1
KUA NA UHURU NA KUTOKUA
2. MATAKWA/MAPENZI MATAMANIO
Wale wanaounyanyua mkono wa itikadi kuwa mtu ana uhuru kamili katika matendo yake anaweza kuamua kadiri atakavyo, mfano majukumu aliyonayo mwanadamu, adhabu zitolewazo kwa wahalifu. Mambo yanayofanywa na jamii ili kuleta mabadiliko ya kihistoria misingi ya sayansi na teknologia yote hayo yanaonyesha kwamba binadamu yuko huru katika matendo.
Hali kadhalika suala la wajihu alionao mtu katika kutekeleza sheria za dini, ujio waMitume na suala la ufufuo na hukumu vyote hivyo bado vinaonyesha kwamba binadamu huyu yuko huru kabisa.
Itakuwa haina maana endapo Mwenyezi Mungu kwa upande mmoja akawa anawalazimu waja wake kufanya mambo halafu akataraji kuwahukumu au kuwazawadia, halitakuwa jambo la haki kwa muumba wa jambo tulifanyalo liwe amelipanga yeye kisha aje kutuhukumu kutokana na yale tuliyofanya kwa kulazimishwa na yeye.
Kama kila linalofanywa na mtu lina ridhaa, ukatili na maovu yote yanayotendeka katika jamii iwe ni kazi yake yeye Mwenyezi Mungu sifa ambazo ni kinyume kabisa. Kama kweli binadamu asingekuwa na uhuru katika mambo yake basi pasingekuwa na sababu ya kuwashutumu viongozi madhalimu wanyonyaji n.k.
Binadamu ana haki ya kulaumiwa au kusifiwa pale tu anapokuwa ana uhuru katika matendo yake vinginevyo sifa zote na lawama kwake hazina maana.
Wale wanaoshikilia msimamo huo wameenda mbali sana wamevuka mpaka kiasi kwamba wanaamini huo uhuru alionao mwanadamu hauna kikomo kwa maana nyingine Mungu hana uwezo wa kuzuia matendo ya binadamu kwa kifupi huo ndio msimamo wa wale wanaoamini kwamba binadamu yu huru.
Wale wanaosema kuwa ni asili tu na matokeo ya matakwa ya mwanadamu ndio vinavyopelekea kutokea kwa mambo mengi duniani wala vitu hivyo havina uhusiano na uwepo wa Mwenyezi Mungu hawa wanajaribu kupinga uwepo wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w)
. Kwa maana nyingine wanajaribu kumwekea Mwenyezi Mungu mwenza katika Uumbaji wake bila ya wao wenyewe kujua.
Kwa hakika kwamsimamo huo binadamu amekuja jikutaa amejiingiza katika itikadi ya ukafiri/ushirikina kukubali kwamba binadamu kabisa kabisa ana uhuru kamili usioweza kuingiliwa na kitu kingine hata Mwenyezi Mungu itakuwa kupunguza mamlaka ya Mwenyezi Mungu kwa viumbe vyake, wakati ukweli ni kuwa mamlaka aliyonayo Mwenyezi Mungu kwa ulimwengu hauna mipaka.
Wakati tunakubali kuwa kuna mazingira ambayo huwa na nafasi fulani katika mabadiliko ya Mwanadamu shari tukubali kuwa hata hayo mazingira yanauhusiano na Mwenyezi Mungu na lazima tukubali kuwa kama Mungu akitaka hata hayo mazingira yasingeweza kuwepo. Kama ilivyo kuwa viumbe wote hapa duniani hawana uhuru wa kuamua kuwepo au kutokuwepo kwao isipokuwa wote wanategemea Mwenyezi Mungu vivyo hivyo viumbe hivyo vinakosa nafasi ya kuwa ndio vyanzo. Mambo yatukiayo hapa duniani hivyo basi tunashawishika kuamini vitu vyote vipo chini ya Mwenyezi Mungu, si tu uwepo wake bali hata matendo yao.
Hatuwezi kulinganisha uhusiano wa Mwenyezi Mungu na viumbe vyake kuwa sawa na ule wa mwanasanaa na kazi yake, mfano mpaka akishapaka rangi sehemu basi ule uzuri wa rangi hautegemei tena mpakaji kwa sababu mpakaji aweza kuondoka na uzuri ukabakia. Kwa hiyo kuamini hivyo nisawa na kumshirikisha Mwenyezi Mungu.
Yoyote yule anayekanusha wajibu majukumu ya Mwenyezi Mungu katika mambo na matendo mbalimbali huyo atakuwa anamwekea Mwenyezi Mungu mipaka katika malaka yake na wale wanaoamini hivyo basi atajiona kuwa yeye hana hatia kwa maovu anayoweza kuwa awatendea wenzie hivyo itikadi kama hiyo ikitawala jamii Basi jamii hiyo haitakuwa na ustawi amani na utulivu.
Kinyume chake wale watu wanaoishi kwa kuamini kwamba Mwenyezi Mungu yupo na ni yeye ndiye mtawala wa kila kitu wataishi maisha bora na ya amani kwa sababu kila mmoja atahisi anawajibu wa kutimiza kwa yule aliyemleta hapa duniani ushahidi wa kuonyesha kwamba hana mshirika tazama Quran tukufu (17:111).
وَقُلِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي لَمْ يَتَّخِذْ وَلَدًا وَلَمْ يَكُن لَّهُ شَرِيكٌ فِي الْمُلْكِ وَلَمْ يَكُن لَّهُ وَلِيٌّ مِّنَ الذُّلِّ وَكَبِّرْهُ تَكْبِيرًا ﴿١١١﴾
"Na sema: Alhamdulillah, Himidi zote ni za Mwenyezi Mungu ambaye hana mwana, wala hana mshirika katika ufalme, wala hana rafiki wa kumsaidia kwa sababu ya udhaifu wake. na mtukuze kwa utukufu mkubwa."
Mwenyezi Mung anasema: Quran 5:120
لِلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا فِيهِنَّ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٢٠﴾
"Mwenyezi Mungu ndiye anayevithibitisha vyote vilivyo mbinguni na vilivyo ardhini na ana mamlaka juu ya vitu vyote hivyo."
Pia tazama Quran (35:44).
أَوَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَكَانُوا أَشَدَّ مِنْهُمْ قُوَّةً وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُعْجِزَهُ مِن شَيْءٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ إِنَّهُ كَانَ عَلِيمًا قَدِيرًا ﴿٤٤﴾
"Je! Hawakusafiri katika ardhi wakaona vipi ulikuwa mwisho wa waliokuwa kabla yao? Na hao walikuwa wana nguvu zaidi kuliko wao. Na hapana kitu kinacho weza kumshinda Mwenyezi Mungu mbinguni wala katika ardhi. Hakika Yeye niMwenye, kujua, Mwenye uweza."
Viumbe vya ulimwengu huu vinahitaji Mwenyezi Mungu ili viweze kuishi kama vile vilivyo hitaji Mungu ili kuwepo/kuja duniani, ubunifu pamoja na matokeo yake ni sawa na ule wa Mwenyezi Mungu kwa sababu ni mwendelezo wa nguvu zake hizo wao ni wajanja sana kwa kuwa wameweza kuvumbua mambo na vitu mbalimbali bali wanatakiwa waelewe kuwa uwezo huo wamemegewa na Mwenyezi Mungu. Kama ilivyo kwataa ya umeme ili iweze kuendelea kutoa mwanga, sharti ipate nguvu kutoka katika kituo cha nguvu ya umeme (mfano bwawa la mtela kwa Tanzania) kwa sharti pawe na chanzo na kisha pawe na umeme ambao pasipo huo taa hiyo haiwezi kuwaka.
Quran tukufu inasema katika sura (35:15) kwamba:
"Binadamu wote wanamhitajia Mungu wala yeye Mwenyezi Mungu si muhitaji kwa wanadamu
"
Al-Imam Ja'afar amani iwe juu yake amesema: "Mamlaka/uwezo na nguvu za Mungu ni kubwa sana kwa nguvu nyingine kuwepo katika dunia bila idhini yake.
Laiti kama Mwenyezi Mungu asingetujalia kuwa na uhuru na kama asingekuwa anatupa nguvu kila wakati kwa kweli tusingeweza kufanya kitu chochote kile, kwani tunaweza kusema kwamba uhuru tulio nao umejigawa katika tapo (2) mbili yaani kwa upande mmoja kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kwa upande mwingine kutoka kwetu sisi wenyewe. Tunaweza kutumia mali ghafi (vitu tulivyopewa na Mungu) aidha kwa manufaa kiuchumi au tunaweza kutumia vibaya hatimae vikatuathiri.
Fikiria kwamba kuna mtu ana moyo wa bandia ambao tunaweza tukazima betri hizo au kuwasha hatimae moyo ukafanya kazi kila tulichokidhibiti pale ni ule mkono wa umeme unaotoka katika betri na kwenda katika ule moyo wa umeme.
Mara baada ya kuwekwa betri moyo ule utafanya kazi na mtu yule akawa yu katika pilika pilika zake mfano akiwa anafanya mambo mabaya au mazuri hiyo itatokana na matakwa yake mwenyewe wala siyo wewe uliye muunganisha na betri. Kwa maana nyingine jinsi ya kutumia mkono ule wa umeme au atakachofanya mara baada ya kuunganishwa na betri ni juu yake.
Vivyo hivyo uwezo tulio nao unafanana sana na suala hili Mwenyezi Mungu anao uwezo muda wowote wa kutupa nguvu zinazotufanya tufanye shughuli zetu.
MTAZAMO WA KATI
Kila kiumbe hapa duniani kinapata muongozo fulani ambaondio unawafanya wafikie hatua ya maendeleo.
Tunafahamu kwamba mimea ina kazi kubwa ya kupambana na mazingira yake pamoja na ukweli kwamba hujifanya ngangari ili kuyashinda mazingira hayo, tukichunguza sifa za mimea na wanyama utagundua kuna tofauti kubwa sana baina ya makundi hayo mawili ya viumbe hai.
Ili wanyama waweze kujipatia mahitaji yao (chakula) hawana budi kujihusisha katika pilika pilika nyingi zaidi kuliko mimea. Wana hitajinyenzo kadhaa katika kufikia mafanikio yao.
Japokuwa wanyama wanaonekana kuwa wanaathiriwa sana na silka lakini kuna wakati huwa na uhuru katika mambo yao. Binadamu ambaye amefikia hatua kubwa sana ya maendeleo kutokana na kuwa na uhuru kamili katika matendo yake ana kiwango kidogo sana cha hulka. Mazingira yanatosheleza kwa kiwango fulani mahitaji ya mimea. Kwa upande wawanyama japokuwa mama anawajibika kufanya juhudi fulani kumbeba, kumnyonyesha na hata kumlinda mtoto wake huyo na madhara mbalimbali hulka huonekana mapema sana kwa mtoto mfano mama halazimiki sana kuchukua hatua za kumfundisha mtoto.
Lakini kwabinadamu tunakuta kwamba hana kiwango kikubwa cha hulka kiasi kwamba uwezo wake wa kupambana na hali isiyofaa kutoka katika mazingira yake ni dhaifu ukilinganisha na wanyama. Hivyo kiwango cha utegemezi kwa wazazi wake kinakuwa ni kikubwa sana na huendelea kwa muda mrefu sana mpaka pale mtoto wa (binadamu) anapofikia kujitegemea kwa kutumia viungo vyake.
Quran tukufu inaelezea kwa makini juu ya udhaifu wa mwanadamu tazama Quran (4:28)
يُرِيدُ اللَّـهُ أَن يُخَفِّفَ عَنكُمْ وَخُلِقَ الْإِنسَانُ ضَعِيفًا ﴿٢٨﴾
"Mwenyezi Mungu anataka kukupunguzieni taabu, na Mwanadamu ameubmwa dhaifu"
Mazingira/asili imemwacha mwanadamu katika hali ya kuwa huru zaidi kuliko ilivyokuwa kwawanyama. Tunaona kuwa binadamu kwa upande mwingine kuwa wana uhuru usioweza kuelezeka na kukua kwa ufahamu.
Wakati binadamu akifurahia uhuru alionao binadamu amekuwa na uhuru wa kuchagua mambo anayoyataka lazima kutakuwa na kitu kitacho kuwa kinapinga hulka.
Mara binadamu anapokuwa katika migogoro kamwe hatoweza kupata ustawi (utulivu) au hawezi kabisa katika hali hiyo ya mgogoro kuchagua njia iliyo bora. Ukizingatia kwamba binadamu yeye ndiye aliyeamua kubeba jukumu kubwa kabisa jukumu la kuufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu na kuutekeleza kama inavyopaswa kufanya kazi ambayo mbingu na ardhi zimeshindwa kulibeba jukumu hilo. Kwa hiyo binadamu atajikuta anakabiliwa namambo mawili nayo ni ima aamue kuwa mfungwa /mtumwa wa hulka na tamaa isiyo na kipimo hivyo ikampeleka pabaya au kwa kutumia uwezo mkubwa wa akili, uhuru ili aweze kujiletea maendeleo yake.
Mara mwanadamu anapokuwa amejitoa kutoka katika shuruti yaani kushurutishwa kufuata mfumo au kitu chochote kile ambacho nafsi yake haipendi (hulka) hapo huwa amekatilia mbali minyororo ya utumwa na hatimae kutumia uwezo wake wa kuzaliwa na ule wa kujifunza basi muundo wake wa fahamu hupotea hii ni kutokana na ukweli kwamba kadiri mtu anapotumia sana sehemu ya kiungo cha mwili wake ndipo kiungo hicho kinavyoweza kuendelea akikiacha bila ya kutumia hudumaa
Uwezo wa kumiliki sayansi na kustarabika yote haya ni matokeoa ya uhuru alionao mwanadamu mara binadamu anapopata uhuru kamili na akaendelea na juhudi zake za kujiletea manufaa basi uwezekano wa kuendelea mbele ni mkubwa sana kadiri ya kipawa alichonacho na uwezo wake unavyokomaa ndipo atakapobadilika kuwa ni chanzo cha ustawi katika jamii.
Matokeo ya uhuru wabinadamu hivi sasa yanaonekana katika kila kona. Na sasa hebu tuone nikitu gani kinachoweza kumzuia mtu kutotumia uhuru au vikwazo vilivopo katika utumiaji na uwezo aliopewa mwanadamu.
Mtazamo sahihi wa shia ambao wameutoa kutoka katika Quran na pia kutokana na maneno ya Maimam ambayo yanawakilisha mtazamo wa tatu ambao ni baina ya makundi yale mawili nayo ni yale ya wale wanaosema kwamba binadamu yupo huru kabisa na lile kundi linalosema kwamba binadamu yupo katika namna (2) anao uhuru na pia uhuru wake umezibitiwa kwa kiasi fulani. Ni wazi kwamba uhuru tulionao katika matendo yetu unatofautiana sana na jinsi jua linavyotembea, pia mwezi, na dunia au jinsi mimea na wanyama wanavyotembea, uhuru tulionao katika kuchagua na kufanya mambo mema au mabaya unatokana na nafasi ya maamuzi yaliyopo katika nafasi zetu. Sasa ni wajibu wetu kutumia nafasi kwa umakini, kabla ya kufanya jambo sharti tulipime hilo jambo na hatimae kufanya maamuzi sahihi. Haya ni mapenzi yake Mwenyezi Mungu kwamba sisi waja wake tuwe na nafasi/uamuzi katika mambo yetu.
Kila tunalolifanya katika ulimwengu sharti litakuwa tayari limeshatambuliwa na Mwenyezi Mungu. Kila nyanjaya maisha yetu sharti Mwenyezi Mungu awe ana ujuzi nalo.
Kwa hiyo Mwenyezi Mungu anayatazama matendo yetu kwa karibu sana kiasi kwamba sisi wenyewe hatuna uwezo wa kutambau jinsi yeye anavyoshughulikia mambo yetu.
Mwisho uhuru wetu hauwezi kuvuka mipaka ya mapenzi yake yeye (Mwenyezi Mungu) pamoja na kuwa na uwezo wa kuyatawala mazingira yake bado mwanadamu anazibitiwa na mambo fulani ambayo yako nje ya uwezo wake mfano amekuja hapa duniani bila ya ridhaa yake na pia hufunga macho (kufa) bila ridhaa yake.
Al-Imam Ja'afar al-Sadiq amani iwe juu yake amesema kwa hakika hayupo katika makundi yote haya mawili yaani kwamba ana uhuru kamili au matendo yake yanazibitiwa na Mwenyezi Mungu bali yupo baina ya makundi haya mawili.
Ni sawa kuwa mwanadamu anao uhuru katika mambo yake lakini kuamini kwamba uhuru alionao hauna mipaka ni sawa kabisa na kumshirikisha Mwenyezi Mungu kwa sababu yeye pekee ndiye mwenye mamlaka yasiyo na mipaka. Bali uhuru alionao mwanadamu umewekwa naMwenyezi Mungu nao una mipaka yake kutegemea mapenzi yake Mwenyezi Mungu.
Kwa mtazamo wa Uislamu binadamu siyo kiumbe kilichopo bila ya makusudio yoyote yale aliyemuumba mwanadamu amempa mwongozo ili kwa kuufuata huo atakuwa amefikia lengo la kuumbwa kwake mfano amepewa akili maarifa, uwezo wa kutambua na ubuni. Makosa yaliyofanywa na makundi yote mawili ni kudhani kwamba huyu binadamu yuko katika uelekeo wa aina mbili tu mmoja ni ule kuwa binadmu hana hata chembe ya uhuru katika mambo yake kila analofanya limepangwa na Mwenyezi Mungu au kuwa anao uhuru usio na mipaka katika matendo kitu ambacho itakuwa sawa na kumwekea Mwenyezi Mungu mwenza (shirki). Bali ukweli ni kwamba matendo ya mwanadamu kwa upande mmoja unaweza kuyahusisha na mwanadamu mwenyewe na kwa upande mwingine sharti yahusishwe na Mwenyezi Mungu, moja kwa moja binadamu anahusika katika matendo yake uhusika wa Mwenyezi Mungu katika matendo ya binadamu sio wa moja kwa moja lakini mahusiano yote hayo ni kweli na sahihi kabisa tazama Quran tukufu (2:6-7),
Wakati mwingine madhambi yanaweza kuwa siyo makubwa kiasi kwamba nafasi ya msamaha isiwepo hali yapo madhambi ambayo mtu akiyafanya anaouwezo wa kuomba msamaha.
Lakini kuna madhambi mengine ukiyafanya Mwenyezi Mungu ndio kwanza anakuelekeza huko huko nahuweka alama/kizibo nyoyo za watu kama hao. Imam amekaririwa akisema kwamba Mwenyezi Mungu ameumba kila kitu kwalengo yaani kila tukio jambo linalotokea lazima pawepo na chanzo cha kutokea kwa hicho kitu/jambo. Mojawapo ya chanzo alichoumba ni mwanadamu na uhuru alionao mwanadamu ili kuweza kwenda sambamba na ile kanuni isemayo kila jambo linachanzo chake.
Hii nikanuni muhimu sana katika maisha yetu machaguo yetu na matakwa tuliyonayo yanakuja kuchukua nafasi ya mwisho kabisa katika muundo ule wa vyanzo.
Aya za Qur'an zinazoelezea mambo yote na Mwenyezi Mungu (yaani kwamba kila kitu kinahusishwa moja kwa moja na Mwenyezi Mungu) hizi zinaelezea ule mfumo kwamba vitu vyote asili yake ni yeye kwa sababu yeye ndiye wa mwanzo ndiye mbunifu wa kila kile kinachoonekena na kisichoonekana. Hata ule uhuru tunaosema kwamba binadamu anao yeye ndiye aliyempa mwanadamu kwa hiyo mwanadamu amepewa uhuru wa kufuata matamanio ya nafsi yake yeye mwenyewe ili asije akalaumu kwamba amepangiwa njia ya kufuata.
Kama kuna shuruti/lazima yoyote ni ile kufuata matamanio ya nafsi yake kwa kuwa hilo lilishapangwa na Mwenyezi Mungu kwamba mwanadamu sharti atumie akili yake katika baadhi ya mambo katika maisha yake. Lakini sio kwamba mwanadamu hulazimishwa kufanya mambo na Mwenyezi Mungu.
Hivyo tunapofanya mambo mazuri uwezo ule wa kufanya mambo hayo unatoka kwake Mwenyezi Mungu isipokuwa chaguo la kufanya linatoka kwetu yaani chaguo la kutumia uwezo ule unatoka kwake Mwenyezi Mungu.
Kuna aya nyingi zinazoonyesha kuwa Mwenyezi Mungu anatambua kwamba huyu mwanadamu ana uhuru mfano tazama Quran (99:7-8)
فَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ خَيْرًا يَرَهُ ﴿٧﴾ وَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ شَرًّا يَرَهُ ﴿٨﴾
"Basi anaye tenda chembe ya wema, atauona! "Na anaye tenda chembe ya uovu atauona!
"Kwa hakika mnawajibika kwa matendo yenu mnayoyatenda"
Quran (16:93)
وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَجَعَلَكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَلَـٰكِن يُضِلُّ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ وَلَتُسْأَلُنَّ عَمَّا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٩٣﴾
"Na Mwenyezi Mungu angelitaka, kwa yakini angeli kufanyeni Umma mmoja. Lakini anamwachia kupotea anaye mtaka na anamwongoa amtakaye. Na hakika mtaulizwa kwa yale mliyo kuwa mkiyafanya."
Pia tazama Quran (6:148).
سَيَقُولُ الَّذِينَ أَشْرَكُوا لَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا أَشْرَكْنَا وَلَا آبَاؤُنَا وَلَا حَرَّمْنَا مِن شَيْءٍ كَذَٰلِكَ كَذَّبَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ حَتَّىٰ ذَاقُوا بَأْسَنَا قُلْ هَلْ عِندَكُم مِّنْ عِلْمٍ فَتُخْرِجُوهُ لَنَا إِن تَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنْ أَنتُمْ إِلَّا تَخْرُصُونَ ﴿١٤٨﴾
"Na watasema walio shirikisha: Lau kuwa Mwenyezi Mungu angetaka tusingeli shiriki sisi wala baba zetu, wala tusingeli harimisha kitu chochote. Vivi hivi walikanusha walio kuwa kabla yao mpaka walipo onja adhabu yetu. Sema: Je, nyinyi mnayo ilimu mtutolee? Nyinyi hamfuati iladhana. Wala hamsemi ila uwongo tu."
Kama ingekuwa uokovu naupotovu wa binadamu unategemea tu matakwa ya Mwenyezi Mungu basi pasingekuwepo na hata chembe ya udhalimu katika dunia/ardhi. Kungekuwa na uongofu tu. Baadhi ya watu waovu ambao wamedai kwamba kila jambo walilolifanya liwe baya au jema lilikuwa naridhaa ya Mwenyezi Mungu Quran ina sema tazama (7:28). Kama ilivyo kwamba Mwenyezi Mungu atawalipa mema wale waliofanya mambo mazuri hapa duniani, Pia atawaadhibu wale waliofanya maovu katika dunia hii.
Mtazamo wa Uislamu kwa mujibu wa shia juu ya hoja hiyo ni kwamba binadamu hana ule uhuru kama watu wanavyodhani uhuru usio na mipaka kiasi kwamba akafanya mambo kinyume na ule utaratibu ulio wekwa na Mwenyezi Mungu(s.a.w.w)
.
Kama watu watakubali kwamba binadamu anao uhuru usio na mipaka basi hiyo itakuwa na maana kwamba Mwenyezi Mungu atakuwa anafarikiana na viumbe vyake hali si kweli hiyo siyo sifa yake Mwenyezi Mungu kwa maana hashindani na viumbe vyake. Wakati huo huo nivizuri ieleweke kwamba mwanadamu sio mfungwa kiasi akashindwa kutumia uhuru na uwezo aliopewa katika mambo yanayomkabili (maisha yake) mwanadamu hayupo kama mnyama ambaye anatawaliwa na hulka. Quran tukufu inasema wazi kwamba Mwenyezi Mungu amemuonyesha mwanadamu njia ya uongofu lakini hakumlazimisha kuifuata njia hiyo wala hakumlazimisha kuingia katika upotevu tazama Quran (76:3).
SHARTI YA KUCHAPA
Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein
Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini
ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.
MWISHO WA KITABU