Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

Uadilifu

UADILIFU WA MUNGU

UADILIFU WA MUNGU

UADILIFU WA MUNGU Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anasema: “Mwenyezi Mungu na Malaika, na wenye elimu wameshuhudia kuwa hakuna aabudiwaye ila  Yeye tu, ni Mwenye kusimamia uadilifu. Hakuna aabudiwaye isipokuwa Yeye tu, Mwenye nguvu na Mwenye hekima.” (Qur’ani, 3:18) “Hakika wale wanaozikataa Aya za Mwenyezi Mungu, na kuwauwa Manabii pasipo haki, na kuwauwa watu wanaoamuru mambo ya uadilifu, basi wape khabari ya adhabu iumizayo.” (Qur’ani, 3:21) “Enyi mlioamini! Kuweni wasimamizi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu  mtoe ushahidi kwa uadilifu. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutowafanyia uadilifu fanyeni uadilifu, huko ndiko kunakomkurubisha mtu na ucha Mungu, na mcheni Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayoyatenda.” (Qur’ani, 5:8) “Kwake ndio marejeo yenu nyote, ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli. Hakika Yeye ndiye huanzisha kiumbe kisha hukirudisha ili awalipe walioamini na kufanya vitendo vizuri kwa uadilifu. Na waliokufuru, (wao) watapata kinywaji cha maji yanayochemka, na adhabu yenye kuumiza kwa sababu walikuwa wakikataa.” (Qur’ani, 10:4)

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini