Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

Elimu za Qurani

UANDISHI WA QURANI

UANDISHI WA QURANI

UANDISHI WA QURANI KUANDIKWA KWA QUR'ANI TUKUFU (SEHEMU YA PILI). {2}-KUPANGILIA AU KUUNDA AYA ZAKE KATIKA KILA SUURA. Upangiliaji wa aya za Qur'an Tukufu kila suura katika utaratibu huu tunaouona katika Qur'an Tukufu, suala hili lilitimia -kwa wingi sana -kulingana na jinsi aya zilivyokuwa zikishuka: Mfano: Suura ilikuwa ikianza na (بسم الله الرحمان الرحيم) kisha aya zote zinazoshuka baada Bislmillah Ar-rahmaan Ar-rahiim zinaandikwa au zinapangwa katika Suura hii, zikifuatana moja baada ya nyingine kwa hatua kulingana na kushuka kwa aya, mpaka inaposhuka Bismillah Ar-rahmaan Ar-rahiim nyingine,basi hapo inajulikana kuwa Suura hii imeisha na imeanza Suura nyingine. Imam (wa sita) Jaafar Swaadiq (a.s) amesema: "Kuisha kwa Suura kulikuwa kunajulikana kwa kushuka ((Bismillah Ar-rahmaan Ar-rahiim)), (na ulikuwa) mwanzo wa Suura nyingine " Na utaratibu huu tunauita {UTARATIBU WA ASILI.}. Nakuna jambo lingine ambalo limefanya kazi ya kupangilia baadhi ya Aya katika utaratibu unaokwenda kinyume na zilivyoshuka,na hii ni kwasababu ya Nassu kutoka kwa Mtume (s.a.w) na uainishaji wake khaasi (kwamba aya hii inatakiwa iwekwe katika Suura fulani na sehemu fulani). Mtume (s.a.w) -mara nyingine- alikuwa anaamrisha kuiweka aya katika sehemu makhsusi ya Suura iliyoshuka kabla na ambayo ilikuwa imeisha.

Ufafanuzi

MAARIFA YA QUR'AN KWA QUR'AN.

MAARIFA YA QUR'AN KWA QUR'AN. MAARIFA YA QUR'AN KWA QUR'AN. SOMO LA KWANZA. IMANI JUU YA ULAZIMA WA KUIFAHAMU QUR'AN TUKUFU. Kwa hakika kufanya tadabbur na kuizingatia Qur'an Tukufu hutegemea kuifahafu Qur'an,kwa ibara nyingine ni kwamba:Huwezi kufanya kuizingatia Qur'an Tukufu ikiwa huifahamu.Kwa sababu utafutaji wa kila kitu hutegemea au huegemea katika kukifikiria kwanza kitu kile na kufikiria faida zake pamoja na kuwa na imani na kitu hicho.Hivyo kabla ya kuitadabbur Qur'an hii na kuizingatia ni lazima kwanza kuifahamu au ni lazima kwanza uhakiak wa Qur'an. Na itakuwa wazi kwa kila mtu kwamba kitakachogundulika baada ya kufanya tadabbur na mazingatio katika Qur'an Tukufu ni ujinga (yaani kushindwa) wa kutofahamu uhakika wake,ispokuwa nikwamba ujinga una aina zake,kuna wakati ujinga unakuwa ni ule wa kupandana! Yaani ujinga juu ya ujinga. Mfano:Mtu hajui kama hajui! Na aina hii ya ujinga ni mbaya zaidi ukilinganisha na aina zingine za ujinga.Na aina nyingine ya pili ya ujinga ni ile inayoambatana na (uangalifu) wa mtu (yaani yuko attention) kuwa hajui.Huyu ni mjinga lakini anajua kuwa ni mjinga.Katika sura hii itakuwa ni rahisi sana kujaribu kutafuta jinsi ya kutatua tatizo la ujinga huu kwa kurejea kwa A'alimu na Mjuzi wa Qur'an Tukufu.

Ufafanuzi

MIUJIZA YA QUR'AN TUKUFU.

MIUJIZA YA QUR'AN TUKUFU. BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM MIUJIZA YA QUR'AN TUKUFU SEHEMU YA PILI. Kabla ya kuendelea mbele zaidi katika mada hii inayozungumzia miujiza ya Qur'an Tukufu,nitapenda kutoa ishara ndogo katika kuelezea umuhimu wa somo liitwalo:{Physics} ambalo ndilo somo mama lililoufikisha Ulimwengu wa Elimu,Maarifa na Ufundi mahala hapa ulipofikia. Neno (Physics) linamaana ya Elimu ya Hali na tabia ya vitu vyote,na ya nguvu zote zilizomo duniani,kwa mfano:Nguvu ya joto,nguvu ya sauti,nguvu ya umeme,nguvu ya Sumaku(Magnetism) pamoja na mabadiliko yanayofanyika kwa nguvu hizo. Mnamo karne ya sita (6th century) kabla ya kuzaliwa kwa Nabii Issa (a.s) wataalamu waliobobea katika Elimu hii ya {Physics} kutoka Yunani{Ugiriki} walianza kuchunguza na kufuatilia asili ya vitu vyote,tabia na hali zake,ili kupata ukweli wa mambo hayo kuhusu chanzo cha Ulimwengu huu.Kabla ya wataalamu hao kuanza kufanya uchunguzi na kufuatili asili ya vitu vyote,walikuwa na maswali mengi sana katika nafsi zao kuhusiana na vitu hivi wanavyoviona kila siku katika uliwmegu huu,je vitu hivi vimekuwepo tu hivi hivi ghafla ghafla pasina kuwepo nguvu nyuma yake ambayo ndio sababu ya kuwepo kwa vitu hivi?Na hili ni swali alilokuwa nalo kila mwanadamu katika nafsi yake!.Jibu hupatikana mara tu baada ya kufanya uchunguz na kujua asili ya vitu hivyo.Hivyo wataalamu hao baada ya maswali kuwa mengi katika bongo zao,wakaamua kufanya uchunguzi na utafiti ili wajue ukweli wa mambo kuhusu chanzo cha ulimwengu na vitu vyote vilivyomo ndani yake.

Ufafanuzi

MUUNDO WA QUR'AN

MUUNDO WA QUR'AN KUANDIKWA KWA QUR'AN (MUUNDO WA QUR'AN). Assalaam Alaikum Warahmatullah Wabarakaatuh. Kwa Muhtasari ningependa kuanza kwa kuashiria katika nukta hii kwamba kuandikwa kwa Qur'an Tukufu(Msahafu) na kuiweka katika mfumo huu ilivyo leo hii,yaani kupangilia aya zake na kupangilia suura zake katika utaratibu huu kuanzia Suuratul Faatiha na kuishia na Suuratun-Naas,na pia kuweka nukta katika herufu kuipanga iwe katika juzuu (mfano juzu ya kwanza (1) mpaka ya Juzu ya Thelathini (30) ) haikuwa ni kazi rahisi nyepesi nyepesi na haikuwa kama hivi mara moja tu ghafla ghafla,na pia mfumo huu haukakamila na kuwa na hivi katika kipindi cha WAHYI cha kwanza,bali shughuli hii imetimia kupitia muda kadhaa na vipindi tofauti tofauti na zama tofauti mpaka kuwa kama hivi tunavyoiona leo hii. Kazi hii ya kuweka aya za Qur'an kwa kuzikusanya katika sehemu moja na hatimaye kuwa kitabu kimoja kilichokusanya aya zote zilizoshuka kwa Mtume wetu Muhammad (s.a.w) ili afikishe ujumbe wa aya hizo kwa wanadamu wote,ilianza katika kipindi cha RISALA na kuishia katika zama ambazo ndani yake zilifanyika harakati mbali mbali (Za Kuiunganisha misahafu yote iliyokuwa imeandikwa na Maswahaba wa Mtume (s.a.w) ili uwe msahafu mmoja unaowaunganisha waislaam wote ), ambazo ni zama za Uthman,Kisha katika kipindi au zama za Khaliyli bin Ahmad An-nahwiy ambaye ndiye aliyetimiza Muonekano wa msahafu au Qur'an hii kwa kuiweka katika hali hii ilivyo kwa sasa. Jambo muhimu na la msingi ambalo ni muhimu tuliashirie katika bahthi hii ni kuhusiana na kutilia umuhimu wa kuisoma Qur'an Tukufu katika upande wa Kukusanywa kwake na kuandikwa kwake na kuwa Msahafu ulio baina ya majarida au magamba mawili.Na kwa kufanya uchunguzi kunako kipindi kile ambacho ndani yake ilikusanywa Qur'an na kuandikwa,na pia tusome mambo yote yaliyojiri katika tukio hili lililoonekana kuwa hatari sana la ukusanyaji na uandikwaji wa Qur'an Tukufu.

Ufafanuzi

TAFAKURI YA QURANI

TAFAKURI YA QURANI KUITAFAKARI QURANI Kuna mambo matatu yanayosaidia kufanya tafakuri sahihi. La kwanza: kuyafikiria maisha ya kupita na mafupi ya hapa duniani na kuepukana na matazamio ya muda mrefu. La pili: kuizingatia Qur'an. la tatu: kuepuka madhambi yanayoudhuru moyo. Kuutambua muda mfupi wa maisha haya ya dunia na kuutambua ukaribu wa mtu na mauti ni mambo yanayounufaisha mno moyo na kumpa muumini msukumo wa kuutumia kwa manufaa kila muda wa maisha yake. Muumini huyu huelekeza mazingatio na tamaa yake katika Makazi ya Milele. Hii humpa hamasa ya kufidia kile kinachokosekana katika maandalizi ya safari na kumfanya ajizuie kutamani starehe za maisha haya mafupi. Iwapo mtu atadumu na tafakuri hii, basi itamuwezesha kuuona undani halisi wa maisha haya. Ataona jinsi hicho kinachoachwa kilivyo kidogo kuliko hata kile kinachosalia kidoleni kwa mtu pale kidole hicho kinapochovya bahari ambapo bahari ndiyo Maisha ya Milele ya Akhera. Jua la dunia hii ndio hilo limezama tena na kana kwamba linazamia chini ya vilele vya milima. Hali na dalili zilizobashiriwa pale zifikapo zama za mwisho zimejitokeza. Mauti na wewe ni kama marafiki wawili walionjiani kwenda kukutana ambapo muda wowote mtakutana na kukumbatiana. Itoshe basi kuyakumbuka maneno haya ya MwenyeziMungu; -"Na (wakumbushe) siku atakayowakusanya (waone) kama kwamba hawakukaa (duniani) ila saa moja tu ya mchana...." (10:45). -Siku watakapokiona (Kiama) watakuwa kama kwamba hawakukaa (ulimwenguni) ila jioni moja au mchana wake (kwa kishindo kitakachowafika)." (79:46).

Ufafanuzi

HISTORIA YA MIUJIZA YA QUR-ANI

HISTORIA YA MIUJIZA YA QUR-ANI HISTORIA KUHUSIANA NA MAUDHUI YA MIUJIZA Ijapokuwa haieleweki ya kwamba maudhui kuhusu miujiza yalianza kipindi gani, lakini muujiza wa qur-ani ndio maudhui ya mwanzo yaliyokuja yanayohusiana na Qur-ani. Na Qur-ani tukufu kwa kuthibitisha madai yake hayo – yaani kuwepo kwa muujiza kuhusiana na kitabu hicho – imetumia neno muujiza, katika kipindi chote hicho kilichopita Qur-ani inapoelezea kuhusu miujiza ya Mitume hutumia neno (ايه na  بينه) kwa kuthibitisha kuwepo kwa miujiza, na kwa sababu hiyo basi neno (istilaha) muujiza (معجزه)  kutokana na riwaya au hadithi zilizokuja ndio neno la mwanzo lililotumika kuthibitishia madai yake hayo1. na baadae ndio zikatumika istilaha (maneno) nyengine, na istilaha hizo ziliendelea kuenea siku hadi siku2. Katika kitabu kitukufu cha Qur-ani vile vile hakujatabiriwa neno (خارق العادة) – khaariqul-addat – (yaani amali au matendo ambayo hakuna mwanaadamu yoyote anayeweza kuyafanya isipokuwa Mitume ya Mwenyeezi Mungu (s.w), na Mitume huyafanya matendo hayo kwa uweza wa Mwenyeezi Mungu (s.w), na kwa idhini ya Mola wao). Kwa hiyo Istilaha neno – muujiza – ni miongoni mwa istilaha ambayo imeanzishwa na Maulamaa wa dini ya kiislamu.

Ufafanuzi

MUUJIZA WA QUR_ANI

MUUJIZA WA QUR_ANI MUUJIZA WA QUR_ANI UTANGULIZI Miongoni mwa mambo muhimu yaliyoelezewa ndani ya Qur-ani ni muujiza wa Qur-ani unaoshuhudiwa katika Kitabu hicho kitukufu, katika zama zilizopita hadi zama zetu za sasa hivi kuna Maulamaa, na Wafasiri wengi wa Qur-ani wanaofanya jitihada ili wauwelewe kwa unadni zaidi ule muujiza wa Qur-ani uliomo ndani ya Kitabu hiki Kitukufu. Katika maandishi haya yafuatayo kwanza kabisa tutaelezea kuhusiana na muujiza wa Qur-ani, na ili kufafanua zaidi kuhusiana na maudhui hayo basi kwanza kabisa tutafafanua (definition), maana ya muujiza, na zaidi tutaelemea kwa kufafanua kwa ufupi yale yanayohusiana na muujiza kwa kuelezea nadhari za Maimamu (a.s), na Maulamaa wa dini ya kiislamu. Na kwa kuendelea tutaelezea njia tofauti zinazothibitisha muujiza wa Qur-ani, ijapokuwa hakuna shaka kwamba njia moja ya kuthibitisha muujiza wa Qur-ani inaweza ikamkanaisha mtu yoyote yule, hata kwa wale wataalamu wa kilugha na wale waliokuwa sio wafuasi wa waislamu wala sio wafuasi wa dini ya Kiislamu, lakini ili kuthibitisha zaidi tutazielezea njia hizo kwani kwa kufanya hivyo kutapelekea muujiza wa Qur-ani uonekane kwa uwazi zaidi.

Ufafanuzi

KUCHOMOZA KWA WAHYI

KUCHOMOZA KWA WAHYI KUCHOMOZA KWA WAHYI Utafiti katika suala la Wahyi ni moja kati ya mambo yaliyo muhimu, na kutokana na kwamba suala hili ndio msingi wa kuyaelewa maneno ya Mwenyeezi Mungu, basi tunaweza kusema kua utafiti juu ya suala hili ndio msingi wa mwanzo katika masuala ya Qur-ani, na katika utafiti huu mtu hua anajiuliza, Wahyi ni nini? Na vipi linatimia fungamano baina ya Mteremshaji Wahyi na Mpokeaji wa Wahyi huo, jawabu za masuali kama haya, hua yanampa mtu njia ya kuelewa ukweli wa Qur-ani. Neno Wahyi katika lugha lina maana tofauti, miongoni mwa maana hizo ni:Kuonesha ishara (kuashiria), maandishi, ujumbe, mazungumzo ya kiundani yaliyofichwa maana yake, kufahamisha kitu kwa kificho, haraka na spidi (speed), na aina yeyote ile ya matamshi, iwe ni kwa njia ya kimaandishi,ujumbe, au kumfahamisha mtu kwa kutumia ishara bila ya kuelewa watu wengine, huitwa wahyiMtafiti mkuu wa kilugha (Raaghib Isfahaniy) anasema: (Wahyi ni ujumbe unaofikishwa kwa njia ya kificho ambao hutimia kwa kupitia ishara na kwa haraka)) Abu Ishaaq vilevile amesema: (asili ya neno wahyi katika lugha limekuja kwa maana ya (ujumbe ulio wa siri), ndio maana Ilhaam ikapewa jina la wahyi.

Ufafanuzi

KUIELEWA QUR-ANI

KUIELEWA QUR-ANI KUIELEWA NA KUIFAHAMU ELIMU YA QUR-ANI Qur-ani ni kitabu kimoja wapo katika vitabu ambavyo Mwenyeezi Mungu ameviteremsha kutoka mbinguni, kitabu hicho toka pale mwanzo ambapo kimeteremshwa, mpaka sasa hivi kimesalimika na hakijaharibiwa, kimehifadhika na kitaendelea kuhifadhika . Mada muhimu ambazo zimo katika kitabu hichi kitukufu ni kumjua Mwenyeezi Mungu na kumfahamu ili tuwe karibu naye, kisha kuyaelewa maneno ambayo ameyazungumza katika kitabu hicho Kabla hatujaingia katika mada muhimu, kwanza kabisa kuna ulazima wa kuifahamu Elimu ya Qur-ani, na vipi tutaweza kupambanua baina ya elimu ya Qur-ani na taf-siri ya Qur-ani, kwa hiyo katika mada hizi ni muhimu na ni vizuri tukaelewa maana ya maneno hayo.

Ufafanuzi

VIAPO NDANI YA QUR-ANI

VIAPO NDANI YA QUR-ANI VIAPO NDANI YA QUR-ANI Kiapo ni sisitizo, na hutumiwa ili kuonesha umuhimu wa maudhui yanayotaka kuliwa kiapo, Kiapo kinatumiwa katika mambo ambayo ni muhimu sana ambayo yanahitajiwa kusisitizwa, (kusudio la sisitizo ni sisitizo liongezwalo kusisitizwa zaidi ya mara moja). Kiasi ya kwamba kutokana na kuwa haitoshelezi kutumia njia zitakazoweza kuthibitisha usisitizo wa jambo hilo, ndio hutumia kiapo ili kulithibitisha. Ndani ya Qur-ani pia kumetumiwa njia za kiapo kama vile walivyokuwa wakitumia WaarabuHapo mwanzo tulielezea kuwa kiapo hutumika kwa kile kitu ambacho ni muhimu sana, kiasi ya kwamba huwafanya wasikilizaji wa kiapo hicho kuwa makini na kuzingatia ni kitu gani muhimu kilichopelekea kuliwa kiapo, kwa hiyo kwa hakika kiapo ni kitu kilicho thabiti kinachowapelekea watu kukubali bila ya kuwa na shaka na lile jambo au tokeo lililotokea ambalo limesababishia kuliwa kiapo. (yaani kwa kuthibitishwa na kukubaliwa na watu wote kile kitu ambacho kimeliwa kiapo yaani kwa lugha ya kiarabu wanasema (مقسم به), vile vile huthibitishwa na kukubaliwa na watu wote kile kitu ambacho kimesababisha kuliwa kiapo, (مقسم عليه)

Ufafanuzi

WAHYI WA MITUME

WAHYI WA MITUME WAHYI WA MITUME Wahyi wa aina hii ndio unaotafautisha wahyi wanaopewa Mitume na wahyi au (ujumbe) unaowafikia watu wengine, wahyi wa aina hiyo katika Qur-ani umekuja zaidi ya mara sabiini. Kwa mfano Allah (s.w) katika (Surat-Shuraa aya ya 7) anasema:- Na namna hivi tumekufunulia Qur-ani kwa Kiarabu ili uwaonye watu wa Makka na walio (katika nchi zilizo) pembeni mwake. (Nao ni ulimwengu mzima kwani Makka iko katikati ya ulimwengu). Na uwaonye siku ya mkutano; Siku isiyo na shaka (kuwa itakuja). Kundi moja litakuwa Peponi na kundi jengine Motoni. Mitume ya Mwenyeezi Mungu ni katika watu watukufu ambao wamefikia katika ukamilifu na walio tayari kupokea wahyi utokao kwa Mwenyeezi Mungu. Imam Hassan Askariy akielezea kuhusiana na jambo hilo anasema:- “Mwenyeezi Mungu Mtukufu ameifanya mioyo ya Mitume kuwa ni mioyo bora miongoni mwa mioyo ya wanaadamu wote ulimwenguni, baadae akawachagua watu wenye mioyo hiyo kuwa ni Watume wake”[2]. Mtume Muhammad (s.a.w.w) anasema:- “Mwenyeezi Mungu hakuwachagua Mitume ila baada ya kuziweka katika ukamilifu akili za Mitume hiyo, na alimfanya Mtume Muhammad (s.a.w.w) kuwa ni m-bora wa umati wake wote”.[3]

Ufafanuzi

UUMBAJI WA MWENYEEZI MUNGU

UUMBAJI WA MWENYEEZI MUNGU UUMBAJI WA MWENYEEZI MUNGU NI VYA MWENYEZI MUNGU VILIVYOMO MBINGUNI NA VILIVYOMO ARDHINI Mwenyeezi Mungu Mtukufu anasema:- Ni vya Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Na hakika tuliwaamrisha waliopewa Kitabu kabla yenu na nyinyi kwamba,mcheni Mwenyezi Mungu. Na kama mkikufuru, basi ni vya Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na ardhini. Na Mwenyezi Mungu ni mkwasi mwenye kusifiwa. Anayetaka malipo ya duniani, basi yako kwa Mwenyezi Mungu malipo ya duniani na akhera na Mwenyezi Mungu ni mwenye kusikia mwenye kuona. Ufafanuzi wa Aya 131 – 134 Suratun-Nisaa Katika juzuu ya kwanza na juzuu hii, tumezungumzia kuhusu kukaririka katika Qur'an. Sasa tutazungumzia kukaririka kwenye Aya hasa hii,kwa sababu ni Aya iliyotajwa na kurudiwa zaidi katika Qur'an . Kisha tutadokeza kukaririka kwa namna maalum ambayo imetajwa kwa kunakiliwa mara mbili katika Aya moja na kurudiwa mara ya tatu katika Aya inayoifuatia moja kwa moja bila ya kuweko kati kitu kingine.

Ufafanuzi

WANAFIQ NDANI YA QUR_ANI

WANAFIQ NDANI YA QUR_ANI WANAMHADAA MWENYEZI MUNGU NA ATAWALIPA KWA KUHADAA KWAO Mwenyeezi Mungu Mtukufu anasema:- Hakika wanaafiki wanamkhadaa Mwenyezi Mungu, na hali ni Yeye ndiye mwenye kuwakhadaa wao. Na wanapo inuka kusali huinuka kwa unyong'onyo, wanajionyesha kwa watu tu, wala hawamdhukuru Mwenyezi Mungu ila kidogo tu. Wanayumba yumba baina ya huku na huko. Huku hawako na huko hawako. Na ambaye Mwenyezi Mungu amemwacha kupotea kabisa hutompatia njia. Ufafanuzi wa aya. Wanafiki walikuwa wakijitia pamoja na Waislamu katika mambo yao yote, ili wasipate kutambulikana kuwa wao wanafiki. Lakini walikuwa hawayaonei raha, wanafanya kwa kuwa hawana budi tu. Wao wanachunga manufaa yao ya kidunia tu – yakiwa kwa makafiri au Waislamu,hawako huku wala hawako huko.

Ufafanuzi

HAKI ZA NDOA NDANI YA QUR_ANI

HAKI ZA NDOA NDANI YA QUR_ANI HAKI ZA NDOA NDANI YA QUR_ANI UNASHIZA WA MUME Mwenyeezi Mungu Mtukufu anasema:- Na mwanamke akichelea kutupwa au kutojaliwa na mumewe, basi si vibaya kwao wakisikizana kwa suluhu. Na suluhu ni bora. Na nafsi zimewekewa machoni mwake tamaa na choyo. Na mkifanya wema na mkamchamngu basi hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za yote mnayo yatenda. Maelezo kuhusiana na Aya: Mambo ya kuachana yanavunjwa nguvu sana katika sharia za kiislamu, na watu wengine mara huchokana wakaona tabu kutekelezeana haki zao za ndoa.

Ufafanuzi

KUMFAHAMU MWENYEEZI MUNGU NDANI YA QUR_ANI

KUMFAHAMU MWENYEEZI MUNGU NDANI YA QUR_ANI KUMFAHAMU MWENYEEZI MUNGU NDANI YA QUR-ANI NJIA ZA KUMFAHAMU MWENYEENZI MUNGU 2 katika makala iliyopita (makala namba moja ) tulielezea nyenzo zinazomuongoza mwanaadamu katika kumfahmu Mwenyeezi mungu. katika sehemu hii ya pili tutaendelea kuzielezea nyenzo hizo na kuzithibitisha kwa aya za qur_ani. DALILI ZA KIAKILI. Hivi kweli kiarabu hiki cha Qur-ani yuko binaadamu anayeweza kukiandika au kukisema? Ndani ya kitabu kitukufu cha Mwenyeezi Mungu kuna aya nyingi za Qur-ani kariym zinazomtaka mwanaadamu afikiri kiakili na awe makini . Miongoni mwa aya hizo ni hizi zifuatazo:- Madhalimu kweli hawa- kama ilivyo katika aya ya 17- wa nafsi zao na kuwadhulumu viumbe wengine wanaowapoteza makusudi. Sio kama wanavyodai baadhi yao,

Ufafanuzi

DALILI ZA KUMFAHAMU MWENYEEZI MUNGU

DALILI ZA KUMFAHAMU MWENYEEZI MUNGU DALILI ZA KIAKILI ZA KUMFAHAMU MWENYEEZI MUNGU 2 Katika makala zilizopita tulielezea njia na dalili za kumfahamu mwenyeezi mungu, na tukayathibitisha hayo kutokana na akili na Aya za qur-ani,katika makala hii basi tutaendelea kuzielezea dalili hizo, na vile vile tutazithibitisha kutokana na Qur-ani. Miongoni mwa dalili hizo ni hizi zifuztzzo:- DALILI ZA MATAMANIO YA KIMOYO (STIMULUS SINCERE) Mbali ya kuwa mwanaadau ana dalili (matamanio) za kiakili ambazo zinathibitika kwa kutolewa dalili na kutafakari vile vile ana matamanio ya nafsi ambayo yamo ndani ya nafsi ya mwanaadamu, matamanio hayo yanampelekea mwanaadamu kupata majibu kutokana na na matendo ya wengine.  Na tuzingatie riwaya hii iliyonukuliwa na Imam Baqiri (a.s). Imam Baqiri (a.s) amesema:- “Siku moja usiku Mtume Muhammad (s.a.w.w) alikuwa kwa mke wake bibi Aisha, bibi Aisha akamuuliza suala Hadharati Muhammad ya kuwa kwa nini unafanya jitihada ya kufanya ibada? Hali ya kwamba Mwenyeenzi Mungu Mtukufu amekusamehe madhambi yako ya nyuma na ya masiku ynayokuja?

Ufafanuzi

DALILI ZA KIAKILI ZA KUMFAHAMU MWENYEEZI MUNGU

DALILI ZA KIAKILI ZA KUMFAHAMU MWENYEEZI MUNGU DALILI ZA KIAKILI ZA KUMFAHAMU MWENYEENZI MUNGU Katika makala zilizopita tulielezea njia za kumfahamu Mwenyeezi Mungu, na tukathibitisha hayo kutokana na dalili za kiakili ambazo tulizithibitisha kutoka ndani ya Qur-ani. Katika makala hii tutaendelea kuziorodhesha Aya za Qur-ani ambazo kiakili zinathibitisha kumfahamu na kumtambua Mwenyeezi Mungu. Mwenyeezi Mungu Mtukufu anasema:-Enyi mlio amini! Msiwafanye wasiri wenu watu wasio kuwa katika nyinyi. Hawataacha kukufanyieni ubaya. Wanayapenda yanayo kudhuruni. Imekwisha fichuka chuki yao katika midomo yao. Na yanayo ficha vifua vyao ni makubwa zaidi. Tumekwisha kubainishieni Ishara ikiwa nyinyi mtayatia akilini.   

Ufafanuzi

KUMFAHAMU MWENYEEZI MUNGU

KUMFAHAMU MWENYEEZI MUNGU DALILI ZA KIAKILI ZA KUMFAHAMU MWENYEENZI MUNGU Katika makala zilizopita tulielezea njia za kumfahamu Mwenyeezi Mungu, na tukathibitisha hayo kutokana na dalili za kiakili ambazo tulizithibitisha kutoka ndani ya Qur-ani. Katika makala hii tutaendelea kuziorodhesha Aya za Qur-ani ambazo kiakili zinathibitisha kumfahamu na kumtambua Mwenyeezi Mungu. Mwenyeezi Mungu Mtukufu anasema:-Enyi mlio amini! Msiwafanye wasiri wenu watu wasio kuwa katika nyinyi. Hawataacha kukufanyieni ubaya. Wanayapenda yanayo kudhuruni. Imekwisha fichuka chuki yao katika midomo yao. Na yanayo ficha vifua vyao ni makubwa zaidi. Tumekwisha kubainishieni Ishara ikiwa nyinyi mtayatia akilini.   

Ufafanuzi

MAYAHUDI HAWAMSADIKI MTUME

MAYAHUDI HAWAMSADIKI MTUME MAYAHUDI HAWAMSADIKI MTUME (S.A.W.W) MAYAHUDI HAWAISADIKI QUR_ANI TAKATIFU WALA HAWAMSADIKI MTUME (S.A.W.W). Mwenyeezi Mungu Mtukufu anasema:- Na kilipo wajia Kitabu kitokacho kwa Mwenyezi Mungu kinacho thibitisha waliyo nayo - na wao walikuwa wakitafutia ushindi kuwashinda makafiri - yalipo wajia yale waliyo kuwa wakiyajua waliyakanusha. Basi laana ya Mwenyezi Mungu juu ya wakanushao!.  Maelezo kuhusiana na Aya Kabla ya kuja Mtume Muhammad (s.a.w.w.), Mayahudi walikuwa wakiwapa khabari Waarabu kuwa karibuni atadhihiria Mtume[2]. Ama kusema kuwa hao Mayahudi walikuwa wakiomba kwa jaha ya Mtume, na wakishinda maadui zao kuwa ndio muradi wa Aya hii – maneno haya hawaakuyasema wale wafasiri wa mwanzo kabisa (salaf) wenye kutegemewa, kama Imam Ibn Jarir[3] Wala hawakuitaja vile vile wale wafasiri wanaotegemea hadithi sahihi za Mtume.

Ufafanuzi

MAYAHUDI HAWAISADIKI QUR_ANI

MAYAHUDI HAWAISADIKI QUR_ANI MAYAHUDI HAWAISADIKI QUR_ANI TAKATIFU2 MAYAHUDI HAWAISADIKI QUR_ANI TAKATIFU WALA HAWAMSADIKI MTUME (S.A.W.W). Katika makala iliyopita tulielezea vipi Mayahudi walimkanusha Mtume Muhammad (s.a.w.w) na kitabu chake, katika makala hii basi tutaendelea na mada yetu hiyo na kutupilia macho mitihani ambayo Mwenyeezi Mungu anawapa waja wake. Basi Mwenyeezi mungu anawajibu Mayahudi kwa kusema hivi:- Na wakafuata yale waliyo zua mashet'ani kuuzulia ufalme wa Su leiman. Na wala Suleiman hakukufuru, bali mashet'ani ndio walio kufuru, wakiwafundisha watu uchawi, na yaliyo teremshwa kwa Malaika wawili, Haaruta na Maaruta katika Baabil. Wala hao hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie: Hakika sisi ni mtihani; basi usikufuru. Wakajifunza kwa hao wawili yale ya kumfarikisha mtu na mkewe. Wala hawawezi kumdhuru mtu ila kwa kutaka Mwenyezi Mungu. Na wanajifunza yatayo wadhuru wala hayawanufaishi. Na hakika wanajua kwamba aliye khiari haya hatakuwa na fungu lolote katika Akhera. Na hakika ni kiovu mno walicho jiuzia nafsi zao laiti wangelijua.

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini