Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

Elimu za Qurani

KAULI YA MWENYEEZI MUNGU JUU YA MAKAFIRI

KAULI YA MWENYEEZI MUNGU JUU YA MAKAFIRI

KAULI YA MWENYEEZI MUNGU JUU YA MAKAFIRI 1 MAKAFIRI WANAMKADHIBISHA NA KUMTUKANA MTUME (S.A.W.W) Makafiri wakimwambia Mtume (s.a.w.w) :- “Wewe si Mtume”, kama tulivyoona na tutavyoona katika Aya nyingi, basi anaambiwa Mtume asijali kukataliwa na wao maadam Mwenyeezi Mungu Mwenyewe Anamkiri kuwa ni Mtume Wake. Kwa kusema:- Sema: Kitu gani ushahidi wake mkubwa kabisa? Sema: Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye shahidi baina yangu na nyinyi. Na nimefunuliwa Qur'ani hii ili kwayo nikuonyeni nyinyi na kila inayo mfikia. Ati kweli nyinyi mnashuhudia kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu wapo miungu wengine? Sema: Mimi sishuhudii hayo. Sema: Hakika Yeye ni Mungu mmoja tu, nami ni mbali na mnao washirikisha. Makafiri ijapokuwa wanaujua ukweli wa dini ya kiislamu – lakini wanaipinga tu na kuwazuilia watu kuifuata – wanajiangamiza wenyewe.

Ufafanuzi

MAKAFIRI WAMKADHIBISHA MTUME

MAKAFIRI WAMKADHIBISHA MTUME MAKAFIRI WANAMKADHIBISHA NA KUMTUKANA MTUME (S.A.W.W) Katika makala iliyopita kuhusiana na kauli ya Mwenyeezi Mungu juu ya makafiri tulielezea kwa muhtasari jinsi Makafiri walivyokuwa wakimkadhibisha na kumtukana Mtume muhammad (s.a.w.w.). Na vile vile hawakukiamini kitabu chake Kitukufu – Qur_ani - . Katika makala hii basi tutaendelea kuielezea mada hiyo kwa kuzingatia Aya za Qur-ani za Mwenyeezi Mungu. Nabii Muhammad (s.a.w.w) alikuwa na hamu kubwa kabisa ya kutaka watu wote wasilimu upesi upesi, wapewe hiyo miujiza wanayoitaka wishe udhia. Lakini Mwenyeezi Mungu alikuwa hapendi Uislamu huo, akipenda wasilimu baada ya kuyafamu vyema hayo wanayoambiwa, sio wanasilimu kwa nguvu za miujiza, kwa kuthibitisha hayo Mwenyeezi Mungu Mtukufu anasema: Na ikiwa ni makubwa kwako huku kukataa kwao, basi kama unaweza kutafuta njia ya chini kwa chini ya ardhi, au ngazi kwendea mbinguni ili uwaletee Ishara -- Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angependa angeli wakusanya kwenye uwongofu. Basi usiwe miongoni mwa wasio jua.

Ufafanuzi

UMUHIMU WA KUFAHAMU QUR_ANI

UMUHIMU WA KUFAHAMU QUR_ANI UMUHIMU WA KUFAHAMU QUR-ANI. UMUHIMU WA KUFAHAMU MAFUNZO NA MAANA YA AYA ZA QUR-ANI. Qur-ani kariym ni maelezo na ujumbe ulio wazi wa Mwenyeezi Mungu kwa ajili ya watu wote. Allah (s.w) anasema:- Haya ni maelezo yaliyo wazi kwa watu (wote) na uongozi na mauidha kwa wamchao. Na katika sura nyengine anasema:- Haya yatosha (kuwa mauidha) kwa watu, ili waonywe kwayo, na wapate kujua kuwa Yeye (Mwenyeezi Mungu) ni Mungu Mmoja tu, na ili wenye akili wakumbuke. Vile vile anasema:- Hizi ni dalili zilizowazi kwa watu (wote); nazo ni uwongofu na rehema kwa watu wanaoyakinisha.

Ufafanuzi

MSINGI WA KUIFAHAMU QUR_ANI

MSINGI WA KUIFAHAMU QUR_ANI MSINGI WA KUFAHAMU QUR_ANI – 1- Tunamshukuru Mwenyeezi Mungu aliyesema katika Qur-ani yake kuwa “imekujieni – kutoka kwa Mwenyeezi Mungu – nuru (kubwa) na kitabu (kitukufu) kinachobainisha (kila linalohitajiwa)”. Na Rehema Zake na Amani zake zimwendee Mtume wake bwana Muhammad (s.a.w.w) , Mwisho wa Mitume wote na ziwaendee Ahli bayt wake (a.s). Vitabu vutote tunavyosoma tunaona ndani yake kuwa kila yanayotajwa humo – katika maelezo, fikra na hoja – yanahusika na jambo makhsusi, na kwa mpango wa utungaji makhsusi na kwa kuendeleza hayo anayoyataka huyo mtungaji. Basi kwa ajili ya kuzoea haya yule anayeanza kuvisoma,akaona kuwa kitakuwa kama hivyo- yamekwisha kupangwa mbali mbali makusudio yake, na yametengwa katika milango mbali mbali, ili aisome kila khabari mahala pake, na anadhani kuwa ataona kila jambo katika mambo yanayohusiana na uhai wa binaadamu limepangwa peke yake kwa mfuatano wake.

Ufafanuzi

ALIYOBAINISHA MOLA KATIKA KUIFAHAMU QUR_ANI

ALIYOBAINISHA MOLA KATIKA KUIFAHAMU QUR_ANI MSINGI WA KUIFAHAMU QUR_ANI.3 ALIYOBAINISHA MOLA KATIKA KUIFAHAMU QUR_ANI Katika makala iliyopita (makala no. 2) ambayo inahusiana na msingi wa kuifahamu Qur-ani, tulielezea misingi aliyobainisha Mwenyeezi mungu na Mtume wake katika kuifahamu Qur-ani, katika makala hiyo tumetaja msingi wa mwanzo, na katika makala hii ya sasa tutaendelea kuelezea msingi mwengine aliyoubainisha Mwenyeezi mungu katika kuifahamu Qur-ani. 2- Na akamtia il-hamu ya nguvu kabisa katika moyo wake kuwa Mungu anamwambia Mimi (Mungu) ndiye Mola wako, na Mola wa ulimwengu wote, na Mimi ndiye Mola wako, na Mungu wa ulimwengu wote. Na Mimi ndiye Mfalme wako, na Mfalme wa ulimwengu wote. Usiwe katika ulimwengu wangu huu huru kabisa kabisa, umetakabari unafanya unavyotaka wala hujali. Wala usiwe mtumwa wa asiyekuwa miye, hakuna asiyekuwa miye anayestahiki kumuabudu, kumtii na kumnyenyekea, na huu uhai uliopewa ndani yake Huriya kidogo, ndiyo wakati wa mtihani, utarejea kwangu badala yake, nitazame uliyoyafanya, niwapambanue wepi waliofuzu, na wepi walioanguka, na njia nzuri ya kufuata ni hii.

Ufafanuzi

FUNGAMANO KATIIKA QUR_ANI

FUNGAMANO KATIIKA QUR_ANI VIPENGELE VYA MIUJIZA YA QUR-ANI -1- (C) D. FUNGAMANO KATIKA QUR-ANI  (MNASABA ULIOPO KATIKA AYA ZA QUR-ANI) Tukiendelea na mada yetu kuhusiana na vipengele vya miujiza ya Qur-ani, katika makala zilizopita tulizungumzia baadhi nyanja za miujiza ya Qur-ani, katika makala hii tunazungumzia nyanja ya nne miongoni mwa vipengele vya miujiza ya Qur-ani. Aya za Qur-ani ziko katika hali ya mparaganyiko, na zimeteremshwa kutokana na minasaba tofauti, lakini kutokana na uzingatiwaji uliozingatiwa na – wanaelimu – katika zama hizi – kuhusiana na yale yaliyomo katika kila sura, wamefikia natija ya kuwa kila sura ina hadafu (dhumuni) maalumu – miongoni mwa Aya za kila sura – na masuala ya muujiza wa Qur-ani ni katika nukta hii hii, katika zama hizi tulizonazo umoja huo wa maudhui yaliyo dhahiri katika kila sura unajulikana kwa jina la (umoja katika maudhui). Ni lazima tukumbushie: Kwamba kuna baadhi ya watu, mbali nakutowa nadharia za kuwa kuna mnasaba baina ya Aya, vile vile wametowa nadaharia nyengine na kusema kuwa kuna mnasaba baina ya sura.

Ufafanuzi

MABAINISHO YALIYOBAINISHWA KWA NJIA NYEPESI

MABAINISHO YALIYOBAINISHWA KWA NJIA NYEPESI VIPENGELE VYA MIUJIZA YA QUR-ANI -1- (B) Katika makala ya mwanzo tulielezea nyanja ya mwanzo ya miujiza. Katika makala hii tutaendelea na nyanja nyengine zifuztazo:- B. MABAINISHO YALIYOBAINISHWA KWA NJIA NYEPESI. Nyanja ya pili miongoni mwa sehemu ya miujiza ya mabainisho ni:- Mabainisho yaliyobainishwa katika Qur-ani yamewapelekea kuwajalibisha na kuwavutia watu wa jamii ya kiarabu, njia zilizotumika katika kuibainisha Qur-ani hazijafanana wala kukaribiana na zile njia zilizozoweleka ambazo zinatumiwa na watu wa jamii ya Kiarabu. Ni jambo la kustaajabisha kuona Qur-ani imetumia maneno yaliyoepukana na kila kasoro na ubainishwaji huo mwepesi umepelekea kukubaliwa na wasikilizaji wa Qur-ani, na umewafanya watu wa jamii ya kiarabu (Waarabu) watoke nje na zile njia zao zilizo maarufu, la kuvutia zaidi ni kwamba Qur-ani imetumia maneno na njia zote nzuri za ubainishaji, na imeepukana na zile njia za aibu, au mbaya (yaani zilizo na kasoro).

Ufafanuzi

KUBADILISHWA KWA HUKUMU NDANI YA QUR_ANI

KUBADILISHWA KWA HUKUMU NDANI YA QUR_ANI KUBADILISHWA KWA HUKUMU NDANI YA QUR-ANI. Mipango yoyote ile inayopangwa kwa ajili ya kuiongoza jamii fulani, hutekelezwa kwa kupitia hatua baada ya hatua, na kwa kutokana na hali ya watu wa zama hizo walivyo pamoja na zama zilivyo, basi inabidi lazima zizingatiwe hali za watu hao, na suala hili hupelekea kufuta baadhi ya sheria za mwanzo na kuweka sheria mpya, ili kuweza kuwakomaza watu hao  katika nyanja tofauti, kisheria na kiutamaduni, Na suala hili linaonekana wazi katika serikali za kidunia na Qur-ani pamoja na vitabu vyote vya mbinguni haiko nyuma katika suala kama hili, kwani kazi ya Qur-ani ni kuwapangia watu maisha yao, ktika mtindo ulio bora, na suala la kufutwa kwa baadhi ya hukumu na kuwekwa hukumu mpya katika upangaji wa sheria hutimizwa suala hilo hatua baada ya hatua hadi watu wa jamii wanaokusudiwa kuongozwa waweze kubobea, na sio kitu cha busara kwamba baada ya kutimizwa sheria hizo na kukamilishwa zije kufutwa na kuwekwa sheria nyengine, kwa hiyo basi ufutwaji na upangwaji wa sheria nyengine mpya hutimizwa katika zama ambazo watu hao watakuwa bado hawajakomaa kisheria, bali wako njiani kukomazwa hatua baada ya hatua.

Ufafanuzi

UFUTWAJI WA HUKUMU NDANI YA QUR_ANI

UFUTWAJI WA HUKUMU NDANI YA QUR_ANI UFUTWAJI WA HUKUMU NDANI YA QUR_ANI. Katika makala iliyopita (makala kuhusiana na Naasikh na Mansukh no 1), tulielezea mada hiyo ambayo inahusiana na kufutwa kwa baadhi ya hukumu ndani ya Qur-ani. Na tukatoa mfano wa kufutwa kwa baadhi ya hukumu hizo kwa mfano – Katika surat Baqarah Aya ya 126, tumeelezea kwa ufupi kuhusiana na kufutwa kwa baadhi ya hukumu. Lakini aya Naasikh ndani ya Qur-ani zimekuja aina tatu tu. Aina ya kwanza:  Naskhu L-hukmu watilaawa jamiy`an (yaani iliyofuta aya za Qur-ani pamoja na hukumu). Na aina ya pili: Naskhu L-hukmu duna tilaawa (yaani iliyofuta hukumu bila ya kufuta aya za Qur-ani). Na aina ya tatu:  Naskhu tilaawa duwna L-hukmu (yaani iliyofuta aya za Qur-ani bila ya kufuta hukumu). Hapana shaka kuwa kuna hekima kubwa za Mola kubadilisha aya zilizo bora yaani Naasikh ni kwa ajili ya kuwapunguzia umma huu mambo mazito kwa mambo mepesi au mambo ya madhara kwa mambo ya faida au manufaa kwao. Ingawa hukumu za aya hizo zimefutwa lakini aya za Qur-ani Tukufu bado zipo ndani ya Qur-ani na mpaka hivi sasa zinasomwa na watu. Na hekima ya Mwenyezi Mungu kuziacha, kwani ingelikuwa zimefutwa sisi tusingezijua aya hizo wala sababu za kufutwa kwake, nazo ni nyingi sana zimetolewa ndani ya Qur-ani Tukufu.

Ufafanuzi

MASHARTI YA KUFUTWA HUKUMU

MASHARTI YA KUFUTWA HUKUMU MASHARTI YA KUFUTWA HUKUMU. Katika makala iliyopita (makala no 2) tulizungumzia kuhusu ufutwaji wa hukumu za Aya ndani ya Qur-ani, katika makala hii basi tutazungumzia masharti ya kufutwa kwa hukumu hizo na kuletwa hukumu nyengine. Ufutwaji wa hukumu una masharti yake nayo ni:- 1. Aya hizo ni lazima ziwepo katika masuala ya hukumu za kisheria, yaani aya zozote zile zitakazokuwa hazizungumzii masuala ya kisheria, haziwezi kuingia katika suala hili. 2. Maudhui ya mwanzo yaliyokuwepo katika aya na yanayotaka kufutwa ni lazima yawe maudhui hayo hayo yaliyokuja katika aya ya pili itakayofuta aya ya mwanzo, (yaani isije ikawa aya ya mwanzo inazungumzia hukumu fulani katika hali ya hiyari, au hali ya siha, na maudhui ya pili yaliyokuja katika aya ya pili yakawa yanazungumzia suala hilo katika hali ya ugonjwa), yaani (hukumu ya mwanzo ilikuwa ikimzungumzia mgonjwa, na hukumu iliyokuja kwa mara ya pili ikamzungumzia mtu mwenye afya kamili). Kwani kila maudhui yaliyokuja katika aya hizo mbili yatakua yana hukumu yake pekee wala hayaingiliani kimaudhui wala kihukumu.

Ufafanuzi

UTAFITI KATIKA KUFUTWA HUKUMU

UTAFITI KATIKA KUFUTWA HUKUMU UTAFITI KATIKA KUFUTWA HUKUMU Tukiendelea na mada yetu kuhusiana na Nasikh na Mansukh, katika makala iliyopita (makala no.3) tulielezea masharti ya kufutwa kwa baadhi ya hukumu na kuletwa hukumu nyengine, katika makala hii tutazungumzia umuhimu kuhusiana na ufutwaji wa hukumu hiyo. Umuhimu wa kuzungumzia suala hili uko wazi kabisa kwani Mwanachuoni anapokuja na kupekuwa hukumu za Kifiqhi ndani ya Qur-ani, au Mwanachuoni anapokuja kutafuta elimu fulani katika Qur-ani ni lazima azielewe hukumu zilizofutwa ili asije akazitumia aya hizo katika kutoa fatuwa katika hukumu fulani.

Ufafanuzi

VIPENGELE VYA MIUJIZA YA QUR_ANI

VIPENGELE VYA MIUJIZA YA QUR_ANI VIPENGELE VYA MIUJIZA YA QUR-ANI (1) A. Wanaelimu wamejadiliana maudhui mbali mbali yanayohusiana na miujiza ya Qur-ani, lakini vile vile wamehitilafiana nadhari kuhusiana na maudhui hayo, maulamaa wa zama zilizopita wametowa nadharia nyengine, na maulamaa wa zama hizi wametoa nadhari nyengine, ijapokuwa katika kauli zao wameongezea na zile nadharia za watu wa zama zilizopita.[1] Wanaelimu wa zama hizi tulizonazo wameigawa miujiza ya Qur-ani katika nyanja tatu zifuatazo:- Miujiza ya mabainisho, miujiza ya kielimu, na miujiza ya kisheria. Katika somo hili tutakizungumzia nyanja hiyo ya mwanzo, yaani miujiza ya mabainisho, na katika somo linalofuata tutaelezea nyanja mbili zilizobakia.

Ufafanuzi

AYA AMBAZO HUKUMU ZAKE ZIMEFUTWA

AYA AMBAZO HUKUMU ZAKE ZIMEFUTWA AYA AMBAZO HUKUMU ZAKE ZIMEFUTWA Ufutwaji wa hukumu zilizokuja katika Qur-ani kwa mtizamo wa Wanachuoni waliopita, suala hili lilikuwa na upana zaidi, na kulikuwa kukipatikana mabadiliko kidogo tu baina ya Aya ya mwanzo iliyokuja na hukumu fulani, na Aya ya pili iliyokuja na hukumu yenye kufanana nayo, basi Wanazuoni wa zamani walikuwa wakiziingiza Aya hizi katika mtiriko wa Aya za Nasikh na Mansukh,   lakini maana ya Nasikh na Mansukh kwa mtizamo wa Wanazuoni wa kileo ni zile Aya tu zenye kufuta hukumu na zinazofutwa hukumu zao ndizo zinazoingia katika mtiririko wa Istilaha hii, yaani Wanazuoni wa kileo wanazihesabu zile Aya zilizochukua nafasi ya hukumu iliyopita ndizo Nasikh, na zile zilizofutwa hukumu zake ndio Mansukhu tu. Basi kwa mtizamo wa Wanazuoni wa zamani, au mbele ya wale wenye kuukubali mtizamo huo kuna Aya nyingi za aina hii hadi kufikia mia mbili na ishirini na nane.

Ufafanuzi

DALILI ZINAZOTHIBITISHA KWAMBA MOLA NI MMOJA

DALILI ZINAZOTHIBITISHA KWAMBA MOLA NI MMOJA DALILI ZINAZOTHIBITISHA YA KWAMBA MOLA NI MMOJA NA WALA HANA MSHIRIKA. Hapana shaka hakuna dalili yoyote inayothibitisha au kukubalika kuwepo kwa waungu zaidi ya mmoja, na kwa wale wenye itikadi hiyo hawana dalili yoyote ya kuthibitisha madai yao. Miongoni mwa watu ambao wana itikadi hiyo ni “firauna” pale alipompa dasturi waziri wake na kumwambia:- Na Firauni akasema: Enyi waheshimiwa! Sijui kama mnaye mungu asiye kuwa mimi. Ewe Haman! Niwashie moto unichomee udongo, unijengee mnara nipate kumchungulia mungu wa Musa. Na hakika mimi namwona yeye ni katika waongo. Mwanaadamu yeyote mwenye akili na aliye huru katika kufikiri na kuzingatia anafahamu ya kuwa hakuna mtu yeyote anayeweza kuumba vitu vilivyomo ulimwenguni, kwa sababu hakuna mtu yoyote mwenye elimu kamili ya vitu hivyo, basi vipi inawezekana kutokea mtu ambaye hana elimu ya vitu hivyo lakini akaweza kuviumba? . Na ni kwa sababu hiyo basi Mitume (a.s) yote ya Mwenyeenzi Mungu imethibitisha na kusema kuwa kuwepo kwa Mwenyeenzi Mungu mmoja ni jambo lililowazi kabisa na lisilo na shaka yoyote.

Ufafanuzi

HUKUMU ZA KIISLAMU

HUKUMU ZA KIISLAMU  HUKUMU ZA KIISLAMU KUJA KWA HUKUMU ZA KIISLAMU KIJUMLA JUMALA Dini ya kiislamu imeelezea sheria za hukumu za kiislamu kijumla jamala, ambapo hakuna dini yoyote iliyoelezea na kufafanua kwa upana sheria zinazohusiana na dini hiyo. Dini ya kiislamu imezigawa hukumu na sheria za kiislamu katika masuala yanayohusiana na sheria za ibada (yaani mja na Mola wake, na katika masuala yanayohusiana na sheria za mja kwa mja, pindi watu watakapozifuata sheria na kanuni hizo zilizoelezewa katika dini ya kiislamu kwa hakika watapata saada ya maisha ya dunia na ya akhera. Katika kanuni na sheria za dini ya kiislamu imeelezewa kwamba kufanya ibada humfanya mwanaadamu aishi katika maisha ya utulivu, na kumfanya awe thabiti katika kukuza uhusiano wake na Mola wake, ambapo hii humpelekea mwanaadamu huyo kuipa nguvu na kuitakasa nafsi yake. kufanya ibada za wajibu au za sunna na kusoma nyuradi wakati wa sala au wakati mwengine wowote humfanya mwanaadamu aitakase nafsi yake na kuwa karibu na Mola wake, na imetiliwa mkazo zaidi iwapo ibada hizo zitafanywa katika sehemu takatifu humfanya mwanaadamu afikie katika ukamilifu katika jamii.

Ufafanuzi

M_BORA WA WAUMBAJI

M_BORA WA WAUMBAJI MBORA WA VUMBE Mpendwa msomaji na mfuatiliaji wa makala zetu, katika makala hii yetu ya leo tumekuletea mambo kadhaa ambayo yanaweza kuwa ni faida kwa waumuni na kwa kila mpenda matukufu na kukuwa kiroho au kupanda daraja kirihio. katika makala hii tumeashiria mambo kadhaa juu ya ubora wa Mwenyezi Mungu, ubora wa mitume, Maimamu, na watu wengine wakawaida. moja katika misingi ya Qur'ani katika kuwaendea watu ni kwamba ubora wa mtu hauwi kwa ubora wa nasaba yake, mali zake, rangi au kabila, bali unakuwa kwa uchamungu wake. hiyo ni moja ya mambo tuliyoyaashiria katika mala yetu hii. hivyo ungana nami mpaka tamati mwa makala hii ili kujipatia faida.

Ufafanuzi

MATAMANIO YA NAFSI

MATAMANIO YA NAFSI DALILI ZINAZOTHIBITISHA KWAMBA MOLA NI MMOJA 2 MATAMANIO YA NAFSI (STIMULUS NATURAL) Viumbe wote tangu wanapozaliwa wanakuwa na matamanio ya nafsi, na matamanio hayo yanawapelekea wanaadamu kupata jawabu ya mahitajio yao ya kidunia na akhera, lakini mbali ya kuwa mwanaadamu ana matamanio ya nafsi vile vile ana matamanio mengine ambayo ni ya juu zaidi, matamanio hayo yamo katika moyo wa mwanaadamu, na hayawezi yakampotosha na kumuweka katika njia mbaya ,kwa sababu Mwenyeenzi Mungu ndiye aliyemjaalia na kumtunukia mwanaadamu neema hiyo. Kwa mfano: - (Mwanaadamu yoyote anapendelea mazuri na anachukia mabaya), mwanaadamu yoyote anajua kwamba kumdhulumu mtu sio jambo zuri, hata kama hajasoma lakini nafsi yake inahukumu ya kwamba dhulma ni dhambi, na vile vile nafsi yake inahukumu kuwa kufanya jambo jema ni vizuri. Matamanio hayo yaliyomo ndani ya nafsi ya mwanaadamu yanaitwa (matamanio ya nafsi). Na matamanio hayo yanamuongoza mwanaadamu katika njia njema.

Ufafanuzi

MIUJIZA INAYOELEZEA MAMBO YA KISHERIA

MIUJIZA INAYOELEZEA MAMBO YA KISHERIA 3. MIUJIZA INAYOELEZEA MAMBO YA KISHERIA Mwanaadamu siku zote yuko katika hali ya kujiuliza masuala kuhusiana na uumbaji na vile vilivyomo ulimwenguni, na anafanya jitihada sana ili kupata jawabu ya kumkinaisha ya masuala yake hayo, miongoni mwa masuala anayojiuliza ni kama haya yafuatayo:- Amekuja kutoka wapi? Sababu gani iliyomfanya aje? Na baadaye atakwenda wapi? Na masuala mengi mengineyo …, ama jitihada zote anazozifanya hajaweza kupata jawabu itakayomuonyesha kwa uwazi siri ya uumbwaji wa dunia hii na vilivyomo. Alla (s.w) katika Suratul- al-Israa Aya ya 85 anasema:- Na wanakuuliza habari ya roho. Sema: “Roho ni jambo lililokhusika na Mola wangu (Mwenyeezi Mungu). Nanyi hamkupewa katika elimu (ujuzi) ila kidogo kabisa. (Nayo ni ilimu ya vitu visivyokhusika na roho)”. Dini – vile ambavyo imeelezewa katika Qur-ani – imeelezea na kuyajibu masuala yote hayo kwa kiasi cha kutosheleza kabisa, kama tutazingatia kwa makini kile ambacho kimeelezewa ndani ya Qur-ani akili za wanaadamu zitakuwa ni zenye kufikiri kwa kiadilifu, na watagunduwa njia ya kuwaongoza katika ukamilifu.

Ufafanuzi

MSUKUMO WA HEWA WENYE KUIHIFADHI ARDHI

MSUKUMO WA HEWA WENYE KUIHIFADHI ARDHI  B. MSUKUMO WA HEWA WENYE KUIHIFADHI ARDHI B Katika makala iliyopita tulionesha mifano inayoashiria elimu, katika makala hii tunaendelea kuelezea mifano mengine, nayo ni hii ifuatayo: Allah (s.w) katika suratul-Anbiyaa Aya ya 32 anasema:- Na tukaifanya mbingu kuwa dari iliyohifadhiwa, lakini wanazikengeuka ishara Zake (Mwenyeezi Mungu). Ardhi imezungukwa na kufunikwa na hewa ambayo unene wake unafikia kilomiter 350, kiwango cha hewa ya gesi ya nitrogen ni asilimia 78/03, na kiwango cha oxygen ni asilimia 20/99, na kiwango cha carbon die oxide ni asilimia 0/04, na mvuke wa maji (water vapour) na gesi nyengine ni asilimia 0/94, kutokana na wingi wa uhifadhiwaji huo wa hewa, na kiwango hicho kikubwa cha gesi huifanya ardhi isiweze kuathiriwa kutokana na mawe mengi yanayoanguka kutoka mbinguni, na kufika sehemu mbali mbali za ulimwengu, kwa hiyo kama kusingelikuwepo na hifadhi hiyo ya ardhi ingelikuwa ni hatari kwa wanaadamu, kwani ni jambo la muhali kuishi katika hali kama hiyo.

Ufafanuzi

MWENYEEZI MUNGU NI MMOJA

MWENYEEZI MUNGU NI MMOJA MWENYEEZI MUNGU NI MMOJA 1 DALILI ZINAZOTHIBITISHA YA KWAMBA MOLA NI MMOJA NA WALA HANA MSHIRIKA. Hapana shaka hakuna dalili yoyote inayothibitisha au kukubalika kuwepo kwa waungu zaidi ya mmoja, na kwa wale wenye itikadi hiyo hawana dalili yoyote ya kuthibitisha madai yao. Miongoni mwa watu ambao wana itikadi hiyo ni “firauna” pale alipompa dasturi waziri wake na kumwambia:- Na Firauni akasema: Enyi waheshimiwa! Sijui kama mnaye mungu asiye kuwa mimi. Ewe Haman! Niwashie moto unichomee udongo, unijengee mnara nipate kumchungulia mungu wa Musa. Na hakika mimi namwona yeye ni katika waongo. Mwanaadamu yeyote mwenye akili na aliye huru katika kufikiri na kuzingatia anafahamu ya kuwa hakuna mtu yeyote anayeweza kuumba vitu vilivyomo ulimwenguni, kwa sababu hakuna mtu yoyote mwenye elimu kamili ya vitu hivyo, basi vipi inawezekana kutokea mtu ambaye hana elimu ya vitu hivyo lakini akaweza kuviumba? . Na ni kwa sababu hiyo basi Mitume (a.s) yote ya Mwenyeenzi Mungu imethibitisha na kusema kuwa kuwepo kwa Mwenyeenzi Mungu mmoja ni jambo lililowazi kabisa na lisilo na shaka yoyote.

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini