Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

Tarehe

MCHANGO WA MAZINGIRA SAFI KATIKA MALEZI

MCHANGO WA MAZINGIRA SAFI KATIKA MALEZI

MCHANGO WA MAZINGIRA SAFI KATIKA MALEZI MUHTASARI Hakika Mwenyezi Mungu aliweka umuhimu maalumu kwa manabii wake, hivyo akawezesha wazaliwe toka ndani ya familia takasifu ili wawe na uwezo wa kuwasafisha watu dhidi ya shirki. Hivyo ndivyo alivyomteua nabii Muhammad (s.a.w.w.). Hakika alihama toka mifupa ya migongo mitakasifu yenye imani na toka mapaja ya utawa mpaka dunia ilipopata sharafu kwa kuzaliwa kwake. Familia ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.) ilikuwa ni familia na damu yenye kuheshimika, kwani yeye ametokana na nabii Ibrahim (a.s.). Pia ilikuwa ikijihusisha na kulinda Haram ya Makka na kuitetea dhidi ya maadui. Babu wa Mtume Abdul Muttalib aliishi zama ambazo ujumbe wa Mwenyezi Mungu ulikuwa umetoweka huku nguvu za shirki zikiwa zimedhihiri na ufisadi na dhuluma vikishamiri, lakini pamoja na hayo yote alikuwa ni mwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu huku akilingania maadili mema, na njia hiyo ndiyo waliyopita watoto wake. Abdul Muttalib alimjali sana mwanae Abdullah, hivyo akamwozesha mwanamke bora toka familia na damu yenye heshima. Lakini matak- wa ya Mwenyezi Mungu yalitaka Abdullah afariki kabla ya kuzaliwa mwanae Muhammad (s.a.w.w.).

Ufafanuzi

MUHAMMAD BIN ABDULLAH (S.A.W.W.) NI UTABIRI WA MANABII (A.S.)

MUHAMMAD BIN ABDULLAH (S.A.W.W.) NI UTABIRI WA MANABII (A.S.) MUHAMMAD BIN ABDULLAH (S.A.W.W.) NI UTABIRI WA MANABII (A.S.) MUHTASARI Matukio ya kihistoria yanaonyesha kuwa mwenendo wa manabii ni wa kiukamilifu wenye lengo moja na njia moja. Pia mwenendo wa Mwenyezi Mungu ni manabii waliyopo kuwabashiri watakaochukua nafasi zao katika unabii. Ikiwa ni huruma toka kwa Mwenyezi Mungu dhidi ya mzigo walio nao wanadamu katika kuamini na kukubali na ni kumrahisishia nabii anayefuata kazi ya uhubiri na ulinganio. Na kwa kuwa Uislamu na Mtume Muhammad vina umuhimu mkub- wa katika historia ya binadamu, na ukizingatia kuwa Uislamu ni dini inayohusu kila kitu na ndiyo dini ya mwisho huku Mtume (s.a.w.w.) akiwa ndiyo mtume wa mwisho, basi Uislamu huo ulibashiriwa tangu zamani na hilo limeelezwa na Qur’ani tukufu. Kuna habari zilizoenea kabla ya Mtume kukabidhiwa utume ambazo zilikuwa zimebeba wasifu kamili wa Mtume Muhammadin (s.a.w.w.) na mazingira yake, zikiwataka watu wamwamini na wajiepushe na upotovu kwa kumfuata yeye. Habari hizi zilisaidia baadhi ya Ahlul-Kitabu na wengineo kuamini dini ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.) bila ya kuomba muujiza wowote mahsusi.

Ufafanuzi

HATUA YA MWANZO KUELEKEA KWENYE MASOMO YA SERA NA HISTORIA YA UISLAMU

HATUA YA MWANZO KUELEKEA KWENYE MASOMO YA SERA NA HISTORIA YA UISLAMU MUHTASARI Sera ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na sera ya kizazi chake kitakasifu ni chanzo muhimu kati ya vyanzo vya maarifa na sheria ya kiislamu. Huzingatiwa pia kuwa ni nyenzo kati ya nyenzo za kufikia wema na mafanikio, kwa sababu kuwafuata wao ni mfano halisi wa kufuata njia ya Mwenyezi Mungu iliyonyooka. Historia ya kiislamu ndio historia ya Uislamu na ndio historia ya watetezi ambao walizama ndani na kujitoa muhanga kila dakika ya maisha yao katika njia ya Uislamu. Nao ni Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kizazi chake kitakasifu kilichotakasika dhidi ya kila aina ya uchafu na kila aina ya dosari. Qur’ani ndio chanzo muhimu cha historia na sera ya Mtume (s.a.w.w.) na historia ya kiislamu. Kwa ajili hiyo vyanzo vyote vingine vya sera na historia vinapimwa kwa Qur’ani, kwa sababu vyanzo vingine vimekosa sifa ya “kumdiriki Mtume (s.a.w.w.)”, “kudiriki yote, umakini, na kutoegemea” kwenye maslahi ya makundi na madhehebu ambayo yalizuka baada ya zama za Mtume (s.a.w.w.). Zama za Mtume wa mwisho (s.a.w.w.) huchukuliwa kama mwanzo wa zama za historia ya kiislamu kisha hufuatiwa na zama za Maimam wema (a.s.).

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini