Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

Kusoma Qurani

DINI INALETA AMANI NA SALAMA

DINI INALETA AMANI NA SALAMA

DINI INALETA AMANI NA SALAMA Miongoni mwa misingi mengine ya uhakiki wa dini ni kuwaletea wanaadamu amani na usalama na kuwaongoza katika njia iliyo sahihi, amah ii haimaanishi kuwa hadafu na malengo ya uhakiki wa dini ni kujenga mahusiano au kufanya suluhu na dini nyengine, bali hadafu asili ni kuondoa na kutokomeza fikra na mitizamo isiyo sahihi ya dini hizo, na kuwalingania wafuasi wa dini hizo katika dini moja tu ya haki, nayo ni dini ya Kiislamu, ujumbe wa Mwenyeezi Mungu uliomo katika dini hiyo unawabainishia wanaadamu wote ulimwenguni kuwa dini ya haki ni dini ya Kiislamu pekee, kwa hiyo hadafu ya ujumbe huo sio kitu chengine isipokuwa ni kuondoa na kutokomeza fikra za dini zisizokuwa sahihi.

Ufafanuzi

FUNGAMANO LA VIONGOZI DUNIANI NA AKHERA

FUNGAMANO LA VIONGOZI DUNIANI NA AKHERA FUNGAMANO LA VIONGOZI DUNIANI NA AKHERA. Viongozi wa jamii ni dalili bora na muhimu inayoonyesha uongofu na upotofu wa wanaadamu, kama inavyoeleweka kuwa mema na mazuri yote yanaonekana na kuthibitika kwa kuwafuata Maimamu wanaoitabua haki, na mabya na maovu yote yana uhusiano na Maimamu wanaofanya maovu na ukafiri. Kuna aina mbali mbali za watu katika dunia, aina hizo za watu ni kutokana na mapendeleo yao ya kiitikadi, na vigezo vya amali zao vitashuhudiwa kutoka kwa viongozi wao wa haki au wa kibatili, siku ya Kiama kutadhihirika fungamano la uwalii wa viongozi wema, na upotofu wa viongozi waovu, basi kila mmoja atavutwa ili amtafute kiongozi wake.

Ufafanuzi

MABASHIRIO YA THAWABU DUNIANI NA AKHERA

MABASHIRIO YA THAWABU DUNIANI NA AKHERA MABASHIRIO YA THAWABU DUNIANI NA AKHERA Starehe na madhila ya Waumini duniani kwao wao ni sawa, kwa sababu hunufaika na starehe za duniani kwa neema za Mola wao, na hunufaika na mashaka ya duniani kwa kukumbuka mabashirio ya Mola wao, kwa sababu nyoyo zao hutulia pale wanapokumbuka mabashirio ya Mwenyeezi Mungu ambayo huwaondolea hofu, na nyoyo zao hufurahika wanapokumbuka ujira wa Mola wao.

Ufafanuzi

MADHARA YA DUNIANI NA AKHERA

MADHARA YA DUNIANI NA AKHERA MADHARA YA DUNIANI NA AKHERA. Watu ambao hawako thabiti katika njia iliyonyooka, wanapopata matatizo madogo tu maishani mwao hujizuilia na kukiuka hukumu za Mwenyeezi Mungu, au huenda katika vikundi vya  watu waovu, watu kama hao hukutwa na madhara Duniani na Akhera. kwa ufafanuzi zaidi ungana nami katika makala hii mpaka mwisho.

Ufafanuzi

MSINGI YAKINI KATIKA UHAKIKI WA DINI

MSINGI YAKINI KATIKA UHAKIKI WA DINI MSINGI YAKINI KATIKA UHAKIKI WA DINI Baadhi ya wahakiki wa dini, badala ya kupata ya kupata natija ya uhakika na iliyo yakini kutokana na kile walichokifanyia uhakiki kuhusiana na dini, muhakiki huyo hubakiwa na dhana tu akilini mwake bila ya kufikia au kuona natija yoyote, hii inaweza ikawa ni kwa sababu ya kuwa malengo ya muhakiki huyo hayakuendana sambamba na uhakiki wake, inawezekana muhakiki huo katika uhakiki wake alikuwa na uadui fulani kuhusiana na dini. kwa ufafanuzi zaidi ungana nami katika makalk

Ufafanuzi

UTAFITI KUHUSIANA NA DINI

UTAFITI KUHUSIANA NA DINI UTAFITI KUHUSIANA NA DINI Tahakiki nyingi zinazofanywa kwa jina la uhakiki wa dini ziko nje ya ukweli wa hali halisi ya uhakika wa dini na taaluma ya dini, au tahakiki hizo zimeichukulia dini kama ni uhakika usio thabiti unaoweza kutolewa nadharia na watu binafsi na sio kuthibitishwa uhakika huo kutokana na ukweli na haki inayoshuhudiwa katika dini hiyo takatifu. Baadhi ya wahakiki wa dini hupotea katika uhakiki wao kwa kutoweza kuhalili yale mambo ambayo yanahusiana na uhakika huo wa dini. kwa ufafanuzi zaidi ungana nami katika makala hii mpaka mwisho.

Ufafanuzi

UHUSIANO THABITI WA DUNIANI NA AKHERA

UHUSIANO THABITI WA DUNIANI NA AKHERA UHUSIANO THABITI WA DUNIANI NA AKHERA. * Kuna uhusiano gani baina ya ulimwengu wa dunia na ulimwengu wa Kiama?. *Kuna uhusiano gani baina ya matendo na amali anazozifanya mwanaadamu duniani na malipo atayolipwa siku ya Kiama? Kuna uhusiano madhubuti wa maisha ya duniani na Akhera, na kuna tofauti baina ya kustahamili mashaka ya duniani na kustahamili adhabu za Akhera, kwa ufafanuzi zaidi ungana nami katika makala hii mpaka mwisho.

Ufafanuzi

UHUSIANO WA DUNIANI NA AKHERA

UHUSIANO WA DUNIANI NA AKHERA UHUSIANO WA DUNIA NA AKHERA * Kuna uhusiano gani baina ya ulimwengu wa dunia na ulimwengu wa Kiama?. *Kuna uhusiano gani baina ya matendo na amali anazozifanya mwanaadamu duniani na malipo atayolipwa siku ya Kiama? Kuna uhusiano baina ya dunia na Akhera, kiasi ya kwamba kutokana na matendo anayoyafanya mwanaadamu duniani, ndio malipo atayolipwa Akhera, ikiwa mwanaadamu atafanya amali na matendo mema, basi atalipwa Pepo. Na ikiwa atafanya madhambi na kumuasi Mola wake, atalipwa moto.

Ufafanuzi

YALIYO MUHIMU NDANI YA DINI

YALIYO MUHIMU NDANI YA DINI YALIYO MUHIMU NDANI YA DINI Ijapokuwa katika uwanja wa dini kuna baadhi ya vitengo vya uhakiki wa dini vinavyopingana na nadharia mpya zinazotolewa kuhusiana na dini, na vitengo hivyo vina wasiwasi wa kupotea misingi asili ya dini, misingi ambayo inawezekana ikawa ndio kiungo cha dini, kwa upande mwengine, katika uwanja huo huo wa dini kuna madai yanayodaiwa na baadhi ya watu ya kuwepo kwa uhakika wa dini tofauti. kwa ufafanuzi zaidi ungana nami katika mkala hii mpaka mwisho.

Ufafanuzi

FUNGAMANO LA FAMILIA NA MARAFIKI

FUNGAMANO LA FAMILIA NA MARAFIKI FUNGAMANO LA FAMILIA NA MARAFIKI Katika dunia, wanaadamu hutegemea familia zao, ukoo wao, au hata marafiki zao katika kuondoa mabalaa yanayowakuta, au kwa ajili ya kutatua matatizo waliyonayo, au kuomba msaada ili kupata mahitajio yao, ama siku ya Kiama wanaadamu wote wataghafilika na kuingiwa na hofu kiasi ya kwamba kila mmoja atakuwa akihangaika ili kujiokoa yeye na nafsi yake bila ya kufikiria wengine. kwa ufafanuzi zaidi ungana nami katika makala hii mpaka tamati.

Ufafanuzi

FUNGAMANO LA MALI NA WATOTO

FUNGAMANO LA MALI NA WATOTO FUNGAMANO LA MALI NA WATOTO Kwa wale watu ambao katika dunia ili kuonyesha nguvu na uwezo wao hutegemea mali na watoto wao kwa ajili ya kuondoa athari mbaya na nuhusi katika maisha yao, basi ni lazima waelewe kuwa siku ya Kiama sio mali wala sio watoto wao havitawaletea faida yoyote siku ya Kiama.

Ufafanuzi

FUNGAMANO LA NASABU SIKU YA KIAMA

FUNGAMANO LA NASABU SIKU YA KIAMA FUNGAMANO LA NASABU SIKU YA KIAMA  Itakapofika siku ya Kiama hakutakuwa na uhusiano wala fungamano lolote baina ya wanaadamu, hata fungamano la nasaba pia litakuwa halina nafasi yoyote katika familia, mwanaadamu hatakuwa na hiyari yoyote katika familia wala nasaba, mlolongo wa muamala na ahadi ambazo watu waliahidiana hazitakuwa na nafasi yoyote katika jamii.

Ufafanuzi

HAKUNA FUNGAMANO KATIKA HILA

HAKUNA FUNGAMANO KATIKA HILA HAKUNA FUNGAMANO KATIKA HILA Duniani kuna baadhi ya watu waovu, na Serikali mbovu ambazo zinaendeshwa katika mfumo usiokuwa sahihi, yaani zinaendeshwa kwa mfumo wa kishetani, serikali ambazo huongozwa kwa kuwafanyia watu dhulma, au huongozwa kwa hila ambazo huwapatia watu hao waovu ridhaa za nafsi zao, na kuwapotoa watu kifikra,

Ufafanuzi

HATUA NA MALENGO YA PLURALISM

HATUA NA MALENGO YA PLURALISM HATUA NA MALENGO YA PLURALISM Hatua ya kwanza: Kubadilisha haki na uhakika wa dini kupitia nidhamu maalumu iliyopangwa, taaluma na maadili ya dini wameyabadilisha, taaluma ambayo ndio njia msingi itakayoweza  kumfikisha mwanaadamu katika ukamilifu, na wameondoa na kutokomeza taaluma na maadili hayo ya dini wakavumbua maadili yao ambayo hayana thamani yoyote katika maisha ya mwanaadamu na hayamfikishi mwanaadamu katika mahitajio yake wala katika ukamilifu.

Ufafanuzi

HATUA NA MALENGO YA PLURALISM No.2

HATUA NA MALENGO YA PLURALISM No.2 HATUA NA MALENGO YA PLURALISM NO.2 Malengo msingi ya kuanzishwa mipango ya kuwa na itikadi na dini tofauti yanatokana na jitihada za Phylosophy mabepari waliokuwa na nguvu na uwezo katika jamii au dunia ile ya nchi za kimagharibi, mafilosofi hao walikuwa wakifanya jitihada zao zote ili kunufaika au kupata manufaa yao binafsi kwa kujenga uhusiano madhubuti na mitandao au vyombo mbali mbali vya habari ili kuitangazia jamii yale waliyodai kuwa yanawaletea wanaadamu saada na mafanikio

Ufafanuzi

MTAZAMO WA PLURALISM KUHUSIANA NA DINI

MTAZAMO WA PLURALISM KUHUSIANA NA DINI MTAZAMO WA PLURALISM KUHUSIANA NA DINI Watu walio na fikra za Pluralism (itikadi ya dini tofauti), wana imani ya kuwa;  Elimu ya tarehe inathibitisha kuwa njia na sheria zozote zile zitakazomuongoza mwanaadamu katika kumfikia mola wake zinakubalika na ni lazima ziheshimiwe, kwa hiyo wafuasi wote wa dini tofauti, ikiwa ni dini ya Mayahudi, Manasara, washirikina, mabuda, mapagani, n.k. ni lazima itikadi zao ziheshimiwe, nay ale waliyo na imani nayo yanawadhamini watu hao kuwa yatawafikisha katika saada.

Ufafanuzi

PLURALISM NA DINI TOFAUTI

PLURALISM NA DINI TOFAUTI PLURALISM NA DINI TOFAUTI Kwa mtazamo wa watu hao, dini zote na makundi yote yaliyomo katika jamii ni lazima yaheshimiwe na yathaminiwe, hata ikiwa dini hizo au makundi hayo yako katika njia potofu, au dini zilizoharifiwa na kupotoshwa, dini hizo zinaweza zikawa dini za Kikiristo, kiyahudi, dini za Buda, dini za Hindu, n.k.  

Ufafanuzi

KUDHIHIRI KWA IMAM MAHDI (AS) No2

KUDHIHIRI KWA IMAM MAHDI (AS) No2 SABABU ZA KUDHIHIRI IMAM MAHDI (A.j) Kudhuhuru kwa Imam kuna sababu na alama maalum na sababu hizo pamoja na alama zinaeleweka kuwa ndio matayarisho ya kuja kwake, tofauti ya vitu hivi viwili (alama na matayarisho) ni kwamba matayarisho yana athari muhimu katika kudhuhuru kwa Imam kiasi kwamba yakikamilika matayarisho hayo basi kudhihiri kwa Imam ni lazima kutokee. katika makala iliyopita tulielezea alama za kudhihiri imam Mahdy(a.j), ama katika makala hii tutaeleazea sababu za kudhihiri kwake. nizipi sababu hizo, ungana nami mpaka mwisho wa makala hii ili kuzijua sababu hizo.

Ufafanuzi

DINI NA SEREKALI

DINI NA SEREKALI DINI NA SEREKALI Kuna kauli za wale wanaosema kuwa:- “jambo lisilokubalika katika serikali ya dini ni kule kutoendana sambamba baina ya serikali ya dini na elimu ya dini ambayo ndio ushahidi unaotumiwa na wanaserikali wa dini hiyo katika kuendeleza malengo ya serikali yao. ilikujua ubatili wa madai haya ungana nami katika makala hi mpaka mwisho

Ufafanuzi

VITUO VYA KIAMA KWA WAUMINI NA WAOVU

VITUO VYA KIAMA KWA WAUMINI NA WAOVU Vituo vya nkiyama kwa waumini na waovu katika makala iliyopita tuzungumzia kuhusu visimamo vya siku ya kiyama, ama katika makala hii tutazungumzia kuhusu vituo vya kiyama kwa waumini na waovu. lakini pia makala hii itakueleza wazi yatakayojiri katika vituo hivyo siku ya kiyama. ili kujua niyapi yatakayojiri siku hiyo, na utofauti kati waumini na waovu, na niyapi atakayofaidika nayo muumini, ungana nami katika makala mpaka tamati.

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini