Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

Wanavyuoni wa Kiislamu

SHEIKH SHALTUT

SHEIKH SHALTUT

SHEIKH SHALTUT Sheikh Shaltut: "Madhehebu ya J'afariya maarufu kwa jina la madhehebu ya Shia Ithnaashariya, ni madhehebu ambayo kisheria inajuzu kufuatwa kama zilivyo madhehebu za Kisuni. Kwa msingi huo, ni vyema kwa Waislamu kuelewa ukweli huo na kujiepusha na taasubi (chuki za kimadhehebu) zisizofaa dhidi ya madhehebu makhsusi; kwani dini ya Mwenyezi Mungu na sheria yake haifuati madhehebu wala haiwezi kuhodhiwa na madhehebu makhsusi. Watu wa madhehebu mbalimbali ya Kiislamu wanafanya ijtihadi na kazi yao hiyo itatakabaliwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu." Sheikh Mahmoud Shaltut alizaliwa tarehe 5 Shawwal mwaka 1310 (Aprili 23, 1893) katika kijiji cha Minyat Bani Mansur katika mkoa wa Buhayrah nchini Misri katika familia ya wanazuoni. Baba yake Sheikh Muhammad alimpa jina la Mahmoud na akafanya jitihada kubwa za kumlea na kumuelemisha mwanae.

Ufafanuzi

UZAYUNI KWA MTAZAMO WA IMAMU KHOMEINI

UZAYUNI KWA MTAZAMO WA IMAMU KHOMEINI UZAYUNI KWA MTAZAMO WA IMAMU KHOMEINI Iwapo tutalitambua suala la kuasisi serikali ya Kiislamu nchini Iran kuwa lilipewa kipaumbele cha kwanza katika fikra za kisiasa za Imam Ruhullah Khomeini, basi hapana shaka kwamba suala la kukomboa Quds tukufu na ardhi za Palestina kwa ujumla kutoka kwenye mikono ya Wazayuni wa Israel lilipewa umuhimu mkubwa katika fikra na kazi za kisiasa za shakhsia huyo nje ya Iran. Moja kati ya hitilafu za kimsingi za Imam Khomeini na utawala wa Kipahlavi wa Shah ilikuwa ni ushawishi wa Wazayuni ndani ya Iran na kuwepo Waisraeli katika nafasi za serikali ya wakati huo ya Shah. Kwa maneno mengine ni kuwa, tunaweza kusema kuwa suala la kukomboa taifa la Iran na taifa la Palestina lilikuwa jambo la dharura na lenye kipaumbele cha kwanza katika fikra za kimapinduzi za Imam Khomeini, jambo ambalo linadhihiri wazi zaidi katika maandiko, hotuba na mapambano yake ya kisiasa. Makala hii fupi inaashiria nukta kadhaa kuhusu maudhui hiyo.

Ufafanuzi

HIJA MBELE YA IMAMA KHOMEINY

HIJA MBELE YA IMAMA KHOMEINY HIJA MBELE YA IMAMA KHOMEINY Ibada ya hija, ni moja ya masuala ya kiibada na kisiasa ambayo yamefaradhihwa katika dini tukufu ya Kiislamu. Ibada hii muhimu hutekelezwa kila mwaka katika ardhi tukufu ya wahyi, na mamilioni ya watu walio na hamu kubwa, kutoka kila pembe ya dunia, watu ambao kwa hakika huwa ni wa mataifa, jamii, rangi na lugha mbalimbali. UMUHIMU WA HIJA NA ATHARI ZAKE Ibada ya hija, ni moja ya masuala ya kiibada na kisiasa ambayo yamefaradhihwa katika dini tukufu ya Kiislamu. Ibada hii muhimu hutekelezwa kila mwaka katika ardhi tukufu ya wahyi, na mamilioni ya watu walio na hamu kubwa, kutoka kila pembe ya dunia, watu ambao kwa hakika huwa ni wa mataifa, jamii, rangi na lugha mbalimbali. Kuna ibada chache kati ya faridha nyingi za Kiislamu iliyopewa uzito na kusisitiziwa Waislamu kama ilivyo hija. Sisitizo la kitabu kitakatifu cha Qur'ani pamoja na nasaha zilizotolewa na viongozi watukufu wa kidini ni nyingi mno na zisizoweza kubainishwa kwa maneno. Abdallah bin Sinaan.

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini