Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

Imam Jawad (a.s)

TAALUMA NA MAFUNZO YA AMALI

TAALUMA NA MAFUNZO YA AMALI

TAALUMA NA MAFUNZO YA AMALI Tuko katika siku za mwisho za mwezi wa Dhul Qaada, ambazo ni siku za kuuawa shahidi mmoja wa Watu wa Nyumba ya Mtume Muhammad (saw). Katika siku kama hizi mwaka 220 Hijiria, Imam Jawad (as), kiongozi mkubwa na mtukufu wa Kiislamu, aliaga dunia na hivyo kuuachia ulimwengu wa Kiislamu huzuni kubwa. Watu wa Nyumba ya Mtume katika utekelezaji wa majukumu yao makubwa waliyopewa na Mwenyezi Mungu, walikuwa waanzilishi wa matukio makubwa ya kifikra, kiutamaduni na kijamii katika ulimwengu wa Kiislamu. Iwapo tutatalii vyema historia na maisha ya Ahlul Beit (as), tunaona kuwa walikuwa na nafasi muhimu katika kulinda misingi na nguzo za dini. Walisimama na kupambana vikali na madhihirisho ya dhulma, upotovu na ufisadi na kufanya jitihada kubwa za kulinda misingi ya Uislamu halisi ili dini hii tukufu idumu milele. Imam Jawad (as) ni miongoni mwa Watu wa Nyumba ya Mtume (saw) ambaye katika kipindi cha miaka 17 ya uimamu wake, daima alikuwa akifanya jitihada za kueneza Uislamu na kuimarisha mafundisho yake tajiri ulimwenguni. Huku tukitoa mkono wa pole kwa Waislamu wote wapenda haki kwa mnasaba wa kuwadia siku ya kukumbuka kuuawa shahidi Imam Jawad (as), tunazungumzia hapa angaa kwa ufupi, maisha ya mtukufu huyo.

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini