Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

IMAM ZEINUL-ABIDIIN

DUA YA TOBA

DUA YA TOBA

DUA YA TOBA Ewe Mola wangu, ambaye sifa za kukusifu za wenye kukusifu haziwezi kutajika. Ewe mwenye mategemeo ambaye mategemeo hayawezi kwenda zaidi yako.Ewe ambaye kwako wewe malipo ya waja wako hayatapotea. Ewe unayeogopwa na waja wako. Ewe uliye khofu ya mja wako na hii ndiyo nafasi imemkuba ghafla kwa madhambi. Ambaye amevutwa na zama za makosa na ambayo yameghalibiwa na sheitani.Kwa hivyo ameshindwa kabisa kutimiza yale uliyokuwa umemwamrisha kuyafanya na yeye hakuyafanya.Yeye amegang'ania tu katika yale uliyokuwa umeyaharamisha na kuyakataza kama kwamba haelewi uwezo ulionao juu yake. Au kama yule anayekanusha ukarimu wako mtukufu kwake yeye hadi macho ya hidaya kufunguliwa kwa ajili yake na mawingu (kiza) cha upofu (wa hidaya) ulipoondolewa kutoka kwake, na alipotambua kwa ukamilifu vile alivyojidhulumu nafsi yake na kuyazingatia kuwa amemwasi Muumba wake.Kwa hivyo ameyaona maovu yake kwa mapana vile yalivyokuwa, akaona ukubwa na uasi na upinzani wake ulivyo kupita kiasi, kwa hivyo amekurejea wewe kwa kutaraji msaada wako kwa kuona aibu mbele yako, akielekea kwako wewe kwa hali halisi kutokana na woga wake, shauku yake ya kutaka kuondolewa kila kitu na hofu zake, ila ni wewe tu ndiye mwenye uwezo wa kuyadonoa hivyo.Hivyo amesimama mbele yako, akiomba. Macho yake yakiwa yanatazama chini ardhini kwa utiifu, na kichwa chake chini kwa unyenyekevu wa Ukuu wako. Katika hali ya kudhalilika ya nafsi anaungama kwako kwa siri zake zote ambazo wewe wazijua zaidi kuliko mimi mwenyewe na katika aibu amezihisabu madhambi yake ambayo wewe umeishakwisha kumhesabia. (Yeye anakuomba wewe kumwokoa kwa kumtoa kutoka madhambi makubwa ambayo ameingia humo wakati wewe unajua na ambavyo imemwaibisha kabisa katika heshima yako ya maamrisho yasiyotimizwa naye, starehe ambazo madhambi yamemgeukia na kumhukumia adhabu ambayo itakayokuwa daima juu yake. Yeye kamwe hakanushi uadilifu wako, Ewe Mola wangu! Iwapo wewe utamwadhibu.Yeye anasadiki kuwa usamehevu kwako wewe ni jambo dogo. Iwap utamsamehe na kumhurumia yeye kwani wewe ni Bwana wa Hisani, ambaye hadhanii kuwa ni vigumu kwako wewe kumsamehe madhambi hata yakiwa makubwa kiasi gani.

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini