Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

Tarehe

KIFO CHA MTUME MUHAMMADI (S.A.W.W) SEHEMU YA PILI

KIFO CHA MTUME MUHAMMADI (S.A.W.W) SEHEMU YA PILI

KIFO CHA MUHAMMAD (s.a.w.w) MTUME WA ALLAH (s.w.t) SEHEMU YA PILI Jumatatu, Rabi al-Awwal 1, 11 H.A. Jumatatu, mwezi 1 Rabi al-Awwal ya 11Hijiria ilikuwa ndio siku ya mwisho ya Muhammad ibn Abdullah (s.a.w.w) , Mtume wa Allah (s.w.t.) katika dunia hii. Kulikuwa na nyakati ambapo alijisikia nafuu kidogo lakini wakati mwingine, alikuwa dhahiri kwenye maumivu makali. Aisha, mke wake, anasimulia ifuatavyo:  “Jinsi siku ilivyosogea kuelekea mchana, Fatima Zahra, binti yake Mtume wa Allah (s.a.w.w) alikuja kumuona Mtume. Alimkaribisha na kumwambia akae kandoni mwake. Kisha akamwambia kitu ambacho sikuweza kusikia lakini alianza kulia. Alipoyaona machozi ya binti yake, alimwambia kitu kingine ambacho pia sikuweza kusikia lakini yeye alianza kutabasamu. Yeye alifanana sana na baba yake katika mwenendo, tabia na Sura.” Muda baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w) , Aisha alimuuliza Fatima ni kitu gani ambacho baba yake alimwambia yeye ambacho kwanza kilimfanya alie na kisha kikamfanya atabasamu.

Ufafanuzi

KIFO CHA MTUME MUHAMMADI (S.A.W.W) SEHEMU YA KWANZA

KIFO CHA MTUME MUHAMMADI (S.A.W.W) SEHEMU YA KWANZA KIFO CHA MUHAMMAD (s.a.w.w) MTUME WA ALLAH (S.W.T.) MALENGO YA MAISHA YA MUHAMMAD MUSTAFA (s.a.w.),  kama Mtume wa Mwisho wa Allah (s.w.t.) katika dunia hii yalikuwa: • Kuangamiza ibada ya masanamu na ushirikina; • Kutangaza rasmi Tauhidi ya Muumba; • Kufikisha Ujumbe wa Muumba kwa wanadamu; • Kukamilisha mfumo wa dini na sheria; • Kutakasa nafsi za wanaume na wanawake; • Kukomesha dhulma, uovu na ujinga; • Kuanzisha mfumo wa amani pamoja na haki; • Kuunda chombo katika namna ya hali ya kisiasa kwa ajili ya utambuzi wa malengo hayo yote yaliyopita, na chombo ambacho kitadumisha mwendo wa kazi yake. Ndani ya ile miaka 23 ya kazi yake kama Mtume wa Allah, Muhammad (s.a.w.) alikuwa amefanikisha malengo yote Haya, na kisha ilianza kuonekana kama ilivyo kwa wanadamu wengine wote, yeye pia ilimbidui aondoke kwenye dunia hii. Kama ilivyoelezwa hapo kabla, alipokea taarifa hii kwa mara ya kwanza pale Suratun-Nasr (msaada), Sura ya 110 ya Qur’an Tukufu, iliyonukuliwa mapema katika kitabu hiki, iliposhushwa kwake.

Ufafanuzi

WITO KWA WAISLAMU KUUENDEA UKWELI (SEHEMU YA TATU)

WITO KWA WAISLAMU KUUENDEA UKWELI (SEHEMU YA TATU) WITO KWA WAISLAMU KUUENDEA UKWELI UTANGULIZI Tofauti kubwa iliyopo baina ya Waislamu wa Kishia na Waislamu wa Kisunni ni juu ya imani ya Ukhalifa na Uimamu baada ya kuondoka kwa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w). Sisi waislamu wa Kishia tunaamini kuwa Imam Ali bin Abi Talib (a.s) ni khalifa na Imam wa kwanza baada ya Mtume (s.a.w.w.) ambapo ndugu zetu Waislamu wa Kisunni wanaamini kwamba Seyidina Abubakar (r.a.) alikuwa ni khalifa wa kwanza. Ingawa kuna tofauti nyingine ndogo ndogo zilizopo baina ya madhehebu makubwa ya Uislamu (Shia na Sunni) kwa mfano katika sheria (Fiqh) kama vile kukunja mikono wakati wa kusali au kuinyoosha n.k. lakini hizi ni tofauti ndogo ndogo sana ambazo zinaweza hata kupatikana ndani ya madhehebu manne ya Kisunni (Imam Shafi, Maliki, Hanafi na Hanbali ). Masuala haya tutayajadili hapo baadaye InshaAllah. Ama Makala haya yanaeleza kwa kina kuwa mrithi wa haki wa Mtume (s.a.w.w.) baada yake ni nani na dalili zote zime tolewa kutoka vitabu vya Sahihi na vinavyo tegemewa na kurejewa. Hivyo nakuomba kuwa sambamba name mpaka tamati mwa msururu wa makala zetu hizi.

Ufafanuzi

WITO KWA WAISLAMU KUUENDEA UKWELI (SEHEMU YA PILI)

WITO KWA WAISLAMU KUUENDEA UKWELI (SEHEMU YA PILI) WITO KWA WAISLAMU KUUENDEA UKWELI UTANGULIZI Tofauti kubwa iliyopo baina ya Waislamu wa Kishia na Waislamu wa Kisunni ni juu ya imani ya Ukhalifa na Uimamu baada ya kuondoka kwa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w). Sisi waislamu wa Kishia tunaamini kuwa Imam Ali bin Abi Talib (a.s) ni khalifa na Imam wa kwanza baada ya Mtume (s.a.w.w.) ambapo ndugu zetu Waislamu wa Kisunni wanaamini kwamba Seyidina Abubakar (r.a.) alikuwa ni khalifa wa kwanza. Ingawa kuna tofauti nyingine ndogo ndogo zilizopo baina ya madhehebu makubwa ya Uislamu (Shia na Sunni) kwa mfano katika sheria (Fiqh) kama vile kukunja mikono wakati wa kusali au kuinyoosha n.k. lakini hizi ni tofauti ndogo ndogo sana ambazo zinaweza hata kupatikana ndani ya madhehebu manne ya Kisunni (Imam Shafi, Maliki, Hanafi na Hanbali ). Masuala haya tutayajadili hapo baadaye InshaAllah. Ama Makala haya yanaeleza kwa kina kuwa mrithi wa haki wa Mtume (s.a.w.w.) baada yake ni nani na dalili zote zime tolewa kutoka vitabu vya Sahihi na vinavyo tegemewa na kurejewa. Hivyo nakuomba kuwa sambamba name mpaka tamati mwa msururu wa makala zetu hizi.

Ufafanuzi

WITO KWA WAISLAMU KUUENDEA UKWELI (SEHEMU YA KWANZA)

WITO KWA WAISLAMU KUUENDEA UKWELI (SEHEMU YA KWANZA) WITO KWA WAISLAMU KUUENDEA UKWELI UTANGULIZI Tofauti kubwa iliyopo baina ya Waislamu wa Kishia na Waislamu wa Kisunni ni juu ya imani ya Ukhalifa na Uimamu baada ya kuondoka kwa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w). Sisi waislamu wa Kishia tunaamini kuwa Imam Ali bin Abi Talib (a.s) ni khalifa na Imam wa kwanza baada ya Mtume (s.a.w.w.) ambapo ndugu zetu Waislamu wa Kisunni wanaamini kwamba Seyidina Abubakar (r.a.) alikuwa ni khalifa wa kwanza. Ingawa kuna tofauti nyingine ndogo ndogo zilizopo baina ya madhehebu makubwa ya Uislamu (Shia na Sunni) kwa mfano katika sheria (Fiqh) kama vile kukunja mikono wakati wa kusali au kuinyoosha n.k. lakini hizi ni tofauti ndogo ndogo sana ambazo zinaweza hata kupatikana ndani ya madhehebu manne ya Kisunni (Imam Shafi, Maliki, Hanafi na Hanbali ). Masuala haya tutayajadili hapo baadaye InshaAllah. Ama Makala haya yanaeleza kwa kina kuwa mrithi wa haki wa Mtume (s.a.w.w.) baada yake ni nani na dalili zote zime tolewa kutoka vitabu vya Sahihi na vinavyo tegemewa na kurejewa. Hivyo nakuomba kuwa sambamba name mpaka tamati mwa msururu wa makala zetu hizi.

Ufafanuzi

MI’RAJ UN-NABII

MI’RAJ UN-NABII MI’RAJ UN-NABII Hakika yeye Allah swt ni mwenye kusikia (na ) Mwenye kuona. Umri wa Mtume Muhammad Mustafa bin ‘Abdullah s.a.w.w. ulikuwa ni miaka 52 ambao ni mwaka wa pili kabla ya Hijrah au ni mwaka 621 A.D. Huko Makka, tarehe 27 ya mwezi Rajab katika mwaka kumi na mbili wa Utume wake, wakati Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. baada ya sala zake za usiku katika nyumba ya binamu wake, binti wa Abu Talib a.s. aitwae ‘Umma Hani na ambapo wote waliokuwa nyumbani walikuwa wamelala, mara Malaika Jibraili a.s. alitokezea na kuja kwake na kumchukua hadi Al-Ka’aba Tukufu huku akiwa amemwendesha Farasi mzuri, mwenye uso kama wa Kibinadamu mwenye mabawa meupe, aliyeitwa Buraq na limwelekeza hadi huko Jerusalemu ambako wao waliutembelea Msikiti. Baada ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuongoza sala ya Mitume iliyokuwa imemtangulia, yeye tena alipanda Farasi wake na alichukuliwa hadi Jannat ( Peponi ) na vile vile kuyaona yale matisho ya Jahannam ( Motoni ). Miongoni mwa zile Nuru za Hidaya za kudumu alizopata kutoka kwa Allah swt, alipewa mafundisho na maamrisho mapya na ile amri ya kusali sala tano za kila siku kwa ajili ya ‘Ummah wake, yeye aliliona jina lake pamoja na jina la Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. likiwa limeandikwa katika Kalimah: ‘Hakuna mungu mwingine illa Allah swt na Muhammad ni Mtume Wake na ‘Ali ibn Abi Talib ni Khalifa baada yake.’ Baada ya kuonyeshwa hayo yote yaliyo kuwemo Jannat ( Peponi ), na Jahannam (Motoni) basi Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alirudishwa hapo nyumbani mwake, alitambua kuwa kuweko kwake nje kulikuwa ni kitambo tu. Huu usiku wa safari unatambuliwa kama Lailat-al-Mi’raj au Usiku wa Mi’raj ambavyo vile vile imelezwavyo katika Qur’an Tukufu, Surah Bani – Israil, 17, Ayah:1 Kwa jina la Allah swt Mwingi wa Rehema na Ne’ema. “Utukufu ni wake Yeye ambaye alimpeleka Mja wake usiku (mmoja tu ) kutoka Msikiti Mtukufu (wa Makka) mpaka Msikiti wa mbali (wa Baytul Mugaddas-Falastini) ambao (tumeubariki na ) tumevibariki vilivyoko pembezoni mwake. (Tulimpeleka hivyo) ili tumwonyeshe baadhi ya Alama zetu.

Ufafanuzi

BWANA DHUL-QARNAIN

BWANA DHUL-QARNAIN BWANA DHUL-QARNAIN Bwana Dhulqarnain alikuwa akiitwa Ayash. Na yeye alikuwa ndiye Mfalme wa kwanza baada ya Mtume Nuh a.s., wengi wa watu wanadhani kuwa yeye ndiye Alexandria wa Kirumi lakini haya si kweli kama vile tunavyopata maelezo kutoka riwaya mbalimbali, vile vile wengi wanauliza iwapo Bwana Dhulqarnain alikuwa ni Mtume? Kwa hivyo jibu sahihi ni kwamba Bwana Dhulqarnain yeye hakuwa mtume bali alikuwa mja mwema wa Allah swt . Allah swt anasema katika Quran, Sura Al-Kahf, 18, Ayah 83 - 98. “Wanakuuliza khabari za Dhul-Qarnain, Waambie: Nitakusimulieni baadhi ya hadith yake. Sisi tulimtilia nguvu katika ardhi na tukampa njia za kila kitu Hata alipo fika machwea-jua aliliona linatua katika chemchem yenye matope mausi. Na hapo akawakuta watu. Tukasema: Ewe Dhul-Qarnaini ! Ama uwaadhibu au watwae kwa wema. Akasema: Ama aliye dhulumu basi tutamuadhibu, na kisha atarudishwa kwa Allah swt wake Mlezi amuadhibu adhabu isiyo julikana. Na ama aliye amini na akatenda mema basi atapata malipo mazuri. Nasi tutamwambia lilio jepesi katika amri yetu. Kisha akaifuata njia. Hata alipofika katikati ya milima miwili, alikuta nyuma yake watu ambao waliweza kwa shida kufahamu neno (wanaloambiwa). Wakasema:“Ewe Dhulqarnain! Hakika Yajuj na Majuj wanafanya uharibifu katika ardhi.Basi je, tukupe ujira ili utie baina yetu na baina yao kizuizi?” Akasema:“Yale ambayo Allah swt amenimakinishia ni bora (kuliko ujira wenu.Nitakufanyieni bure);Lakini nisaidieni kwa nguvu zenu. Nitaweka baina yenu na baina yao kizuizi chenye imara.” Nileteeni vipande vya chuma.” Hata alipoijaza nafasi iliyo katikati ya milima miwili,alisema:“Pulizeni”mpaka alipokifanya (kile chuma) kuwa moto,alisema “Nileteeni shaba iliyoyayuka niimwage juu yake.” Hivyo (Yajuj na Majuj) hawakuweza kuukwea wala hawakuweza kuutoboa. Akasema:“Hili ni rehema itokayo kwa Allah swt . Na itakapofika ahadi ya Allah swt ya kufika Qayama, atauvunjavunja. Na ahadi ya Allah swt ni kweli tu.” Je ni kwa nini akaitwa Dhulqarnain ? Zipo sababu nyingi zinazopatikana za kuitwa kwake Dhulqarnain kwa sababu mojawapo ni kwamba yeye ncha zote za dunia Mashariki mpaka Magharibi alikuwa anaendesha hukumu yake, alikuwa ameishinda, na Allah swt alimpa uwezo juu ya Nuru na Kiza (Dhulmat) na ndio hii sababu moja kubwa ya kupata jina hili la Dhulqarnain.

Ufafanuzi

WATU WA PANGONI (KAHF)

WATU WA PANGONI (KAHF) WATU WA PANGONI (KAHF) Allah swt anatuambia katika Qur'an Tukufu, Sura Al Kahf, 18, ayah 9-14: Bali unadhani ya kwamba wale watu wa Pangoni na Maandishi walikuwa ni ajabu miongoni mwa ishara zetu ? Vijana hao walipo kimbilia kwenye pango walisema: Allah swt wetu Mlezi ! Tupe rehema itokayo kwako, na tutengenezee uwongofu katika jambo letu. Tukayaziba masikio yao kuwalaza humo pangoni kwa muda wa miaka kadhaa wa kadhaa. Kisha tukawazindua ili tujue ni lipi katika makundi mawili lilio hisabu sawa muda walio kaa. Sisi tunakusimulia khabari zao kwa kweli. Hakika wao walikuwa ni vijana walio mwamini Allah swt wao Mlezi. Na Sisi tukawazidisha uwongofu. Na tukazitia nguvu nyoyo zao walipo simama na wakasema: Allah swt wetu Mlezi ni Allah swt Mlezi wa mbingu na ardhi. Hatutamwita mwenginewe kabisa badala yake kuwa ni mungu. Hivyo itakuwa tumesema jambo la kuvuka mpaka.

Ufafanuzi

WATU WA TEMBO ( AS-HAB-I-FIIL )

WATU WA TEMBO ( AS-HAB-I-FIIL ) WATU WA TEMBO ( AS-HAB-I-FIIL ) Najjashi (Negus), alikuwa ni Mfalme wa Abisynnia ambaye alijichukulia jukumu la kueneza Ukristo na alifanya kila jitihada alizoziweza ili aweze kuirudisha vile ilivyo kuwa miongoni mwa watu wake na ikafuatwa na wingi wa raia zake. Alipopata habari kuwa watu kutoka sehemu mbalimbali za Ulimwenguni walikuwa wakienda Makka kuhiji huko Al Ka’abah Tukufu, basi naye aliamua kuvumbua jambo ambalo litawavutia watu kutokwenda Makkah kuizuru Al Ka’abah Tukufu na badala yake waende nchini mwake. Hivyo, basi yeye alijenga Kanisa moja kubwa katika Sana’, mji uliopo Yemen na kuipamba vizuri kwa kila kitu cha kuvutia zikiwemo mazulia, mapazia n.k. Kwa hakika lilikuwa ni jambo la kuvutia sana kwa mtu yeyote aliye angalia kwa kuona ufundi wa kistadi uliotumika katika ujenzi wake. Najjashi alifikiria kuwa baada ya kuona maajabu ya ujenzi huo wa Kanisa watu hawatakwenda tena Makkah kuzuru Al-Ka’abah Tukufu na badala yake watakwenda Sana’ kuzuru hilo Kanisa, na vile vile watu wa Makkah pia watakuja kuhiji hapo Sana’, Yemen. Pamoja na hayo yote watu wa Makkah hawakujali chochote. Vile vile sio kwamba ni watu wa Yemen na Abisynnia tu walioisahau Makkah, laa, wao kama kawaida yao waliendelea na safari zao za kwenda mji mtukufu wa Makkah na kuzuru Al Ka’abah Tukufu.

Ufafanuzi

PEPO ( JANNAT ) YA SHADDAD

PEPO ( JANNAT ) YA SHADDAD PEPO ( JANNAT ) YA SHADDAD JE SHADDAD NI NANI … Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alipokwenda katika Mi’raj alikutana na Malakul Mauti. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwuliza : “Je ni wakatigani ambapo wewe kwa hakika ulisikitika katika kutoa roho ya wanaadamu ?” Kwa hayo Malakul Maut akajibu : “Ewe Mtume wa Allah swt ! Zipo nyakati mbili tu ambapo mimi kwa hakika nilisikitika mno wakati wa kutoa Roho nazo ni, kwanza kulikuwa na jahazi moja iliyokuwa baharini ikiwa na wasafiri walikuwamo humo, na Allah swt aliniamrisha kuipindua jahazi hiyo na kuzitoa roho zote za wasafiri waliokuwamo isipokuwa mwanamke mmoja aliyekuwa ana mimba. Nami nikafanya hivyo hivyo nilivyoamrishwa. Mwanamke huyo aliweza kuelea kwa msaada wa ubao alioupata wakati wa kuzama. Wakati mwanamke huyo anaelea, alimzaa mtoto, ndiye aliyeitwa Shaddad. Alipomzaa mtoto huyo, mama huyo akafa( hapa niliposikitika wakati wa kuitoa roho ya mama huyu) na mtoto akabakia peke yake majini juu ya ubao, ambapo kwa amri za Allah swt aliweza kufika salama u salimini hadi nchi kavu (kisiwa kilichokuwapo karibu).Hapo Allah swt alimwamrisha Swala mmoja kumnyonyehsa maziwa mtoto huyo kwa muda usipungua miaka miwili. Ulifika wakati ambapo kulitokezea wasafiri kisiwani hapo na walipomwona mtoto huyo na alivyokuwa mzuri, walishauriana kumpelekea mfalme kwani alikuwa hana mtoto. Na walifanya hivyo, na Mfalme alimpenda mtoto huyo na kumchukua kama mtoto wake ….. Mtume Adam a.s. tangu aje duniani humu ilipofika miaka 2647 ndipo Mtume Hud a.s. alipozaliwa na kulipofika miaka 2700 ndipo Shaddad bin ‘Aad alipokuwa Mfalme na ni Mfalme huyu ambaye ametengeneza mfano wa Jannat (Peponi) yenye bustani za kupendeza humu duniani. Humu yeye alijenga majumba ya kuvutia na kupendeza, na aliweka wajakazi warembo:wasichana kwa wavulana kutoka sehemu mbalimbali humu duniani ambao kwa hakika waliifanya pepo yake ipendeze na kuvutia. JE KUNA MTU ALIYEBAHATIKA KUIONA PEPO HIYO? Katika zama za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuna mtu mmoja aitwaye ‘Bwana ‘Abdullah bin Kalaba ndiye aliyebahatika kuiona. Na hapa tunaelezea vile inavyopatikana katika vitabu vya historia. WASEMAVYO WANAHISTORIA “Katika Bara la Uarabuni kulikuwa na Shakhsiyyah moja aliyekuwa akiitwa ‘Bwana ‘Abdullah bin Kalaba ambaye alikuwa na Ngamia wake aliyekuwa ametoroka na kupotelea katika majangwa ya ‘Aden na katika kumtafuta huyo ngamia wake alifika katika majangwa ambapo aliuona mji mmoja ukivutia. Mji huo ulikuwa umezungukwa na ngome. Ndani ya mji huo kulikuwa na majumba ya kupendeza na yenye kuvutia sana. Na juu ya kila jengo kulikuwa na bendera zilizokuwa zikipepea. Yeye anasema kuwa alifanikiwa kuingia ndani ya mji huo. ‘BWANA ‘ABDULLAH ANAELEZEA ALIVYIONA PEPO YA SAHADDAD “Mimi niliteremka chini kutokea ngamia wangu na nikamfunga katika nguzo mojawapo. Nikauchukua upanga wangu nikawa ndani ya ngome hiyo. Milango yake ilikuwa ni madhubuti na ya kupendeza sana kiasi kwamba kamwe nilikuwa sijawahi kuona kabla ya hapo. Milango ilikuwa imetengenezwa kwa ubao mzuri sana na manukato mazuri sana na ufundi uliotumika ulikuwa ni wa utalaamu wa hali ya juu sana na juu ya mbao zake kulikuwa kumepachikwa Yaqut za rangi mbalimbali. Ukiangalia chumba kimoja utakisahau chumba cha pili katika ngome hiyo. Madirisha yake yalikuwa yametengenezwa kwa dhahabu na shaba, ukiona milango , kuta na sakafu yake ilivyokuwa iking’ara na kwa hakika kila kitu humo utakachokiona utastaajabika mno.” ‘Bwana ‘Abdullah alipoyaangalia majengo hayo yaliyokuwa mazuri na yenye kuvutia alishangazwa kuona kuwa hapakuwapo na mtu yeyote, na alijaribu kusonga mbele akaona miti ambayo imejaa maua ikiwa inapeperushwa na upepo mzuri sana. Na chini mwake kulikuwa na mito iliyokuwa ikitiririsha maji. Kwa hakika hii ndiyo ile Jannat ambayo Allah swt ametupa habari zake. Basi mimi kwa hayo nilimshukuru Allah swt kwa kunijaalia bahati hiyo. Mimi niliokota vipande vidogo vidogo vyenye harufu nzuri mno ya Mishk na Ambar. Na hapo nikawaza kuwa sasa itabidi nitoke zangu nje kwa haraka. Nilipofika katika mji wa Yemen huko niliwasimulia watu kuhusu Jannat hii. Kwa hakika nilishangazwa kuona kuwa habari zangu hizi zilienea kila mahali kama upepo.

Ufafanuzi

MALAIKA: HARUT NA MARUT

MALAIKA: HARUT NA MARUT MALAIKA: HARUT NA MARUT Imepokelewa riwaya kutoka kwa Imam Muhammad al-Baquir a.s. kuwa: Baada ya kifo cha Mtume Sulayman bin Daud a.s., Ibilisi alitengeneza uchawi na kuuviringa na nyuma yake aliandika kuwa mzigo huu umetengenezwa na Asif bin Barkhiyyah kwa ajili ya ufalme wa Mtume Suleyman, na kwamba imetolewa kutoka hazina ya ilimu. Na kwa nguvu zake kila jambo linawezekana. Na baada ya hapo aliifukia chini ya kiti cha Mtume Sulayman a.s. Na baadaye aliifukua chini ya kiti hicho na kuidhihirisha mbele ya watu wa zama hizo. Kwa kuyaona hayo, wale waliokuwa Makafiri walianza kusema kuwa Mtume Suleyman a.s. aliweza kuwatawala kwa uchawi lakini wale waliokuwa Mumin walikuwa wakisema kuwa Mtume Sulayman a.s. alikuwa ni Mtume wa Allah swt na mwenye taqwa. Allah swt anatuambia kuwa ni Sheitani ndiye asemaye kuwa Mtume Suleyman a.s. alikuwa ni mchawi. Na jambo hilo ndilo walilolifuata na kuliamini Mayahudi. Lakini Mtume Suleyman a.s. kamwe hakufanya tendo lolote la kukufuru au la ushirikina hivyo kamwe hawezi kuwa mchawi. Wale wanaohalalisha uchawi ni makafiri kwa sababu Masheitani walikuwa wakifanya uchawi na kuwafundisha watu uchawi na ushirikina. Baada ya kupita zama za Mtune Nuh a.s., kulikuja zama moja ambamo wakazi wake walikuwa wakijishughulisha mno na mambo ya uchawi na ushirikina, kwa sababu ya kufuata imani hizo zilizopotofu, kulikuwa kukitendeka matendo maovu kabisa. Hivyo wakazi walikuwa wameupuuzia Uislamu, na kwa hayo Allah swt aliwatuma malaika wawili waliokuwa wakiitwa Harut na Marut, ambao walitumwa katika mji uitwao Babul, katika maumbile ya mwanadamu ili waweze kuwazuia wanadamu wasiendelee na uchawi na ushirikina uliokuwa umepindukia kiasi. Malaika hao walitii amri ya Allah swt na walimwelezea Mtume wa zama hizo kuwa uwafundishe mambo fulani fulani wakazi wako ili waweze kujiepusha na uchawi na ushirikina huo uliokuwa umewapotosha kabisa. Basi Mtume huyo aliwaambia watu wake kuwa wajifunze mafunzo hayo makhsusi ili waweze kujiepushe na uchawi na kamwe wasiwatendee chochote wenzao. Allah swt anatuambia kuwa katika mji huo wa Babul kulikuwapo na Mayahudi ambao wao kwa hakika walikuwa wakitenda kinyume na kile walichokuwa wakiambiwa na Mtume huyo, yaani wao badala ya kuutokomeza uchawi, wao ndio wakawa waabudu wa uchawi na wakawa wakifanya uchawi. Malaika wakawaambia sisi tunawafundisheni haya kwa ajili ya kutaka kuwajaribu na kuwajua wale waliona imani ya kurudi kwa Allah swt na hivyo kujiepusha na uchawi. Na kutaka kuwatambua wale walioasi na kutumia ilimu hii kwa ajili ya kuwadhuru wengine.

Ufafanuzi

MAISHA YA MTUME SALEH

MAISHA YA MTUME SALEH MAISHA YA MTUME SALEH Mtume Saleh a.s. aliitwa: Mtume Saleh a.s. bin Abud bin Asif bin Nasikh bin Abud bin Hadir bin Thamud bin Amir bin Sam bin Nuh. Kabila lake lilikuwa likiishi mipaka ya Kusini ya Syria katika milki iliyokuwa ikijulikana kama Al-hijr au Al-Hajar na ilijulikana kama Wadiul-Qura. Mtume Saleh a.s. alikuja baada ya Mtume Hud a.s. na alitokana na kizazi cha tisa cha Mtume Nuh a.s. URITHI Baada ya kuangamiza Allah swt Qaumu A'ad ambao hawakuyasikiliza maneno ya Mtume wao Hud a.s. na baada ya kufa hao wote ikabaki ardhi yao bila majumba wala wakazi wala mimea hata wanyama na baada ya haya yote Allah swt aliirithisha ardhi yao kwa Qaum nyingine nao ni Qaum Thamud. Wakaja Qaumu Thamud mahali pakawa Qaum-u-‘Aad Allah swt aliwaneemesha neema nyingi kuliko Qaum ‘Aad. Walijenga Qaum Thamud majumba kati ya majabali na wakalima mabustani na makonde na wakatoboa mito lakini pamoja na masikitiko makubwa hazikuwa akili zoa zina maendeleo kuliko Qaum iliyotangulia. Ni hao hao ambao waliabudu masanamu na mawe na wakadhani kwamba neema yao haitoondoka na wala haitatoweka. UJUMBE Na mbele ya utakafiri huu na ujinga Allah swt alimtuma kwao mwanamme miongoni mwao anayeitwa Mtume Saleh a.s. na yeye miongoni mwa watukufu wao na mwenye akili katika wao ambaye alimuamini Allah swt wake na Allah swt alimchagua yeye ili awaongoe hawa Majahili waliopotea akawalingania wao kwenye ibada ya Allah swt na akatilia mkazo na akawaimiza wao juu ya Tawhid yaani kumpwekesha Allah swt na kuacha kumshirikisha Yeye ni Yeye ambaye aliwaumba wao na akawaumbia wao ardhi na akawapa wao miongoni mwa fadhila Zake na neema Zake kisha akawakataza wao kuabudia masanamu ambayo wameyatengeneza wao wenyewe. Kwani hayo masanamu hayadhuru wala hayanufaishi chochote na wala hayamtoshelezi mtu kutoka kwa Allah swt chochote kisha akawakumbusha wao kwamba yeye ni miongoni mwa wao na yeye anapenda kuwanufaisha wao na wanapojipatia maslaha yao na akawaamrisha wao wamtake msamaha Allah swt na watubu kwake Yeye kwani yeye ni mwenye kusikia na mwenye kujibu na anakubali toba kwa yule mwenye kutaka msamaha kwake.

Ufafanuzi

MAISHA YA MTUME LUT

MAISHA YA MTUME LUT MAISHA YA MTUME LUT Mtume Lut a.s. alikuwa ni ndugu wa kijamaa wa Mtume Ibrahim a.s. yaani mtoto wa mamake mdogo na dada yake Mtume Lut a.s. aliolewa na Mtume Ibrahim a.s. Tendo ovu kabisa lililokuwa katika ukoo wa Mtume Lut a.s. ni tendo la Ulawiti 1 TABIA MBAYA Ulizidi ufisadi katika mji mmoja miongoni mwa miji ya zamani kiasi kwamba atakapoona mtu ufisadi unatendwa na mmoja kati yao basi hakatazwi na mtu mwingine atakapo shuhudia heri inafanywa na ndugu yake basi humkemea mpaka aache heri anayoifanya. Kila mtu katika kijiji hicho alikuwa katika upotevu na uovu na ujinga, hawasikii wala hawasikilizi ilikuwa ni mamoja kwao apatikane mtu wa kuwapa mawaidha wao au mtu wa kuwanasihi wao kulikuwa hakuna tofauti yoyote. Walikuwa ni watu waovu na wabaya zaidi na wenye tabia mbaya miongoni mwa watu, uhai wao (ulikuwa ni khiana na tabia mbaya) na wote hao wakati huo walikuwa ni wenye tabia mbaya sana na nia mbaya. Lakini unaonaje ewe msomaji je walijizuia na maovu yao haya au walizidi katika upotevu na ufijari na madhambi ? KUENEA MAMBO YA HARAMU Ilikuwa kama kwamba nafsi zao hazikutosheka na kule kusema uongo na kuwa na tabia mbaya na ghadr na mengineyo mengi, wakasababisha na kuleta mambo ya unyama ambayo hakutangulia kufanya yeyote kabla yao. Je ni mambo gani hayo? Hakika waliacha mambo aliyoyahalalisha Allah swt kwao kwa wanawake na wakawa hawaoi wanawake ! Wakawaacha wake zao na kuanza maovu ya kuingiliana na wanaume wenzao. Jambo ambalo Allah swt aliliharamisha kabisa. Na laiti wao wangesitiri haya maovu au wakajaribu kujiepusha kutoka katika maovu haya au kujiweka mbali nayo ingelikuwa afadhali lakini wao walijitumbukiza katika mambo hayo na wakawa wanayatangaza wazi wazi mpaka ukaenea ufisadi na kukaenea mambo ya haramu na zikawa tabia zao mbaya ni rahisi kiasi kwamba zikawa zimefikia daraja kubwa sana na yote hayo yalikuwa ni madhambi na ufisadi wala hawezi mtu yeyote kuyafanya wala kufikiria binaadamu au kupiga picha ya binaadamu katika akili yake.

Ufafanuzi

URITHI WA IMAM ALI (A.S.)

URITHI WA IMAM ALI (A.S.) URITHI WA IMAM ALI (A.S.) MUHTSARI Qur’ani imetilia umuhimu mambo yote yanayohusu maisha na mus- takabali wa mwanadamu, hivyo Mtume (s.a.w.w.) na kizazi chake nao wakafuata njia hiyo ya Qur’ani, wakisimama imara kutafsiri makusudio ya Qur’ani na kubainisha ishara na alama zake. Suala la wema na uovu ni suala la mwanzo kabisa walilotilia umuhimu na kuliashiria, hivyo wakafafanua kipimo cha wema na uovu huku wakifafanua alama na mwonekano wa mtu mwema na mtu mwovu. Waligusia vinavyosababisha wema na uovu, hivyo kwa maelezo hayo wakatoa mfumo kamili wa ukamilifu wa mwanadamu katika maisha.

Ufafanuzi

SIFA ZA IMAM ALI (A.S.) NA MWONEKANO WAKE

SIFA ZA IMAM ALI (A.S.) NA MWONEKANO WAKE SIFA ZA IMAM ALI (A.S.) NA MWONEKANO WAKE URAFIKI MUHTASARI Huruma ya kutekeleza ahadi ni huruma ya kina kwa Imam Ali (a.s.), huruma ambayo ilikuwa imejenga moyo wake huku ikidhihirika katika matendo na mienendo yake, hiyo ni hata mbele ya adui yake. Akitarajia kuwaongoza waliopotea na kuwarudisha katika njia sahihi wale waliokengeuka. Ama kuhusu uadilifu ni kuwa laiti kama ungejitokeza kwa mtu basi angekuwa ni Ali bin Abu Talib (a.s.) na wala si mwingine, kwani alikuwa ni nguvu kali ya kutekeleza uadilifu kwa watu wote. Alikuwa ni mjuzi anayemjua mwanadamu, jamii na kanuni za Mwenyezi Mungu, hivyo kidole chake hakikuacha haki na uadilifu kwa maana yote ya uadilifu na vipengele vyake vyote katika maisha. Kila kitu katika utu wa Imam Ali (a.s.) kimekamilika na chenye muundo mmoja, kwani hatupati tofauti yoyote katika sifa zake na mwonekano halisi wa utu wake, hivyo akastahiki kuwa alama kati ya alama za utukufu wa Mwenyezi Mungu na mfano bora kwa wanadamu wote katika kumtii Mwenyezi Mungu, na kujenga imani ya Mwenyezi Mungu, kifikira, kimwenendo na kihuruma, hivyo yeye ni mfano mwema wa mtawala shupavu na mtawaliwa mwaminifu mtiifu, na yeye ni sura halisi ya nia njema, utiifu, ibada na nguvu ya haki. Imam Ali (a.s.) alikuwa mkarimu sana kuliko watu wote huku akiwa na mkono mkunjufu. Alikuwa na ukarimu wa hali ya juu huku akijitofautisha kwa kuwa na moyo salama usiokuwa na chuki hata kwa maadui zake, hivyo hakuridhia jambo mbadala lichukue nafasi ya ukweli, kikauli au kivitendo. Sifa zote hizi ziliungana na sifa ya kujiamini mbele ya haki kwa kiwango cha juu. Mwana wa Abu Talib alijitofautisha na wengine kwa jihadi iliyoende lea katika vipindi vyote vya maisha yake yote huku akiwa na maadili bora na mtazamo wa ndani wa makini uliyonyooka, akiwa na ubainifu safi na utambuzi wa haraka na nguvu za kupambana, hivyo akawa ni kiongozi bora na mfano wa juu baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) katika kila sifa bora.

Ufafanuzi

MWONEKANO WA UTU WA IMAM ALI BIN ABU TALIB (A.S.)

MWONEKANO WA UTU WA IMAM ALI BIN ABU TALIB (A.S.) MWONEKANO WA UTU WA IMAM ALI BIN ABU TALIB (A.S.) MUHTASARI Imam Ali (a.s.) alijitenga kwa kuwa na sifa mahsusi ambazo zilimtofautisha na maswahaba wengine, zikamwajibisha awashinde wote waliotaka kulingana nae miongoni mwa maswahaba na wasiokuwa maswahaba. Aya za Qur’ani zimejaa fadhila hizi za pekee huku maelezo ya Mtume (s.a.w.w.) yakiashiria sifa hizi zilizomtofautisha Ali (a.s.) na wengine. Ushahidi wa maswahaba na waliokuja baada ya maswahaba unaashiria undani wa fadhila za Ali (a.s.) ndani ya umma huu japokuwa watu wengi hawakufuata uimamu wa mtu huyu mtukufu.

Ufafanuzi

DONDOO ZA MAISHA YA MBORA WA MAWASII

DONDOO ZA MAISHA YA MBORA WA MAWASII DONDOO ZA MAISHA YA MBORA WA MAWASII KIONGOZI WA WAUMINI ALI BIN ABU TALIB MUHTASARI Ali bin Abu Talib (a.s.) alitokana na asili ile ile aliyotokana nayo Mtume (s.a.w.w.) hivyo nasaba yake na nasaba ya Mtume (s.a.w.w.) ni moja. Ali (a.s.) alitofautiana na maswahaba wengine kwani hakuna shirki yoyote iliyomuingia. Kisha akawa ni mtu mahsusi kwa Mtume (s.a.w.w.) hivyo akawa akimfunza mafunzo yatokanayo na hekima za Mwenyezi Mungu na elimu ya Mola Wake, jambo ambalo hakulipata swahaba mwingine yeyote. Ali (a.s.) alidhihirisha utiifu na ufuataji kamilifu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (s.a.w.w.), akajipamba kwa maadili mazuri, akajitolea nafsi na kila lenye thamani kwa ajili ya itikadi ya Uislamu. Mwenyezi Mungu alimteua awe wasii wa Mtume Wake (s.a.w.w.) hivyo akasimamia jukumu la uwasii kwa ukamilifu mpaka adui akakiri hilo kabla ya rafiki. Imam Ali (a.s.) alibeba majina na lakabu nzuri ambazo zinaonyesha jinsi alivyoshikamana sana na Mwenyezi Mungu na alivyokuwa na itikadi salama ya Mwenyezi Mungu na maadili bora mazuri.

Ufafanuzi

URITHI WA MBORA WA MITUME

URITHI WA MBORA WA MITUME URITHI WA MBORA WA MITUME AKILI NA UKAMILIFU WA MWANADAMU MUHTASARI Mtume (s.a.w.w.) ni mfano hai wa ukamilifu wa mwanadamu. Pia urithi wake ndio wenye thamani baada ya Qur’ani. Hakika yeye alikunywa toka chemchemu ya ufunuo mpaka akabubujisha ukamili- fu wake kwa wanadamu kwa kiwango kinachotosheleza kuwapeleka wanadamu mbele upande wa ukamilifu na kuwafikisha kileleni mwa ukamilifu. Tumechagua mifano ya ufasaha wake na semi zake fasihi kuhusu akili, elimu na njia ya kufikia wema na ukamilifu. Tumechagua kwa kiwango ambacho kitawaangazia wenye kufuata njia yake, hivyo wale watafuta ukweli hawatojizuia kutumia madhumuni ya semi hizo.

Ufafanuzi

TABIA NA MWONEKANO WA HITIMISHO LA MANABII 3

TABIA NA MWONEKANO WA HITIMISHO LA MANABII 3 TABIA NA MWONEKANO WA HITIMISHO LA MANABII 3 UKARIMU MUHTASARI Hakika Mtume (s.a.w.w.) alikuwa mkarimu sana, hivyo alikuwa akieneza upendo, ukarimu, wema na mali kwa watu wote, huku akitoa msamaha, huruma na ulaini kwao. Ili awaokoe toka kwenye ujinga wao na apate kuwaunganisha pamoja wawe kitu kimoja. Mtume (s.a.w.w.) alikuwa anaishi na waislam kama mmoja wao huku haya zikimtukuza kwa kumpa haiba na heshima, huku unyenyekevu ukimzidishia heshima na utukufu. Hivyo alikuwa akiwahurumia wadogo na kuwaheshimu wakubwa. Alikuwa akisikia ushauri wa mnasihi ilihali yeye ni mwenye akili zitokazo mbinguni kwa njia ya ufunuo.

Ufafanuzi

TABIA NA MWONEKANO WA HITIMISHO LA MANABII 2

TABIA NA MWONEKANO WA HITIMISHO LA MANABII 2 TABIA NA MWONEKANO WA HITIMISHO LA MANABII 2 MSOMI ASIYEWAHI KUSOMA WALA KUANDIKA Muhtasari Mtume wa Mwenyezi Mungu Muhammad bin Abdullah hakujifunza mikononi mwa mwanadamu yeyote, lakini alikuja na Kitabu cha kie- limu na kimaarifa cha kimataifa ambacho kimewataka wanadamu wote katika zama zote walete mfano wake. Kupitia Kitabu hicho Mtume (s.a.w.w.) aliweza kumtoa mwanadamu toka jamii ya kijinga mpaka jamii ya kielimu iliyokamilika yenye kustaarabika, huku akihimiza usiku na mchana juu ya utafutaji wa elimu na maarifa mbalimbali. Hivyo kupitia Kitabu hicho aliasisi dola kubwa na kujenga ustaarabu wa pekee ambao mfano wake hau- jashuhudiwa na mwanadamu. Mtume (s.a.w.w.) alibeba maana kamili ya ibada kwa Mwenyezi Mungu Muumba, hivyo alikuwa na mahusiano ya karibu sana na Mola Wake Mtukufu, mahusiano ambayo yalitokana na ujuzi, mapenzi, utashi, na moyo mkunjufu, hivyo akawa ni kiigizo chema katika swala yake, funga, dua na uombaji msamaha, kiigizo ambacho kinamchorea mwanadamu njia ya ukamilifu kuelekea kwa Muumba, Mjuzi. Mtume (s.a.w.w.) alianza harakati akiwa amebeba jukumu kubwa huku akimtegemea Mwenyezi Mungu katika kila harakati na kila jambo, hivyo akawa ni shujaa, jasiri na mkakamavu katika kulingania njia ya Mwenyezi Mungu. Mtume (s.a.w.w.) aliishi mbali na ladha za dunia na starehe zake, hivyo alikuwa ni sehemu ya mafakiri na masikini, akishirikiana nao katika taabu zao huku akitarajia rehema za Mola Wake, mnyenyekevu Kwake, mwenye kujitenga na kila ujeuri utokanao na starehe za dunia na furaha za mapambo yake.

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini