Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

MAKALA MBALIMBALI

TAWASSULI (SEHEMU YA NNE)

TAWASSULI (SEHEMU YA NNE)

TAWASSULI (SEHEMU YA NNE)

Ufafanuzi

DU’A YA MWEZI WA RAMADHANI (SEHEMU YA 8)

DU’A YA MWEZI WA RAMADHANI (SEHEMU YA 8) DU’A YA MWEZI WA RAMADHANI (SEHEMU YA 8) UPANA DHAHIRI WA NENO ASIIR Kwa hakika, kipengele hiki cha du’a ni mojawapo ya vipengele vyenye kuumiza moyo. Watu wengi wasio na hatia ulimwenguni pote leo hii wanateseka vifungoni. Wakati ambapo kundi miongoni mwao ni waathiriwa wa ukandamizaji na uvunjaji wa sheria zilizotengenezwa na binadamu, kuna tabaka ambalo kwa kutokuwa kwao kabisa na hatia kumewafanya kuwa magerezani. Kuwa magerezani ni sehemu moja tu ya hadithi. Ukandamizaji na mateso ambayo wafungwa hawa wasio na hatia huyapata ni makali mno yasiyoelezeka. Aina hii ya utesaji husababishwa na aina ya mtazamo walionao maasikari wa magereza tofauti, ambao hupokea nguvu ya kuamua watakavyo kutoka kwa wakubwa zao, ambao nao wana mamlaka kutoka kwenye serikali zao. Maelezo yafuatayo kutoka shirika la kimataifa la haki za binadamu (Amnesty international) yanazungumzia ukweli huu: “Utesaji hautokei katika ombwe. Jamii na mazingira ya kisiasa, na usambazaji wa zana na mbinu kwa ajili ya kusababisha maumivu, hutegemea juu ya kushindwa kwa ridhaa ya kisiasa. Kama serikali za ulimwenguni zingelikuwa na ridhaa ya kisiasa kusimamisha mateso, zingelifanya hivyo.”7 Ili kuelewa uzito wa jambo hili, mtu anaweza kurejelea maandishi makhususi yanayopatikana, juu ya mateso gerezani katika Internet kutoka mashirika ya haki za binadamu, kama vile Human Rights Watch [hrw.org] na mfano kama hayo. Hata hivyo, kwa sababu ya ufupi wa ufafanuzi huu tutataja mifano mifupi ya hali ilivyo ya magereza ya ulimwenguni hapa: WAFUNGWA WANAOUMIA KWA MATESO 1) Wanaume, Wanawake Na Watoto “...lakini mateso yanaendelea na hayakuishia kwenye serikali za kidikteta za kijeshi au tawala za kimabavu; mateso yanafanywa pia kwenye serikali za kidemokrasia. Ni wazi pia kwamba waathiriwa wa mateso ni watuhumiwa wa makosa ya jinai na wafungwa wa kisiasa, watu wa kipato cha chini halikadhalika na wapinzani, watu wanaolengwa kwa sababu ya mitazamo yao hali kadhalika na imani zao. Wao ni wanawake na wanaume, watoto na watu wazima pia.”8 2) Wanawake: “ Amnesty International (AI) imeandika matukio mengi yasiyo na idadi ya wanawake kuteswa katika mahabusi. Katika maelezo yake ya mizozo ya kijeshi, imetoa taarifa ya mfumo unaotumika wa unyanyasaji wa kijinsia kama silaha ya kivita.”9 3) Watoto: Ukweli kwamba watoto wanaweza wakateseka kwa mateso, lazima kiwe ni kitu kibaya mno cha kusitusha. Utegemezi wao na kutokuwa kwao salama lazima kuwape wao kinga kutokana na maovu ya wakubwa wanayopeana wenyewe kwa wenyewe. Kutokuwa kwao kabisa na hatia lazima kuwaweke mbali na kufikiwa na maovu hayo. Bado mateso dhidi ya watoto yameenea; watoto wanateswa na polisi na mjeshi ya usalama

Ufafanuzi

DU’A YA MWEZI WA RAMADHANI 1

DU’A YA MWEZI WA RAMADHANI 1 DU’A NA KANUNI YA SABABU NA MATOKEO Katika kitabu chake ‘Chehl Hadith’ (Hadithi Arbaini), Imam Khomeini (Allah atukuze roho yake) anasimulia ushauri wa mawazo kutoka kwa mwalimu wake wa Irfani (elimu ya kiroho) Ayatullah Shah Abadi (r.a.) akisema: “Shekhe wangu ambaye ni arif mkubwa, moyo wangu uwe ni fidia kwake alikuwa akisema: ‘Usimlaani yoyote japokuwa ni kafiri ikiwa hujui alikuwa katika hali gani ila tu ikiwa umejulishwa na walii aliye Ma’asum kwa kuwa yawezekana kwamba alisilimu kabla ya kufa kwake.’ Kwa hivyo usiwe na mazowea ya kulaani laani bila ya kujua hakika ya unayemlaani.”10 Mahali pengine pia Imam amesema kuwa: Mwalimu wetu mkuu ‘Arif Shah Abadi, roho yangu iwe fidia kwake alikuwa akisema: ‘Usije ukamdharau yoyote hata kama ni kafiri, kwa kuwa kuna uwezekano wa yeye kuongoka kutokana na nuru iliyoko kwenye nafsi yake. Na ubaya na dharau zako, zikakusababishia hali mbaya na ya kuhuzunisha katika maisha ya akhera.11 Bila shaka kuamrisha mema na kukataza maovu ni tofauti na kudharau. Kwa hivyo ni bora kutowalaani makafiri kwa kuwa haijulikani mtu atafariki akiwa katika hali gani. Na lau utamlaani mtu kisha akafariki akiwa kwenye uongofu, hali yake hii yaweza kuwa kizuizi kwa maendeleo yako ya kiroho. Hivyo basi tunapokisoma kifungu hiki cha dua, yatakiwa tujishughulishe kutenda matendo mema kwa ajili ya waislamu waliofariki kwa hali halisi ya kuwatakia furaha waliokufa.

Ufafanuzi

LAKINI JE NENO MAWLA HALINA MAANA YA RAFIKI?

LAKINI JE NENO MAWLA HALINA MAANA YA RAFIKI? LAKINI JE NENO MAWLA HALINA MAANA YA RAFIKI? Japokuwa idadi kubwa ya Wanavyuoni wa Sunni wa zama zote na maoni yote wamethibitisha tukio hilo na maneno ya kihistoria ya Mtume (s.a.w.w.), lakini imekuwa ni vigumu kwao kukubaliana na yaliyotokea baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w.). Lakini nakala hii fupi haiwezi kutaja kwa ufafanuzi matukio hayo. La muhimu ni kwamba Wanavyuoni wengi wa Sunni wamedai kwamba Mtume (s.a.w.w.) alimtangaza 'Ali (a.s.) kuwa ni rafiki na msaidizi wa Waislamu! Kuna mitazamo mingi ya tukio hili inaoonyesha jinsi lilivyokuwa na umuhimu. Miongoni mwayo ni kufunuliwa kwa Aya nyingi za Qur'an, mkusanyiko mkubwa wa watu, hatua za mwisho za maisha ya Mtume (s.a.w.w.), watu kuthibitisha kwamba Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na mamlaka makuu, kupongezwa baada ya tukio hilo na 'Umar, na sababu sababu nyingine nyingi ambazo haitoshi kuzitaja katika nakala hii fupi; yote yanaonnyesha juu ya kutawazwa kwa wasii wa Mtume (s.a.w.w.). Ni dhahiri kwamba neno mawla lilitumika kwa maana ya mamlaka kamili baada ya Mtume na si kwa mamlaka ya muda tu.

Ufafanuzi

NI KINA NANI WALIOKUWAMO KATIKA AHLUL-BAYT?

NI KINA NANI WALIOKUWAMO KATIKA AHLUL-BAYT? NI KINA NANI WALIOKUWAMO KATIKA AHLUL-BAYT? Imeonyesha kwamba familia ya Mtume (s.a.w.) mara kwa mara hutajwa kama Ahlul-Bayt, 'Itrah na Aal - ikiwa ni pamoja na bintiye Fatima al-Zahra', mumewe Imam 'Ali, na watoto wao Imam al-Hasan na al-Huseyn (a.s.). Ikiwa ni familia ya watu watano, Mtume (s.a.w.) akiwa ni kiongozi wao, ambao walikuwa hai wakati Aya za Qur'an zikishuka kuhusu sifa zao kwa Mtume (s.a.w.). Hata hivyo, maimamu tisa kutoka kwa wajukuu wa Imam Husein (a.s.) pia ni katika wateule wa familia hii, wa mwisho akiwa ni Imam Mahdi (a.s.). Mtume (s.a.w.) amesema: " "Mimi na 'Ali na al-Hasan na al-Huseyn na wajukuu tisa wa al-Huseyn ni watakatifu na wenye heshima." [al-Juwayni, Fara'id al-Simtayn, (Beirut, 1978), Uk. 160. Fahamu kwamba heshima ya al-Juwayni kama Mwanachuoni mkuu wa Hadith imethibitishwa na al-Dhahabi katika Tadhkirat al-Huffaz, Juz. 4, Uk. 298, na pia Ibn Hajar al-'Asqalani katika al-Durar al-Kaminah, Juz. 1, Uk. 67] " "Mimi ni mkuu wa Mitume na 'Ali ibn Abi Talib ni mkuu wa mawasii, na baada yangu mawasii wangu watakuwa ni kumi na wawili, wa mwanzo wao akiwa ni 'Ali ibn Abi Talib na wa mwisho ni al-Mahdi." [al-Juwayni, Fara'id al-Simtayn, Uk. 160] " "Al-Mahdi ni katika sisi Ahlul-Bayt" na "al-Mahdi atakuwa ni katika familia yangu, katika wajukuu wa Fatima" [Ibn Majah, al-Sunan, Juz. 2, Uk. 519, Na.s 4085-6; Abu Dawud, al-Sunan, Juz. 2, Uk. 207]

Ufafanuzi

SAYYIDAT ZAINABUL-KUBRA (A.S).

SAYYIDAT ZAINABUL-KUBRA (A.S). SAYYIDAT ZAINABUL-KUBRA (A.S) Sayyidat Zainab ni mmoja kati ya watoto wa Imam Ali (a.s) na Fatima Az-zahraa (a.s).Imam Ali (a.s) alikuwa na watoto ishirini na saba (27) wakiume na wakike.Watoto hao mama zao ni tofauti. mtukufu msimaji makala hii naileta kwako kwa mnasaba wa mazazi ya mama huyo mtukufu, na ili kupata historia kamali ya mama huyo adhimu ungana nami mpaka mwisho mwa makala hii.

Ufafanuzi

HISTORIA YA UMMUL-BANIINA KWA UFUPI

HISTORIA YA UMMUL-BANIINA KWA UFUPI UTANGULIZI ASALAMU ALAIKUM WASOMAJI WAPENZI Sina budi kumshukuru Mola Mtukufu pamoja na kumtakia amani Mtume mtakatifu Yeye pamoja na kizazi chake, kwa mara nyengine tena Muumba Mtakatifu ameniwezesha kushika kalamu na kuyazungumzia maisha ya bibi Ummul-Banii katika Makala hii. Ninatarajia ndugu wasomaji mtafaidika kwa kiasi fulani kutokana na Makala hii. Hii ni makala maalumu ielezayo historia fupi juu ya mwanamke shupavu aliyejawa na fadhila, mwanamke ambaye alikuwa ni mke wa Imamu Ali (a.s) Baada ya kufiwa na mkewe wa mwanzo ajulikanaye kwa jina la Fatimatu Zahraa. Kipindi kirefu kilipita baada ya kufariki bibi Fatima Zahraa (a.s), huku Ali (a.s) akiwa katika hali ya ukiwa, na mwishowe Ali (a.s) alimuendea nduguye ajulikanaye kwa jina la Aqiil, na kumtaka amchunguzie mwanamke aliye shujaa katika makabila ya Kiarabu. Aqiil alikuwa ni mjuzi sana wa kuzitambua Nasabu za makabila Kiarabu, hapo basi Aqiil hakuchelewa kuyatekeleza maamrisho ya nduguye, na muda si mrefu akawa ameshakuja na habari nono mbele ya Imamu Ali (a.s). Jicho la Aqiil halikumuona mwanamke aliyekuwa na ubora pamoja na ushujaa zaidi kuliko Fatima Kilaabiyya (Ummul-Baniina), na hapo ndipo lilipo angukia chaguo la Aqiil. Imamu Ali (a.s) kwa kuwa alikuwa akimuwamini vizuri sana nduguye (Aqiil) katika utambuzi na ujuzi wake wa kuyatambua makabila mbali mbali ya Kiarabu pamoja na Nasabu zake, akawa ni mwenye kuridhika na chaguo la nduguye, muda si mrefu Ali (a.s) akatuma posa na hatimae ndoa ikafungwa.

Ufafanuzi

BIBI ZAINAB (A.S)

BIBI ZAINAB (A.S) BIBI ZAINAB (A.S) Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amelipongeza taifa la Iran kwa mnasaba wa kuadhimisha siku ya kuzaliwa Bibi Zainab bint Ali (sa) ambayo inaadhimishwa hapa nchini kama Siku ya Wauguzi. Huku akiashiria taathira za harakati ya kihistoria ya mtukufu huyo katika Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na mchango wa imani na masuala ya kiroho katika uwezo na adhama ya mapinduzi hayo, amesema: "Jambo lililolifanya taifa la Iran liwe kigezo na kutoa ilhamu katika dunia ya Kiislamu kwenye kipindi cha miaka 30 iliyopita ni kufuata shakhsia adhimu wa kidini akiwemo Bibi Zainab (as). Ameongeza kwamba uwezo wa taifa la Iran unatokana na kuathirika na masuala hayo ya kimaanawi. Ayatullah Ali Khamenei amesema kuwa uwezo wa taifa la Iran hautokani na zana za kijeshi na kuongeza kuwa japokuwa taifa hili limepiga hatua kubwa za maendeleo katika nyanja za zana za kujilinda, lakini sababu kuu ya uwezo na adhama ya nchi na taifa la Kiislamu ni imani yake.

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini