidi na tabia zilizozoweana na baadhi yetu hujikanya sisi wenyewe tuziepuke ili saumu zetu zisibatilike.Pana ucha Mungu huu ambao wenye akili hukimbilia na kuongeza maombi yao kwa M/Mungu , lakini mwezi huu kwa bahati mbaya wapo wanaoupatia faida yake na wapo wataopata khasara muda wote huku wamekaa na njaa ya bure. Kwa kuwa Mola huangalia yale yaliyo nyoyoni mwetu, basi anawajua wale wote wanaomuabudu kwa dhati kwenye ibada hii ya saumu na wale ambao wanawachelea wanaadam kuwanongona. Mola anawatambua pia wale wanaosikitika kwa kufika mwezi huu ambao pato lao la kila siku wanadhani limekosekana kwa mwezi huu kuwa pingamizi kwao.

Ufafanuzi

RAMADHANI HUKO T.Z

RAMADHANI HUKO T.Z RAMADHANI TANZANIA Tanzania haitafautiani na nchi nyingine za Afrika Mashariki katika kuupokea Mwezi Mtukufu wa Ramadhani . Unapokaribia mwezi wa Ramadhani Waislamu wa Tanzania hujitayarisha kwa hali na mali , wengi huwa na furaha isiyokifani kwani Wanaamini kwamba mwezi huu wa baraka na Imani za waja huongezeka maradufu. Unapoingia mwezi 29 Shaabani Waisilamu huanza kufuatilia kuandama mwezi na baada ya sala ya Magharibi tu Waumini hushughulika katika kuangalia mwezi.Mandhari za watu na mienendo yao iliyozoeleka nayo hubadilika , Mahoteli mengi hufungwa na hili huonekana wazi kwa upande wa visiwa vya Zanzibar, vyenye wakaazi wengi waislamu, wakinamama nao huvaa huijabu na kujitanda vizuri wakielewa kuwa mwezi wa Ibada umewadia. Misikiti inamiminika Waumini kwa kutekeleza ibada za swala za faradhi na za Sunna kama vile Tarawehe ,Tahajudi, na Witri katika sura ambayo Waumini wanaiishi katika kipindi chote cha kuingia hadi kumalizika mwezi Mtukufu, na hasa katika kumi la mwisho la Ramadhani ambapo Waislamu humiminika misikitini kwa ibada ya Itikafu kwa lengo la kutafuta Fadhila za Lailatul Kadri .Mgeni yeyote anayetembelea Tanzania hasa Zanzibar anaelewa kuwa , ni kweli mwezi Mtukufu umeingia.Darsa nyingi hufanyikamisikitini baada ya Sala ya Alasiri.

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini