Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

Kusoma Qurani

SIFA TUKUFU ZA MITUME NO.3

SIFA TUKUFU ZA MITUME NO.3

SIFA TUKUFU ZA MITUME (A.S) NO 3. Katika makala iliyopita tulielezea kuhusu sifa tukufu za Mitume (s.a), na tukaelezea miongoni mwa sifa hizo kuwa ni elimu, katika makala hii tutaendelea kuelezea sifa nyengine ambazo wanatakiwa Mitume (a.s) kuwa nazo. Sifa ya tatu ni kuweza kuleta miujiza. 3. Muujiza. Muujiza yaani ni kufanya matendo ambayo wengine hawana uwezo wa kuyafanya, na tukifikiria kiakili tutagundua kuwa kuna umuhimu wa kuwepo muujiza, kwa sababu kuwepo muujiza kunaleta mafanikio kwa watu wote duniani. Miujiza ya Mitume ni dalili tosha iliyowazi inayothibitisha madai yao, kuwa Mitume hiyo imeteremshwa kwa idhini ya Mola wao.

Ufafanuzi

SIFA TUKUFU ZA MITUME NO.2

SIFA TUKUFU ZA MITUME NO.2 SIFA TUKUFU ZA MITUME (A.S) NO 2. Katika makala iliyopita tulielezea kuhusu sifa tukufu za Mitume (s.a), na tukaelezea miongoni mwa sifa hizo kuwa ni elimu, katika makala hii tutaendelea kuelezea sifa nyengine ambazo wanatakiwa Mitume (a.s) kuwa nazo. Sifa ya pili ni kuwa Maasumu. 2. Ismat (maasumu). Ismat au (maasumu) ni kujiepusha na kufanya madhambi au kumuasi Mwenyeezi Mungu, kifikra kimoyo, au kimatendo, sifa hii ni miongoni mwa sifa muhimu wanazotakiwa Mitume kuwa nazo,ili wafikie kupewa cheo cha Utume, kwa sababu kuwa maasumu ni dalili muhimu inayowapelekea watu kuwaamini na kuwa na matumaini na Mitume hiyo. Kila mwanaadamu anayemcha Mola wake akamtii na kufuata maamrisho yake anaweza akajaaliwa kupata sifa hiyo tukufu ya kuwa maasumu, na Mwenyeezi Mungu Mtukufu huwajaalia Mawalii wake kuwa na sifa hiyo, kwa sababu Yeye ni Latifu, basi huwaongoza waja wake na kuwaepusha na hatari ya kumuasi Mola wao au kufanya madhambi.

Ufafanuzi

SIFA TUKUFU ZA MITUME NO.1

SIFA TUKUFU ZA MITUME NO.1 SIFA TUKUFU ZA MITUME (A.S) NO 1. *Ni sifa gani muhimu wanazotakiwa Mitume kuwa nazo ili waweze kupewa Wahyi na ujumbe kutoka kwa Mwenyeezi Mungu kwa ajili ya kuwaongoza wanaadamu? SIFA TUKUFU ZA MITUME Mitume Mitukufu ya Mwenyeezi Mungu imetumwa ili kuwaongoza wanaadamu katika njia ya Mwenyeezi Mungu, Allah (s.w) amewachagua  viongozi hao kuwa ni watu bora katika jamii . Kwa hiyo watukufu hao ni lazima wawe na sifa njema tukufu zitakazowavutia watu na kuwatia matumaini ya kuwa mitume hiyo ina uwezo wa kuwaongoza waja hao katika njia njema,miongoni mwa sifa hizo ni kama hizi zifuatazo:- Kuwa na elimu ya  juu kabisa, kuja na miujiza, na kuwa na isma au (maasumu) – isma yaani kutokuwa na madhambi na kujiepusha na kumuasi Mwenyeezi Mungu Mtukufu -

Ufafanuzi

MAFANIKIO YA MITUME NO 5

MAFANIKIO YA MITUME NO 5 MAFANIKIO YA MITUME *Ni dalili gani zilizowasaidia Mitume kuweza kufikisha ujumbe wao kwa wanaadamu? MAFANIKIO YA MITUME YA MWENYEEZI MUNGU NO.4 Katika makala iliyopita, (makala namba tatu) tulielezea sababu na dalili zilizopelekea Mitume kupata mafanikio katika kufikisha ujumbe wao kwa wanaadamu, katika maelezo ya makala hiyo tulielezea dalili mbili, katika makala hii tutaelezea sababu nyengine zilizosababisha kuwaletea Mitume mafanikio katika malinganio yao. 5. KUTOISHI MAISHA YA KIFAHARI, NA KUWA MBALI NA ANASA ZA DUNIA. Mitume ya Mwenyeezi Mungu iliishi maisha yasiyokuwa ya kifahari, na hii ni alama moja wapo iliyowafanya wasadikike (waaminiwe), na ukweli wao ulidhihirika pale walipojiweka mbali na anasa za dunia, na kufikiria maisha yao ya Akhera, na hii ni moja miongoni mwa siri za mafanikio yao, zilizowafanya watu wawaamini na kuwatii.

Ufafanuzi

MAFANIKIO YA MITUME NO 4

MAFANIKIO YA MITUME NO 4 *Ni dalili gani zilizowasaidia Mitume kuweza kufikisha ujumbe wao kwa wanaadamu? MAFANIKIO YA MITUME YA MWENYEEZI MUNGU NO.4 Katika makala iliyopita tulielezea kwa ufupi kuhusu mafanikio ya Mitume, katika makala hii tutaendelea na mada yetu hiyo hiyo, ama kwa kubainisha kwa kina sababu zilizopelekea Mitume kufanikiwa katika kufikisha ujumbe wao na malinganio yao ya kuwataka wanaadamu wamuabudu Mola mmoja tu. miongoni mwa sababu hizo zilizopelekea mafanikio katika kufikisha ujumbe ujumbe wao ni hizi zifuatazo:- 5. KUTOISHI MAISHA YA KIFAHARI, NA KUWA MBALI NA ANASA ZA DUNIA. Mitume ya Mwenyeezi Mungu iliishi maisha yasiyokuwa ya kifahari, na hii ni alama moja wapo iliyowafanya wasadikike (waaminiwe), na ukweli wao ulidhihirika pale walipojiweka mbali na anasa za dunia, na kufikiria maisha yao ya Akhera, na hii ni moja miongoni mwa siri za mafanikio yao, zilizowafanya watu wawaamini na kuwatii.

Ufafanuzi

AINA ZA DINI NO.2

AINA ZA DINI NO.2 AINA ZA DINI NO 2 Katika makala iliyopita, (makala namba moja) tulielezea aina mbili za dini, na tukaelezea natija zinazopatikana kuhusiana na maelezo tuliyoyaelezea katika makala hiyo, katika makala hii tutendelea kwa kuelezea natija nyengine zinazohusiana na dini. miongoni mwa natija hizo ni hizi zifuatazo:- A: Kuletwa taaluma na hukumu za Mwenyeezi Mungu kupitia lugha na tamaduni maalumu – lugha ya kiarabu – haina maana ya kuwa dini ya kweli na dini ya haki ilikuwa ni dini ya kiarabu inayofafanuliwa au kuelezewa kupitia mtindo wa tamaduni maalumu. Bali dini na mapendeleo aliyonayo mwanaadamu ndani ya nafsi yake.mapendeleo ambayo yanaendana na matakwa ya dini ya Mwenyeezi Mungu.

Ufafanuzi

AINA ZA DINI NO. 1

AINA ZA DINI NO. 1 AINA ZA DINI Dini zimegawika katika sehemu mbili:- 1.Dini zinazotokana na kizazi cha Nabii Ibrahimu (a.s), dini hizo ndizo dini za Allah (s.w). 2. Dini zinazotokana na tamaduni maalumu za watu, dini hizo sio dini sahihi. Dini ya Wahyi ni dini ya Nabii Ibrahimu (a.s) na ndio dini iliyoletwa kutoka kwa Mwenyeezi Mungu Mtukufu. ni bayana maalumu inayowafunga watu wote katika mfumo mmoja, na katika mwenendo maalumu, na inawalazimu wao kuitii dini hiyo. Wahyi wa dini ni wenye kukubalika na kufahamika katika tamaduni zote, hii ni kwa sababu wahyi huo unawiana na kuwendana na matakwa ya dini, matakwa ya dini ni matakwa ya wanaadamu wote, ikiwa dini inakubalika na kufahamika na wanaadamu wote, na ikiwa dini ina uwezo wa kufuta, na kuondoa mambo yanayoleta madhara na yasiyo na faida yoyote katika maisha ya mwanaadamu, au inaweza kuweka na kuwaletea wanaadamu maadili mema yaliyo na faida katika maisha yao, na yanayowaletea saada ya duniani na Akhera, hii ni kwa sababu lugha ya dini ni lugha iliyomo ndani ya nafsi za wanaadamu wote , na ni lugha inayofahamika na kila mmoja wetu, na ni lugha inayowaletea wanaadamu athari nzuri katika maisha yao.

Ufafanuzi

DINI KATIKA MTAZAMO WA QUR_ANI

DINI KATIKA MTAZAMO WA QUR_ANI DINI KATIKA MTAZAMO WA QUR_ANI Ni sahihi kuwa neno “Dini” kwa mtazamo wa wanalugha ni neno lililozoeleka, na kila mmoja analifahamu neno hilo, lakini maana hasa ya dini si ile maana ambayo kila mmoja wetu amezoea kuisikia. Dini katika mtazamo wa kitaalamu (kiistilaha) lina maana pana zaidi. Dini sio neno kuu lililokusanya ndani yake aina au maana zote za dini kiasi ya kwamba wakati lisilikapo liwe linamaanisha aina yoyote ile ya dini, ufafanuzi wa dini unaokubalika unatakiwa uwe umepatikana katika dini yenyewe, yaani katika vitabu vya dini. Kwa hiyo maana asili ya neno hilo inayokusudiwa hapa, ni dini ya Kiisalamu. Ndio, neno hilo lina maana maalumu, na linatumika katika dini ya Kiislamu tu.

Ufafanuzi

MAFANIKIO YA MITUME NO.3

MAFANIKIO YA MITUME NO.3 MAFANIKIO YA MITUME *Ni dalili gani zilizowasaidia Mitume kuweza kufikisha ujumbe wao kwa wanaadamu? MAFANIKIO YA MITUME YA MWENYEEZI MUNGU NO.3 Katika makala iliyopita, (makala namba mbili) tulielezea sababu na dalili zilizopelekea Mitume kupata mafanikio katika kufikisha ujumbe wao kwa wanaadamu, katika maelezo ya makala hiyo tulielezea dalili mbili, katika makala hii tutaelezea sababu nyengine zilizosababisha kuwaletea Mitume mafanikio katika malinganio yao. 3. IKHLASI Miongoni mwa mawaidha ya Mitume na chanzo cha mafanikio yao ni ikhlasi, kila walilofanya Mitume ni kwa ajili ya ridhaa ya Mola wao, kama inavyosema Qur-ani:- قُلْ إِنَّمَا اَعِظُكُم بِوَاحِدَةٍ اَن تَقُومُوا لِلَّهِ مَثْنَي وَفُرَادَي ثُمَّ تَتَفَكَّرُوا مَا بِصَاحِبِكُم مِّن جِنَّةٍ إِنْ هُوَ إِلاَّ نَذِيرٌ لَّكُم بَيْنَ يَدَيْ عَذَابٍ شَدِيدٍ[1] Sema: Mimi nakunasihini kwa jambo moja tu - ya kwamba msimame kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wawili-wawili na mmoja-mmoja; kisha mfikiri. Mwenzenu huyu hana wazimu. Yeye si chochote ila ni Mwonyaji kwenu kabla ya kufika adhabu kali.

Ufafanuzi

MAFANIKIO YA MITUME NO.2

MAFANIKIO YA MITUME NO.2 MAFANIKIO YA MITUME *Ni dalili gani zilizowasaidia Mitume kuweza kufikisha ujumbe wao kwa wanaadamu? MAFANIKIO YA MITUME YA MWENYEEZI MUNGU NO.2 Katika makala iliyopita tulielezea kwa ufupi kuhusu mafanikio ya Mitume, katika makala hii tutaendelea na mada yetu hiyo hiyo, ama kwa kubainisha kwa kina sababu zilizopelekea Mitume kufanikiwa katika kufikisha ujumbe wao na malinganio yao ya kuwataka wanaadamu wamuabudu Mola mmoja tu. miongoni mwa sababu hizo zilizopelekea mafanikio katika kufikisha ujumbe ujumbe wao ni hizi zifuatazo:- 1. UKWELI NA UAMINIFU kweli na uaminifu ni dalili muhimu zinazowafanya watu waamini na wawe na uhakika ya kile wanachobashiriwa, kama tunavyoona ukweli na uaminifu wa Nabii Yussuf ulimfanya yeye apewe cheo cha kuwa waziri katika kasri nchini Misri, na akawa waziri wa Mfalme wa nchi ya Misri

Ufafanuzi

MAFANIKIO YA MITUME NO 1

MAFANIKIO YA MITUME NO 1 MAFANIKIO YA MITUME *Ni dalili gani zilizowasaidia Mitume kuweza kufikisha ujumbe wao kwa wanaadamu? MAFANIKIO YA MITUME YA MWENYEEZI MUNGU NO.1 Mwenyeezi Mungu Mtukufu katika Qur-ani anasema hivi kuhusu Mitume:- اُوْلَـئِكَ الَّذِينَ هَدَي اللّهُ فَبِهُدَاهُمُ اقْتَدِهْ قُل لاَّ اَسْاَلُكُمْ عَلَيْهِ اَجْراً إِنْ هُوَ إِلاَّ ذِكْرَي لِلْعَالَمِينَ[1] Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amewahidi. Basi fuata hidaya yao. Sema: Mimi sikuombeni ujira. Haya hayakuwa ila ni mawaidha kwa walimwengu wote. Kwa hiyo kama tukifuata njia waliotuonesha Mitume, hapana shaka tutaongoka, basi ili kufuata njia hizo, ni lazima tuelewe siri ya mafanikio ya Mitume hiyo. Ama ni lazima tuzingatie kuwa tunaposema mafanikio ya Mitume haina maana kuwa watu wote wameongoka na kufuata njia ya Mitume, kwa sababu Mwenyeezi Mungu anasema:- لَّسْتَ عَلَيْهِم بِمُصَيْطِرٍ[2] Wewe si mwenye kuwatawalia.

Ufafanuzi

MAFANIKIO YA MITUME NO 6

MAFANIKIO YA MITUME NO 6 MAFANIKIO YA MITUME *Ni dalili gani zilizowasaidia Mitume kuweza kufikisha ujumbe wao kwa wanaadamu? MAFANIKIO YA MITUME YA MWENYEEZI MUNGU NO.6 Katika makala iliyopita, (makala namba tano) tulielezea sababu na dalili zilizopelekea Mitume kupata mafanikio katika kufikisha ujumbe wao kwa wanaadamu,  katika makala hii tutaelezea sababu nyengine zilizosababisha kuwaletea Mitume mafanikio katika malinganio yao.

Ufafanuzi

MAUMBILE YA DINI

MAUMBILE YA DINI Dini imegawika katika maumbile mawili yafuatayo: - Umbile la dhahiri (umbile la nje): Umbile hilo linamsaidia mwanaadamu katika kuifahamu na kunufaika na misingi ya dini kijumla jamala. - Umbile la batini (umbile la ndani). Umbile hilo linamsaidia mwanaadamu katika kufahamu na kunufaika na mambo mbali mbali yaliyomo ndani ya dini, zikiwemo hukumu za mbalimbali katika mambo ya jamii, siasa, uchumi,n.k. Hukumu hizo humletea mwanaadamu athari nyingi nzuri katika maisha yake, kwa hiyo mwanaadamu anapaswa kuwa na elimu ya dini ya kutosha na mwenye kufanya jitihada ili kutambua umuhimu wa falsafa ya dini.

Ufafanuzi

NADHARIA KUHUSIANA NA DINI NO.3

NADHARIA KUHUSIANA NA DINI NO.3 NADHARIA KUHUSIANA NA DINI NO.3 Katika makala iliyopita, (makala namba mbili) tulielezea baadhi ya majibu yanayohusiana na nadharia iliyotolewa kuhusiana na ufafanuzi wa dini, katika makala hii tutaendelea kuijibu nadharia hiyo. Tano: Kuna uhakika gani ndani ya hatima na malengo hayo ya mwisho, hatima ambayo inaweza kumfanya Mwenyeezi Mungu asiwe na nafasi yoyote katika hatima hiyo, na kinyume chake, hatima hiyo iwe inaendana sambamba na washirikina au wale wasio na itikadi ya kumuamini Mwenyeezi Mungu?

Ufafanuzi

NADHARIA KUHUSIANA NA DINI NO.2

NADHARIA KUHUSIANA NA DINI NO.2 NADHARIA KUHUSIANA NA DINI NO.2 Katika makala iliyopita, (makala namba moja) tulielezea nadharia iliyotolewa kuhusu ufafanuzi wa dini, tukajibu nadharia hiyo katika vipengele viwili, katika makala hii tutaendelea kuijibu nadharia hiyo. Tatu: Watu waliotoa nadharia hiyo wana dalili gani inayothibitisha kuwa, kuzingatia na kuwa na fungamano na hatima ya malengo muhimu ya mwisho ni imani? Hivi kweli tukirudia katika historia ya mwanaadamu anaweza kupatikana mtu ambaye hata kwa dakika moja hakuwa na mazingatio? Sasa vipi tunaweza kusema kuwa mazingatio hayo ni imani? Hali ya kwamba watu wote hata wale wasio na itikadi na Mwenyeezi Mungu, au washirikina wote walikuwa na sifa hiyo ya kuwa na mazingatio ya mambo tofauti, natushuhudie Aya hii ifuatayo,

Ufafanuzi

NADHARIA KUHUSIANA NA DINI NO.1

NADHARIA KUHUSIANA NA DINI NO.1 NADHARIA KUHUSIANA NA DINI NO.1 Kuna nadharia tofauti zilizotolewa na watu mbali mbali kuhusiana na ufafanuzi wa dini, kila kundi au watu limeifafanua dini kutokana na mtazamo wake binafsi au itikadi aliyonayo, katika makala hii tutaelezea nadharia tofauti zilizotolewa na baadhi ya watu kuhusiana na dini, miongoni mwa nadharia hizo ni hizi zifuatazo:- Baadhi yao wamesema kuwa; “ Dini sio itikadi wala amali au matendo maalumu, na haiwezekani kuiweka imani na suna za dini kuwa kitu kimoja, (mwanaadamu wakati anapokuwa na dini huzingatia mambo yanayohusiana na hatima na malengo ya mwisho, mambo hayo yanaweza kuwa ni siku ya mwisho, Mwenyeezi Mungu, au mambo mengine yoyote yale), na anapozingatia hatima na malengo ya mwisho, humfanya yeye awe na hisia ya kuwa na uhakika wa mambo hayo, kuwa na hisia ya uhakika wa mambo ina maana ya kuwa; mwanaadamu huona thamani ya vitu na mambo mbalimbali, huona nguvu na uwezo wa Mola wake, basi hapo hutafuta taadhima na heshima ya Mola wake. Hii humfanya yeye adiriki ulazima wa kuwa na tabia njema, na hii ni hatua ya mwanzo inayomfanya mwanaadamu afanye jitihada zake zote kwa ajili ya kufikia katika uhakika wa hatima ya mambo.

Ufafanuzi

NJIA ZA UFUMBUZI WA DINI NO.2

NJIA ZA UFUMBUZI WA DINI NO.2 NJIA ZA UFUMBUZI WA DINI NO 2 Katika makala iliyopita tulielezea njia mbili zinazoweza kumuongoza mwanaadamu katika uhakiki wake wa dini, katika makala hii tutajibu ile kauli isemayo kuwa; dini imeteremshwa kulingana na tamaduni za watu, hivi kweli kauli hiyo ni sahihi? kwa hakika kauli hiyo sio sahihi kwa mujibu wa maelezo haya yafuatayo. Dini imekuja kurekebisha na kusawazisha tamaduni potofu na kuwaongoza watu katika maadili yaliyo mema. katika sehemu hii natuangalie baadhi ya mambo mabaya yaliyokuwa yakifanywa na baadhi ya watu, vikundi au makabila, mambo ambayo yamesawazishwa na kutengenezwa kupitia dini takatifu ya Allah (s.w).

Ufafanuzi

NJIA ZA UFUMBUZI WA DINI NO.1

NJIA ZA UFUMBUZI WA DINI NO.1 NJIA ZA UFUMBUZI WA DINI NO. 1 Tunaweza kuufafanua ufumbuzi wa dini katika njia mbili zifuatazo:- 1. kwa kuifanyia uhakiki nafsi ya mwanaadamu mwenyewe. 2. Katika ulimwengu wa MIYTHAAQ (میثاق). Ulimwengu wa Miythaaq unarejea katika kile kipindi ambacho Mwenyeezi Mungu alimuumba mwanaadamu. Pale Allah (s.w) alipowauliza waja wake,  وَإِذْ اَخَذَ رَبُّكَ مِن بَنِى آدَمَ مِن ظُهُورِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَاَشْهَدَهُمْ عَلـٰي اَنفُسِهِمْ اَلَسْتَ بِرَبِّكُمْ قَالُواْ بَلَي شَهِدْنَا اَن تَقُولُواْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّا كُنَّا عَنْ هَذَا غَافِلِينَ[1] Na pale Mola wako Mlezi alipo waleta katika wanaadamu kutoka migongoni mwao kizazi chao, na akawashuhudisha juu ya nafsi zao, akawaambia: Je, Mimi si Mola Mlezi wenu? Wakasema: Kwani! Tumeshuhudia. Msije mkasema Siku ya Kiyama sisi tulikuwa tumeghafilika na hayo. kwa ufafanuzi zaidi juu ya mada hii na aya hii ungana nami mpaka tamati mwa makala hii.

Ufafanuzi

UHAKIKI WA DINI NO.5

UHAKIKI WA DINI NO.5 UHAKIKI WA DINI NO.5 UHAKIKI WA DINI KUPITIA MSINGI WA IJTIHADI. Hatua ya kwanza: Umuhimu wa maudhui (mada). 1. Kila haki imebeba maumbile mawili, umbile la ndani na umbile la nje, maumbile hayo huthibitishwa na kusadikishwa kutokana na ukweli wa haki hiyo, kwa ufafanuzi zaidi tunaweza kusema hivi:-Haki ni kama kombe na lulu, lulu ambayo hupatikana katika kombe hiyo, kombe ni umbile la nje na lulu ni umbile la ndani, hivyo kuna uwiano baina ya vitu hivyo viwili, bila ya kuonekana kombe hatuwezi kuthibitisha kuwa katika kombe hiyo mna (lulu) ndani yake au mna kitu chengine. Kwa hiyo kadiri itakavyoonesha kuwa umbile la nje lina thamani na muhimu, basi umbile la ndani pia litakuwa ni muhimu na lenye thamani zaidi. Katika makala iliyopita, tulielezea umuhimu wa uhakiki wa dini kupitia msingi wa Ijtihadi, katika makala hiyo tulielezea misingi mitatu inayoweza kumuongoza mwanaadamu katika uhakiki wake wa dini, katika makala hii tutaendelea kuelezea misingi mengine ya uhakiki wa dini. hivyo kuwa sambamba nami npaka tamati mwa makala hii.

Ufafanuzi

UHAKIKI WA DINI NO.4

UHAKIKI WA DINI NO.4 UHAKIKI WA DINI NO.4 UHAKIKI WA DINI KUPITIA MSINGI WA IJTIHADI. MAUMBILE YA DINI Hatua ya kwanza: Umuhimu wa maudhui (mada). 1. Kila haki imebeba maumbile mawili, umbile la ndani na umbile la nje, maumbile hayo huthibitishwa na kusadikishwa kutokana na ukweli wa haki hiyo, kwa ufafanuzi zaidi tunaweza kusema hivi:-Haki ni kama kombe na lulu, lulu ambayo hupatikana katika kombe hiyo, kombe ni umbile la nje na lulu ni umbile la ndani, hivyo kuna uwiano baina ya vitu hivyo viwili, bila ya kuonekana kombe hatuwezi kuthibitisha kuwa katika kombe hiyo mna (lulu) ndani yake au mna kitu chengine. Kwa hiyo kadiri itakavyoonesha kuwa umbile la nje lina thamani na muhimu, basi umbile la ndani pia litakuwa ni muhimu na lenye thamani zaidi. Katika makala iliyopita, tulielezea umuhimu wa uhakiki wa dini kupitia msingi wa Ijtihadi, katika makala hiyo tulielezea misingi mitatu inayoweza kumuongoza mwanaadamu katika uhakiki wake wa dini, katika makala hii tutaendelea kuelezea misingi mengine ya uhakiki wa dini.

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini