Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

Elimu za Qurani

IDADI YA AYA ZA QUR_ANI

IDADI YA AYA ZA QUR_ANI

IDADI YA AYA ZA QUR_ANI Watu wamehitilafiana nadhari kuhusiana na adadi ya aya za Qur-ani, lakini hitilafu hizo haimaanishi kwamba Qur-ani zinahitilafiana. Kwani ni jambo lililowazi na lisiloshaka ndani yake ya kwamba Qura-ni haijazidi wala kupunguwa Qur-ani zote ni moja na ni zenye kufanana hitilafu zilizopo ni katika adadi ya aya za Qur-ani, baadhi yao wamesema ya kwamba chanzo cha hitilafu hizo kinatokana pale Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu alipokuwa akisoma aya kwa masahaba zake alisita kidogo ili waelewe mwanzo na mwisho wa aya,  lakini kwa bahati mbaya baadhi ya masahaba wa Mtume walidhani kuwa pale Mtume alipokuwa akisita hakumaanishi kupambanua baina ya aya mbili, kwa hiyo waliziunganisha aya hizo na aya zinazofuata na kuhesabu kuwa ni aya moja tu, na baadhi ya masahaba wengine pale ambapo Mtume alipokuwa akisita walihesabu kuwa ni mwisho wa aya.

Ufafanuzi

HEKIMA ZA ALLAH (S.W) KWA WENYE KUFUATA HAKI

HEKIMA ZA ALLAH (S.W) KWA WENYE KUFUATA HAKI HEKIMA ZA MWENYEEZI MUNGU KWA WENYE KUFUATA HAKI. Ijapokuwa milki na hekima za Mwenyeezi Mungu katika dunia ni jambo lililowazi kabisa kwa wale ambao wanatafuta haki, lakini siku ya kiama watu wote watajua na kuelewa uhakika huo. Kama vile ambavyo tunaona katika dunia kuwa baadhi ya watu hukumbwa na adhabu kali ya Mwenyeezi Mungu, na wakati huo basi hufahamu hekima zake Allah (s.w),kuhusiana na maelezo hayo Allah (s.w) anasema:- وَلاَ يَزَالُ الَّذِينَ كَفَرُوا فِى مِرْيَةٍ مِّنْهُ حَتَّي تَاْتِيَهُمُ السَّاعَةُ بَغْتَةً اَوْ يَاْتِيَهُمْ عَذَابُ يَوْمٍ عَقِيمٍ  . الْمُلْكُ يَوْمَئِذٍ لِّلَّهِ يَحْكُمُ بَيْنَهُمْ فَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فِى جَنَّاتِ النَّعِيمِ[1] Na walio kufuru hawatoacha kuwa katika wasiwasi kwa hilo mpaka Saa iwafikie ghafla, au iwafikie adhabu ya Siku Tasa. Ufalme wote siku hiyo utakuwa wa Mwenyezi Mungu. Atahukumu baina yao. Basi walio amini na wakatenda mema watakuwa katika Bustani zenye neema. Siku ya Kiama hekima ya Mwenyeezi Mungu itadhihirika kwa uwazi kabisa kiasi ya kwamba hakuna mtu mwenye haki au atakayeweza kuzungumza bila ya idhini ya Mola wake.

Ufafanuzi

SAUTI TUKUFU YA QUR_ANI

SAUTI TUKUFU YA QUR_ANI SAUTI TUKUFU YA QUR_ANI SAUTI TUKUFU YA QUR_ANI INAYOMVUTIA MWANAADAMU NA KUMUWEKA KATIKA UTULIVU Abu Jahli, Abu Sufiyani, na Akhnas bin Shariq walikuwa ni washirikina maarufu, vichwa ngumu na ni maadui wa Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu, na - hadharati Muhammad (s.a.w.w) - watu hao walichukiwa sana walipoona kwamba sauti ya Qur-ani inawavutia watu kwa kuingia katika dini ya kiislamu, na walifanya jitihada sana ili kuuzima na kuuondowa uislamu, lakini kwa uweza wake Mola hawakufikia wala kufanikiwa katika natija (malengo) yao. Siku moja watu watatu hao kila mmoja peke yake na bila ya kufahamu malengo ya mwenziwe waliamua kwenda nyumbani kwake Mtume (s.a.w.w) usiku, watu hao walijificha sehemu iliyokuwa na giza katika ukuta wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w) wakisikiliza sauti ya Qur-ani iliyokuwa ikisikilika nyumbani kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Ufafanuzi

UHUSIANO BAINA YA UFALME NA HEKIMA ZA ALLAH S.W

UHUSIANO BAINA YA UFALME NA HEKIMA ZA ALLAH S.W UHUSIANO BAINA YA UFALME NA HEKIMA ZA MWENYEEZI MUNGU * Milki na ufalme wa Mwenyeezi Mungu uko katika hali gani?. * Kuna uhusiano gani baina ya milki (ufalme) na hekima za Mwenyeezi Mungu?. * Ufalme wa Mwenyeezi Mungu umedhihirika vipi katika uumbaji wake?. * Hivi kweli hekima za Twaaghuuti na hekima za Mwenyeezi Mungu zisizo mpaka zinaendana sambamba?. MILKI (UFALME) NA HEKIMA ZISIZO MPAKA ZA MWENYEEZI MUNGU (S.W.). Milki na ufalme wa viumbe vyote duniani ni wa Mwenyeezi Mungu (s.w), na viumbe vyote duniani viko chini ya ufalme wake Yeye Mola Muwezi, hata mali na vitu vyote vinavyomilikiwa na wanaadamu ni amana kutoka kwake Yeye Allah (s.w). Kwa hiyo vitu vyote vinavyomilikiwa na wanaadamu kiuhakika sio milki yao, kwani milki ya uhakika ni yake Yeye Allah (s.w). Milki na hekima isiyo mpaka ya Mwenyeezi Mungu ni dhati na ya uhakika, na vitu vyote duniani vilivyo na akili na visivyo na akili vinatii na kuheshimu amri zake Allah (s.w). Kuna dalili nyingi zilizo wazi zinazothibitisha hekima za Mwenyeezi Mungu, na Yeye ndiye muaminifu katika kuhukumu kutokana na kanuni hizo. Na hii ni kwa sababu Mwenyeezi Mungu ni mwenye kujua uhakika na siri zote katika dunia, na anajua yale anayoyahitajia mwanaadamu katika maisha yake.

Ufafanuzi

SALA NDANI YA QUR_ANI

SALA NDANI YA QUR_ANI SALA NDANI YA QUR_ANI Aya hizi zinazofuata zinahusiana na sala gani? [1] 1: وَإِذَا ضَرَبْتُمْ فِى الاَرْضِ فَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ اَن تَقْصُرُواْ مِنَ الصَّلاَةِ إِنْ خِفْتُمْ اَن يَفْتِنَكُمُ الَّذِينَ كَفَرُواْ إِنَّ الْكَافِرِينَ كَانُواْ لَكُمْ عَدُوّاً مُّبِينا Na mnaposafiri katika ardhi, si vibaya kwenu kama mkifupisha Sala; iwapo mnaogopa ya kwamba wale waliokufuru watakutaabisheni. Bila shaka makafiri ni maadui zenu dhahiri.  2  وَمِنَ اللَّيْلِ فَتَهَجَّدْ بِهِ نَافِلَةً لَّكَ عَسَي اَن يَبْعَثَكَ رَبُّكَ مَقَاماً مَّحْمُودا ً[2]: Na katika usiku jiondoshee usingizi (kidogo) kwa (kusoma) hivyo (Qur-ani ndani ya sala). Hiyo ni (ibada) zaidi kwako. Huwenda Mola wako akakuinua cheo kinachosifika.  3: يَا اَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نُودِى لِلصَّلاَةِ مِن يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَي ذِكْرِ اللهِ وَذَرُوا الْبَيْعَ ذٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ[3] Enyi mlioamini! Kukiadhiniwa kwa ajili ya Sala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kumtaja Mwenyeezi Mungu na acheni biashara. Kufanya hivi ni bora kwenu. Ikiwa mnajua (hivi basi fanyeni). 4: وَاَقِيمُواْ الصَّلاَةَ وَآتُواْ الزَّكَاةَ وَارْكَعُواْ مَعَ الرَّاكِعِينَ[4] Na simamisheni Sala (Enyi Mayahudi) na toeni Zaka na inameni (yaani rukuuni) pamoja na wanaoinama (yaani kuweni Waislamu).

Ufafanuzi

HEKIMA YA ALLAH (S.W) KWA NABII IBRAHIMU (A.S)

HEKIMA YA ALLAH (S.W) KWA NABII IBRAHIMU (A.S) HEKIMA YA ALLAH (S.W) KWA NABII IBRAHIMU (A.S). Kisa cha Nabii Ibrahim (a.s) kinaonyesha Utukufu katika Miujiza ya Mwenyeezi Mungu, na Miujiza ni moja wapo miongoni mwa utukufu na hekima za Mwenyeezi Mungu katika nidhamu za kimaumbile, kwa sababu, kama tunavyojua kuwa vitu vyote ni vya Mwenyeezi Mungu basi athari ya vitu vyote hivyo pia ni ya Mwenyeezi Mungu, lakini baadhi ya wakati Mwenyeezi Mungu huleta muujiza ili kuthibitisha uhakika wa vitu hivyo, na baadhi ya wakati huleta athari za kimaumbile katika kuthibitisha hayo. Mfano: Pale alipouamrisha moto uwe baridi kwa ajili ya Nabii Ibrahim (a.s), au kubadilika fimbo ya Nabii Mussa (a.s) na kuwa nyoka, na miujiza mengine mingi aliyoileta ili kuthibitisha utukufu wake.

Ufafanuzi

HIJABU NDANI YA QUR_ANI NO.2

HIJABU NDANI YA QUR_ANI NO.2 HIJABU NDANI YA QURAN .2 Tukiendelea na mada yetu kuhusiana na umuhimu wa kuvaa hijabu katika jamii, katika makala hii tutandelea kuelezea athari nyengine muhimu za kuvaa hijabu  katika jamii. ATHARI NYENGINE Mbali ya hayo niliyokuelezea kuvaa hijabu kwa mwanamke wa kiislamu kunawasababishia wengine kutokana na mwanamke huyo kuwa karibu na Mola wake,wavutiwe na tabia za mwanamke huyo na wao wafanya yale ambayo Mola wao anataka, hivyo tunaweza kuwagawa watu katika makundi matatu. 1. Watu wema na wanadumu katika uongofu wao. 2. Watu aliokuwa sio wema ambao wanakubali makosa waliofanya na wanapojirekebisha huwa thabiti katika msimamo wao, watu walio katika makundi haya mawili ni kidogo sana. 3. Watu wa kundi la tatu wanategemea hali ya jamii ilivyo, ikiwa jamii iko katika tamaduni nzuri na wao hufuata namna ya utamaduni wao ulivyo,na ikiwa jamii haiko katika tamaduni nzuri na wao vile vile hufuata  namna ya utamaduni wao ulivyo.

Ufafanuzi

HIJABU NDANI YA QUR_ANI

HIJABU NDANI YA QUR_ANI HIJABU NDANI YA QUR_ANI Katika makala zilizopita tulielezea umuhimu wa kuvaa hijabu katika jamii, na tukaashiria baadhi ya masuala ambayo yanaweza kujitokeza akilini mwa kila mtu na tukayajibu baadhi ya masuala hayo kadri ya uwezo wetu, kwa kuthibitisha kwa Aya za Qur-ani takatifu. Tukiendelea na mada yetu hiyo, katika makala hii tutaendelea kuyajibu masuala hayo. Suala lilikuwa hivi:- Dada mpendwa wewe uliuliza kwamba una malengo gani mpaka uvae hijabu, na usivae nguo za zinazokwenda na wakati na kujipamba? Tukiendelea na majibu yetu tunasema kuwa:- Kuvaa hijabu kunaleta usalama wa watu na jamii.

Ufafanuzi

THAMANI YA UADILIFU 4

THAMANI YA UADILIFU 4 THAMANI YA UADILIFU Mafunzo ya dini ya Uislamu yameweza kuweka athari kubwa zenye thamani kwenye fikra za wanaadamu, mafunzo haya si tu yameweze kufungua milango mipya ya kielimu katika nyanja za kijografia na kibaiolojia pamoja na kijamii, bali mafunzo hayo yameubadilisha mfumo wa fikra za wanaadamu, na suala ni lenye umuhimu sana katika maisha ya mwanaadamu na jamii. Ni bidii ya kila mwalimu kutoa mafuzo mapya yenye faida kwa wanafunzi wake, na kila mfumo unaokuja katika katika jamii hujaribu kutoa mafunzo mapya kwa ajili ya wafuasi wa mfumo huo, lakini ni mifumo michache inakuja na kuweza kuubadilisha mzima wa fikra za wafuasi wake na kuwafunza namna mpya kabisa ya kufikiri.

Ufafanuzi

KAULI KUHUSIANA NA UADILIFU 3

KAULI KUHUSIANA NA UADILIFU 3 KAULI KUHUSIANA NA UADILIFU. 4 Mafakihi, na Maulamaa wamehitalifiana katika kutafsiri maana ya uadilifu. - Kuna miongoni katika wao mwenye kusema, ya kwamba ni dhahiri ya uislam bila ya kudhihirisha  ufasiki. - Mwingine akasema, ni tabia iliyomo ndani ya nafsi inayopelekea kufanya wajibu na kuacha yale  yaliyoharamishwa. - Wengine wakasema, ni sitara na kujistahi. - Na wengine wakasema ni kuacha kutenda madhambi makubwa na kutoendelea na kumuasi  Mwenyeezi Mungu kwa kufanya madhambi madogo. Katika makala zilizopita tulizungumzia kauli mbali mbali za Maulamaa  kuhususiana na uadilifu, na tukaashiria baadhi ya Aya za Qur-ani zinazohusiana na maudhui hayo, katika makala hiitunaendelea na mada yetu hiyo, na vile vile tutaashiria baadhi ya hutuba zilizomo ndani ya Nahjulbalagha zinazoelezea kuhusu uadilifu.

Ufafanuzi

KAULI KUHUSIANA NA UADILIFU 2

KAULI KUHUSIANA NA UADILIFU 2 KAULI KUHUSIANA NA UADILIFU.2 Mafakihi, na Maulamaa wamehitalifiana katika kutafsiri maana ya uadilifu. - Kuna miongoni katika wao mwenye kusema, ya kwamba ni dhahiri ya uislam bila ya kudhihirisha  ufasiki. - Mwingine akasema, ni tabia iliyomo ndani ya nafsi inayopelekea kufanya wajibu na kuacha yale  yaliyoharamishwa. - Wengine wakasema, ni sitara na kujistahi. - Na wengine wakasema ni kuacha kutenda madhambi makubwa na kutoendelea na kumuasi  Mwenyeezi Mungu kwa kufanya madhambi madogo. Katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:- "Msifuate hawaa (yaani kufanya maasi kwa kufuata yale ambayo nyoyo zinapendelea kuyafanya) ili  mfanye uadilifu."  Na ili kuthibitisha kuwa uadilifu ni kuhalifu hawaa. Amirul-muminin Ali (a.s.) alimsifu ndugu yake, kwa Mwenyezi Mungu, katika aliyomsifu kuwa; "Alikuwa akijiwa ghafla na mambo mawili huangalia lipi lililo karibu zaidi na hawaa kisha akalikhalifu." Na akasema: "Mwanzo wa uadilifu wake ulikuwa ni kukanusha hawaa ya nafsi yake." Amesema Mjukuu wake, Imam Jafar as-Sadiq: "Ama katika mafaqih atakayekuwa anaichunga nafsi yake, mwenye kuihifadhi dini yake, mwenye kukhalifu hawaa yake, mwenye kutii amri ya Mola wake basi ni juu ya watu kumfuata."  Na mkiupotoa au mkaachana nao basi Mwenyezi Mungu ana habari ya myatendayo.

Ufafanuzi

KAULI KUHUSIANA NA UADILIFU

KAULI KUHUSIANA NA UADILIFU KAULI KUHUSIANA NA UADILIFU. Mafakihi,na Maulamaa wamehitalifiana katika kutafsiri maana ya uadilifu. -Kuna miongoni katika wao mwenye kusema, ya kwamba ni dhahiri ya uislam bila ya kudhihirisha  ufasiki. - Mwingine akasema, ni tabia iliyomo ndani ya nafsi inayopelekea kufanya wajibu na kuacha yale  yaliyoharamishwa. - Wengine wakasema, ni sitara na kujistahi. - Na wengine wakasema ni kuacha kutenda madhambi makubwa na kutoendelea na kumuasi  Mwenyeezi Mungu kwa kufanya madhambi madogo. Katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:- "Msifuate hawaa (yaani kufanya maasi kwa kufuata yale ambayo nyoyo zinapendelea kuyafanya) ili  mfanye uadilifu."  Na ili kuthibitisha kuwa uadilifu ni kuhalifu hawaa. Amirul-muminin Ali (a.s.) alimsifu ndugu yake, kwa Mwenyezi Mungu, katika aliyomsifu kuwa; "Alikuwa akijiwa ghafla na mambo mawili huangalia lipi lililo karibu zaidi na hawaa kisha akalikhalifu." Na akasema: "Mwanzo wa uadilifu wake ulikuwa ni kukanusha hawaa ya nafsi yake."

Ufafanuzi

HEKIMA YA KUVAA HIJABU

HEKIMA YA KUVAA HIJABU HEKIMA NA MALENGO YA KUVAA HIJABU Katika makala hii tutaelezea baadhi ya hekima na malengo machache tu ya kuvaa hijabu, na katika makala ijayo tutaendelea kuelezea hekima hizo.  Dada mpendwa wewe uliuliza kwamba una malengo gani mpaka uvae hijabu, na usivae nguo za zinazokwenda na wakati na kujipamba? JAWABU: Mimi nna uhakika kwamba kama utakaa na kufikiri kwa makini kuhusu suala hilo basi ni lazima utafahamu malengo ya kuvaa hijabu. Kwa maoni yangu mimi mwanamke yoyote atakaesoma maelezo hayo ataelewa umuhimu na malengo ya kuvaa hijabu.  1. KUDHIHIRISHA URAFIKI KATIKA KUMPENDA MOLA Hakuna shaka wewe ushashuhudia baadhi ya watu walio karibu nawe, inawezekana rafiki, au mtu mwengine yoyote mkawa mmekinaiana na akatumia lugha mbali mbali za kukuonesha wewe kwamba anakujali na ni rafiki wake wa karibu sana, ikatokea siku ukawa na shida na ukamfata mmoja wa rafiki zako hao na kumuomba akusaidie kiasi fulani cha pesa, lakini akakujibu kwamba yeye pia anahitaji kusaidiwa pesa na wewe, siku nyengine ukamwambia akuazime kitabu akakujibu kwamba yeye vile vile anataka kusoma, fikiria kila unapokuwa na shida anakuzungusha huku na huku kuonesha kwamba hataki kukusaidia, wewe unaweza kumfikiria nini mtu kama huyo.

Ufafanuzi

MWENYEEZI MUNGU NI MLINZI

MWENYEEZI MUNGU NI MLINZI MWENYEEZI MUNGU NI MLINZI * Inaposemwa kwamba Mwenyeezi Mungu ni Walii (Mlinzi) ina maana gani?. * Hivi kweli Ulinzi wa Mwenyeezi Mungu kwa watu wote ni sawa?. * Hivi kweli kuna uwiano baina ya ulinzi wa Mwenyeezi Mungu na ulinzi wa shetani?. Uwalii (Ulinzi) wa Mwenyeezi Mungu. Hapana shaka mwanaadamu anapata saada ya dunia na Akhera pale tu atakapoukubali uwalii na ulinzi wa Mwenyeezi Mungu,  Kwa sababu Mwenyeezi Mungu ni Mwenye nguvu na rehema katika matatizo yoye yanayomfika mwanaadamu, na Yeye ndiye Mwenye kumuongoza na kumsaidia mwanaadamu pindi anapokutwa na matatizo au mitihani yake Allah (s.w).

Ufafanuzi

MWENYEEZI MUNGU NI WALII KWA WAJA WOTE

MWENYEEZI MUNGU NI WALII KWA WAJA WOTE MWENYEEZI MUNGU NI WALII KWA WAJA WOTE Uwalii wa Mwenyeezi Mungu kwa waja wote, na uwalii Wake kwa waja makhsusi na maalumu. Mwenyeezi Mungu Mtukufu aliyeumba vitu na viumbe vyote duniani ndiye Walii na mlinzi wa kuongoza na kusimamia mambo ya viumbe wote duniani, na Mwenyeezi Mungu ndiye Mlinzi wa kuwasimamia waja hao, hakuna shaka kuwa nidhamu ya kimaumbile na kuendelea kwa maisha ya wanaadamu iko chini ya ulinzi wake Allah (s.w), na ulinzi huo huitwa (wilayat takwiniyah) – yaani uwalii wa kimaumbile - Na uwongofu wa wa wanaadamu unaonyesha (wilayat tashriiyyah) – yaani uwalii usio wa kimaumbile – Mwenyeezi Mungu huwapa waja wake wote wilayat tashriiyah, yaani Mwenyeezi Mungu huwaongoza na kuwasimamia waja wake wote, na uwalii huu ni manufaa kwa waja wote duniani. Isipokuwa kwa baadhi ya wale ambao waliochagua chaguo baya katika kumchagua Mola wao. – yaani wanaabudu asiyekuwa mola anayestahiki kuabudiwa – na wakamfanya mungu wao huyo ndiye muongozi na msimamizi wa mambo yao.

Ufafanuzi

WILAYATI NA WALII NDANI YA QURAN

WILAYATI NA WALII NDANI YA QURAN WILAYATI NA WALII NDANI YA QUR_ANI. UFAFANUZI WA NENO WILAYAT (WALII). Neno walii kilugha lina maana tofauti, miongoni mwa hizo ni:- Walii yaani kuwa karibu bila ya umbali wa masafa, kama ilivyokuja katika Qur-ani:- يَا اَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ لاَ تَتَّخِذُواْ آبَاءكُمْ وَإِخْوَانَكُمْ اَوْلِيَاء إَنِ اسْتَحَبُّواْ الْكُفْرَ عَلـٰي الإِيمَانِ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَاُوْلَـئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ[1] Enyi mlio amini! Piganeni na wale makafiri walio karibu yenu, na wakute ugumu kwenu. Na jueni ya kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja na wacha- Mngu. * Ikiwa una maadui walio hatari kwako, muanze aliye karibu yako,umlaze vizuri, waogope walio mbali ipatikane salama. Walii ni mtu ambaye anasimamia na kuongoza mambo bila ya kupitia kwa mtu mwengine

Ufafanuzi

SIFA TUKUFU ZA QUR_ANI NO.2

SIFA TUKUFU ZA QUR_ANI NO.2 MSINGI WA QUR_ANI TAKATIFU NO.2. Katika makala zilizopita tulielezea misingi ya kuifahamu Quran takatifu, na tukaelezea baadhi ya sifa za Suratul-Faatiha, katika makala hii tunaendelea kuzielezea sifa nyengine za sura hiyo hiyo. Suratul-Fatiha. Imeitwa kwa jina tukufu hili kwa ajili ya mnasaba na muwafka wake, kwani tamko la Fatiha katika lugha ya kiarabu maana yake ni chanzo (mwanzo_cha kila kitu kile- kikiwa maneno au kitendo, basi hii Suratul-Fatiha ndiyo dibaji na ndio utangulizi wa Qurani. Wakati wa kuteremka kwake. Imeteremka sura hii mwanzo wa kuja Utume. Na hii ndio sura ya awali kuteremka kamili. Kabla yake ziliteremka Aya tu zilizomo katika sura ya Iqraa na Suratul-Muddathiri na Suratul-Muzzammil.

Ufafanuzi

SIFA TUKUFU ZA QUR_ANI

SIFA TUKUFU ZA QUR_ANI MSINGI WA QUR_ANI TAKATIFU NO.1. Katika makala zilizopita tulielezea misingi ya kuifahamu Quran takatifu, na tukaelezea baadhi ya sifa za Suratul-Faatiha, katika makala hii tunaendelea kuzielezea sifa nyengine za sura hiyo hiyo. Suratul-Fatiha. Imeitwa kwa jina tukufu hili kwa ajili ya mnasaba na muwafka wake, kwani tamko la Fatiha katika lugha ya kiarabu maana yake ni chanzo (mwanzo_cha kila kitu kile- kikiwa maneno au kitendo, basi hii Suratul-Fatiha ndiyo dibaji na ndio utangulizi wa Qurani. Wakati wa kuteremka kwake. Imeteremka sura hii mwanzo wa kuja Utume. Na hii ndio sura ya awali kuteremka kamili. Kabla yake ziliteremka Aya tu zilizomo katika sura ya Iqraa na Suratul-Muddathiri na Suratul-Muzzammil.

Ufafanuzi

SHARTI ZA KUFIKIA MJA KATIKA UKAMILIFU NO.3

SHARTI ZA KUFIKIA MJA KATIKA UKAMILIFU NO.3 SHARTI ZA KUFIKIA MJA KATIKA UKAMILIFU NO.3 Tukiendelea na mada yetu inayohusiana na masharti na vizuizi vinavyompelekea mwanaadamu asiweze kufikia katika ukamilifu, katika makala hii tutaelezea masharti sharti jengine linalomfanya mwanaadamu asifikie katika ukamilifu. Sharti hilo ni:- Kunufaika na muongozo wa Mitume na Maimamu (a.s). Ili tumfahamu Mwenyeezi Mungu zaidi ni lazima tujiepushe na yale aliyotukataza, ili tunufaike na uongofu na uwalii wa Mitume na Maimamu (a.s), kwa sababu Mtume Muhammad (s.a.w.w) ndio kiumbe bora aliye karibu na Mwenyeezi Mungu, na ni m-bora zaidi kuliko hata Malaika.

Ufafanuzi

SHARTI ZA KUFIKIA MJA KATIKA UKAMILIFU NO.2

SHARTI ZA KUFIKIA MJA KATIKA UKAMILIFU NO.2 SHARTI ZA KUFIKIA MJA KATIKA UKAMILIFU NO.2 Tukiendelea na mada yetu inayohusiana na masharti na vizuizi vinavyompelekea mwanaadamu asiweze kufikia katika ukamilifu, katika makala hii tutaelezea masharti sharti jengine linalomfanya mwanaadamu asifikie katika ukamilifu. Sharti hilo ni:- 3) Chuki na kukalidi matendo ya wengine. Sharti ya tatu miongoni mwa masharti yanayomfanya mwanaadamu amfahamu Mola wake ni kujiepusha na chuki, kukalidi au kuiga matendo ya wengine bila ya kuwa na dalili au elimu nayo. Kutafuta na kujua uhakika wa mambo, ni siri kubwa inayomfanya mwanaadamu afanikiwe katika maisha yake ya kila siku, na akili na fitra ya wanaadamu ndio nyenzo bora zinazomsaidia mwanaadamu huyo kufikia katika mafanikio,na kwa sababu hiyo basi aya nyingi ndani ya Qur-ani zinawataka wanaadamu wafikiri na wakumbuke. Kiasi ya kwamba ikiwa mwanaadamu atafikiri na kuzingatia kwa makini anaweza kufahamu utukufu mkubwa wa Mwenyeezi Mungu katika uumbaji wake, na ataelewa kuwa madai ya mungu asiyekuwa Mola wa haki hayana uwezo wa kufaya lolote katika dunia hii.

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini