Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

Kusoma Qurani

MATAKWA YA MOLA KWA MITUME NO.2

MATAKWA YA MOLA KWA MITUME NO.2

MATAKWA YA MOLA KWA MITUME NO.1 Allah (s.w) amewapa Mitume yake nyadhifa mbali mbali, miongoni mwa nyadhifa hizo ni kufikisha ujumbe wake kwa waja wake, ujumbe huo waliopewa Mitume na Mola wao kuufikisha kwa walimwengu ni kwa ajili ya kumuongoza mwanaadamu na kumpatia saada ya duniani na Akhera. kwa sababu hiyo basi Mitume walitumia njia zote tatu katika kufikisha ujumbe wa Mwenyeezi Mungu kwa watu. katika makala iliyopita tulielezea baadhi ya njia hizo, na katika makala hii tutaelezea njia nyengine.

Ufafanuzi

MATAKWA YA MOLA KWA MITUME NO.1

MATAKWA YA MOLA KWA MITUME NO.1 MATAKWA YA MOLA KWA MITUME NO.1 Allah (s.w) amewapa Mitume yake nyadhifa mbali mbali, miongoni mwa nyadhifa hizo ni kufikisha ujumbe wake kwa waja wake, ujumbe huo waliopewa Mitume na Mola wao kuufikisha kwa walimwengu ni kwa ajili ya kumuongoza mwanaadamu na kumpatia saada ya duniani na Akhera. kwa sababu hiyo basi Mitume walitumia njia zote tatu katika kufikisha ujumbe wa Mwenyeezi Mungu kwa watu. Ili kufahamu zaidi tutazielezea njia hizo moja baada ya jengine: 1. Hekima Hekima ni elimu ambayo inamuwezesha mwanaadamu kudiriki na kupambanua uhakika wa mambo bila ya kuzidisha au kupunguza.

Ufafanuzi

UJUMBE WA MITUME

UJUMBE WA MITUME UJUMBE WA MITUME YA ALLAH (S.W) NO.1 Mitume Mitukufu ya Mwenyeezi Mungu ilifanya jitihada zao zote ili kufikisha ujumbe waliopewa na Mola wao, na watukufu hao walitumia njia na miongozo mbali mbali iliyoweza kufikisha ujumbe huo, ujumbe ambao ni amana waliopewa na Mola wao kwa ajili ya kuwafikishia walimwengu, kwa hiyo ikiwa wanaadamu watafuata na kutii maamrisho ya watukufu hao hapana shaka watafikia katika malengo yale yaliyokusudiwa na Mola Mtakatifu. Vipi Mitume iliwalingania watu katika dini ya Mwenyeezi Mungu?. Ndani ya Qur-ani neno (tabligh) limekuja na maana ya (kufikisha ujumbe wa Mwenyeezi Mungu kwa watu), kama tunavyosoma kuhusiana na Mitume ya Mwenyeezi Mungu:- الَّذِينَ يُبَلِّغُونَ رِسَالاَتِ اللهِ وَيَخْشَوْنَهُ وَلاَ يَخْشَوْنَ اَحَداً إِلاَّ اللهَ وَكَفَي بِاللهِ حَسِيباً[1] (Hao wa zamani) walio kuwa wakifikisha (ujumbe) risala za Mwenyezi Mungu na wanamwogopa Yeye, na wala hawamwogopi yeyote isipo kuwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ndiye atoshaye kuhisabu.

Ufafanuzi

ATHARI NJEMA BAADA YA UTUME NO.4

ATHARI NJEMA BAADA YA UTUME NO.4 ATHARI NJEMA BAADA YA UTUME NO.4 BAADA YA KUBASHIRIWA UTUME Mapinduzi ya Mitume hayakuwa na harakati zisizokuwa na malengo, bali yalikuwa ni hadafu na madhumuni ya juhudi zilizofanywa kwa ajili ya kufikia katika malengo maalumu, nayo ni kusuluhisha jamii, na kuwatakasa watu wa jamii nzima duniani. Hapana shaka kuwa Mitume imeteuliwa miongoni mwa watu. Katika makala no.3 tulielezea baadhi ya athari njema zilizopatikana baada ya Mitume kubashiriwa utume, katika makala hii tunaendelea na mada yetu hiyo hiyo, athari nyengine zilizopatikana

Ufafanuzi

ATHARI NJEMA BAADA YA UTUME NO.3

ATHARI NJEMA BAADA YA UTUME NO.3 ATHARI NJEMA BAADA YA UTUME NO.3 2. KUJENGA UMOJA NA KUONDOA HITILAFU Mitume ilifanya jitihada sana ili kujenga umoja ulio thabiti na kuondoa hitilafu miongoni mwa watu, kwa sababu baadhi ya wakati katika jamii unaweza ukaonekana umoja kidhahiri tu, na baada ya muda mfupi umoja huo ukaondoka, umoja ambao ulitokana na mipaka ya fikra za watu au maisha waliyokuwa wakiishi, au ulitokana na mapendeleo yao ya kimoyo, kama inavyoonekana kwa watu wa mwanzo ambao walijenga umoja kutokana na sababu hizo au nyenginezo, lakini baada ya watu hao kukua kifikra, walijiwa na masuala tofauti akilini mwao, na wakaingiwa na hadafu na madhumuni tofauti ambazo zilileta athari katika nyoyo zao, hatimae kutokana na fikra walizokuwa nazo zilisababisha kuleta hitilafu baina yao.

Ufafanuzi

ATHARI NJEMA BAADA YA UTUME NO.2

ATHARI NJEMA BAADA YA UTUME NO.2 ATHARI NJEMA BAADA YA UTUME NO.2 Baada ya Mitume kupewa Utume na kuja katika jamii ya watu kwa ajili ya kuwalingania na kuwataka waamini dini ya Mola mmoja, Mola ambaye ndiye mmiliki wa kila kitu duniani, katika kipindi hicho watu walikuwa wakiishi maisha ya tabu na mashaka bila ya kuona mafanikio yoyote au kuwa na matumaini katika maisha yao, lakini baada ya kuja Mitume jamii ilitokwa na mashaka hayo. Na Mitume iliwaletea furaha na mategemeo ambayo ndiyo muhimu katika maisha ya wanaadamu,  furaha ambayo ilienea miongoni mwa watu wote, na furaha hiyo iliwapa matumaini na kuwaondolea madhila waliyokuwa nayo kabla ya kuja mitume, basi jamii iliikubali dini mpya waliyokuja nayo Mitume, na wakawa wako tayari kufanya kila wanaloweza na kustahamili tabu na mashaka na kila yanayowakuta ili kuwa pamoja na Mitume hiyo.

Ufafanuzi

ATHARI NJEMA BAADA YA UTUME NO.1

ATHARI NJEMA BAADA YA UTUME NO.1 ATHARI NJEMA BAADA YA UTUME NO.1 Baada ya kuja Mitume, watu ambao walikuwa wakiabudu masanamu na waliopotoka na kupotea kwa kufuata sunna za kijahilia walizinduka, na hata wengine walikubali kufuata njia za Mitume hiyo baada ya kujiona kuwa hawakuwa katika mwenendo sahihi, kama inavyosema Qur-ani:- وَجَاء مِنْ اَقْصَي الْمَدِينَةِ رَجُلٌ يَسْعَي قَالَ يَا قَوْمِ اتَّبِعُوا الْمُرْسَلِينَ[2] Na akaja mtu mbio kutokea upande wa mbali wa mjini, akasema: Enyi watu wangu! Wafuateni hawa walio tumwa. * Wafuateni hawa walio tumwa – yaani wafuatwe Mitume - Na vile vile kwa wale ambao walikuwa wakitafuta uhuru wao na wamechoka na dhulma na kutokuwepo uadilifu, kwa watu madhalimu waliokuwa wametawala zama hizo, kwa kuja Mitume waliweza kupigania haki na uhuru wao. Kwa mfano;Baadhi ya watu wa Bani Israel walikubali kufuata desturi za Mtume wao, wakiwa chini ya uongozi wa - Taluti - walisimama kidete na kuwa madhubuti kwa kukabiliana na jeshi la – Jaluti –

Ufafanuzi

KUBASHIRIWA UTUME

KUBASHIRIWA UTUME BAADA YA KUBASHIRIWA UTUME Mapinduzi ya Mitume hayakuwa na harakati zisizokuwa na malengo, bali yalikuwa ni hadafu na madhumuni ya juhudi zilizofanywa kwa ajili ya kufikia katika malengo maalumu, nayo ni kusuluhisha jamii, na kuwatakasa watu wa jamii nzima duniani. Hapana shaka kuwa Mitume imeteuliwa miongoni mwa watu, kwa kuzingatia Aya hii:- لَقَدْ مَنَّ اللّهُ عَلـٰي الْمُؤمِنِينَ إِذْ بَعَثَ فِيهِمْ رَسُولاً مِّنْ اَنفُسِهِمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَإِن كَانُواْ مِن قَبْلُ لَفِى ضَلالٍ مُّبِينٍ[1] Hakika Mwenyezi Mungu amewafanyia wema mkubwa Waumini vile alivyo waletea Mtume aliye miongoni mwao wenyewe, anaye wasomea Aya zake, na anawatakasa, na anawafunza Kitabu na hikima, ijapo kuwa kabla ya hapo walikuwa katika upotovu ulio wazi.

Ufafanuzi

NJIA ZA KUKABILIANA NA WAKHALIFU NO.2

NJIA ZA KUKABILIANA NA WAKHALIFU NO.2 NJIA ZA KUKABILIANA NA WAKHALIFU NO.1 Njia walizotumia Mitume katika kukabiliana na waliowakhalifu. Mitume ya Mwenyeezi Mungu walitumia njia tofauti katika kukabiliana na maadui wao ambao waliwakhalifu. Baadhi ya njia hizo ni kama hizi zifuatazo:- 1. KUJIBAGUA NA MAKAFIRi. Mwanzoni mwa malinganiajo ya Mitume, kundi la makafiri lilisisitiza na kuwasisitiza watu kubaki katika itikadi za kikafiri, na hawakukubali kuacha itikadi zao hizo, hata walifanya jitihada sana kuwavuta na kufanya mambo yatakayowavutia Mitume na wafuasi wao katika itikadi zao za kikafiri, katika hali kama hiyo basi, hatua ya mwanzo waliyochukua Mitume ni kutangaza na kuwataka wafuasi wao kukabiliana na kupingana na makafiri, Mitume ilitangaza kujibagua na makafiri.

Ufafanuzi

NJIA ZA KUKABILIANA NA WAKHALIFU NO.1

NJIA ZA KUKABILIANA NA WAKHALIFU NO.1 NJIA ZA KUKABILIANA NA WAKHALIFU NO.1 Njia walizotumia Mitume katika kukabiliana na waliowakhalifu. Mitume ya Mwenyeezi Mungu walitumia njia tofauti katika kukabiliana na maadui wao ambao waliwakhalifu. Baadhi ya njia hizo ni kama hizi zifuatazo:- 1. KUJIBAGUA NA MAKAFIRi. Mwanzoni mwa malinganiajo ya Mitume, kundi la makafiri lilisisitiza na kuwasisitiza watu kubaki katika itikadi za kikafiri, na hawakukubali kuacha itikadi zao hizo, hata walifanya jitihada sana kuwavuta na kufanya mambo yatakayowavutia Mitume na wafuasi wao katika itikadi zao za kikafiri, katika hali kama hiyo basi, hatua ya mwanzo waliyochukua Mitume ni kutangaza na kuwataka wafuasi wao kukabiliana na kupingana na makafiri, Mitume ilitangaza kujibagua na makafiri.

Ufafanuzi

DHAHIRI NA BATINI YA QUR_ANI NO.1

DHAHIRI NA BATINI YA QUR_ANI NO.1 BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI DHAHIRI NA BATINI YA QUR_ANI NO.1 Taawili (tafsiri ya dhahiri shahiri) ni tafsiri yenye kumurika maneno kupitia darubini ya udhahiri wa mambo, na maana dhahiri za maneno zilivyo. Taawili ni kufasiri na kutafuta maana za maneno kupitia darubini ya nguvu za kiakili zenye uwezo wa kujua maana dhahiri na kuilenga ile maana halisi iliyojificha ndani ya maneno. Kwa hiyo kwa msingi huo tunaweza kusema kuwa tafsiri ya dhahiri shahiri ni tafsiri ya wazi yenye kuonekana dhahiri shahiri bila ya mashaka yoyote.

Ufafanuzi

DHAHIRI NA BATINI YA QUR_ANI NO.2

DHAHIRI NA BATINI YA QUR_ANI NO.2 DHAHIRI NA BATINI YA QUR_ANI NO.2 Katika makala zilizopita tulielezea njia za uhakiki wa dini, na tukafafanua kwa ufupi dhahiri na shahiri ya Aya za Qur-ani katika makala hii tutandelea kufafanua dhahirina batini ya Aya za Qur-ani na na njia nyengine wanazotumia wahakiki wa dini katika uhakiki wao. Mwenyeezi Mungu anasema:- Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee. Mwenyezi Mungu Mkusudiwa Hakuzaa wala hakuzaliwa. Wala hana anaye fanana naye hata mmoja.

Ufafanuzi

HATIMA YA WALIOWAHALIFU MITUME

HATIMA YA WALIOWAHALIFU MITUME HATIMA YA WALIOWAKHALIFU MITUME * Kwa nini baadhi ya watu walisimama kidete kuwakhalifu Mitume? * Waliowakhalifu Mitume walitumia njia gani katika kupingana na Mitume?. Katika makala iliyopita tulielezea sababu zilizowafanya baadhi ya watu kuwakhalifu Mitume, na tukaelezea njia walizotumia maadui hao katika kukabiliana na Mitume, na tukaashiria kwa ufupi tu hatima ya watu hao, katika makala hii tutaendelea kwa kuelezea kwa kina hatima ya wapotofu hao.

Ufafanuzi

MALENGO YA WAHAKIKI WA DINI NO.1

MALENGO YA WAHAKIKI WA DINI NO.1 MALENGO YA WAHAKIKI WA DINI NO.1 Jitihada za wahakiki zinaweza zikawa kwa ajili ya malengo na hadafu tofauti: - -Baadhi ya wahakiki hufanya uhakiki wao kwa ajili ya kueneza na kusambaza ukoloni mambo leo, unaotoka katika mataifa makubwa wenye nia ya kutaka kuutawala ulimwengu kifikra na kiutamaduni. -Baadhi ya wahakiki hufanya uhakiki wao kuhusiana na dini wakiwa na malengo ya kutaka kutambua ukweli na uhakika wa dini hiyo.

Ufafanuzi

NJIA ZA MAADUI KUPINGANA NA MITUME

NJIA ZA MAADUI KUPINGANA NA MITUME NJIA ZA MAADUI KATIKA KUPINGANA NA MITUME NO.1 Katika makala zilizopita tulielezea dalili zilizowafanya maadui wa Kiislamu kupingana na Mitume ya Mwenyeezi Mungu, katika makala hii tutaelezea njia walizotumia maadui hao katika kukabiliana na Mitume hiyo Mitukufu. Tangu hapo mwanzo, baada tu ya Mitume kupewa utume walikumbana na watu ambao waliwakhalifu kutokana na malinganio waliyokuja nayo Mitume hiyo. Kwa sababu malinganio hayo yalikuwa hayawiani na itikadi zao au manufaa yao ambayo walikuwa wakiyahitajia, hivyo watu hao walisimama kedete kuupinga ujumbe wa Mwenyeezi Mungu waliokuja nao Mitume hiyo.

Ufafanuzi

NJIA ZA UHAKIKI WA DINI NO.1

NJIA ZA UHAKIKI WA DINI NO.1 NJIA ZA UHAKIKI WA DINI NO.1 Uhakiki wa dini unapatiwa ufumbuzi kwa kuzingatia mikondo (mambo) mitatu. Taaluma ya ndani ya dini, taaluma ya nje ya dini, na utendaji wa amali. 1. Wahakiki wanaotaka kutambua uhakika na haki ya dini wanaweza kuitafiti dini na kuipatia ufumbuzi wake kupitia vigezo hivi vifuatavyo:- - Kupitia elimu na taaluma ya nje ya dini, yaani kupitia misingi mikuu ya dini, (umbile la nje la dini). - Kupitia elimu na taaluma ya ndani ya dini, yaani kuzingatia maamrisho, makatazo, hukumu mbali mbali n.k. (umbile la ndani la dini). - Kuwa na elimu na taaluma katika kuyafanyia amali yote yaliyoamrishwa na Mwenyeezi Mungu kwa kuyafanyia amali kimwenendo na kimatendo, na kujiepusha na yale aliyoyakataza Mola Mtakatifu.

Ufafanuzi

WALIOWAHALIFU MITUME NO.1

WALIOWAHALIFU MITUME NO.1 WALIOWAKHALIFU MITUME NO.1 Katika makala iliyopita tulielezea kuhusu wafuasi wa kweli wa Mitume ya Mwenyeezi Mungu (s.w) na sifa walizonazo watiifu hao. katika makala hii tutaendelea kuelezea sababu zilizowafanya baadhi ya watu kuwakhalifu Mitume ya Mwenyeezi Mungu. Tangu hapo mwanzo, baada tu ya Mitume kupewa utume walikumbana na watu ambao waliwakhalifu kutokana na malinganio waliyokuja nayo Mitume hiyo. Kwa sababu malinganio hayo yalikuwa hayawiani na itikadi zao au manufaa yao ambayo walikuwa wakiyahitajia, hivyo watu hao walisimama kedete kuupinga ujumbe wa Mwenyeezi Mungu waliokuja nao Mitume hiyo.

Ufafanuzi

WALIOWAHALIFU MITUME NO.2

WALIOWAHALIFU MITUME NO.2 DALILI ZILIZOWAFANYA WAWAKHALIFU MITUME. Tangu hapo mwanzo, baada tu ya Mitume kupewa utume walikumbana na watu ambao waliwakhalifu kutokana na malinganio waliyokuja nayo Mitume hiyo. Kwa sababu malinganio hayo yalikuwa hayawiani na itikadi zao au manufaa yao ambayo walikuwa wakiyahitajia, hivyo watu hao walisimama kedete kuupinga ujumbe wa Mwenyeezi Mungu waliokuja nao Mitume hiyo. Qur-ani Karym imeelezea kwa uwazi dalili zilizowafanya watu hao wawakhalifu Mitume, njia walizotumia katika kupingana nao na hatima ya watu hao, katika somo hili tutaelezea njia hizo, kwa sababu kuzifahamu njia hizo kutawapelekea wafuasi wa Mitume kuzifahamu hila za maadui wao, na kuwafanyia wepesi katika kustahamili tabu na matatizo watakayoweza kuyapata.

Ufafanuzi

WALIOWAHALIFU MITUME NO.3

WALIOWAHALIFU MITUME NO.3 WALIOWAKHALIFU MITUME NO.3 waliowakhalifu Mitume Sio washirikina tu, bali kuna makundi na watu tofauti waliowakhalifu Mitume, miongoni mwao ni washirikina, makafiri. Maadui, n.k. na baadhi ya wakati kulitokea watu amabo kidhahiri walidai kuwa wamewaamini Mitume hiyo, lakini kwa kweli walikuwa ni wanafiki, yaani wakiwa pamoja na Mitume hudai kuwa wao wanawaamini Mitume, na wakiwa pamoja na makafiri hudai kuwa wako pamoja na makafiri, hivyo imani zao zilikuwa ni dhaifu, na walisababisha madhara zaidi katika dini ya Kiislamu kuliko hata hao makafiri, katika sehemu hii tutatoa mifano na mwenendo waliokuwa wakitumia watu kama hao:-

Ufafanuzi

WALIOWAHALIFU MITUME NO.4

WALIOWAHALIFU MITUME NO.4 WALIOWAKHALIFU MITUME. waliowakhalifu Mitume Sio washirikina tu, bali kuna makundi na watu tofauti waliowakhalifu Mitume, miongoni mwao ni washirikina, makafiri. Maadui, n.k. na baadhi ya wakati kulitokea watu amabo kidhahiri walidai kuwa wamewaamini Mitume hiyo, lakini kwa kweli walikuwa ni wanafiki, yaani wakiwa pamoja na Mitume hudai kuwa wao wanawaamini Mitume, na wakiwa pamoja na makafiri hudai kuwa wako pamoja na makafiri, hivyo imani zao zilikuwa ni dhaifu, na walisababisha madhara zaidi katika dini ya Kiislamu kuliko hata hao makafiri, katika sehemu hii tutaendelea kutoa mifano na mienendo waliokuwa wakitumia watu kama hao.

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini