Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

Elimu za Qurani

QUR_ANI NA WATOTO

QUR_ANI NA WATOTO

QUR_ANI NA WATOTO  UTANGULIZI Baada ya kupita miaka mingi na kuonekana uzoefu na tajruba (experience) ya kutoa mafunzo ya Qur-ani katika maudhui tofauti yanayowafunza watoto kuielewa Qur-ani, mafunzo hayo yanafundishwa kwa njia ya ishara ili kuwasaidia watoto kuihifadhi Qur-ani kwa urahisi zaidi. Na watu wengi wameyapokea mafunzo hayo na kuridhika nayo, na kwa sababu hiyo basi imetulazimika kutayarisha kitabu hiki ambacho kimekusanya maudhui tofauti , aya za qur-ani, tarjuma (translate), na michoro ambayo inamaanisha na kuonesha ufahamu wa aya hizo za qur-ani, nah ii inasaidia watoto kutamka herufi  za Qur-ani kwa urahisi zaidi.

Ufafanuzi

SIFA TUKUFU ZA MWENYEEZI MUNGU

SIFA TUKUFU ZA MWENYEEZI MUNGU KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU SIFA TUKUFU ZA MWENYEEZI MUNGU. Qur-ani kariym amemsifu na kumuelezea Mwenyeezi Mungu kwa sifa zilizo bora na kamili kabisa, na imejiepusha na kumuelezea kwa sifa mbaya. Katika Suratul-Hashri Aya ya 22-24 tunasoma:- هُوَ اللهُ الَّذِى لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ هُوَ الرَّحْمَنُ الرَّحِيمُ[1] Yeye ndiye Mwenyeezi Mungu ambaye hakuna aabudiwaye kwa haki isipokuwa Yeye tu. Anayejuwa yaliyofichikana na yaliyo dhahiri. Mwenye kuneemesha neema kubwa kubwa na Mwenye kuneemesha neema ndogo ndogo.  هُوَ اللهُ الَّذِى لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ الْمَلِكُ الْقُدُّوسُ السَّلاَمُ الْمُؤْمِنُ الْمُهَيْمِنُ الْعَزِيزُ الْجَبَّارُ الْمُتَكَبِّرُ سُبْحَانَ اللهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ[2] Yeye ndiye Mwenyeezi Mungu ambaye hakuna aabudiwaye kwa haki isipokuwa Yeye tu; Mfalme, Mtakatifu, Mwenye salama, Mtoaji wa amani, Mwenye kuyaendesha Mwenyewe mambo yake, Mwenye shani, Anayefanya analolitaka, Mkubwa. Mwenyeezi Mungu Yu mbali na hao wanaomshirikisha naye. هُوَ اللهُ الْخَالِقُ الْبَارِئُ الْمُصَوِّرُ لَهُ الاَسْمَاء الْحُسْنَي يُسَبِّحُ لَهُ مَا فِى السَّمَاوَاتِ وَالاَرْضِ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ Yeye ndiye Mwenyeezi Mungu, Muumbaji, Mtengenezaji, Mfanyaji wa sura (za namna namna za viumbe); Mwenye majina (sifa) mazuri. Kinamtukuza kila kilichomo mbinguni na ardhini. Naye ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima.  Sifa hizo njema na nzuri za Mwenyeezi Mungu zimetajwa na kuelezewa katika Qur-ani, ama katika vitabu vyengine zimeelezewa vyengine kabisa kiasi ya kwamba uelezewaji huo ulioelezewa katika vitabu vyengine haufanani na sifa za Mwenyeezi Mungu.

Ufafanuzi

VIPENGELE VYA MUUJIZA WA QUR_ANI

VIPENGELE VYA MUUJIZA WA QUR_ANI VIPENGELE VYA MUUJIZA WA QUR-ANI (2). A Katika somo lililopita tulielezea na kukumbushana kuwa muujiza wa Qur-ani umegawika katika vipengele vitatu, vipengele hivyo ni muujiza wa mabainisho, muujiza wa kisheria, na muujiza wa kielimu, kipengele cha mwanzo ambacho ni muujiza wa mabainisho tulikielezea katika makala iliyopita, na vipengele viwili vilivyobakia tutavielezea katika makala hii. 2. MIUJIZA YA KIELIMU ILIYOMO NDANI YA QUR-ANI: Makusudio yaliyokusudiwa katika muujiza wa kielimu ni ishara za kielimu zilizoashiriwa katika baadhi ya aya za Qur-ani, mabainisho hayo ya kielimu hayakuwa hadafu (madhumuni) asili katika ubainishwaji wake, kwa sababu Qur-ani ni kitabu cha uongofu, na hadafu au dhumuni asili ya kuteremshwa kitabu hicho ni kumfunza mwanaadamu njia za kuishi ili afikie katika saada ya Mwenyeezi Mungu na sio kubainisha masuala ya kielimu, kwa hiyo kama katika Aya za Qur-ani tutakabiliana na ishara za kielimu ni kwa sababu maelezo hayo yaliyomo ndani ya Qur-ani yametokana na elimu pamoja na hikima za Mwenyeezi Mungu.

Ufafanuzi

ADABU ZA KUSOMA QUR_ANI

ADABU ZA KUSOMA QUR_ANI ADABU ZA KUSOMA QUR_ANI. - Kuihifadhi (kuiweka safi) Qur-ani ni sunna.- Kuwa tohara au (kuwa na udhu), kujitia mafuta mazuri, kuelekea kibla wakati wa kusoma Qur-ani ni sunna. - Kusoma Qur-ani katika sehemu tukufu, kwa mfano msikitini,au sehemu nyengine tukufu ni suna, na kusoma Qur-ani katika sehemu zisizokuwa nzuri kwa mfano chooni, n.k ni karaha (kunakirihisha). - Kusoma Qur-ani kwa sauti ya juu ni sunna. - Kumsalia Mtume Muhammad (s.a.w.w) kabla ya kusoma Qur-ani ni sunna. - Kusoma Audhu bilahi mina Shayttani rajiymi kabla ya kusoma Qur-ani ni sunna. - Kusoma Qur-ani kwa lahni ya lugha ya kiarabu na sauti nzuri ni sunna. - Kusoma Qur-ani kwa usahihi katika herufi zake ni sunna. - Kusoma Qur-ani kwakutafakari, uangalifu, na kufahamu maana ya aya zake ni sunna. - Kucheka wakati wa kusoma Qur-ani ni karaha na kunakirihisha. - Ni sunna wakati inaposomwa Qur-ani wasikilizaji wanyamaze kimya. - Kukata kusoma Qur-ani, au kuzungumza wakati unaposoma Qur-ani kunakirihisha. Hivi unaelewa kwamba herufi za lugha ya kiarabu ni herufi ishirini na nane, na herufi zote hizo zimejikusanyaka katika aya mbili za Qur-ani.

Ufafanuzi

ATHARI YA TAWHIYD NA KUKAMILIKA KWA MWANAADAMU

ATHARI YA TAWHIYD NA KUKAMILIKA KWA MWANAADAMU 2- ATHARI YA TAWHIYD KATIKA KUKAMILIKA MWANAADAMU KIELIMU Itikadi ya kuamini Mola mmoja ni alama inayoonesha ukamilifu wa mwanaadamu kielimu, na ubora wa mwanaadamu kuliko malaika. Mwenyeezi Mungu Mtukufu anasema:- شَهِدَ اللّهُ اَنَّهُ لاَ إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ وَالْمَلاَئِكَةُ وَاُوْلُواْ الْعِلْمِ قَآئِمَاً بِالْقِسْطِ لاَ إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ[1] Mwenyezi Mungu, na Malaika, na wenye ilimu, wameshuhudia kuwa hakika hapana mungu ila Yeye, ndiye Mwenye kusimamisha uadilifu; hapana mungu ila Yeye Mwenye nguvu na Mwenye hikima. Basi iwapo mtu atauona utukufu wa Mwenyeenzi Mungu na uumbaji wa ulimwengu, na akazishuhudia aya za Mwenyeezi Mungu, lakini asiamini Mola mmoja huyo, basi mtu huyo atakuwa ni miongoni mwa majahili, na ni alama moja wapo inayoonesha ujahili wa mtu huyo. Kama vile Qur-ani inavyosema:- اَمَّن جَعَلَ الاَرْضَ قَرَاراً وَجَعَلَ خِلاَلَهَا اَنْهَاراً وَجَعَلَ لَهَا رَوَاسِيَ وَجَعَلَ بَيْنَ الْبَحْرَيْنِ حَاجِزاً اَإِلَهٌ مَّعَ اللهِ بَلْ اَكْثَرُهُمْ لاَ يَعْلَمُونَ[2] Au nani yule aliye ifanya ardhi mahali pa kutua, na akajaalia ndani yake mito, na akaweka milima? Na akaweka baina ya bahari mbili kiziwizi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Bali wengi wao hawajui. Na kwa wale ambao hawaamini ya kuwa Mola ni mmoja tu ijapokuwa ni wenye kutoa nadhari katika elimu mbali mbali mfano elimu ya tajruba, au wakawa wana cheo katika jamii, lakini kwa upande wa elimu ya Qur-ani na tamaduni ya kiislamu wakawa ni majahili.

Ufafanuzi

DALILI ZINAZOTHIBITISHA ELIMU YA ALLAH

DALILI ZINAZOTHIBITISHA ELIMU YA ALLAH DALILI ZINAZOTHIBITISHA ELIMU YA ALLAH (S.W) Katika makala iliyopita tulielezea elimu ya Mwenyeezi Mungu isiyo na mwanzo wala mwisho, katika makala hii tutazielezea dalili ambazo zinathibitisha elimu hiyo ya Allah (s.w). Dalili mbili zinazothibitisha utukufu usio mpaka wa elimu ya Mwenyeenzi Mungu. 1- Muumba (uumbaji). Hapana shaka yoyote kuwa viumbe vyote ulimwenguni vimeumbwa na Mwenyeenzi Mungu mmoja, naye akaviweka katika nidhamu maalumu,viumbe vyote duniani vinamhitajia Mwenyeenzi Mungu katika kila kitu, kiasi ya kwamba pindi nidhamu hiyo isipokuwa katika mfumo maalumu kutasababisha mparaganyiko katika nidhamu hiyo. Hivyo Mwenyeenzi Mungu Mtukufu anathibitisha hayo kwa kusema kuwa yeye hakughafilika wala hatoghafilika na viumbe vyake alivyoviumba.

Ufafanuzi

ELIMU YA ALLAH HAINA MPAKA

ELIMU YA ALLAH HAINA MPAKA ELIMU YA MWENYEENZI MUNGU HAINA MPAKA * Elimu ya Mwenyeenzi Mungu ikoje? Na ina kiwango gani? * Hivi kuna tofauti baina ya elimu ya Mwenyeenzi Mungu na elimu ya wanaadamu?. Baada ya kuwa na akida na kuamini Mola mmoja, vile vile tunakiwa tuwe na imani ya elimu yake, kwani kuitambua elimu ya Mwenyeenzi Mungu kunaleta athari nyingi muhimu katika itikadi na matendo yetu. Elimu ya Mwenyeenzi Mungu haina mwanzo wala mwisho, kiasi ya kwamba upeo wa elimu hiyo umekusanya vitu vyote alivyoviumba na asivyoviumba, hapana shaka Mwenyeenzi Mungu ana elimu ya kila kitu, ikiwemo elimu ya zama zilizopita na zijazo. Katika somo hili kwa kutumia aya za Qur-ani kariym tutaelewa na kuifahamu elimu ya Mwenyeezi Mungu, na umahiri alioutumia Mwenyeezi Mungu katika kuviumba vitu vyote duniani na akhera.

Ufafanuzi

ELIMU YA ALLAH HAINA MWANZO WALA MWISHO

ELIMU YA ALLAH HAINA MWANZO WALA MWISHO ELIMU YA ALLAH HAINA MWANZO WALA MWISHO Katika makala iliyopita ambayo inahusiana na elimu ya Mwenyeezi Mungu, tulielezea kuwa kuna njia mbili katika kufafanua elimu ya Mwenyeezi Mungu, makala hiyo ya mwanzo tulielezea njia moja, na katika makala hii no 2 tutaelezea njia nyengine, nayo ni hii ifuatayo:- 2- Elimu isiyo ya moja kwa moja, (Yaani kwa kupitia Mitume ya Mwenyeenzi Mungu wanaadamu hutunukiwa elimu hiyo). Kama vile tunavyosoma ndani ya Qur-ani. Na Mwenyezi Mungu amekutoeni matumboni mwa mama zenu, hali ya kuwa hamjui kitu, na amekujaalieni masikio na macho na nyoyo ili mpate kushukuru. Maelezo kuhusiana na aya Inatajwa Qudra ya Mwenyeenzi Mungu na uweza wake na neema zake, basi na zizingatiwe na zishukuriwe.

Ufafanuzi

FAIDA ZA KUSOMA QUR_ANI

FAIDA ZA KUSOMA QUR_ANI FAIDA ZA KUISOMA QUR_ANI: Kuisoma Qur-ani kunaleta faida mbali mbali katika maisha ya mwanaadamu, miongoni mwa faida hizo ni :- 1. Mwenyeezi Mungu humuondolea mabalaa msomaji Qur-ani. 2. Kusoma Qur-ani ni kafara za madhambi. 3. Mwenye kusoma Qur-ani huepukana na moto wa jahannam na huwa katika amani na adhabu za Mwenyeezi Mungu. 4. Muumini mwenye kusoma Qur-ani Mwenyeezi Mungu humuangalia mtu huyo kwa jicho la rehema. 5. Mwenye kusoma Qur-ani siku ya kiama huwa pamoja na Manabii . 6. Mwenye kusoma Qur-ani siku ya kiama huvuka njia akiwa pamoja na Manabii. 7. Mwenye kusoma Qur-ani Mwenyeezi Mungu humpa mtu huyo ujira na malipo ya Mitume wake.

Ufafanuzi

KUITUKUZA QUR_ANI

KUITUKUZA QUR_ANI KUITUKUZA QUR_ANI Walidi bin Mughera alikuwa ni mmoja katika maadui wa kiislamu na Mtume Muhammad (s.a.w.w), Siku moja wakati alipokuwa akisikiliza Qur-ani alisema:- “ Qur-ani ni kitabu kizuri kutokana na yaliyomo ndani yake, na ni kitabu chenye kuleta jazba kwa mwanaadamu. Qur-ani ni kitabu bora na hakuna kitabu bora chengine zaidi ya Qur-ani, Maelezo hayo yalimfikia Abu Jahli, na Abu Jahli alikwenda kwa Walidi bin Mughera na kumwambia:- “Kaumu yako imekusanya mali na kukuletea wewe ili uwache kuisifu Qur-ani, mughera alimjibu abu jahli kwa kusema:- “Mimi nina mali zaidi ya kaumu yangu, na ninajuwa njia za uzungumzaji, kwa hakika maneno anayozungumza Muhammad (s.a.w.w.) ambayo yamo katika Qur-ani sio mashairi.

Ufafanuzi

MNADO NDANI YA QUR_ANI

MNADO NDANI YA QUR_ANI TAHADIY(MNADO) NDANI YA QUR_ANI Moja katika dalili muhimu nyengine za miujiza ya Qur-ani ni Aya zinzozungumzia na kutoa mnado. Madhumuni ya aya za tahadiy (mnado)ni aya ambazo zinazungumzia juu ya maadui wanaoupinga uislamu na Qur-ani, aya hizo zinawataka maadui na makafiri kama wanasema kweli walete aya kumi,na kama hawatoweza kuleta aya hizo basi nawalete angalau aya moja mfano wa Qur-ani, miongoni mwa aya hizo ni:-  فَلْيَاْتُوا بِحَدِيثٍ مِّثْلِهِ إِن كَانُوا صَادِقِينَ[1]   Basi nawalete Hadithi kama hizi; ikiwa wanasema kweli (kuwa hii Qur-ani akaitunga Nabii Muhammad).  قُل لَّئِنِ اجْتَمَعَتِ الإِنسُ وَالْجِنُّ عَلـٰي اَن يَاْتُواْ بِمِثْلِ هَـذَا الْقُرْآنِ لاَ يَاْتُونَ بِمِثْلِهِ وَلَوْ كَانَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ ظَهِيراً Sema “ hata wakijikusanya watu (wote) na majinni ili kuleta mfano wa hii Qur-ani basi hawangaliweza kuleta mfano wake; hata kama watasaidiana (vipi) wao kwa wao.

Ufafanuzi

QUR_ANI KATIKA MTAZAMO WA KIMAGHARIBI

QUR_ANI KATIKA MTAZAMO WA KIMAGHARIBI QUR_ANI KATIKA MTIZAMO WA KIMAGHARIBI Kuna vitabu vingi vilivyoandikwa na wataalamu waliokuwa sio waislamu, wataalamu hao katika vitabu vyao hivyo wameelezea na wameukubali utukufu wa kitabu hicho kitukufu, vile vile katika vitabu hivyo mmetajwa majina ya watu ambao wameukubali utukufu wa Qur-ani. Katika kipengele hiki tutasoma kwa ufupi majina ya wataalamu hao: - Carlituwn- As- kun ni Doctor wa ufumbuzi wa mwanaadamu anayeishi Amerika, anasema:- Moja katika jambo kubwa na tukufu linaloonekana katika kitabu kitukufu cha Qur-ani ni balagha iliyomo katika kitabu hicho, pindi itakapokuwa Qur-ani inasomwa kwa usahihi hapana shaka kwamba msikilizaji wa Qur-ani akiwa anaielewa lugha ya kiarabu au haielewi, anafahamu au haifahamu, itamletea athari kubwa na athari hizo zitabakia katika akili yake, basi hapana shaka kwamba balagha iliyomo katika Qur-ani haiwezi kutarjumiwa.

Ufafanuzi

TAWHIYD NA NIDHAMU YA DUNIA

TAWHIYD NA NIDHAMU YA DUNIA TAWHIYD NA NIDHAMU YA DUNIA Hakuna shaka ya kuwa Mwenyeenzi Mungu Mtukufu ameviumba vitu vyote duniani vikiwa katika nidhamu maalum, na Allah (s.w) anasema:- الَّذِى خَلَقَ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ طِبَاقاً مَّا تَرَي فِى خَلْقِ الرَّحْمَنِ مِن تَفَاوُتٍ فَارْجِعِ الْبَصَرَ هَلْ تَرَي مِن فُطُورٍ[1] Aliye umba mbingu saba kwa matabaka. Huoni tafauti yoyote katika uumbaji wa Mwingi wa Rehema. Hebu rudisha nadhari! Unaona kosa lolote? Nidhamu hiyo ya uumbaji inathibitisha kuwepo kwa Mola mmoja, na Mola huyo ndiye aliyeviumba vitu vyote duniani, na kasha akaviweka katika nidhamu maalumu. Kwani kama kuna mungu zaidi ya mmoja kusingelikuwa na nidhamu yoyote na kungelikuwa na hitilafu na tofauti baina ya muumba mmoja na mwengine, basi natuzingatie ayah ii inayothibitisha kauli hiyo.

Ufafanuzi

HEKIMA YA ALLAH KATIKA NIDHAMU ISIYO YA KIMAUMBILE

HEKIMA YA ALLAH KATIKA NIDHAMU ISIYO YA KIMAUMBILE HEKIMA YA ALLAH KATIKA NIDHAMU ISIYO YA KIMAUMBILE Alama nyengine inayothibitisha na kuonesha hekima ya Mwenyeezi Mungu ni kwamba, Mwenyeezi Mungu hakumuacha mwanaadamu bila ya kumuonesha njia itakayomuongoza katika njia njema, na siku ya mwanzo alimuelewesha Nabii adam (a.s) uhakika wa dunia. وَعَلَّمَ آدَمَ الاَسْمَاء كُلَّهَا ثُمَّ عَرَضَهُمْ عَلـٰي الْمَلاَئِكَةِ فَقَالَ اَنبِئُونِى بِاَسْمَاء هَـؤُلاء إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ[1] Na akamfundisha Adam majina ya vitu vyote, kisha akaviweka mbele ya Malaika, na akasema: Niambieni majina ya hivi ikiwa mnasema kweli. Mwenyeezi Mungu amemchagua Nabii Adam (a.s) kuwa ni Mtume wa mwanzo duniani, na kwa kuendelea kuituma Mitume mengine alithibitisha hekima yake katika nidhamu isiyokuwa ya kimaumbile, kama tunavyomsikia Nabii Ibrahim (a.s) akisema:- رَبَّنَا وَابْعَثْ فِيهِمْ رَسُولاً مِّنْهُمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِكَ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَيُزَكِّيهِمْ إِنَّكَ اَنتَ العَزِيزُ الحَكِيمُ[2] Ewe Mola Mlezi wetu! Waletee Mtume anaye tokana na wao, awasomee Aya zako, na awafundishe Kitabu na hikima na awatakase.Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima. Mwenyeezi Mungu Mtukufu na Hakiym alituma sheria zake kupitia Mitume yake mitukufu kutokana na maendeleo ya wanaadamu,hadi zama za Mtume Muhammad (s.a.w.w) ambaye ni Mtume wa mwisho na dini yake ndiyo dini kamili aliyokuja nayo kutoka kwa Mola wake (s.w).

Ufafanuzi

HEKIMA ZA ALLAH KATIKA NIDHAMU YA KIMAUMBILE

HEKIMA ZA ALLAH KATIKA NIDHAMU YA KIMAUMBILE HEKIMA ZA ALLAH KATIKA NIDHAMU YA KIMAUMBILE Tukiangalia na kuzingatia kwa makini siri ya uumbaji wa viumbe vyote duniani, na tukifikiria nidhamu ya vitu hivyo vinavyostaajabisha na kujalibisha hapana shaka uhakika wa wanaadamu utadhihirika. Nidhamu hiyo tukufu tunaiona katika viumbe mbali mbali duniani, kuanzia ndege, wanyama, viumbe wanaoishi katika ardhi na baharini, n.k…vyote hivyo ni alama inayoonesha uwezo na hekima za Mwenyeenzi Mungu, na vyote hivyo vinathibitisha kutokuwepo aibu yoyote katika uumbaji wa Mwenyeenzi Mungu.

Ufafanuzi

KUDHIHIRIKA KWA QUDURA YA MOLA

KUDHIHIRIKA KWA QUDURA YA MOLA KUDHIHIRIKA KWA QUDURA YA MOLA Mwenyeezi Mungu Mtukufu Mwenye uwezo na qudra ameiumba dunia kutokana na nidhamu maalumu. Na kwa sababu hiyo basi anawapa jawabu kaumu ya Mayahudi kwa kusema:-  وَقَالَتِ الْيَهُودُ يَدُ اللهِ مَغْلُولَةٌ غُلَّتْ اَيْدِيهِمْ وَلُعِنُواْ بِمَا قَالُواْ بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ يُنفِقُ كَيْفَ يَشَاءُ وَلَيَزِيدَنَّ كَثِيراً مِّنْهُم مَّا اُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ طُغْيَاناً وَكُفْراً وَاَلْقَيْنَا بَيْنَهُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاء إِلَي يَوْمِ الْقِيَامَةِ كُلَّمَا اَوْقَدُواْ نَاراً لِّلْحَرْبِ اَطْفَاَهَا اللّهُ وَيَسْعَوْنَ فِى الاَرْضِ فَسَاداً وَاللّهُ لاَ يُحِبُّ الْمُفْسِدِينَ[1] Na Mayahudi walisema: Mkono wa Mwenyezi Mungu umefumba. Mikono yao ndiyo iliyo fumba, na wamelaaniwa kwa sababu ya waliyo yasema. Bali mikono yake iwazi. Hutoa apendavyo. Kwa yakini yaliyo teremshwa kwako kutoka kwa Mola wako Mlezi yatawazidisha wengi katika wao uasi na kufuru. Na Sisi tumewatilia uadui na chuki baina yao mpaka Siku ya Kiyama. Kila mara wanapo washa moto wa vita, Mwenyezi Mungu anauzima. Na wanajitahidi kuleta uharibifu katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu hawapendi waharibifu.

Ufafanuzi

NYENZO ZA ELIMU YA MWENYEEZI MUNGU

NYENZO ZA ELIMU YA MWENYEEZI MUNGU NYENZO ZA ELIMU YA MWENYEEZI MUNGU Kuwepo kwa Mwenyeezi Mungu ni uhakika usiopingika, Mwenyeezi Mungu Mtukufu ametakasika na kila kitu, Yeye hana jinsia yoyote yaani (si mwanamke wala si mwanamme), lakini ili wanaadamu waweze kuelewa na kufahamu nyenzo tofauti zinazohusiana na elimu ya Mwenyeezi Mungu wanatakiwa waifahamu Qur-ani kwa vizuri, Qur-ani tukufu imetumia lafdhi (maneno) yanayomaanisha hisia, kwa mfano, kusikia , kuona… katika kumsifu na kumtakasa Mwenyeezi Mungu,Kwa mfano, ilipoelezewa kuhusiana na elimu ya Mwenyeezi Mungu ya kwamba Yeye anajua na anasikia kila kitu limetumiwa neno (سمیع) yaani anasikia, kama pale hadharati Zakariyya (a.s) alipokuwa akimuomba na kumtakasa Mola wake.

Ufafanuzi

QUDRA YA MOLA ISIYO NA MPAKA

QUDRA YA MOLA ISIYO NA MPAKA QUDRA YA MOLA ISIYO NA MPAKA * Uwezo na kudura ya Mwenyeezi Mungu katika nidhamu ya dunia inadhihirika vipi? *Kuna uhusiano gani baina ya sifa ya elimu ya Mwenyeezi Mungu, na sifa ya uwezo wa Mwenyeezi Mungu? *  Hivi kweli hiyari ya mwanaadamu inaendana sambamba na Qudra (uwezo) ya Mwenyeenzi Mungu?. Qudura ya Mwenyeezi Mungu isiyo na mpaka. Baada ya elimu ya Mwenyeezi Mungu, miongoni mwa sifa nyengine muhimu kamilifu za Mwenyeezi Mungu ni Qudra na uwezo wake Yeye Allah (s.w), ambayo sifa hiyo ndiyo chanzo cha sifa nyingi nyengine za kitukufu za Allah (s.w). Viumbe vyote alivyoviumba Mwenyeenzi Mungu, vikubwa na vidogo, miti, mimea na wanyama, vinaonesha Qudra yake Allah (s.w), na alionesha Qudra yake hiyo pale alipomuumba mwanaadamu ambaye ni kiumbe bora takatifu, basi Mwenyeezi Mungu alipomuumba mwanaadamu huyo alijipongeza kwa kusema:- Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. “Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji”.

Ufafanuzi

UTUKUFU WA MWANAMKE

UTUKUFU WA MWANAMKE UTUKUFU WA MWANAMKE MWANAMKE NDANI YA QUR_ANI Wanakuuliza nini sharia ya wanawake. Sema: Mwenyezi Mungu ana kutoleeni fatwa juu yao, na mnayo somewa humu Kitabuni kukhusu mayatima wanawake ambao hamwapi walicho andikiwa, na mnapenda kuwaoa, na kukhusu wanyonge katika watoto, na kwamba mwasimamie mayatima kwa uadilifu. Na kheri yoyote mnayo fanya Mwenyezi Mungu anaijua. Ufafanuzi Aya hii inahadidisha adhabu ya wenye kuwadhulumu wanawake, kama ilivyoshadidishwa adhabu ya wenye kuwadhulumu mayatima. hao wote takriba ni wanyonge basi isiwe “Mnyonge Msonge.” Kwa ufupi maana ya Aya ni kuwa waislamu walimtaka Mtume kuwabainishia hukumu ya wanawake. Mwenyezi Mungu (s.w.t) akamwambia Mtume wake: waambie Mwenyezi Mungu amewabainishia sehemu ya hukumu hii na sasa anawabainishia sehemu nyingine, la muhimu kwenu ni kufanya uadilifu na kuitumia hukumu hiyo. Kisha akawabainishia Mwenyezi Mungu (s.w.t.), katika Aya inayofuatia hukumu ya mwanamke, anayehofia unashiza wa mumewe na kuachana na mumewe.

Ufafanuzi

UUMBWAJI WA MBINGU NA ARDHI

UUMBWAJI WA MBINGU NA ARDHI UUMBWAJI WA MBINGU NA ARDHI Mwenyeezi Mungu Mtukufu katika suratun Nisaa aya ya 131- 134 anasema:- Maana ya Aya hizo tukufu ni:- Na ni vya Mwenyezi Mungu tu vyote viliomo katik mbingu na viliomo katika dunia. Na kwa hakika tuliwausia walio pewa Kitabu kabla yenu,na nyinyi pia, kwamba mumche Mwenyezi Mungu. Na mkikataa, basi ni vya Mwenyezi Mungu viliomo mbinguni na viliomo duniani. Na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, anajitosha, na Msifiwa. Na ni vya Mwenyezi Mungu viliomo katika mbingu na viliomo katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Mlinzi. Akitaka atakuondoeni, enyi watu! Na awalete wengineo. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa hayo. Anaye taka malipo ya dunia, basi kwa Mwenyezi Mungu yapo malipo ya dunia na Akhera. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona.

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini