Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

Imam Sajjaad (a.s)

DUA YA IMAM ZAYNUL ABIDIN

DUA YA IMAM ZAYNUL ABIDIN

BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM DUA YA IMAM ZAYNUL ABIDIN (a.s.) KATIKA KUOMBA TAWBA Ewe Mola wangu, ambaye sifa za kukusifu za wenye kukusifu haziwezi kutajika. Ewe mwenye mategemeo ambaye mategemeo hayawezi kwenda zaidi yako.Ewe ambaye kwako wewe malipo ya waja wako hayatapotea. Ewe unayeogopwa na waja wako. Ewe uliye khofu ya mja wako na hii ndiyo nafasi imemkuba ghafla kwa madhambi. Ambaye amevutwa na zama za makosa na ambayo yameghalibiwa na sheitani. Kwa hivyo ameshindwa kabisa kutimiza yale uliyokuwa umemwamrisha kuyafanya na yeye hakuyafanya. Yeye amegang'ania tu katika yale uliyokuwa umeyaharamisha na kuyakataza kama kwamba haelewi uwezo ulionao juu yake. Au kama yule anayekanusha ukarimu wako mtukufu kwake yeye hadi macho ya hidaya kufunguliwa kwa ajili yake na mawingu (kiza) cha upofu (wa hidaya) ulipoondolewa kutoka kwake, na alipotambua kwa ukamilifu vile alivyojidhulumu nafsi yake na kuyazingatia kuwa amemwasi Muumba wake.

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini