Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

Elimu za Qurani

SHARTI ZA KUFIKIA MJA KATIKA UKAMILIFU

SHARTI ZA KUFIKIA MJA KATIKA UKAMILIFU

SHARTI ZA KUFIKIA MJA KATIKA UKAMILIFU Katika makala iliyopita tulielezea sharti na vizuizi vinavyomfanya mwanaadamu asifikie katika ukamilifu, na hii ni kwa sababu hakuweza kumfahamu Mola wake, katika makala hii tutaendelea kuelezea masharti na vizuizi vinavyomfanya mwanaadamu asiweze kufikia katika ukamilifu. Ijapokuwa kumfahamu Mwenyeezi Mungu ni mahitajio ya nafsi yaliyomo ndani ya nyoyo za wanaadamu, na fitra hiyo inawiana na akili na dalili, lakini kukua kwa fitra hiyo na kudhihirika matumaini ya akili na ya kimoyo mwanaadamu anahitajia mazingira yaliyo salama ili aishi katika mfumo wa maisha ambao utamuongoza yeye kufikia katika njia ya saada. Kwa hiyo jamii ambayo inatawaliwa au iko mikononi mwa hukuma za kitaluti, na hukuma hizo zinawalazimisha raia wake kuwatii na kufuata wanayoyaamrisha, raia hao hawatonufaika na neema za Mwenyeezi Mungu,na hawatoweza kumfahamu Allah (s.w). jamii kama hiyo itakuwa haina suluhu yoyote na raia wake watabadilika na kuwa watu mafasiki.

Ufafanuzi

MSINGI WA QUR_ANI TAKATIFU

MSINGI WA QUR_ANI TAKATIFU MSINGI WA QUR_ANI TAKATIFU Qur-ani ni kitabu kitukufu kilichoteremshwa Na mwenyeezi Mungu ili kuwaongoza watu katika njia njema. Katika kitabu hicho kuna misingi muhimu inayomuwezesha mwanaadamu kutambua hadafu na madhumuni ya kuja katika ulimwengu huu. MSINGI WA KUFAHAMU QUR_ANI. Tunamshukuru Mwenyeezi Mungu aliyesema katika Qur-ani yake kuwa “Imekujieni – kutokana kwa Mwenyeezi Mungu- nuru kubwa na kitabu (kitukufu), kinachobainisha kila linalohitajiwa, na rehema zake na amani zake zimwendee Mtume wake, bwana Muhammadm, mwisho wa Mitume wote, na sala na salamu ziwaendee Ahlulbayt wake. Kabla hatujaelezea msingi wa kufahamu Qur-ani sioni vibaya kuashiria sifa za baadhi ya sura zilizomo ndani ya Qur-ani, na kama muda utaturuhusu basi nitafafanua na kuelezea msingi wa kufahamu Qur-ani, na kama muda hautukuruhusu basi nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kuelezea msingi wa kufahamu Qur-ani katika makala zitakazofuata.

Ufafanuzi

UMUHIMU WA KUVAA HIJABU NO.3

UMUHIMU WA KUVAA HIJABU NO.3 UMUHIMU WA KUVAA HIJABU KATIKA JAMII. NO.3 Katika makala zilizopita tulielezea umuhimu wa kuvaa hijabu katika jamii, na tukaashiria baadhi ya masuala ambayo yanahusiana na umuhimu wa kuvaa hijabu, tunamshukuru Mola kwa kutupa nguvu za kuweza kuyajibu masula hayo, katika makala hii tutaendelea na mada yetu hiyo hiyo, tunategemea mtafaidika na tutakayoyaeleza yanayohusiana na umuhimu wa kuvaa hijabu. Miongoni mwa dalili nyengine zinazopelekea wanawake kuvaa hijabu ni kama hizi zifuatazo:- AMA DALILI YA PILI NI KUHIFADHI HESHIMA NA THAMANI.  Ikiwa katika jamii uongo utakithiri, na watu wasema kweli wakasema “watu wote hao wenye kusema uongo, usemaji kweli wetu sisi una faida gani?” kisha na wao vile vile wakajiunga na kundi la wasema uongo, na kwa kutokana na kuzidi kwa hiyana katika jamii watu wenye amana nao wakajiunga na kundi la wenye hiyana, na kwa kutokana na watu wengi wasiochunga suala la mavazi, wenye kulithamini suala hilo vile vile wakajiunga na wasiolithamini suala hilo, kama mambo yatakuwa hivyo basi katika jamii mambo yote yenye thamani yatapotea, na kizazi kitakachokuja baadae masuala yenye thamani kubwa katika jamii ambayo tumeyataja hapo nyuma kama vile(amana, ukweli, huruma) yatakuwa ni mageni kwao, na wala hawatoyatambuwa maana yake.

Ufafanuzi

UMUHIMU WA KUVAA HIJABU NO.2

UMUHIMU WA KUVAA HIJABU NO.2 UMUHIMU WA KUVAA HIJABU KATIKA JAMII. NO.2 Katika makala zilizopita tulielezea umuhimu wa kuvaa hijabu katika jamii, na tukaashiria baadhi ya masuala ambayo yanahusiana na umuhimu wa kuvaa hijabu, tunamshukuru Mola kwa kutupa nguvu za kuweza kuyajibu masula hayo, katika makala hii tutaendelea na mada yetu hiyo hiyo, tunategemea mtafaidika na tutakayoyaeleza yanayohusiana na umuhimu wa kuvaa hijabu. Miongoni mwa masuala yaliyoulizwa ni haya yafuatayo:- MIMI SINA MALENGO YA KULETA UFISADI WALA UPOTOSHAJI. Katika barua yako umeniandikia hivi: “Ingawaje mimi navaa nguo zinazokwenda na wakati mbele za wanaume, na nnajipamba lakini katu sina lengo la kuleta ufisadi au upotoshaji.

Ufafanuzi

UMUHIMU WA HIJABU KWA MWANAMKE

UMUHIMU WA HIJABU KWA MWANAMKE HIJABU NA MWANAMKE ANAPOKUA NYUMBANI KWAKE Uliniandikia kua “ hivi ni kwa nini mwanamke akitaka kusali ni lazima avae hijabu hata kama atakua yupo peke yake ndani ya nyumba”? Dada yangu daima usisahau ya kua Mola wako siku zote huwatakia waja wake kheri na maslahi, na hakuna hata sheria moja ya Mola wako isiyokua na hekima, ima waja waifahamu hekima hiyo au wasiifahamu, hii ni sheria ya Mwenyezi Mungu, vile vile ndani ya sheria hii mna hekima, na miongoni hekima hizo ni hizi zifuatazo:- 1. Mazowezi ya kumpandisha mtu daraja. Sala ina fadhila nyingi, na vile vile ni moja kati ya mazowezi ya kumpandisha mtu daraja, ndani ya sala sisi tuna mambo chungu nzima tunayojizoweza nayo, kama vile kumpwekesha Mola, kumkhofu, pamoja na kusoma Qur’ani, basi sala kitu kimoja kilichokusanya mambo tofauti yenye thamani, na hijabu kwa wanawake ndio hivyo hivyo, kama vile Mola asemavyo na Qur-ani inavyosema, hijabu kwa mwanamke huwa inampa thamani maalum mwanamke, na ni moja kati ya mambo yenayomkamilisha mwanamke huyo. 2. Kutangaza rasmi kumtii na kumcha Mwenyeezi Mungu  Mkuu wa jeshi anawaambia wafuasi wake, “mwanajeshi mzuri na mwenye kujua wadhifa ni lazima siku zote afike uwanjani hali ya kuwa amevaa fomu. Sasa fikiria iwapo mwanajeshi mmoja atataka kuonana na mkuu wa jeshi wakati anapokwenda Idarani kwake, ikisha yeye avae fomu anapokwenda kuonana nae, kufanya kwake hivyo kutakuwa kutamaanisha kwamba yeye amekubali kufuata amri ya mkubwa wake. Kwa hiyo basi, kuhudhuria pahali alipokuwepo mkubwa wako huku ukiwa katika utaratibu kamili alioutaka yeye, kutakuwa kunaelezea utiifu wa mtu huyo hata kama hakuzungumza kwa ulimi wake.

Ufafanuzi

UMUHIMU WA KUVAA HIJABU NO.1

UMUHIMU WA KUVAA HIJABU NO.1 UMUHIMU WA KUVAA HIJABU KATIKA JAMII. NO.1 Katika makala zilizopita tulielezea umuhimu wa kuvaa hijabu katika jamii, na tukaashiria baadhi ya masuala ambayo yanahusiana na umuhimu wa kuvaa hijabu, tunamshukuru Mola kwa kutupa nguvu za kuweza kuyajibu masula hayo, katika makala hii tutaendelea na mada yetu hiyo hiyo, tunategemea mtafaidika na tutakayoyaeleza yanayohusiana na umuhimu wa kuvaa hijabu. Miongoni mwa masuala yaliyoulizwa ni haya yafuatayo:- KWA NINI HAMUWAAMBII WANAUME WASIWAANGALIE WANAWAKE? KWANI JAMBO HILO LITAWAFANYA WANAWAKE WASIVAE HIJABU Naelewa kwamba kwa kutokana na hatua nilizozielezea hadi kufikia hapa utakuwa huna haja ya kuuliza suala kama hili, kwa sababu wewe mwenyewe umeshaona kwamba sio kwamba wanaume tuwameambiwa wasiwaangalie wanawake tu, bali kuna msisitizo mkubwa zaidi ya huo, kwani wao ndio wa mwanzo kukatazwa kabla ya wanawake kuamrishwa kuvaa hijabu, kama ilivyo katika Suratun-Nuur, pale Mola alipowataka wanawake kuvaa hijabu, kwanza aliwaanza wanaume kuwaambia wasiwaangalie wanawake, na amemwambia Mtume (s.a.w.w) akisema “waambie waumini wa kiume wainamishe macho yao.

Ufafanuzi

TAWHIYD NA NIDHAMU YA DUNIA

TAWHIYD NA NIDHAMU YA DUNIA TAWHIYD NA NIDHAMU YA DUNIA Katika zama za kijahilia jamii ya kiarabu ilikuwa haina itikadi ya kumuamini Mola mmoja, bali kila kabila lilikuwa likiamini na kuabudu sanamu maalumu, na kutokana na sababu hiyo basi kulikuwa hakuna umoja wa mawafikiano yoyote katika jamii ya kiarabu, kila siku kulikuwa kuna vita baina ya kabila na kabila, lakini baada ya kudhuhuru (kuja) uislamu na kupinga kuabudu masanamu hali ilibadilika na waarabu wengi wakaiamini dini ya kiislamu, wakaijenga jamii yao na wote kuwa kitu kimoja, na katika kipindi kidogo tu baada ya kuja uislamu sio jamii ya kiarabu tu iliikubali dini ya kiilamu kwa shauku kubwa bali hata jamii mbili kongwe kabisa kihistoria yaani Irani na Rumu waliipokea na wakaukubali uislamu kwa mikono miwili. Kwa upande mwengine sio kwa sababu tu makafiri walilinganiwa kuamini Mola mmoja na kuokoka na shirki ya kuamini miungu tofauti, bali kutokana na kuwa dini zote za mbinguni ambazo ni Masihi, Yahudi na Islamu dini zote hizo ni za Mwenyeezi Mungu, na dini zote hizo zinawalingania wanaadamu kuamini Mola mmoja tu, basi tutaona kwamba ijapokuwa katika dini kunahitilafiana katika mambo mbali mbali ama vile vile kuna ushirikiano wa mambo katika tawhid, yaani waislamu, wakiristo, na mayahudi wote wana itikadi ya kuamini Mola mmoja.

Ufafanuzi

TOFAUTI YA WANAADAMU

TOFAUTI YA WANAADAMU TOFAUTI YA WANAADAMU Katika makala iliyopita tulielezea kuhusu hekima za Mwenyeezi Mungu, na tukathibitisha hekima hizo kutokana na alama tunazozishuhudia katika ulimwengu huu mtukufu, katika makala hii tutaelezea alama nyengine zinazoonesha na kuthibitisha hekima za Mwenyeenzi Mungu ni uumbaji wa wanaadamu katika hali tofauti, kama inavyosema Qur-ani:- Yeye ndiye anaye kuundeni ndani ya matumbo ya wazazi kwa namna apendayo. Hapana mungu ila Yeye, Mwenye nguvu na Mwenye hikima. Ushahidi mwengine unaoonesha rehema za Mwenyeenzi Mungu ni kuzaliwa kwa mamilioni ya wanaadamu katika maumbile tofauti, kabila, lugha,lahaja, n.k yote hayo yanaonesha tofauti iliyopo miongoni mwa wanaadamu.

Ufafanuzi

UKAMILIFU WA MWANAADAMU

UKAMILIFU WA MWANAADAMU

Ufafanuzi

ISTILAHA CHACHE KUHUSIANA NA QUR_ANI

ISTILAHA CHACHE KUHUSIANA NA QUR_ANI

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini